Unabii 94
MIMI, YAHUVEH, Nasema, “Msipuuze Hasira ZANGU kwa kuwa imekuwa Ikiongezeka kama Moto Mkubwa”
Imeandikwa/Kuzungumzwa katika Upako wa ROHO MTAKATIFU (RUACH HA KODESH) Kupitia Mtume & Nabii Elisheva Eliyahu Disemba 22, 2007; “Ujumbe Mdogo” Imetajwa katika Unabii 93
Neno hili lilikuja kwa sababu Sabato, Elisheva Aliongozwa kusoma Ezekieli, Sura 9-16. Pia alikuwa anaombea mwanamume aliyemuona katika ndoto kitambo kidogo. Mwanamume anayeitwa “Caleb” katika neno hili la Kinabii ni mwanamume Elisheva alikuwa amemuona kwenye ndoto. Anatofautishwa na nywele nyeupe kama theluji na bila laini usoni mwake. Ana tabasamu ambalo halikuacha uso wake bila kujali askari walichokuwa wanamfanyia, kumaanisha alikuwa anateswa na kunyimwa chakula. Pia alikuwa analia, lakini hakuna yeyote aliyeona.
Katika ndoto Elisheva alienda kwake. Alijitokezea kwake. Alikuwa anaomba na amevaa kitambaa cha maombi. Alimpa mkate kidogo wa ushirika, kama mkate usiochachwa. Alisema, “Usijali, Narudi tena na ninaporudi nitakuletea mkate zaidi na mvinyo.” Mwanamume huyu anapenda YAHUSHUA. Alijua yupo Yerusalemu. Alikuwa na kazi ambayo ni ya kuwatia moyo wengine, basi, kila wakati ana tabasamu usoni mwake-akificha huzuni yake kibinafsi na mateso kwa ajili ya YAHUSHUA.
Elisabeth (Elisheva) alipoamka kutoka kwa ndoto hii alishangazwa na upendo aliouhisi kwa mwanamume huyu.
* * * * * * *
Yafuatayo ni Unabii ulivyokuja
—na Nabii Elisheva, akizungumza katika "Ndimi Takatifu," kama ROHO wa MUNGU Alivyomjalia kutamka (Matendo ya Mitume 2:3-4) kwa lugha za wanadamu na malaika (1 Wakorintho 13:1). Elisheva anazungumza katika ndimi Unabii ukitokea (1 Wakorintho 14:6).
Inayo MAJINA ya KIEBRANIA ya MUNGU:
YAH/YAHU יה ni JINA TAKATIFU la MUNGU, kama vile “Alleluia” au “Hallelu YAH” הללו–יה ambayo humaanisha “Msifu YAH”: YAHUVEH/YAHWEH י-ה-ו-ה MUNGU BABA; YAHUSHUA/YAHSHUA יהושוע MWANA WA PEKEE WA MUNGU—(HA MASHIACH המשיח inamaanisha “MASIHI”; ELOHIM אלוהים INAMAANISHA “MUNGU.”)
Ufunuo wa “SH’KHINYAH GLORY” שכניה תפארה —kama JINA la KIBINAFSI la RUACH HA KODESH רוח הקדש, (katika Kiiengereza “ROHO MTAKATIFU”) —upo kwenye tovuti hii.
(HA SH’KHINAH {SHEKINAH} ni Kiebrania inamaanisha UWEPO WA MUNGU.)
Zaidi ya hayo, ABBA YAH אבא יה humaanisha “BABA YAH” na IMMA YAH אמא יה humaanisha “MAMA YAH.”
Maandiko yaliyotajwa yametoka KJV au NKJV, isipokuwa pale palipotajwa vinginevyo. Bonyeza kwa upande wa kulia zile nambari za maelezo ya chini (footnote) kufungua ukurasa mwingine.
* * * * * * *
Maneno ya YAHUVEH kwa Elisheva Aliyosema yaongezwe mbele ya Unabii zote:
Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako.
Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako.
Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha.
Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo.
Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli.
‘‘Mimi ndimi BWANA YAHUVEH: hilo ndilo JINA LANGU! Sitampa mwingine UTUKUFU WANGU, wala sanamu SIFA ZANGU.” Isaya 42:8
(Unabii 105)
Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kutoka Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati:
“Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”
—2 Mambo ya Nyakati 36:16
Alafu, Julai 2016:
Ole kwa yeyote atakayethubutu kujaribu kuwadhuru— hawa wawili walio na upako. Mtajuta kuzaliwa kwenu. Msiwaguse masihi WANGU, msiwadhuru Manabii WANGU (Zaburi 105:15; 1 Mambo ya Nyakati 16:22). Ingekuwa ni heri kwenu kama MIMI, BABA YAHUVEH, Ningerarua ndimi zenu!
(Unabii wa 128)
Na kutoka Nabii Ezra:
Nawaonya nyote—nyote mnaokuja dhidi ya Huduma hii NA UNABII hizi na Elisheva na Mimi, Wahudumu wa Huduma ya Amightywind—Nawaonya nyote sasa, Msiwaguse Masihi wa YAH, msiwadhuru Manabii WAKE’ (Zaburi 105:15; 1 Mambo ya Nyakati 16:22) kabla Ghadhabu za Gongo la YAH zije juu yenu. Lakini kwa wale waliobarikiwa na wao ni baraka katika Huduma hii, na ni waaminifu, na wamepokea Unabii hizi, baraka tele zitakuja juu yenu—yote kulinda yale ambayo ni ya YAH katika JINA la YAHUSHUA.
* * * * * * *
Unabii 94 Unaanza:
Disemba 26, 2007
…Kutoka leo, nyinyi watano mnapoichukua [ushirika], mwanamume huyu hafai kuachwa nje [ya maombi yenu]. Na nitawapa ufunuo zaidi ya yeye ni nani. Kwa sasa, mnaweza kumuita “Caleb.”
Siku hii, Elisheva, Ninakuamuru wewe, “Furahia siku hii.” Ninataka kukuona ukicheza. Ninataka kukuona ukifanya yale ambayo umekuwa ukifurahia NAMI. Acha akili yako ipumzike. Kwa kuwa Nitakuonyesha na Nitakufunulia wewe na Unabii mpya utaachiliwa kuhusu Israeli, kuhusu hazina zilizofichwa-Nikianza na Ezekieli 9.
Kwa jua haya! Hakuna binadamu yeyote anayeweza kukunyamazisha! Hakuna pepo yoyote inayoweza kukunyamazisha! MIMI, YAHUVEH, Nina nguvu ya kukunyamazisha na kwa unyenyekevu wewe huwa Miguuni MWANGU daima.
MIMI hucheka kila wakati Nasikia ukisema, “Mimi niko tu kwa mambo yangu.” Wewe haupo kwa mambo yako. Elisheva, wewe huwa upo kwa mambo YANGU! Wakati unapocheza mchezo, upo mbele ya kiti CHANGU cha Enzi. Kila wakati, niko akilini mwako.
Kwa kuwa Elisheva Nimekuinua na sasa Neno litakuja kutetea wale ambao ni WANGU kwa kweli-kule Israeli, wanaohisi wako pekee yao. Mnawaita Wayahudi wa Kimasihi. Hawana nabii. Lakini nimekuinua wewe na kukuweka ulipo na utatumika kuwaletea Mana kutoka Mbinguni.
Utatumika kutamka Hukumu ZANGU kwa wale wengine. Utatumika kuleta Mvinyo WANGU Mpya. Kwa kuwa Ninao Watakatifu waliofungwa pale Gaza. Ninao Watakatifu wanaoteswa kando ya maadui. Nina Bibi Arusi waliofungwa pale Gaza. Na Ninakuita uwaombee wapate uhuru.
Nina Bibi Arusi pale Lebanon. Ndio, Nina Bibi Arusi pale Iraq pia-wamefichwa, wamepuuzwa, wanaohitaji Neno kutoka Mbinguni. Nina Bibi Arusi kule Uchina. Wao ni Bibi Arusi wa Kichina. Kwa hivyo shetani anataka kukunyamazisha, kukufanya uwe kimya lakini Ninakuambia: utaongea kwa sauti ya juu tena zaidi.
Nyinyi wote-nyinyi wote anzeni kusoma Maandiko ambayo Nimemtolea Elisheva. Chimba katika kila neno. Kwa kuwa Ninakuambia kuna mgodi wa dhahabu uliofichwa ambao bado haujaja na haupo mbali.
Mnapoona vitu vikifanyika kule Israeli, jueni tu MIMI sitakejeliwa virahisi.
Tayari Nimetoa Unabii na ndani yake Nikasema-kuwa MIMi, YAHUVEH, Nasema-‘Hamuezi kupeana kile ambacho sijawapa kupeana.’ Tena, weka Kumbukumbu hii mbele ya dunia. Kwa kuwa Nimezungumza.
Kuna matokeo ambayo lazima yatatekelezwa.
Kwa kuwa Nimewaamuru Israeli kutubu.
Jihadhari na fikra ambazo zitakuja mnaposoma Maandiko haya ambayo Nimeamuru Elisheva kusoma siku hii na kuyawaza. Utakaposikia sauti Ikisema, “YAHUVEH hawezi kufanya hivyo,” jua haya, ndio Nitafanya vivyo hivyo.
Msipuuze Nguvu YANGU. Msipuuze Hasira YANGU kwa kuwa imekuwa ikiongezeka kama moto mkubwa. Imesababisha jehanamu kuma moto zaidi. Wanazungumza juu ya ongezeko la joto duniani. Moto ya jehanamu ndiyo inayoongeza joto hapa duniani-pamoja na yale ambayo imezikwa na kufichwa huku ulimwenguni kuliko na baridi zaidi. Changanya haya yote na uchafuzi wa binadamu-kemikali kwenye hewa. Kwa kuwa ni sababu zaidi ya moja. Matajiri wanafikiria ni wao tu watakaoepuka.
Wanaamini uongo shetani anayowaambia. Lakini Neno LANGU lasema, “Wapole ndio watakaorithi ulimwengu huu.” (Zaburi 37:11; Mathayo 5:5) wanyenyekevu-sio walio na kiburi na matajiri.
Nyinyi ni matajiri kupitia Imani yenu KWANGU.
Nyinyi ni matajiri kupitia Hazina ambazo wengine hawawezi kuona;
Nimewapa Ulinzi ambao pesa yoyote haiwezi kununua.
MIMI Ndiye MABAWA AMBAYO MNAJIFICHA CHINA YAKE (Zaburi 91).
MIMI-NDIYE-Ninayewapa moyo.
DAMU YANGU ILIYOMWAGWA pale Kalivari
Ndiyo KITU ya pekee inayowaokoa.
Kupitia JINA LANGU!
Kupitia DAMU YANGU!
Mna USHAHIDI (1 Yohana 5:9)!
Mna USHUHUDA!
Hata kwa wale ambao kwa hii dunia maisha yao inazimwa,
Ni gamba tu wanalozungumzia.
Hawawezi kuua
Kile ambacho chafaa kuwa-Milele (Mathayo 10:28).
Kukosa kuwa kwa mwili ni kuwa kando YANGU,5
Kwa wale ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo.
Mwisho wa Unabii.
Imezungumzwa, imeandikwa Disemba 22, 2007
Nabii Elisheva Eliyahu.
[Amalizia maoni kwenye kinaza sauti:]
[Elisheva:] Tunatuma baraka kwa Caleb, BABA YAHUVEH, katika JINA LA YAHUSHUA. Tunatuma maneno ya kumtia moyo. Tunatuma maombi. Tunakushuru kuwa amesikia maombi yetu. Tunakushukuru, BABA YAHUVEH kuwa atatuandikia. Ataweza kupata kompyuta. Sijui yuko wapi BABA YAHUVEH. Sijui ni vipi utafanya haya. Lakini kwa njia fulani, kwa namna fulani, neno hili litapeanwa na atapata Unabii hizi kuwatia moyo wote ambao ni Bibi Arusi wa Israeli, pale Yerusalemu, katika JINA la YAHUSHUA, kule Lebanon, mahali popote walipotawanyika kote duniani, BABA wa MBINGUNI.
WEWE Ulisema kuwa una Ringmaiden mmoja tu. Shetani anaposikia hiyo anafikiria kuwa amenipata kweli, lakini tu kama WEWE utairuhusu BABA YAHUVEH. Hata taabu hii iliyokuja mwenye mwili huu dhaifu, BABA YAHUVEH, ni WEWE tu pekee unayeweza kuiponya katika JINA la YAHUSHUA. Ni wewe tu ambaye ni MKOMBOZI, YAHUSHUA. Ni kwa DAMU YAKO ILIYOMWAGWA. Asante. Asante.
Sisi (Caleb na mimi) ni moja. Ninapoteswa pia yeye huhisi kuteswa. Sisi wote ni moja. Sisi wote tunafaa kuchukua ushirika na kila ushirika. YEYE Amesema [YAH Amesema], “Kwa sasa Nimekupa jina Caleb.”
Ezekieli [9]! Ipo pale pale. Ni ya YAHUVEH. Shetani yupo na [UFO] na YAHUVEH ana kwa kweli [Magari ya Malaika, magari ya moto], yale ambayo yalileta haya. Ni “chombo kinachopaa ambacho hakijulikani.” Na Ezekieli aliona gurudumu kule hewani na sio tu kuliwepo na gurudumu lakini gurudumu, ndani ya gurudumu.
Kuhusu Israeli pia, kuna kitu kinachoingia kule Israeli. Anzeni kusoma Ezekieli 9. Tunayo Unabii. Ni kuhusu Mwandishi, Nabii anayeenda na kuweka alama kwa wale watakatifu na wale bila alama kule Israeli watauwawa. YEYE [YAHUVEH] Amekasirika. Amekasirikia Israeli. Amekasirikia maovu. Amekasirika sasa hivi. Alisema shetani alitaka kuniua mimi kwa sababu hakutaka Neno hili litoke.
Ilikuwa kwa sababu… haikuwa juu yangu. Sawa, siri zimefichwa-zikianza na Ezekieli 9 na tena Akanifanya nisome [sura ya] 13 mpaka kule kwa nabii bandia. Wow, haya ni makuu. Huyu ni YAHUVEH lakini. Huyu ni YAHUVEH Aliye na mamlaka ya UFO nzuri na viumbe vilivyo na mabawa.
Hawazungumzii magari. Sio magari. Bibilia yangu inasema ina uso wa kiumbe kilicho na mabawa. Ina uso wa binadamu, uso wa simba na uso wa tai. Nne tena.
[Na] mabawa, unaposoma Ezekieli 10, inazungumzia juu ya gurudumu na inaongelea juu ya nyuso.
Hata sijidai kuelewa. Hata sidai kwa sababu haya ni mazito. Haya ni mazito kweli na hayajafanyika bado lakini ipo karibu kufanyika. Kwa sababu ninaamini nimepata Ufunuo huu sasa hivi unaokuja na ninaamini kile ambacho aliens watakapokuja hapa ulimwenguni na wanapigana na binadamu, Ninaamini kuwa YAHUVEH Atatuma malaika WAKE, silaha ZAKE pia kupigana vita wakati uo huo kwa sababu binadamu hatuwezi kuwashinda hawa aliens.
Lazima tupate usaidizi usio wa kawaida kutoka Mbinguni. Na Anaituma kwa wale Watakatifu. Lakini imeshikana na Israeli kwa sasa. Na kila kitu kinachoendelea kule Israeli. Haya ndiyo ninayofikiria Unabii mpya utataja juu ya Israeli, kabisa. SIFA kwa YAHUSHUA!
Mwisho wa Rekodi.
Yakobo 5:1-8 1Basi sikilizeni, ninyi matajiri, lieni na kuomboleza kwa ajili ya hali mbaya sana inayowajia. 2Utajiri wenu umeoza na mavazi yenu yameliwa na nondo. 3Dhahabu yenu na fedha yenu vimeliwa na kutu. Kutu yake itashuhudia dhidi yenu nayo itaila miili yenu kama vile moto. Mmejiwekea hazina kwa ajili ya siku za mwisho. 4Angalieni! Ule ujira wa vibarua waliolima mashamba yenu mliouzuia kwa hila unapiga kelele dhidi yenu na vilio vya wavunaji vimefika masikioni mwa Bwana wa majeshia. 5Mmeishi duniani kwa anasa na kwa starehe, mmejinenepesha kama vile katika siku ya karamu. 6Mmewahukumu na kuwauwa watu wenye haki , ambao walikuwa hawapingani nanyi.
7Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja Kwake Bwana. Angalieni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua za kwanza na za mwisho. 8Ninyi nanyi vumilieni tena simameni imara, kwa sababu kuja kwa Bwana kumekaribia.
Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!