Unabii 90

Je, JINA la ROHO MTAKATIFU ni nini? JINA la RUACH HA KODESH ni nini? “MIMI NI MAMA SHKHINYAH, pia huitwa MAMA HEKIMA, na MIMI ni UTUKUFU WA YAHUVEH!” Imeandikwa/Imezungumzwa katika Upako wa MAMA SHKHINYAH

Kupitia Mtume na Nabii Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu) Ilipokewa Februari 27 – Ilitolewa Agosti 27 – 2007

“Shekinah” inatoka kwa neno la Kiebrania HaSh’khinah inayomaanisha “Uwepo” unaofahamika kama UWEPO MKUU na unaeleweka mara nyingi kama UONYESHO WA UTUKUFU WA YAHUVEH ulio na binadamu. Shkhinah ni neno la kike la Kiebrania. Katika Yohana 17 tunasoma juu ya UTUKUFU WA YAHUVEH:

UTUKUFU ule Ulionipa nimewapa wao, ili wawe na umoja kama SISI tulivyo wamoja. MIMI ndani Yao na WEWE ndani YANGU, ili wawe wamekamilika katika umoja na ulimwengu upate kujua ya kuwa Umenituma MIMI, na WEWE Umewapenda kama Unavyonipenda MIMI. BABA, Ninataka wale ulionipa MIMI wawe pamoja NAMI pale Nilipo, ili waweze kuuona UTUKUFU WANGU, ule ulionipa MIMI kwa kuwa Ulinipenda MIMI hata kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. (Yohana 17:22-24)

Tunajua kuwa YAHUVEH Aliwapa wanafunzi wa YAHUSHUA, RUACH HA KODESH (ROHO MTAKATIFU) baada ya YAHUSHUA kurudi Mbinguni (Matendo ya Mitume 2:2-4). “MAMA” SHKHINYAH,1 ROHO MTAKATIFU, ni UTUKUFU WA YAHUVEH!

⃰ ⃰ ⃰ ⃰ ⃰ ⃰ ⃰

Yafuatayo ni Unabii ulivyokuja

—na Nabii Elisheva, akizungumza katika “Ndimi Takatifu,” kama ROHO wa MUNGU Alivyomjalia kutamka (Matendo ya Mitume 2:3-4) kwa lugha za wanadamu na malaika (1 Wakorintho 13:1). Elisheva anazungumza katika ndimi Unabii ukitokea (1 Wakorintho 14:6).

Inayo MAJINA ya KIEBRANIA ya MUNGU:

YAH/YAHU יה ni JINA TAKATIFU la MUNGU, kama vile “Alleluia” au “Hallelu YAH” הללו–יה ambayo humaanisha “Msifu YAH”: YAHUVEH/YAHWEH י-ה-ו-ה MUNGU BABA; YAHUSHUA/YAHSHUA יהושוע MWANA WA PEKEE WA MUNGU—(HA MASHIACH המשיח inamaanisha “MASIHI”; ELOHIM אלוהים INAMAANISHA “MUNGU.”)

Ufunuo wa “SH’KHINYAH GLORY” שכניה תפארה —kama JINA la KIBINAFSI la RUACH HA KODESH רוח הקדש, (katika Kiiengereza “ROHO MTAKATIFU”) —upo kwenye tovuti hii.

(HA SH’KHINAH {SHEKINAH} ni Kiebrania inamaanisha UWEPO WA MUNGU.)

Zaidi ya hayo, ABBA YAH אבא יה humaanisha “BABA YAH” na IMMA YAH אמא יה humaanisha “MAMA YAH.”

Maandiko yaliyotajwa yametoka KJV au NKJV, isipokuwa pale palipotajwa vinginevyo. Bonyeza kwa upande wa kulia zile nambari za maelezo ya chini (footnote) kufungua ukurasa mwingine.

* * * * * * *

Maneno ya YAHUVEH kwa Elisheva Aliyosema yaongezwe mbele ya Unabii zote:

Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako.

Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako.

Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha.

Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo.

Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli.

‘‘Mimi ndimi BWANA YAHUVEH: hilo ndilo JINA LANGU! Sitampa mwingine UTUKUFU WANGU, wala sanamu SIFA ZANGU.” Isaya 42:8

(Unabii 105)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kutoka Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati:

“Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

—2 Mambo ya Nyakati 36:16

Alafu, Julai 2016:

Ole kwa yeyote atakayethubutu kujaribu kuwadhuru— hawa wawili walio na upako. Mtajuta kuzaliwa kwenu. Msiwaguse masihi WANGU, msiwadhuru Manabii WANGU (Zaburi 105:15; 1 Mambo ya Nyakati 16:22). Ingekuwa ni heri kwenu kama MIMI, BABA YAHUVEH, Ningerarua ndimi zenu!

(Unabii wa 128)

Na kutoka Nabii Ezra:

Nawaonya nyote—nyote mnaokuja dhidi ya Huduma hii NA UNABII hizi na Elisheva na Mimi, Wahudumu wa Huduma ya Amightywind—Nawaonya nyote sasa, Msiwaguse Masihi wa YAH, msiwadhuru Manabii WAKE’ (Zaburi 105:15; 1 Mambo ya Nyakati 16:22) kabla Ghadhabu za Gongo la YAH zije juu yenu. Lakini kwa wale waliobarikiwa na wao ni baraka katika Huduma hii, na ni waaminifu, na wamepokea Unabii hizi, baraka tele zitakuja juu yenu—yote kulinda yale ambayo ni ya YAH katika JINA la YAHUSHUA.

* * * * * * *

Elisheva: Nilifunzwa kutoka Mbinguni vile kutamka JINA la ROHO MTAKATIFU. YEYE Anabeba JINA LA YAH katika JINA LAKE kama vile YAHUSHUA kwa sababu YEYE NDIYE WINGU LA UTUKUFU unaozunguka BABA YAH na YEYE pia ni Muumbaji Msaidizi na BABA YAH & YAHUSHUA. Hii ndiyo sababu tunatamka JINA LAKE kama SHKHINYAH. Yeye daima huleta utukufu kwa BABA YAH na YAHUSHUA!

* * *

Hakuna mwombezi mwingine mbele ya Kiti cha Enzi ILA YAHUSHUA. Ni kupitia JINA LAKE pekee na pia kupitia DHABIHU YA DAMU, inayoitwa AGANO JIPYA LA DAMU, ndipo palipo na WOKOVU.

—ROHO MTAKATIFU, katika Unabii 90

* * *

MSIABUDU “Malkia BANDIA wa Mbinguni”!

Kunao pepo, miungu ya kike, kama Ashtoreth ambao wafuasi wao hudai kuwa yeye ndiye “Malkia wa Mbinguni.” Sisi hatuabudu miungu ya kike kama maadui wetu wengine walivyotusema! “Malkia bandia wa mbinguni” sio wa MUNGU YAHUVEH, lakini ni wa shetani! Huyu sio ROHO MTAKATIFU, SEHEMU YA TATU YA UTATU, lakini ni kejeli ya shetani kwa kuwa shetani huiga kila kitu MUNGU YAHUVEH hufanya!

Tafadhali msichanganye Unabii 90 & 93 wakati ROHO MTAKATIFU (katika Kiebrania RUACH HA KODESH) Anajiita YEYE kama “MALKIA WA MBINGUNI WA PEKEE” na kuabudu miungu bandia! Sisi hatuabudu mungu bandia Ashtoreth au malkia bandia yeyote! Tunaabudu MUNGU YAHUVEH, MWOKOZI YAHUSHUA (‘YESU’) & RUACH HA KODESH (ROHO MTAKATIFU), Anayejulikana pia kama MALKIA WA MBINGUNI WA KWELI. MUNGU BABA, MWANA & ROHO MTAKATIFU ndio VIONGOZI KAMILI wa Ufalme wa MUNGU na Mbinguni. ROHO MTAKATIFU akiwa kike basi Atajulikana kama “MALKIA” na sio MFALME WA MBINGUNI. Kama wa kike, YEYE Ndiye “MALKIA WA MBINGUNI WA KWELI.”

Hadithi nyuma ya Unabii 90

Imeandikwa Agosti 2007

Ninaomba barua pepe za chuki zisije, kutoka kwa wale walio na roho ya Farisayo, wale walio na dini na sio uhusiano na YAHUVEH na YAHUSHUA na hawana jambo lolote kuwa upako ni nini.

Ninajua kuwa nimepewa upako kama Nabii Mtakatifu na sio mashindano ya nani anayejulikana zaidi au ningeshindwa, YAHUSHUA aliniambia haya kitambo. Manabii bandia ndio wale wanaotoa jumbe nzuri tu ili wasiwakosee watu. Tafadhali ombeeni Huduma hii na mimi mwenyewe na wale walio wasaidizi na washirika humu ndani, na inawahusu pia Bibi Arusi wa YAHUSHUA.

Tafadhali Bibi Arusi wa YAHUSHUA andikeni na jitambulisheni, hatimaye, tutatembelea nchi zenu na kama mnataka kushirikiana nasi, basi tuanze kujuana. Moja ya zawadi kubwa hapa ulimwenguni ni kuwajua Bibi Arusi Mtakatifu wa YAHUSHUA, wale wanaompenda na kumwabudu na kumweka YAHUVEH na YAHUSHUA kwanza katika maisha yao na upendo wao.

Neno hili lilipewa kwa sababu nilianza kuomba na kutafuta jina lake RUACH ha KODESH (ROHO MTAKATIFU). RUACH ha KODESH ni jina, maelezo ya kazi. Hata hivyo, sio jina lake RUACH ha KODESH (ROHO MTAKATIFU).

Niliweka kwenye mtandao ninaloita ‘Ndoto ya Meza ya Karamu’ na sitawahi kusahau upendo yule mwanamke mrembo aliyenizidi kwa umri alinionyesha. Alikuwa mrembo sana, bila laini au kasoro yoyote usoni mwake na niliweza kutambua kuwa alikuwa mwanamke wa umri ulionizidi. Alikuwa na nywele nyeupe, ndefu, tena zilizokuwa na mawimbi zilizolala mgongoni mwake. Ananipenda na upendo wa Mama aliyejitolea; inaonekana machoni na usoni mwake, naweza kuhisi vile anavyonithamini. Katika ndoto, niliweka kichwa changu kwa upendo begani mwake, katika ile ndoto.

Elisheva Sherrie Eliyahu

Agosti 2007

Ndoto ya Meza ya Karamu

Ilipokewa Aprili 16, 1999.

Ufunuo wa ndoto hii ulikuja katika mwezi na siku ile ile, Aprili 16, 2002, miaka tatu baadaye!

Nilikuwa na ndoto kuwa nilikuwa nimekaa katika jumba kubwa. Nilihisi ni kama ilikuwa Israeli. Najua haikuwa Marekani. Nilikaa karibu na meza nzuri iliyokuwa na kitambaa cha sanda na mapambo mazuri kwenye meza na viombo vizuri sana na viombo vya fedha ambazo sijawahi kuona. Lakini, hakukuwa na chakula mezani. Nilikaa mezani karibu na mwanamke mrembo aliyenizidi kwa umri na nikaweka kichwa changu kwa bega lake nikihisi upendo wake wa mama.

Kulikuwa pia na mwanamume aliyenizidi kwa umri katika jumba hilo na alikuwa ameniambia kuwa kila kitu mezani kilikuwa kimebarikiwa, hata kitambaa hata viombo vya fedha! Kila kitu kilikuwa tayari. Tulikuwa bado tu tunawangoja wageni na haswa, mtu au watu, sina uhakika, kutoka kule zabibu spesheli zilipandwa zilizotumika kutengeneza mvinyo. Kiersk au Kierska ilikuwa imeandikwa kwenye chupa. Kulikuwa na mwanaume aliyenizidi kwa umri na nywele nyeupe pale pia na alikuwa kama baba mpendwa kwangu na alinionyesha chupa hiyo.

Katika sehemu nyingine ya mvinyo uliofunikwa kulikuwa na utambaa niliokuwa nimeushonelea kikapu kikubwa kilichojaa zabibu kubwa za rangi ya zambarau kwenye mzabibu. Zabibu hizi zilikuwa kubwa na zenye rangi. Ni kama utambaa huu nilioudarizi ulikuwa katika pahali pa heshima na nilimwonyesha rafiki yangu wa karibu aliyekuwa amekaa karibu nami mezani, sikuwahi darizi hapo awali.

Mwanamke huyu niliyekuwa nimemlalia, alikuwa kwangu kama mama, na yule mwanaume kama baba. Nilihisi kuwa nilikuwa salama salmini katika pahali pale na kuwa nilipendwa sana. Nilifurahia na nikamwambia rafiki yangu kuwa KILA KITU kilichotumika kwa chakula chajio hicho kilikuwa kimebarikiwa!

Jikoni kulikuwa na nafasi wazi tena kubwa ambapo tulikuwa tunaweza kuona ndani, lakini bado iliyoambatanishwa kote. Sahani ziliweza kupitishwa ndani na nje na tuliweza kuona ndani, lakini sikumwona yeyote humo jikoni. Mlango wa kuingia humo jikoni ulikuwa kwenye upande wa kulia. Ile nafasi wazi iliyoangalia humo jikoni ilikuwa mbele ya meza yetu. Tulikuwa tu tunawangoja hawa wageni, haswa wale kutoka kule mvinyo mpya uliokuwa haujafunguliwa ulitengenezwa. Tulimngoja huyu mtu au hawa watu wawasili kwanza.

Mwisho wa Ndoto

Thibitisho kupitia Barua Pepe:

Mpendwa [Elisheva] Sherrie,

Ndoto yako uliyoniambia, nahisi ni juu ya karamu ya arusi ya MWANA-KONDOO!!!

Jambo la muhimu ilikuwa meza kubarikiwa kwanza kabla ya chakula kuandaliwa na “utambaa wa chakula chajio” ulioudarizi.

Kila mtu atakuwa na matendo ambayo atayaweka mbele ya BWANA lakini yatakuwa kama vibacha vichafu, lakini wewe Elisabeth [Elisheva] Sherrie, YAHUSHUA amekubariki na akabariki kibacha chako na akaibadilisha kuwa utambaa.

Kudarizi ni aina ya kufuma na kufuma ni aina ya UTANDO na picha iliyomo inawakilisha wakati, juhudi, na huduma ya kitu. Naamini kuwa utambaa huu unawakilisha mitandao yako. Naamini pia kuwa Jikoni ile inaweza wakilisha Mbinguni na Chumba cha Kula kinawakilisha pahali pengine. Kwa sababu inaonekana kuwa kutakuwa na kazi ya kufanya kabla sote tuende Mbinguni. Ndio kwa sababu upo katika chumba hiki.

YAHUSHUA pia alisema kuwa hatakunywa mvinyo hadi kurudi Kwake, inawezekana kuwa hapa ndipo mvinyo huu utatoka? Haya tu ndiyo ninayoyajua kwa sasa.

Aliyetuma neno hili hataki jina lake lijulikane.

Ufunuo wa Ndoto ya Meza ya Karamu

Aprili 16, 2002

Tarehe Aprili 16, 2002, Saa 8:00 Usiku wakati wa kusoma Bibilia, BABA YAHUVEH Alinipa ufunuo zaidi ya Ndoto hii ya Meza ya Karamu ambayo ilikuja siku ile ile, 1999.

Kierska ni KHERSA (Kursi), kitongoji karibu na pwani mashariki ya Bahari ya Galilaya. Nilikuwa nikingonja ufunuo huu wa pahali hapa ni wapi kwa sababu hawa ndio wageni wawili amekuwa akiwangoja ambao wanaleta Mvinyo Mpya nao. Hawa wageni wawili waja kabla tu ya Karamu ya Arusi ya Mwana-Kondoo.

YAHUSHUA sasa Anawapa ufunuo huu kuwaita hawa wanaume wawili (2) ambao ni manabii, na ambao katika ndoto yake anawangoja hawa wanaume wawili (2) walio na mvinyo mpya na wanatoka nchini ambapo mvinyo huu mpya unatengenezwa (KHERSA).

Tumefurahia sana, kwa sababu haya yanathibitisha jinsi tulivyo karibu na Karamu ya Arusi ya MWANA-KONDOO na kukuja kwa YAHUSHUA kwa Bibi Arusi WAKE!

Kumbukeni tunamngoja mtu au watu ambao wanakuja kutoka Kiersk au Kierska ambapo mvinyo upo chupani na hukaa kwenye rafu. Pahali hapa ndipo zabibu zilipotoka na mvinyo hutoka. Mtu huyu au watu hawa wanaokuja kutoka mahali mvinyo huu hutoka ni spesheli sana. Ikiwa mnajua au wafahamu haya, tafadhali wasiliana na Huduma hii.

Iliyoongezwa Agosti 27, 2007 – wakati wa kutolewa kwa Unabii 90

Nimekuwa nikishangaa ni mwanamke mgani anayeweza kunipenda vile. Katika dunia hii, sijawahi kuwa na mwanamke ambaye ananishauri mimi kama Mama, sijawahi jua upendo wa shangazi au nyanya duniani humu. Katika ndoto iyo hiyo nilikuwa na mtu nimwangaliaye kama baba pia, aliyekuwa na nywele nyeupe aliyenipenda sana na alikuwa akionyesha kazi ya mshono wa sanaa niliyokuwa nimeifanya na fahari, kwenye ukuta mbele ya meza ya karamu ili wote wangeweza kuiona. Katika dunia hii sijawahi kuwa na mwanaume yeyote anayenisimamia kama Baba, au uhusiano wowote wa upendo na mwanaume yeyote ila tu ndugu zangu katika YAHUSHUA ambao baada ya kupitia majiribio najua wamejaribiwa na kuthibitishwa kuwa waaminifu.

Kwa hivyo, mwanamke huyu ni nani huko Mbinguni? Upendo wake ulikuwa mkubwa sana na wa kweli mpaka nikahisi umenizunguka kwa njia kuu tangu ndoto hiyo. Sina huzuni tena kuwa sijawahi kujua vile ilivyo kuwa na Mama au Baba anayenipenda. Najua kuwa huko Mbinguni nina pendo kuu la Mama na Baba mtu yeyote angeweza kulitumainia. Lakini bado, mwanamke huyu ni nani? Mama yangu aliyenizaa hapa duniani nina uhakika yuko jehanamu, alinipa tu chuki na mateso. Kwa hivyo, Mama huyu aliye na upendo huko Mbinguni ni nani?

* * * * * * *

Sasa ninalo jibu. Sasa nahitaji maombi yenu kunipa ujasiri wa kulinena (Unabii 90), kwa sababu makanisa ya kidini watakasirika na hata wale walioamini mafundisho ya mwanadamu na maandiko yaliyotafsiriwa vibaya katika Agano Jipya wataniita nabii bandia, na lakini bado najua kuwa najua kuwa najua, nimepewa siri kutoka Kiti cha Enzi Mbinguni.

Bibilia inasema, “YAHUVEH hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi WAKE manabii siri YAKE” (Amosi 3: 7). Sasa nina furaha kuu ya kutoa siri hii kwa wote watakaoitambua sauti ya RUACH ha KODESH. Unabii huu unaweza kuwa wenye utata zaidi ya zingine zilizotolewa hadi sasa. Lakini bado nafanya haya kwa utiifu ili wengine waliohuzunika kwa ukosefu wa uhusiano wa upendo kati ya mama na mtoto watagundua kuwa kama wamemkubali YAHUSHUA wamekuwa nao wakati huu wote. Hakuna yeyote aliyenifunza haya, kwa kweli ni ufunuo kutoka Mbinguni.

* * *

Katika Mithali na Zaburi, je, mnajua kuwa hekima anafananishwa na Mwanamke (She)? Bila kusita zaidi acha niwaelezee vile nilivyojua jina lake RUACH ha KODESH tunayemthamini pia anaitwa Roho Mtakatifu. Haya basi, hapa ndipo nitakapotoa siri hii nyeti iliyotolewa kwangu na bado iliyobarikiwa zaidi kushinda zingine hadi sasa.

Kwa kadiri Unabii 90 unavyokwenda, yote yalianza wakati nilikuwa naoga kabla hatujaondoka Afrika Kusini. Tuliishi Port Alfred, mbele ya bahari wakati tukio hili la kiroho lilipotokea. Nilikuwa naomba pekee yangu na nikamuuliza BABA YAHUVEH, katika JINA LA YAHUSHUA, “Jina lake RUACH ha KODESH baadhi ya ‘jina’ ROHO MTAKATIFU ni nini? Niliomba na kusema, Baba YAHUVEH, ulilidhihirisha jina lako, YAHUSHUA ulilidhihirisha jina lako, lakini ROHO MTAKATIFU ana jina au hili tu ni jina au maelezo ya kazi?”

Nilikuwa naoga kwenye jacuzzi, nimegundua kuwa maji inayotokota katika jacuzzi ni ishara ya maji ya uzima na mimi huwa nauliza Malaika Watakatifu kuyakoroga hayo maji, kama zamani za kale (Yohana 5:4). Wakati mwingi mimi hupata Upako mkuu nikiwa naoga na kuabudu na kuimba nyimbo za sifa katika wakati huu. Jumbe za Unabii na funuo huja wakati huu na ni vigumu sana mimi kuoga bila kuomba, kuimba na kumsifu YAHUVEH, YAHUSHUA, na RUACH ha KODESH. Kuna Uhusiano wa karibu na Baba yetu YAHUVEH ambao mimi huhisi vikali nikiwa naimba nyimbo za sifa na ibada kutoka moyoni mwangu kwa WAO wote watatu (3).

(Na nilipokuwa natafuta jibu la swali hili, “Jina lake RUACH ha KODESH tunayemthamini ni nini katika tafsiri za Kiebrania na Kiaramu, soma Kitabu cha Hekima, imedharauliwa kwa sababu Mfalme James (King James) hakuruhusu iongezwe. Msiyategemee pekee yale ambayo Warumi waliandika. “Jitahidi kujionyesha kwa MUNGU kuwa umekubaliwa na YEYE.” 2 Timotheo 2:15)

* * *

Nataka kusema hapa, kuwa haya yanayofuata ni moja ya unabii nyingi zilizopewa kwangu, ambazo bado hazijawekwa kwenye mtandao. Kuna mengi ambayo yanafanyika msiyoyajua. Tulikuwa na shughuli tele kule Afrika Kusini na hata sasa tunavyosafiri dunia hii. Sihisi kwa njia yoyote kuwa nina thamani ya kutosha, kupewa heshima hii kuwajulisha jina lake ROHO MTAKATIFU. Ni heshima kuu kuitwa Nabii na bado ni jambo la kuogopa pia. Nitajibu kwa yale yote nisemayo na nisiyoyasema.

Sasa nalitoa neno hili kama nilivyoongozwa na RUACH ha KODESH. Nitakayowauliza tu ni mchukue muda na kuisoma zaidi ya mara moja, na kwa wale ambao watasikia sauti ya RUACH ha KODESH ambaye sasa nimwitaye MAMA HEKIMA au MAMA SHKHINAH GLORY, mkiskia sauti yake tafadhali niandikieni. Tafadhali wafunze wengine hata kama watawakataa kwa kufanya hivyo. Tadhali jifunzeni haya yote niliyoyakusanya hadi sasa, jifunzeni na muone kuwa sisemi yoyote ambayo hayamo katika maandiko. Ni wafasiri wa Agano Jipya pekee waliobadilisha ROHO MTAKATIFU kujulikana kwa jinsia ya kiume lakini kwa ukweli jinsia YAKE ni ya kike.

Ufunuo huu ulipewa kwangu kule Afrika Kusini, lakini nimengoja hadi thibitisho zaidi zije kutoka Mbinguni, kunijulisha ni lini nitautoa. Niliomba kujua ni lini nitautoa ujumbe huu zaidi ya nyengine hadi sasa kwa sababu ya chuki itakayotumwa dhidi yangu kutoka kwa wale wanaojidai kuwa Wakristo au wanafunzi wa YAHUSHUA na bado kwa matunda yao wanajua kuwa wana umbo la utakatifu na hawana utakatifu ndani yao (2 Timotheo 3:5).

Makanisa ya kidini watasaga meno yao kwa hasira kwa sababu hawajali ukweli na funuo zilizopewa kwa Mwanamke Mtakatifu aliye Nabii. Kutakuwa na wale wa dhati ambao wanataka pekee kuyatamka yale yaliyotafsiriwa vibaya yaliyomo kwenye Agano Jipya wakimwita Roho Mtakatifu kwa jinsia ya kiume.

Ni lazima niwakumbushe jinsi vile kiburi ya binadamu huingia ndani zaidi ya mara moja wakati inapokuja kwa jinsia ya kike katika Maandiko Matakatifu na wale waliotafsiri haya Maandiko Matakatifu walikuwa na upendeleo dhidi ya mwanamke kiongozi wa kiroho?

* * *

Hata kama unabii huu ulipewa kwangu mwezi wa Februari 27, 2007 sikuambiwa niutoe hadi mwezi wa Agosti 27, 2007. Ninataka mjue kuwa ni watu kadhaa tu ambao wamejua kuhusu Unabii huu.

Nilingoja kwa makusudi na nilikuwa na furaha kila siku kuwa bado singeweza kuutoa ujumbe huu mpya wa kinabii, kwa sababu kwa ukweli hakuna yeyote ambaye anapenda kukataliwa au kutukanwa sanasana na Wakristo wanaojidai kumwabudu Masihi yuyu huyu kama tunavyo sisi lakini wanamwita YEYE YESU KRISTO na sisi tunamwita kwa JINA LAKE Kiebrania na Kiaramu YAHUSHUA au YAHSHUA ikitegemea na nani unayemwongelesha.

Kwa maadui wangu na wale ambao watajazwa na wivu na kusema kwa nini RUACH ha KODESH alikuchagua wewe kutoa ujumbe huu? Hilo ni swali nzuri, nina uhakika kuwa nabii yeyote angefanya vivyo hivyo. Najua tu nilichaguliwa na hata kama mwili hauna furaha kwa maneno ya chuki yatakayotumwa upande wangu, najua pia siwezi kumfeli RUACH ha KODESH Mpendwa na YAHUVEH.

Wachache wameniuliza, “Utangoja hadi lini ili uutoe unabii?

Nilisema, “najua tarehe lakini kwanza lazima nipate Maandiko zaidi kuyaimarisha haya.” Mwezi wa Agosti 27, 2007 ndio tarehe Mbinguni ilichagua kwa kuzaliwa kwa Unabii huu na kuzaliwa kwa mpangilio mpya kwenye mtandao wa huduma hii. Jaribu kufikiria mshangao wangu nilivyokuwa naandika haya sasa, bado nikiwa Ulaya na angalia tarehe ya Unabii ulipopewa, Februari 27, 2007 na Unabii 89 ulipewa Januari 27, 2007. Tarehe zote 3 zipo katika siku ya 27 wa mwezi.

* * * * * * *

Neno la Kiebrania ruach (Kiaramu rucha) ni la kike katika lugha hiyo kama haya maneno RUACH ha KODESH na RUACH HA KADOSH. Katika Unabii 90 ROHO MTAKATIFU MWENYEWE Ametumia, “RUACH HA KODESH,” kama moja ya majina YAKE. Ruach inamaanisha “roho,” “upepo,” “pumzi,” au “hewa.” Sawa ya Kiyunani ni pneuma na Kilatini ni spiritus.

Katika Yohana 14:16 (KJV), jukumu la RUACH HA KODESH linaelezewa na YAHUSHUA kama ile ya “MFARIJI” na utambulisho wa “MFARIJI” na YAH Akiwa kama “mama” tunavyosoma huko Isaya 66:13, “Nitakufarijibisha huko Yerusalemu, kama mama anafariji mtoto wake.” (GNT). Kwa kuongezea, kuna vifungu vingi ambavyo Bibilia ya Peshitta yenyewe inashughulikia RUACH HA KODESH na vitenzi vya kike na/au maelezo ya kike. Kwa kweli Peshitta ya Kiaramu ya Warumi 8:16 huanza na, “Na YEYE (jinsia ya SHE haswa) hupeana ushuhuda kwa roho zetu’.

* * * * * * *

YAHUSHUA huonyesha ROHO ANA JINSIA YA KIKE: Katika kujibu swali kutoka Nikodemo aliyeuliza, “Lakini mtu awezaje kuzaliwa akiwa mzee?” ‘‘Je, anaweza kuingia mara ya pili kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe?” (Yohana 3:4) YAHUSHUA akamjibu, ‘‘Hakuna mtu yeyote anayeweza kuingia katika Ufalme wa MUNGU isipokuwa amezaliwa kwa maji na kwa ROHO [NLT]. Mwili huzaa mwili pekee, lakini Roho huzaa roho. [BSB]” (Yohana 3:5-6).

Wakati ambapo YAHUSHUA Anajibu Anakiri kuwa YEYE Alizaliwa kutoka kwa Roho pia. Anasema kuwa YEYE hakuwa mwili tu bali alikuwa ROHO kabla ya kuja KWAKE humu duniani, au vipi? Kwa hivyo, ufunuo huu uliopewa kwangu umenijia nilipokuwa nayasoma haya tena kabla ya kuyaweka kwenye mtandao. YAHUSHUA pia anakiri kuwa ilibidi Azaliwe kutoka kwa ROHO na bila shaka hii inamaanisha yule tumwitaye ROHO MTAKATIFU. Kuna watatu tu kwenye UUNGU au vipi? BABA MTAKATIFU YAHUVEH, MWANA MTAKATIFU YAHUSHUA, na ROHO MTAKATIFU katika Kiebrania Aitwaye RUACH ha KODESH.

Tulikuwa nini kabla ya kuwa mwili? Tulipoumbwa Mbinguni lazima tulikuwa viumbe vya roho, kwa ukosefu wa maneno bora. Maandiko yanasema, “Mwili na damu haziwezi kuurithi Ufalme wa Mbinguni.” Kwa hivyo, tuliumbwaje kule Mbinguni?

* * *

Naamini kuwa huu ni unabii ambapo RUACH ha KODESH Atazungumza na kutupa majibu, kwa njia ambayo sijawahi kusikia. Naamini kuwa maarifa haya yatatikisa dunia hii kwa kiroho na kimwili. Naamini kuwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI watakuwa na macho ya kiroho kuona na masikio ya kiroho kusikia.

Neno hili lililotoka Mbinguni limeniletea amani na furaha, sasa nachukua nafasi hii kulitoa kwa Ndugu na Dada zangu Watakatifu.

Nimekuwa kwenye mtandao miaka 14 nikitabiri na matunda ya huduma hii imethibitisha kuwa ni nzuri. Mkizisoma ripoti zote za wokovu mtaona jinsi Huduma hii hufika mbali. Mimi si Nabii bandia ambaye huiga habari na kudai kuwa ni Unabii. Mtakapokosa kusikia Unabii mpya, jueni kuwa nangoja wakati fulani YAHUVEH Atasema, ‘Toa Neno hilo’. Mimi hutii tu.

Nakiri kuwa wakati Neno hili liliachiliwa kwangu nilishangazwa. Sikuwahi sikia mambo kama haya. Alafu nikatafuta katika Maandiko Matakatifu na nikapata ushahidi hata kwenye Bibilia ya KJV.

Ninaongezea maandiko machache ili myatafune. Nakiri kuwa hii ni nyama ya kiroho yenye nguvu na sio ya wasio na nguvu katika imani.

Adamu hakuzaliwa, aliumbwa kutoka kwa vumbi. Hawa hakuzaliwa, aliumbwa kutoka kwa mbavu ya Adamu. Watoto wa Adamu na Hawa walizaliwa kupitia namna kawaida ya kuzaliwa. YAHUSHUA Alizaliwa lakini kule Mbinguni sio hapa duniani, vipi? Msiniulize, haya ni mapya kwangu pia. Tunajua Mariamu bado alikuwa bikira alipojifungua. Mnayafuata kweli yale niyasemayo? Hii ni nyama ya kiroho yenye nguvu, mtaimeza na kuitafuna au mtaitema? Chaguo ni lako!

Haya, mimi sina maarifa ya kutosha kuyatatua haya. Nina tu elimu ya sekondari, kwa hivyo hamwezi kuniita moja ya wale wasomi wajinga. Huu kwa kweli ni ufunuo kutoka Mbinguni na ninaomba mtabarikiwa nao kama nilivyo na wengi waliopata kujua haya. Hamtahisi kuwa mko pekee yenu tena hata kama nyinyi ni yatima kama mimi. (Kulingana na Merriam-Webster neno ‘begotten’ inamaanisha, “kuzaa kama baba.” Katika Kigiriki neno ‘begot’ ni “apokueo” inatoka kwa neno ‘kuo’ au ‘kueo’ inayomaanisha kuwa na mimba. Kwa hivyo, ‘apokueo’ inamaanisha ‘kumleta mtoto humu duniani kutoka tumboni au kuzaa kumaanisha anapopata mimba.)

* * * * * * *

Labda hoja ya kwanza inayoweza kupewa katika msaada wa jinsia ya kike ya ROHO MTAKATIFU ni uhusiano wake na ‘ROHO YA HEKIMA’ ya Kutoka 28:3 na Waefeso 1:17. Katika Agano la Kale na Agano Jipya, Hekima mara nyingi hutajwa katika jinsia ya kike: “Hekima amejenga nyumba yake, amechonga nguzo zake saba. (Mithali 9:1)

Sura za Mithali 8 & 9 kwa kweli ni kielelezo kirefu cha HEKIMA kilichoonyeshwa kama mwanamke. Katika Mathayo 11: 19 & Luka 7:35 tunasoma: “Nayo HEKIMA imethibitishwa kuwa kweli na watoto wake wote.” Katika Luka 11:49 tunasoma: ” Kwa sababu ya jambo hili, MUNGU KATIKA HEKIMA Yake alisema, ‘Tazama, nitatuma kwao Manabii na Mitume…” Katika kifungu hiki, BWANA wetu Anafananisha ‘HEKIMA YA MUNGU’ na ROHO MTAKATIFU Aliyewapa UONGOZI WA MUNGU kwa wale walioandika haya Maandiko (2 Petro 1:21), kumaanisha kuwa ROHO MTAKATIFU & ROHO WA HEKIMA ni MOJA.

Katika Agano la Kale, neno ‘lingine la ‘Hekima’ ni chokmah iliyo na mwisho wa kike. Kumbuka neno ‘Hekima’ katika Kigiriki inatafsiriwa katika neno ‘Sophia’ ambalo ni jina la kike. Kwa hivyo, sanasana ukisoma Bibilia ya KJV ambapo Agano Jipya limetafsiriwa katika Kigiriki, Hekima inafaa kutafsiriwa kama Sophia. Ni nini ilikuwa lengo la wafasiri kutoongeza haya? Katika nyakati hizi za mwisho ukweli ambao umekuwa ukifichwa unadhirishwa kwa nyakati hizi za mwisho. Na sasa kutoka Hekima ya Sulemani:

HEKIMA haitaingia kamwe katika roho ya mwenye kufanya vibaya […] kwani ROHO MTAKATIFU WA MAELEKEZO hukimbia udanganyifu (1: 4-5)

HEKIMA [-] ndani YAKE ni ROHO MWENYE AKILI, MTAKATIFU (7: 21-22)

Kwani HEKIMA […] ni safi sana, YEYE Anaenea na Anaingia katika vitu vyote. YEYE ni PUMZI YA NGUVU ZA MUNGU, DHIHIRISHO SAFI WA UTUKUFU WA MWENYEZI (7: 24-25)

YEYE Anaweza kufanya kila kitu; MWENYEWE bila kubadilika, YEYE huboresha ulimwengu, na, kizazi baada ya kizazi, hupita ndani ya nafsi Takatifu, YEYE huwafanya kuwa Marafiki na Manabii wa MUNGU (7:27)

Na ni nani angeweza kujua mapenzi YAKO, usingempa HEKIMA WAKO na kumtuma ROHO WAKO MTAKATIFU kutoka juu? (9:17)

YAHUSHUA MASIHI hulinganisha “ROHO YA UKWELI” na ROHO MTAKATIFU (Yohana 16:13). HEKIMA (SOPHIA) na ROHO MTAKATIFU hufanya kazi sawa. (1 Wakorintho 2:7-11: Warumi 5:5; 1 Yohana 5:6-7, KJV). Upendeleo wa wanaume wa wanateolojia wa baadaye usingekuwa dhidi ya wanawake, Kanisa ingekuwa imekubali matamshi katika Agano la Kale kama maelezo halisi ya RUACH ha KODESH (ROHO MTAKATIFU).

* * *

Hoja ya pili inayoweza kupewa katika msaada wa jinsia ya kike ya ROHO MTAKATIFU inapatikana katika majina mengi yanayoweza kutumika kuwataja YAHUVEH na ROHO MTAKATIFU.

Jina lake MUNGU katika lugha ya Kiebrania ni “ELOHIM”. Wasomi wengi wanakubali kuwa neno hilo lina mwisho wa wingi, ambao wengi hutumia kuonyesha tarajio la UTATU la Agano la Kale. Kile ambacho wasomi wengi hawajui au hawajali kuwajulisha baraza lao kwamba “ELOHIM” sio wingi wa “EL” jina la jinsia ya kiume. Jina hili ni wingi wa jina la jinsia ya kike, “ELOAH.” Neno ELOHIM basi ingekuwa na jinsia ya kiume na kike ingekuwa imehusiana nayo. WAUMBAJI wetu wangekuwa na jinsia zote mbili na bila shaka tunajua kuwa kulingana na Kitabu cha Mwanzo RUACH HA KODESH pia YAHUSHUA walifanya kazi na YAHUVEH kuumba Ulimwengu huu:

Kwa hiyo ELOHIM Alimuumba mtu kwa mfano WAKE mwenyewe, kwa mfano wa ELOHIM Alimuumba, mwanaume na mwanamke Aliwaumba (Mwanzo 1:27).

Hii inaonyesha kuwa jinsia zote zipo katika UUNGU. Kwamba ROHO MTAKATIFU ni uwakilishi uliyotengwa wa kanuni ya kike inaungwa mkono zaidi na neno la Kiebrania kwa Roho, “Ruach” neno la kike.

Ninanukuu sasa Jerome, mwandishi wa Vulgate ya Kilatini, (nakubali sijasoma Kilatini Vulgate, lakini nilipata hii kwa kusoma baada ya kupewa Unabii huu.) Matamshi ya Jerome juu ya Isaya 11:

Katika Injili ya Waebrania ambayo Wanazarayo walisoma yasema, “Sasa hivi MAMA YANGU, ROHO MTAKATIFU, ALINICHUKUA.” Sasa, hamna yeyote ambaye anafaa kukerwa na haya, kwa sababu “roho” katika Kiebrania ana jinsia ya kike, bali katika lugha yetu [Latin] ana jinsia ya kiume na katika Kigiriki hana jinsia. Katika Uungu, hata hivyo, hamna jinsia yoyote.

Maelezo haya ya Jerome yana ushuhuda ya kushangaza -takwimu ya kawaida zaidi haiwezi kufikiria-kwamba neno la Kiebrania la Roho, “Ruach,” ni la kike. Hii inamaanisha kuwa kwa Wakristo wa Karne ya 1-ambao walikuwa wakifanya kazi sana katika ulimwengu wa Kiaramu; (Makanisa ya Paul yalikuwa madogo kwa kulinganisha) – RUACH HA KODESH Alikuwa Kiumbe cha Kike. Ilipotea katika tafsiri kutoka kwa Kiebrania kwenda kwa Kiyunani, na kisha ilibadilishwa kuwa jinsia ya kiume wakati ilitafsiriwa kutoka kwa Kiyunani hadi Kilatini.

* * *

Hatimaye, upendeleo wa kitheolojia unasababisha Wakristo kuamini tofauti ya jinsia sio muhimu, ikizingatiwa kuwa hakuna jinsia katika MUNGU na kwamba kwa hivyo, haijalishi; na bado jinsia ya kiume inapendelewa kila wakati. Na karne nyingi ya tabia hii ya Viongozi wa Wakristo, mafundisho ya mwanadamu na mawazo, nataka ukweli na naombea ukweli wa YAHUVEH tu. Nafikiria jambo hili ni muhimu. Haturuhusiwi kubadilisha hata “nukta wala jina” moja ya Sheria, na kama MUNGU Amewakilishwa kama ‘KIUMBE’ akiwa na jinsia zote mbili za kike na kiume, basi sisi ni wajinga kuficha jambo hili katika tafsiri zetu za Maandishi Matakatifu.

* * * * * * *

Fikiria familia yoyote, na ni nini huifanya kuitwa hivyo? Siimanishi ujinga wa ushoga wa nyakati za Sodoma na Gomora, ambayo dunia hii inakabiliwa nao sasa. Niamini mimi kuwa YAHUVEH hatakejeliwa kwa muda mrefu, kama vile Sodoma na Gomora walivuna walichopanda zamani, basi itakuwa vivyo hivyo tena na wale ambao wanakubaliana na kufanya vitu hivi.

Familia ina Baba, Mama na Watoto. Haya ndiyo ninayoyasikia na kuyanena, “MIMI, YAHUVEH Niliumba simba kumzaa simba pekee, mwanamke kumzaa binadamu pekee na basi vivyo hivyo kuwa MUNGU pekee Anaweza kumzaa MUNGU. YAHUSHUA Ndiye MWANA WA PEKEE WA YAHUVEH! Kwa hivyo, nani ndiye MAMA WA MBINGUNI Aliyemzaa YAHUSHUA? Je, hii ndiyo siri ya yale yanayomaanisha ‘kuzaliwa’ katika RUACH HA KODESH?

RUACH ha KODESH ni Roho, alafu anayezaliwa tena kutoka KWAKE huwa roho na RUACH ha KODESH huishi ndani ya miili zetu hadi kufa au kunyakuliwa hadi Mbinguni, itakayotangulia kwanza. Ni RUACH ha KODESH na asili yake ya milele ambaye maandiko husema, “Kutokuwa katika Mwili ni kuwa na BWANA YAHUSHUA.” (2 Wakorintho 5:8)

Nilipokea ufunuo huu nilipokuwa najaribu kuweka ushahidi nyuma ya Neno lipya la Unabii 90. Maandiko husema, “Ni Neno ambalo huua lakini ROHO hupeana maisha.” (2 Wakorintho 3:6). Uhusiano huu mpya kati ya binadamu na RUACH ha KODESH ni moja ya vitu ambavyo hubainisha mtu ambaye ameokoka.

Kwa wale ambao watajaribu kuniita nabii bandia, fanya utafiti wako mwenyewe, jitahidi kujionyesha kwa MUNGU kuwa umekubaliwa na YEYE. Kila Mwebrania anajua katika lugha ya Kiebrania kuwa ‘Ruach’ sio jina la kiume! Mnaniambia, kwa nini ‘Hekima’ katika Maandiko Matakatifu hata katika KJV Anatajwa katika jinsia ya kike (‘SHE’)? Je, RUACH ha KODESH sio HEKIMA?

Nilikaa kwenye Paja la BABA YAHUVEH! Upendo wa BABA wa MBINGUNI

Iliongezewa Juni 20, 2010

Mnamo Juni 20, 2010, Nilizungumza na BABA YAHUVEH na nikaketi kwenye paja LAKE—na kama vile nilikuwa nimepumzisha kichwa changu juu ya Bega la TAKWIMU LA KIKE kama ilivyoandikwa kwenye Kitabu cha Mithali ‘”MAMA HEKIMA” kwenye Ndoto ya Meza ya Karamu—Pia niliweka kichwa changu juu ya Bega la BABA YAHUVEH, BABA yangu wa MBINGUNI. Nataka kuyatoa haya hapa kwa sababu haya yalitokea wakati ambao nilikuwa nikiteswa sana na mengi ni kwa sababu nilikuwa nikitambulishwa kama mwongo kwa kutoa Unabii 89 na 90.

Mkutano

Ingawa nililala, najua hii haikuwa “ndoto” kwa maana ya kawaida ya neno. Kwa maana najua ilikuwa ukweli. Yote ilianza na mimi kuomba kwa YAHUVEH na kulia kwa sauti kubwa kwa uongo mpya wa kashfa ambao maadui wanasema kwa kusudi la kuwafukuza kondoo na wana-kondoo mbali na Huduma hii. Hisia zangu hazikuweza kuvumilia zaidi ya haya. Nilisema kwa sauti kubwa:

BABA YAHUVEH kwa JINA LA YAHUSHUA MASIHI, TAFADHALI NIPELEKE MBINGUNI! SITAKI KUWA HAPA DUNIANI TENA! SIOMBI KUFA, BALI NATAKA TU KUJA MBINGUNI JINSI ULIVYOMCHUKUWA Eliya wa Kale! DUNIA HII NI CHAFU SANA NA SIOMBI KUFA KWANI SITAKI KAMWE MWILI WANGU AMBAO UMEISHI KWA UTAKATIFU KWAKO KUZIKWA KWENYE DUNIA HII CHAFU!

Alafu, nilikuwa nikitazama mfano wa kile kilichoonekana kama mtu mkubwa sana lakini sikuwahi kuona USO WAKE. Na bado najua ilikuwa BABA YAHUVEH! Alikuwa Amekaa kwenye kiti kilichokuwa kimeundwa na kitambaa laini chumbani mwangu! Siwezi kuielezea kwa maana najua kuwa YAHUVEH hutumia ardhi kama kiti cha miguu kwa hivyo hakika hakuweza kutosha kwenye kiti hicho au nyumba hii na bado Alinijia kwa njia hii.

Alisema, “Njoo hapa,” kwa sauti kali. Niliogopa kwamba nilisema kitu kibaya na sikuenda KWAKE. Badala yake nilikumbuka jinsi Ayubu alivyoingia katika shida kwa kumhoji YAH.

Kisha Akanyoosha Mikono YAKE na kwa Sauti ya upole Akasema, “Nimesema njoo hapa.” Na kama mtoto mdogo nikaenda kwa BABA yangu na kukaa kwenye Paja LAKE. Na nikaanza kufunua moyo wangu na sababu zote sikuwa nataka kuwa duniani humu tena. Nilimwambia kuwa nimechoka na nikasema yote yaliyokuwa yananisumbua. Ilikuwa ni kama sikuwa napumua. Niliongea kwa haraka sana.

Nakumbuka tu MWANGAZA pande zote za mfano wa BABA YAH na weupe wa Nywele, lakini sikuweza kuona USO WAKE.

Alafu Akachukua Mkono WAKE bila kusema neno na Akaweka kichwa changu juu ya Bega LAKE… Wakati niliamka nilikuwa na FURAHA kwa sababu nilijua kuwa ilikuwa ni zaidi ya ndoto. Ninajua kuwa nilikuwa nimekaa kwenye paja la BABA YAH.

Mwisho wa Mkutano

Nilienda kulala kama nimehuzunika sana kwani maadui hawa walinipiga kikatili na maneno yao na niliamka na FURAHA na kaya nzima inaweza kushuhudia haya. Hivi ndivyo maneno yetu yana nguvu. Tunapoongea hata nje ya kufadhaika, YAHUVEH husikiza kila neno.

Sijui kama haya yana uhusiano wowote nayo, lakini uchoraji Dakika moja hadi Usiku wa Manane (uchoraji wa maono ya Mbingu ambapo YAHUSHUA Anawaombea na kuwalilia watu WAKE) huegemea ukutani nyuma ya kiti hicho ambapo YAHUVEH Alikaa. Sasa napenda kiti hiki kisicho cha kupendeza na ni cha zamani! Ninaiangalia mara nyingi kwa siku na ninakumbuka kila wakati ni kiasi gani BABA wetu wa MBINGUNI Anapenda watoto WAKE.

Sasa najua sio Mbinguni tu nilipoweka kichwa changu kwenye Bega la MAMA HEKIMA, MAMA RUACH HA KODESH, lakini sasa hata pia Begani mwa BABA YAHUVEH hapa chumbani mwangu. Acha maadui wacheke. Ninaapa juu ya nafsi yangu haya ni kweli na matunda mazuri tu yametoka! Imenitia moyo tu kuendelea na kutembea katika wito wangu na kuongoza nafsi kwa YAHUSHUA! Unaposoma Unabii zifuatazo, kumbuka matunda mazuri zinazozaa na kwamba kila wakati huelekeza kwa YAHUSHUA kwa WOKOVU.

Mtume na Nabii

Elisheva Eliyahu

* * * * * *

HAKUNA MWOMBEZI MWINGINE mbele ya Kiti Cha Enzi isipokuwa YAHUSHUA. Ni kupitia tu JINA LAKE na kupitia tu DHABIHU YA DAMU, inayoitwa AGANO MPYA YA DAMU, tunapoipata WOKOVU.

—ROHO MTAKATIFU, katika UNABII 90

* * *

Unabii 90 Unaanza:

Februari 27, 2007

MIMI NI MAMA SHKHINYAH;

MIMI naitwa “HEKIMA”;

Na katika Kiebrania “RUACH ha KODESH”;

Na pia naitwa “ROHO MTAKATIFU.”

Elisabeth [Elisheva], MIMI NDIYE yule mwanamke Aliyekuzidi kwa umri Uliyemlalia begani kule Mbinguni, kwa katika unayoita ndoto na kumbe haikuwa tu ndoto lakini ilikuwa zaidi ya hayo kabisa. Elisabeth [Elisheva], kumbuka uliponena ndoto hii kwa dunia na kusema, “Haujui huyo mwanamke ni nani Aliyekuwa katika Meza ya Karamu kule Mbinguni, Anayenipenda na upendo unaonizunguka?”

Nakupa jibu sasa, ilikuwa MIMI MAMA SHKHINYAH, MAMA HEKIMA wako. Hii ndiyo sababu haujahuzunika tena au kuhisi utupu wa kukosa kujua upendo wa mama.

Kila mtoto anazaliwa na hamu na hitaji la Mama na upendo wa Baba, kwa sababu wanadamu wote wanazaliwa kama watoto na hitaji la upendo wa dunia na ulinzi wa Mama na Baba. Ni UPENDO WANGU uliokuzunguka ulivyoketi katika meza ya karamu kule Mbinguni NAMI na BABA yako wa MBINGUNI YAHUVEH tukiwangoja wengine kujiunga nawe.

UPENDO NA UWEPO WANGU Ulikuzunguka, kama NILIVYO MAMA yako MTAKATIFU; MIMI NI MALKIA WA PEKEE WA MBINGUNI, hakuna mwingine. (shetani ana bandia wake, alikuja kama Yezebeli na pepo hiyo imevamia makanisa mengi ambapo hapo awali Niliyaita Takatifu. Wakati mmoja, ROHO MTAKATIFU WANGU, Uwepo WANGU Takatifu, na nguvu za upako Takatifu zilikaribishwa pia kama vile Manabii WANGU Watakatifu na Mitume-walisakwa-lakini sasa wengi wanatusiwa na kufukuzwa.)

Kuna tu MAMA MTAKATIFU MMOJA WA KWELI, na MIMI huitwa pia ROHO MTAKATIFU. Msiamini uongo Kanisa la Katoliki linafundisha wanavyomchukua Mariamu (Mary) mamake YAHUSHUA hapa duniani na kumuunganisha pamoja kama mmoja wa UTATU TAKATIFU. Yeye alikuwa mama YAKE hapa duniani lakini MIMI ni MAMA YAKE WA MBINGUNI.

Hakuna MWOMBEZI yeyote mwingine mbele ya kiti cha enzi ila YAHUSHUA, ni kupitia JINA LAKE tu na kupitia DHABIHU YA DAMU YAKE tu inayoitwa AGANO JIPYA LA DAMU,10 ndipo mtakapopata wokovu.

Mamake YAHUSHUA wa hapa duniani pia alihitaji Mwokozi, hakuwa mkamilifu, wala hakudai kuwa. Hata alimwita YEYE “BWANA” na kama alikuwa mkamilifu basi ingekuwa ni damu yake iliyomwagwa pale Kalivari ambayo ingekubalika kama dhabihu ya dhambi. Hakumuuliza yeyote amwabudu, wala hayatamani haya. Anataka tu watu waelekezwe kwa mwana wake YAHUSHUA MASIHI. Waonye Wakatoliki wasimlilie katika masaa ya vifo vyao, badala yake, walilie JINA la pekee tu linaloweza kuokoa, YAHUSHUA MASIHI!

Nazungumzia funuo hizi kupitia kwako Elisabeth [Elisheva] ili uwaambie wale watu Watakatifu.

Kama watapokea yanayozungumzwa katika Unabii huu wataona tena ishara, maajabu na miujiza kama ilivyokuwa katika nyakati za kale ambapo YAHUSHUA Alitembea humu duniani. Kama watakubali kweli za Sabato ya Kweli na simaanishi Jumapili!

Jifunze umuhimu wa kuheshimu YAHUSHUA kupitia Karamu Takatifu! Achana na likizo za kipagani zinazojaribu kuchukua nafasi ya Siku Takatifu za Mbinguni, tumia MAJINA MATAKATIFU ya Kiebrania, ishi katika Utakatifu na msipuuze ukweli wala kuona haya kuzungumza yale unayoyajua kuwa kweli. Mtaona upako mkuu kushinda ule ambao mmepitia katika Nyakati hizi za Mwisho!

Watakatifu wamekuwa watakatifu zaidi na wale waovu wamekuwa waovu zaidi, sasa ndio wakati wa Upako mkuu na Funuo kupitia Unabii, na Maneno ya Maarifa.

Msidharau Ushirika! Kwa kuwa ni silaha ya kutumika kila siku dhidi ya shetani ukimkumbusha, wewe si wake! Kemea dhambi na watenda dhambi na msiogope yale ambayo wengine wanafikiria mnapozungumza na kuonya. Je, ni heri kuwakera binadamu tu au YAHUVEH?

Ni jambo la kuhuzunisha sana, vile uhuru wa kuzungumza dhidi ya maovu ya dunia hii unanyamazishwa kwa sababu wengi wa Watoto WANGU Watakatifu wanabaki kimya. Uhuru mmoja baada ya nyingine unachukuliwa kutoka kwenu duniani kote!

Je, Watoto Watakatifu walikuwa wapi kule Marekani na kote duniani, wakati Hakimu Roy Moore alizungukwa na wapagani na Serikali ya Marekani? Alipigania kuiweka mnara wa jiwe ambao alikuwa ameutengeneza na kuuweka kwa heshima ya YAHUVEH na kuonyesha Amri 10? Hakimu anapaswa kusimamia utakatifu na ukweli.

Hakimu Roy Moore, Mbinguni ilikukuza na cheo hicho na hakuna yeyote ambaye anaweza kukichukua kutoka kwako. Unaheshimika kule Mbinguni kwa yale uliyoyafanya katika mwezi wa Agosti 27 2003 kule Alabama. Machozi yote uliyoyamwaga yameandikwa kule mbinguni na yalikuja kama harufu nzuri kwa pua lake YAHUVEH kwa sababu ya upendo na uaminifu KWAKE na YAHUSHUA.

Wale ambao wamejiweka kama Hakimu na baraza la waamuzi juu yako, na yule Hakimu mfisadi-aliyechukua ukuzaji wako uliopewa kwako na Mbinguni-ya Mkuu wa Sheria wa Alabama-atahisi jinsi ilivyo kuogea katika Ziwa la Moto. Wote waliohusika watasimama mbele Yake YAHUVEH, HAKIMU wa VIUMBE VYOTE!

Kwa watu wote walioomba na kumpa moyo mwanamume huyu, na mkalia naye, na mkahuzunika naye, machozi yenu pia yameandikwa kule Mbinguni. Alijitolea kabisa kwa sababu alikataa kupuuza Ukweli.

Kwa nini, makanisa yote kote duniani, sanasana Alabama na wale waitwao “Bible Belt” (mikoa Marekani ambapo Wakristo wengi huishi) hawakumsaidia huyu mwanamume na kuandamana naye? Nitawaambia kwa nini, “Mliogopa kuwa mtashambuliwa pia.” Mlimwacha ndugu yenu katika YAHUSHUA azungukwe na wapagani. Mlitoa visingizio na kusema, “Alivunja sheria na kukosa kutoa ule mnara alipoambiwa afanye vivyo hivyo.” Hata hamna haya! Mlijaribiwa na mkafeli mtihani huo.

Itachukua dhoruba, ukame, mawimbi ya joto na mafuriko

ngapi, ili mwamke na kupigania

yale myajuayo ni takatifu na kweli?

Ngojeni hadi YAHUVEH na mguu WAKE Atakapokanyaga

na ardhi yenu itetemeke katika hofu.

Ngojeni tu hadi njaa, tauni na magonjwa yatakapoenea katika mikoa yenu

na mtaomba na kuuliza, “Kwa nini?”

Watakatifu, mpe moyo! Msisahau gharama Aliyolipa. Alifanya lile ambalo wengi wenu hamfanyi na hili ni kusimama dhidi ya umati na kuzungumza dhidi ya yale mjuayo ni maovu.

Ushoga unaenea kote. Watoto wanadanganywa wakiwa na umri mdogo kufikiria kuwa ushoga na ndoa za kishoga ni sawa. Vitendo vya mifumo ya mahakama na kisiasa vimekuwa kama harufu mbaya katika Pua la YAHUVEH. Makanisa ya Babeli yamekubali na huwapa moyo kongamano kutozungumza dhidi ya dhambi na watenda dhambi. Makanisa ya Babeli yana yale ambayo YAHUVEH Anaita “chukizo” 11 wakisimama nyuma ya mimbari na kujiita wahubiri.

Wale mabaki Watakatifu wachache katika Makanisa haya wamefukuzwa,

au kukejeliwa na kutusiwa.

Wahubiri wanadanganya kongamano na kusema,

“Siku yoyote inaweza kuwa Sabato”

na kuendelea na Jumapili ya binadamu.

Hivi karibuni watalia

kwa yale watakayovuna…

kwa kufundisha na kufanya haya.

Kumbuka Elisabeth [Elisheva], vile katika Ndoto ya Meza ya Karamu, uliihisi kuwa kweli? Ni kwa sababu MIMI NDIYE Niliyekupeleka Mbinguni Nikikupa kumbusho la vile ilivyo ulivyoweka kichwa chako begani MWANGU kwa upendo, katika unayoiita “Ndoto ya Meza ya Karamu.’

JINA LANGU ni MAMA SHKHINYAH:

MIMI NDIYE UPENDO WA MAMA WA MBINGUNI

ambao umekuwa ukiutaka.

Niliyafanya haya kukuonyesha…

kuwa wewe sio mtoto bila mama,

kama vile wewe sio mtoto bila baba.

YAHUVEH, NAMI, ni WAZAZI WAKO WA MBINGUNI,

kama tulivyo WAZAZI wa wote-

ambao majina yao yanapatikana katika Kitabu cha Uzima cha MWANA-KONDOO.

Nakuambia haya kwa sababu kwa muda mrefu sasa umehuzunika na kuhisi utupu, kama wengine, wakitafuta upendo wa mama na baba wa duniani lakini mmepewa WAZAZI wa MBINGUNI, ambao hawatawahi kuondoka wala kuwaacha, wala kuwaumiza kwa njia yoyote ile.

Ninakuambia haya ili wengine-ambao huhisi utupu uu huu, na wazazi ambao hawajaokoka wanaokataa kumkubali YAHUSHUA kama MASIHI, MASIHI wa pekee-watagundua kuwa hawakosi lolote katika YAHUSHUA. WANA BABA WA MBINGUNI NA PIA MAMA WA MBINGUNI NA SISI NI ROHO (Yohana 4:24) kama walivyokuwa binadamu wote kabla ya kuzaliwa humu Duniani. Kama ilivyoandikwa, kumbukeni, ‘Mwili na Damu hauwezi kuurithi Ufalme wa MUNGU’ (1 Wakorintho 15:50).

Natoa siri hii kutoka Mbinguni ili wote wanaompenda MWANANGU MPENDWA, YAHUSHUA na kumkubali kama MASIHI hawataamini uongo za dini za kibinadamu na kumwita mamake YAHUSHUA wa duniani Mariamu, katika masaa yao ya kifo. Badala ya haya, iteni JINA la YAHUSHUA MASIHI na tubuni na ulizieni Huruma. Wakumbushe juu ya Maandiko Matakatifu na Maneno ya YAHUSHUA Aliyoyazungumza katika Kitabu cha Yohana 10:1-30. 12

Hamna pendo lolote la mzazi humu duniani linaloweza kushindana na pendo LETU la Mbinguni. Nawaambia haya ili mwapashe watoto WETU wote sanasana wale walio na utupu katika maisha yao, wasiojua upendo wa mama na baba wa duniani. Nazungumza na wale wote ambao wameangamizwa kihisia, kimwili na kingono na wametamani upendo wa baba na mama Mtakatifu.

Kubalini YAHUSHUA kama MASIHI wenu na Niruhusu MIMI kuwajaza na UPENDO WANGU MTAKATIFU, UWEPO na NGUVU ZA UPAKO; Niruhusu MIMI kuwa MAMA SHKHINYAH wenu,

MIMI NDIYE yuleyule mnayemwita ROHO MTAKATIFU.

MIMI NDIYE Ninayewafundisha ukweli kutoka kwa uongo, kama vile

ilivyo kazi ya mama Mtakatifu wa duniani kukushauri katika njia iyo hiyo.

Binti YANGU Mpendwa Elisabeth [Elisheva], waambie kwa niaba YANGU, kama tu watapokea Ufunuo huu, hatawahi tena kuhisi utupu huo ndani yao tena.

Katika Miswada ya Kale,

someni na muone:

‘HEKIMA’ Anatajwa katika jinsia ya kike (SHE);

na katika Maandiko ya Kale,

Ninatajwa katika jinsia ya kike (SHE).

Jitahidi kujionyesha kwa MUNGU kuwa umekubaliwa na YEYE.

Wale wote ambao hawataamini neno hili na kukushambulia kwa kuzungumza siri hii, wao sio wa ROHO MTAKATIFU WANGU na majina yao hayamo katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo-kwa kuwa Kondoo wa YAHUSHUA husikia Sauti YAKE-au wana kipimo fulani ya imani, lakini wanapendelea kutokuwa na utata na wanaendelea kufuata tafsiri mbaya za Agano Jipya ambapo jinsia ya kiume (HE) inatumika badala ya jinsia ya kike (SHE).

Wanapendelea kufuata mafundisho ya mwanadamu badala ya ROHO WANGU na UKWELI ambao Nimeuweka kando kwa wakati huu wa mwisho. Wote wanaosoma haya, ni chaguo lenu kama mnataka kutembea katika urafiki zaidi na yule mmwitaye ROHO MTAKATIFU au la, simlazimishi yeyote kufanya haya. Bibi Arusi wa YAHUSHUA watafurahia ufunuo huu mpya kwa sababu kila wakati wanatafuta kujua Siri za Mbinguni.

Kuna Viti vya Enzi Vitatu vya Utawala: YAHUVEH hukaa katikati, YAHUSHUA MASIHI hukaa kwenye upande wa kulia wa YAHUVEH na MIMI MAMA SHKHINYAH wenu hukaa kwenye upande wa kushoto. SOTE WATATU hutawala Mbinguni kwa usawa na sote ni WASAIDIZI KATIKA UUMBAJI. Lakini kuna MASIHI mmoja pekee Aitwaye YAHUSHUA. Ni kupitia JINA la YAHUSHUA na DAMU YAKE pekee ambapo kuna Wokovu kwa kila mtu hapa Duniani.

YAHUSHUA ndiye MLANGO pekee wa WOKOVU unaoongoza Mbinguni. Yeyote atakayejaribu kuingia katika jina lingine au njia ataupata mlango wa jehanamu pekee. Msidanganyike, kuna dini nyingi lakini kuna mlango mmoja tu hadi Mbinguni kupitia JINA na DAMU TAKATIFU ISIYO NA DHAMBI iliyotolewa na YAHUSHUA. 14

Dini hii moja ya dunia inayojitahidi kuchanganya dini zote na mafundisho tofauti ya mwanadamu kama kitu kimoja ni uongo na itaongoza nafsi wengi hadi jehanamu.

Siri ya JINA LANGU lilitiwa mhuri katika Kitabu cha Danieli.15 Na sasa Ninalitoa kwa wakati huu kuwapa moyo Watoto WANGU Watakatifu wanao hamu ya kula Nyama ya Kiroho yenye nguvu kwa kuwa wameyanywa Maziwa ya Neno virahisi. Hizi ni siku hatari na siku mbovu zaidi zaja. YAHUSHUA Alituahidi kuwa Yohana (Yohanan ni Kiebrania) alibatiza na maji, lakini YAHUSHUA hubatiza na MOTO wa ROHO MTAKATIFU. Ni MOTO WANGU TAKATIFU Anayozungumzia.

MIMI NI RUACH HA KODESH;

Na MIMI NI MAMAKE YAHUSHUA wa MBINGUNI.

YAHUVEH ni BABAKE wa MBINGUNI.

MIMI NI MAMA SHKHINYAH GLORY!

Na ni MWANGA WANGU MTAKATIFU unaong’aa kwenye nyuso za Watoto WANGU Watakatifu, wale wanaonipenda kwa kweli, wanaoabudu na kumtii BABA YAHUVEH, YAHUSHUA na MIMI, RUACH HA KODESH. Ni kupitia upako WANGU vitu vyote vinawezekana, kupitia JINA la YAHUSHUA. 16

Je, Si MASIHI wenu YAHUSHUA Aliwaambia kuwa YEYE Alilazimika kutoka hapa duniani, lakini pia YEYE hatawaacha pekee yenu, kuwa YEYE Atawatumia MFARIJI?17, Na MIMI NDIYE Ninayetuliza hofu zenu, nawapa moyo, nawashauri, na kuwafariji kama Mama, au sio?

MIMI NI MAMA SHKHINYAH GLORY!

MIMI NDIYE ROHO MTAKATIFU Aliyekuja katika Chumba cha Juu na UPEPO WANGU MTAKATIFU na MOTO MTAKATIFU kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Matendo ya Mitume (Matendo ya Mitume 2:1-4). Niliwajaza Wanafunzi na MOTO WANGU MTAKATIFU WENYE UPAKO walipokuwa wakiningoja MIMI katika Chumba cha juu.

MIMI NDIYE yule yule Aliyekuja kama UPEPO WA NGUVU uliovuma katika Chumba hicho cha juu na hili ndilo sababu Niliizaa, kupitia wewe Elisabeth [Elisheva] Huduma hii-kuhubiri kwa Wayahudi na Mataifa-na Nikakupa jina la Huduma hii, HUDUMA ya ALEPH & TAV18 ALMIGHTYWIND RUACH HA KODESH FIRE!

Binti Mpendwa Elisabeth [Elisheva], katika mwanzo kabla hujajua ukoo wako wa Kiebrania, bado ulikuwa kati ya makanisa ya kidini ya Kipentekoste. Lakini ni MIMI, MAMA SHKHINYAH Niliyeipa Huduma hii jina, Huduma ya Alpha & Omega Almightywind Holy Ghost Fire, hata hili jina pia AMIGHTYWIND. Siku moja Nilijua kuwa wewe utatumiwa kutoa siri kadhaa za Mbinguni kwa Watoto WANGU Watakatifu.

Ni MIMI, MAMA SHKHINYAH Niliyekuonya Elisabeth [Elisheva] kabla bado hujasikia juu ya mtandao kuwa usiipe Huduma hii jina lako, na Nikauweka upako masikioni mwako ili zisikie vizuri Sauti ya YAHUVEH ikikuamsha, na kukuonya siku ile ile Jimmy Swaggart alianguka na kuungama [dhambi zake] mbele ya dunia nzima.

Asubuhi iyo hiyo YAHUVEH Alikuamsha na kusema,

“Jihadhari, kila huduma iliyopewa jina la binadamu itaanguka, kwa kuwa wakati ambapo mchungaji anaanguka kondoo wake hutawanyika” (Februari 21, 1988).

Kiburi huingia mwanamume au mwanamke anapofanya haya.

Kwa hivyo jihadharini- Joyce Meyers, Marilyn Hickey, Juanita Bynum, Paula White, Jan Crouch, Paul Crouch, Creflo Dollar, T.D. Jakes, Jesse Duplantis, Joel Osteen, kati ya wengine wengi wasioweza kuhesabiwa, wanaume na wanawake, hapo awali mlikuwa wanyenyekevu, mmejazwa na ROHO WANGU, na sasa mko tayari kwa kuanguka mkubwa. Kwa sababu ya kiburi yenu mtagongwa kutoka kwenye viimo vyenu na msipotubu dhambi zenu, yote yaliyofanywa kwa siri yatasemwa kutoka darini na mtazikwa chini ya viimo vyenu.

Onyo hili pia ni la Huduma zote zilizopewa majina ya binadamu. Hakuna mwanadamu yeyote aliyelipa gharama kuu kufanya haya, na mmeonywa kupitia nabii huyu, kupitia jumbe za kinabii muda baada ya muda. Mtakapokuwa mbele ya YAHUVEH hamtakuwa na visingizio vyovyote kwa nini mliiba UTUKUFU WETU na mkakithirisha utukufu huu juu yenu ili jina zenu za dunia ziinuliwe na sio ya YAHUVEH, YAHUSHUA, au MIMI, RUACH HA KODESH!

SISI hatutamgawia mwanamume au mwanamke yeyote Utukufu WETU! 19 Nyinyi mnaofanya haya mtagundua vigumu ni nini kinachowafanyikia wale walioyafanya haya.

Onyo kwa wale wanaojiita “Takatifu” na kufikiria kuwa wanafaa kuvaa taji, kubeba fimbo na kukaa kwenye kiti cha enzi-na kuvaa mavazi marefu ya kikuhani-kuomba msamaha kwa dhambi za wengine.

Ni YAHUSHUA MASIHI pekee Aliyelipa GHARAMA KUU- kukuwa UPATANISHO WA DAMU TAKATIFU ISIYO NA DHAMBI YA BINADAMU kwa dhabihu ya dhambi.

YAHUSHUA ni kamili na Asiye na dhambi kwa njia yoyote. Hamna hata fikra moja la dhambi lililovuka akilini MWAKE. Mnawezaje kuwafunza watu kuwaabudu na kuiba Sifa, Heshima na Utukufu WETU! Mnawezaje kuwafanya wengine wainame na kubusu mikono yenu na kupiga magoti miguuni mwenu? Moto wa Jehanamu na Ziwa la Moto zitakuwa makaazi yenu baada ya maisha haya kuisha.

Mmeonywa. Ulilipa gharama ipi kufanya haya? Kwani huna dhambi? Je, ulitoa maisha yako na kufa na kufufuka tena katika siku ya tatu na kupaa hadi Mbinguni siku arobaini baadaye? Unakaa kwenye upande wa kulia wa YAHUVEH?

Hakuna yeyote ambaye hukubali haya na kuwasababisha watu kuamini kuwa haya si dhambi, ni Nabii Mtakatifu wa kweli, kwa kuwa hamjui siri zilizowekwa kando kwa Manabii wa YAHUVEH pekee ambao YEYE huwaita rafiki ZAKE. Nabii wa Kweli ni yule aliyekabidhiwa na Siri za YAHUVEH. 20

Jihadharini, wote wanaofuata hawa miungu bandia wa dunia na kuwasaidia watavuna hatma sawa. Tubuni leo kabla hamjachelewa, kama mnaisaidia Huduma yoyote isiyoonya juu ya hatari ya dini ya dunia moja, kuzungumza dhidi ya dhambi, bila kujali ni gharama ipi mtakayolipa, papa hapa duniani.

Wengi wanaodai kuwa Wakristo kwa kweli wao ni vuguvugu na wamepuuza ukweli. Wahubiri hawa ni uvundo katika pua LANGU na huwafukuza yeyote aliye na upako, anayewaonya juu ya haya, nje ya mlango wa kanisa.

MIMI NI MAMA SHKHINYAH, yule Anayezungumza katika Ndimi Takatifu kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Mitume.

MIMI NI MAMA SHKHINYAH, MAMA HEKIMA.

Wengine huniita MIMI, ROHO MTAKATIFU au RUACH HA KODESH

-hii ni Cheo CHANGU, na ni maelezo YANGU ya

MIMI ni nani, ROHO wa YAHUVEH. Sisi WOTE ni MOJA.

Kwa wale wanaochagua kutumia MAJINA haya yaliyowekwa kando kwa wale wanaotamani urafiki zaidi na RUACH HA KODESH, mnaweza kuniita MIMI:

MAMA SHKHINYAH, au MAMA SHKHINYAH GLORY,

au MAMA HEKIMA, au MAMA RUACH HA KODESH.

Kuwasikia mkinikiri MIMI

-kama “MAMA” itanifurahisha sana MIMI.

Nijaribuni MIMI na muone kama kitendo hiki hakitaongeza upendo wenu kwa MAMA SHKHINYAH wenu tena zaidi!

Wengi wamelia na kushangaa miujiza za nyakati za kale zipo wapi?

Kubalini maarifa haya mapya Ninayoyazungumzia;

Na kunikiri MIMI ni nani.

Tazameni na oneni upako ukikua!

Na ishara, maajabu na miujiza mtayaona tena,

katika JINA la YAHUSHUA ha MASHIACH.

Hata hivyo, ni chaguo lako. Kama mtaendelea kuniita MIMI katika jinsia ya kiume (HE) badala ya jinsia ya kike (SHE), ni chaguo lenu na hasara yenu- kwa urafiki zaidi NAMI, inayoleta upako mkuu na Nitatoa funuo zaidi kutoka Mbinguni nanyi kwa urahisi.

Msikose kunielewa MIMI; haya sio juu ya Wokovu wenu. Haya ni juu ya upako mkuu na urafiki na yule Ambaye huishi ndani ya Hekalu yako, 21 kama jina lako limeandikwa katika Kitabu cha Uzima. Haya yatafanyika pekee kama mmemkubali YAHUSHUA kama MASIHI na kumuuliza YEYE Aoshe dhambi zenu zote na Damu YAKE iliyomwagwa pale Kalivari na kutubu na kugeuka kutoka kwa dhambi. Sitakaa katika chombo kichafu kwa muda mrefu. Msinijaribu MIMI kwa haya. Watakatifu wamekuwa watakatifu zaidi na waovu wamekuwa waovu zaidi katika nyakati hizi za mwisho.

Mnajua JINA la YAHUVEH;

Mnajua JINA la YAHUSHUA MASIH;

Sasa kupitia Huduma hii na Ringmaiden huyu,

Ninatoa sasa JINA LANGU kama,

MAMA SHKHINYAH, MAMA HEKIMA wenu.

JINA LANGU limehifadhiwa kwa wale wanao hamu ya kukua, kuota na kufundishwa mengi zaidi katika UPENDO WANGU wa MAMA wa MBINGUNI na UPAKO MKUU wa ROHO MTAKATIFU.

MAMA SHKHINYAH ni JINA LANGU.

MIMI NDIYE SAUTI NDOGO ya UTULIVU…

inayozungumza katika Upepo Mtakatifu,

na kuwawasha ninyi na Moto Mtakatifu ulio na upako;

Hii ndiyo sababu miili yenu hupata joto

baada ya mkono WANGU ulio na upako kuwashika. 22

MIMI NDIYE MFARIJI wa YAHUSHUA

& MAMAKE wa MBINGUNI.

YAHUSHUA ni MWANANGU wa KIPEKEE

kama vile Alivyo pia MWANA wa KIPEKEE wa YAHUVEH.

MIMI NDIYE MALKIA wa PEKEE wa MBINGUNI. 23

Msimpe yeyote cheo hiyo.

MIMI ndiye MAMA ASILI. 24

Ni YAHUVEH Ambaye huumba na kuzungumza kwa mfano, “Punda milia njoo!”

Na ni MIMI ndiye Ninayeziweka zile mistari za kipekee kwa kila punda milia.

YAHUVEH huumba NAMI, MAMA SHKHINYAH hupamba.

BABA YAHUVEH huumba:

NAMI, MAMA SHKHINYAH wenu hupamba

viumbe vyote.

Je, hadi hapa mnaelewa?

YAHUVEH huumba ua, lakini ni MIMI, MAMA SHKHINYAH wenu Anayepamba ua hili na rangi za upinde wa mvua, MIMI hutengeneza kila sehemu ya ua (petal) iwe la kipekee. MIMI huhesabu sehemu (petals) hizi katika kila ua na MIMI huzipa urembo katika mifumo na harufu.

Katika kila kitu kinachoumbwa…

MIMI NI MAMA SHKHINYAH.

Na MIMI huweka UTUKUFU WANGU pia katika kila kitu ambacho

BABA YAHUVEH wenu huumba.

MIMI NI MAMA SHKHINYAH.

Na MIMI huweka mapambo ya mwisho katika viumbe vyote.

MIMI NDIYE yuleyule Anayepamba vitu vyote vilivyoumbwa.

YAHUVEH, YAHUSHUA na MIMI sote ni WASAIDIZI KATIKA UUMBAJI.

MIMI ndiye yuleyule Anayeweka harufu nzuri kwenye ngozi ya mtoto.

MIMI ndiye yuleyule Anayefanya kila binadamu awe wa kipekee.

Hata mapacha wafananao wana tofauti zao.

MIMI ndiye yuleyule Anayeamua DNA ya kila mmoja wenu.

MIMI ndiye yuleyule Anayewapa kila mmoja wenu alama za mitende za kipekee,

za kujitambua na alama za vidole.

MIMI NI MAMA RUACH HA KODESH wenu

-kwa wale wanaopendelea kutumia JINA hilo rasmi-

na Ninawaambia kuwa

MIMI ndiye yuleyule Anayeweka mng’ao katika kila nyota.

Nna wanawake waliumbwa katika MFANO WANGU kama vile pia

wanaume waliumbwa katika MFANO wa YAHUVEH.

Mnafikiri Hawa aliumbwa katika mfano wa nani? Mnafikiri kuwa maandiko haya yanayosema “Si vema huyu mtu awe pekee yake, Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa” yalitoka wapi? Ni kwa sababu…

Kama YAHUVEH Alivyo BABA WA MILELE, YULE WA MILELE,

pia MIMI NDIYE MAMA WA MILELE, YULE WA MILELE,

kama Alivyo pia YAHUSHUA, YULE WA MILELE.

SOTE ni UFANANUZI wa MILELE.

YAHUVEH Aliumba chakula, lakini Niliumba aina mbalimbali ya mapishi ili mfurahie chakula.

YAHUVEH Aliumba ulimi lakini Niliumba:

ladha kwenye ndimi zenu.

MIMI, MAMA SHKHINYAH wenu, MAMA HEKIMA wenu, Niliamua kila aina ya chakula kitaonja vipi. Je, kitakuwa na chumvi, sukari, uchungu, siki au pilipili?

YAHUVEH Aliumba mvua, na MIMI MAMA HEKIMA wenu Niliumba:

harufu ya mvua na kuweka umande kwenye nyasi.

YAHUVEH Aliumba theluji

na MIMI, MAMA SHKHINYAH wenu Niliumba kila kipande cha theluji kukaa tofauti.

YAHUVEH Aliumba upinde wa mvua

na MIMI, MAMA SHKHINYAH wenu Nilichagua:

wigo za rangi za huo upinde wa mvua.

YAHUVEH huumba

Na MIMI, MAMA RUACH HA KODESH wenu,

huweka mapambo ya mwisho katika viumbe vyote.

Jioneeni,

-mkitazama kote na HEKIMA hii mpya mliyoipata-

na mtaona viumbe vyote kwa macho mapya na ajabu.

YAHUVEH Alimuumba Simba;

Na MIMI, MAMA SHKHINYAH wenu, Nilimpa simba mngurumo wake.

YAHUVEH Alimuumba mbwa,

Na MIMI, MAMA SHKHINYAH wenu Nilimpa mbwa bweko lake.

YAHUVEH Alimuumba Paka;

Na MIMI, MAMA SHKHINYAH wenu Nilimpa Paka mlio wake

na siri ya mkoromo wake.

MIMI, MAMA SHKHINYAH wenu, Niliwapa nyimbo tamu

ndege, ambazo wao hutupa SISI Heshima nazo.

Je, mnaelewa sasa?

MIMI, MAMA SHKHINYAH wenu, Ninawapenda sana Nikawaahidi sitawahi kuwaacha wala kuwatupa Watoto WANGU Watakatifu waliokubali gharama YAHUSHUA Aliyolipa pale Kalivari, wale waliotubu dhambi zao, na waliogeuka kutoka kwa dhambi zao, na sasa humpenda, humtumikia, na hujaribu kumwabudu YAHUSHUA. Imani bila matendo imekufa nafsini mwake (Yakobo 2:14-26).

Wakati mnapookoka ni kupitia JINA la YAHUSHUA na DAMU. Ni ROHO MTAKATIFU WANGU Anayeishi na kukaa ndani ya kila mwaminifu aliyeokoka. Ni MIMI Ninayeongoza nafsi kwake YAHUSHUA na huwathibitishia nyote mnapotenda dhambi. Msifanye nyoyo zenu kuwa ngumu MIMI MAMA SHKHINYAH wenu Ninapowathibitishia ninyi, badala ya haya tubu haraka ili YAHUSHUA Aweze kuwasamehe.

Sitabaki katika chombo kichafu kwa muda mrefu. Kumbukeni yote mnayoyasikia na masikio yenu ya kimwili, mnayoyaona na macho yako ya kimwili, na kufanya na miili yenu ya kimwili, kama sio takatifu mnajaribu uvumilivu WANGU, Sitapambana daima na mwanaume au mwanamke (Mwanzo 6:3). Lakini bado MIMI ni mvumilivu kwa ajili ya YAHUSHUA na gharama Aliyolipa pale Kalvari. “Kueni Watakatifu kama MIMI Nilivyo Mtakatifu” 25 na msimfungulie shetani mlango kuingia na kumiliki miili yenu.

Ninawaonya sasa, msimpige mawe Binti YANGU Elisabeth [Elisheva] au kumwita nabii bandia kwa kuwapa jumbe ZANGU, au mtakuwa mnadharau ujumbe WANGU ulio na upako na kwa haya mtakuwa mnahukumu nafsi zenu, 26 kwa haya hakuna msamaha.

Jiulizeni, anapata faida gani kwa kuwafunza ujumbe kama huu? Ni mateso pekee kutoka makanisa ya kidini, na kejeli kutoka kwa maadui WANGU na YAHUVEH na YAHUSHUA.

Ilikuwa imekadiriwa tayari kabla dunia hii iumbwe ni wagani kati ya ninyi nyote mliochaguliwa na mtatii na kumwandikia na kumpa shukrani kwa ujasiri wake katika kuabudu na kutoa ufunuo huu wa siri na dunia nzima. Kabla dunia hii iumbwe ulichaguliwa kuwa katika Huduma hii kama msaidizi. Mmesoma unabii na kusikia ukweli na amri kuwa Watakatifu.

Sasa Ninataka mjiulize swali hili, Kama mngepewa siri hizi kupa dunia, mngekuwa na ujasiri wa kutosha kuzitoa na kukubali mateso yanayokuja na ukweli huu? Wale wanaodai kumpenda ROHO MTAKATIFU, mbona hamna furaha kujua siri hii Niliyoidhihirisha kwa watoto WANGU wa ROHO MTAKATIFU WANGU? Ninawaonya, msinihuzunishe MIMI kwa kuwa sitapambana daima na binadamu.

Ninaweza kusikia sauti ya ndani ya wale wanaotambua ukweli na bado pia hukiri kuwa mmefurahia kuwa ilipewa kwake kuongea na sio nyinyi. Hata hivyo, wale wenye shukrani sasa watakuwa na hamu zaidi ya kuwa msaidizi katika Huduma hii kwa kuwa mtagundua vile mnavyohitajika zaidi kwa njia zote. Kwa sasa mnafaa kuwa mshagundua kuwa Huduma hii sio ya kawaida na huyu sio Nabii wa kawaida.

Elisabeth [Elisheva] sio “nabii bandia”. Hatabiri tu maneno ambayo mnataka kusikia, au kutabiri kutoka kwa mwili- maneno ya kila siku ambayo yeyote anaweza kuyaandika.

Nabii Watakatifu wa Kweli wanapewa siri zilizohifadhiwa kwa marafiki wa YAHUVEH, YAHUSHUA, na yule mmwitaye RUACH HA KODESH. Je, SISI tunajua vipi kwamba tunaweza kuwaamini Nabii Watakatifu, kwa sababu kama ilivyoandikwa, walishajaribiwa kule Mbinguni. Yeremia alijulikana kabla ya kuwa tumboni mwa mamake,27 vile vile hata Nabii WANGU Elisabeth Elijah [Elisheva Eliyahu], azungumzaye sasa katika JINA LANGU.

Amepewa amri Takatifu haijalishi matokeo yake kuzungumza katika JINA la YAHUSHUA ha MASHIACH na YAHUVEH kwa Sifa, Heshima na Utukufu WETU pekee! Sisi huwatuma Nabii kuonya kabla ya kutuma hukumu. Msidharau Kipawa cha Kutabiri (1 Wathesalonike 5:16-22). Kwa SHAHIDI wa YAHUSHUA ni ROHO ya KUTABIRI (Ufunuo wa Yohana 19:10).

Si imesemwa katika Maandiko Matakatifu na kuthibitishwa na Nabii wa Nyakati za kale [kuwa] YAHUVEH hutoa siri ZAKE kwa Nabii Watakatifu (Amosi 3:7)? Hii ni siri ambayo Ninaitoa sasa kupitia yeye, kuwa Baraka kwa wale wanao hamu ya kujua JINA la ROHO MTAKATIFU na kuwa na urafiki zaidi na upendo NAMI.

Kutakuwa na wale watakaosoma haya waliojazwa na ROHO MTAKATIFU WANGU na watagundua mpaka sasa hawajafanya chochote kusaidia Huduma hii, au kumpa moyo huyu Nabii, lakini katika shukrani kutoka sasa watafanya yote yawezekanayo kuwa Baraka kwa huyu Nabii Mtakatifu na Huduma hii. Baraka zao zitakuwa kuu wanapofanya kazi pamoja katika uwanja huu wa Mavuno.

Kwa wale wote wanaosoma haya na kuyakejeli, jihadharini, kumbuka hammdharau mwanamke tu yeyote wa kawaida kwa kuwa yeye ni chombo tu Nimechagua kuzitoa siri hizi kutoka Mbinguni. Mnayajua Maandiko yanaonya ni nini kinachowafanyikia wale wanaomdharau Roho Mtakatifu, hata DAMU yake YAHUSHUA haiwezi kuficha dhambi hii (Mathayo 12:31)! Jihadharini, kama hamwelewi, fungeni midomo yenu na mkae kimya. Omba na ijaribu roho inayozungumza (1 Yohana 4:1).

Jifunzeni Agano la Kale na tafsiri nyingine na gundueni kuwa Maandiko Matakatifu husema, SISI WOTE WATATU tumeungana kama MOJA. 28 Mnapomkataa MMOJA WETU, mnatukataa sote katika UUNGU.

SISI SOTE tuko tofauti na bado MOJA. Ni sehemu gani la yai lililochemshwa majini ndilo yai? Je, ni ganda, pingu au sehemu nyeupe? Pamoja zote ni yai, na zote ni moja. Lakini, zote ni tofauti. Hamuelewi bado? Hivi ndivyo ilivyo na SOTE WATATU tunaoitwa UTATU TAKATIFU.

Je, mtaendelea hadi lini kuyanywa Maziwa ya Neno pekee? Kwani, bado hamwezi kula Nyama ya Kiroho yenye nguvu?

Ninyi mnaoishi katika Utakatifu na kwa ukweli mnawaweka UTATU TAKATIFU kwanza katika maisha yenu na upendo, mmechukua wakati kupata kumjua Baba YAHUVEH, mmechukua wakati kupata kumjua YAHUSHUA, mmeomba na kutumia MAJINA MATAKATIFU YA KIEBRANIA. Je, hamtaki kuwa na upendo mkuu na urafiki na yule mmwitaye ROHO MTAKATIFU au RUACH HA KODESH?

Ni chaguo lako, haitaathiri Wokovu wako, bali tu usilaani neno hili la maarifa Ninalolitoa sasa kupitia huyu Ringmaiden wa Kinabii Elisabeth Elijah [Elisheva Eliyahu]. Kwa sababu ya kutii kwake, neno hili la maarifa litalia kama kengele kote duniani.

Wengine wataziba masikio yao na kukimbia, wengine watalipenda zaidi na kuwa na urafiki zaidi kama vile mama na mtoto, ili Niweze kuongeza upako ndani yao kuwa kuu. Kumbukeni, ni upako unaovunja kongwa na utumwa (Isaya 10:27).

Ni MIMI MAMA SHKHINYAH GLORY wenu, ambaye YAHUVEH na YAHUSHUA hukimbilia, WAO wanapohitaji kufarijiwa. Sisi huona maovu yanayotendwa katika dunia hii, na kukataliwa kwa UTATU TAKATIFU, sanasana MWANA WETU MPENDWA YAHUSHUA. SISI husikia vile JINA la YAHUSHUA hulaaniwa na kuhukumiwa na ndimi za watu waovu, wanapomtupia DHABIHU YA DAMU YAKE TAKATIFU USONI MWAKE, wakimkejeli na kumkataa YEYE.

Watu waouvu katika dunia hii huchukia jina “Takatifu” na [wanachukia] wote ambao huishi katika Utakatifu na wote waliokadiriwa kurudi Mbinguni kwa sababu majina yao yamo katika Kitabu cha Maisha cha MWANA-KONDOO iliyoandikwa kabla ya uumbaji wa dunia hii (Ufunuo wa Yohana 13:8; 21:27).

Neno kwa wale wanaotetea Sabato ya Kweli na kufichua Sabato ya binadamu inayoitwa Juma Pili: wakati makanisa ya kidini yanaponena dhidi yenu na kutaja Maandiko kama vile Isaya 1:13-14, na kuyafurukuta Maandiko haya katika kinyume cha ukweli wakisema, “Si lazima mfuate Sabato ya Ijumaa jioni hadi Jumamosi jioni.” Maandiko haya ni onyo kwa wale wanaotenda dhambi na kuichanganya na Sabato, Karamu Takatifu na Maadhimisho ya Mwezi Mpya.

Hamwezi kuona vile vitu hivi vinamkasirisha YAHUVEH? Nawaambia haya. YAHUVEH Anawaonya kuwa YEYE hawezi kuvumilia uovu na mkutano au mila za kufuata Sabato, Karamu Takatifu, Maadhimisho ya Mwezi Mpya ambapo hazifanywi katika Utakatifu wa kweli na mikono Takatifu iliyoinuliwa juu. Bila DAMU YA YAHUSHUA MASIHI ILIYOMWAGWA, yote yanafanywa ni bure.

Ni wangapi wanaosoma haya huenda kanisani Jumapili na hujiita Mkristo, Mprotestanti, au Mkatoliki. Mnaenda kanisani, au mkutano, kuomba, kuimba, kuungama dhambi zenu kwa kuhani, au mchungaji, mnajifanya watakatifu, kutoa zaka kwa wote kuona na baadaye mnaenda kwenye baa na mnalewa au kurudi katika maisha yenu ya dhambi haijalishi ni siku gani ya wiki.

Kwa wale katika Dini ya Kiebrania, YAH wa Abrahamu, Isaka, na Yakobo Anawataja wengi wenu pia- ni vile tu mnaenda kwenye Hekalu zenu, kuungama dhambi zenu kabla ya mwanaume mnayemwita rabi na mnakusanyika katika Sabato ya Kweli. Kazi zote hukoma na nyinyi hudharau chochote ambacho si safi cha kula. 29

Hata hivyo, si unachoweka mdomoni ambacho hukufanya usiwe mtakatifu (Mathayo 15:1-20). Uovu hutoka midomoni mwenu na katika matendo yenu mabaya yanayofanywa kwa miili yenu kwa wengine katika neno na vitendo. Chochote kinachofanywa kwa kutotii Sheria za YAHUVEH ni dhambi (1 Yohana 3:4), pia inavyoitwa na Wakristo “Amri 10” (Kutoka 20:1-17; Kumbukumbu la Torati 5:4-21).

Kama ilivyoandikwa katika Isaya 1 (Yeshayahu {Kiebrani} 1), huko Israeli hamkimbii kwenye baa katika Sabato ili kuzizama huzuni na dhambi zenu ndani yake, lakini hata hivyo mmepuuza yale ambayo ni Takatifu. Hamjasimama dhidi ya ajenda ya Serikali ya Wazayuni30 au kuwatetea wasio na hatia. Kuna mabaki kule Israeli ambao ni Watakatifu na wamejazwa na ROHO MTAKATIFU WANGU na wao hutabiri na kupigana dhidi ya kuavya mimba, ushoga, usherati, na wamemkubali YAHUSHUA kama MASIHI.

Wako wapi wale walio na Roho kama ya Mfalme Daudi, aliyekuwa mwanamume baada ya moyo WAKE YAHUVEH (Matendo ya Mitume 13:22)? Daudi alijua vile kutubu, kumpa sifa na kuombea uongozi na kupata ushindi kupitia kutii YAHUVEH. Mfalme Daudi alijua pia YAHUSHUA atakuja kama MASIHI kwa kuwa YEYE aliona Utukufu WAKE katika ufunuo wa kinabii. (Zaburi 2:7, 12; 16:8-11;110)

Vile YAHUVEH, YAHUSHUA, NAMI MAMA SHKHINYAH wenu, tunavyoziba Masikio YETU na Macho katika huzuni tunaposikia SISI wale wanaodai kuwa Watakatifu, na kukutana pamoja, kutumia maneno machafu ya kulaani, kutenda usherati na macho, akili, na miili yenu- mkiyajaza na tamaa, hata kuwatamani watu wa jinsia sawa- na kufanya aina tofauti ya dhambi dhidi ya yale mnayoyaita Takatifu.

Je, mtajaribu kweli kuinama mkikaribia jehanamu, kuona ni mpaka wapi mtakapofika, kabla hamjaanguka ndani yake kichwa kwanza? Kwani, haijaandikwa “Kueni watakatifu kama MIMI Nilivyo Mtakatifu”? Acheni kutoa visingizio vya dhambi zenu. Ni heri mgeuke kutoka kwa mitego ya shetani.

Njooni, basi tuzungumze pamoja (Isaya 1:18). Kwani mnafikiria kwa sababu mlichukua wakati kukusanyika kanisani au kwenye hekalu sasa mna leseni ya kutenda dhambi na dhambi hizi ndizo mlizoulizia msamaha na kugeuka na kuyarudia tena mkifahamu mnachofanya. Kwa kuyafanya haya, mmethibitisha, kwamba hamkua na nia ya kugeuka kutoka kwa dhambi. Hamdanganyi yeyote, na wale mnaowaita wapagani wanawakejeli kisiri! Kwa kuwa hamna tofauti kati yao nanyi.

Kama mama wa duniani anavyowafariji watoto wake, MIMI SHKHINYAH, RUACH HA KODESH wenu, MAMA HEKIMA wenu, Nafanya tena zaidi ya haya. MIMI huishi ndani YENU na hufanya kazi kupitia ninyi na ni kupitia UPAKO WANGU MTAKATIFU MIMI hufanya maonyesho ya ishara, maajabu na miujiza.

Ni kupitia JINA la MWANANGU YAHUSHUA, kwa sababu ya DHABIHU YA DAMU YAKE, UPAKO WANGU MTAKATIFU huvunja kongwa na utumwa wote. MIMI ndiye RUACH HA KODESH na MIMI sio Mwanamume (‘HE’), binadamu alipotafsiri Agano Jipya, herufi ‘S’ ilitolewa kwenye neno ‘He’, MIMI ni Mwanamke (‘SHE’).

Elisabeth [Elisheva], jihadhari, wale walio na roho za dini na wana umbo la utakatifu lakini hawana UTAKATIFU ndani yao (2 Timotheo 3:5), watakuangamiza. Hawana uhusiano wa upendo na wa kutii kati yao na YAHUVEH, na YAHUSHUA na watathibitishiwa na watakushambulia na kukuita majina mengi maovu.

Kumbuka kuwa ujumbe huu wanaoushambulia sio wako, ni ujumbe wa Mbinguni. Usiwe na hofu, kuna wale ambao majina yao yamo katika Kitabu cha Maisha cha MWANA-KONDOO, ambao watashangilia na kusema, wamekuwa wakiyatafuta majibu kujua mengi juu ya ROHO MTAKATIFU ni nani. Watashangilia na jua kuwa wanajua haya ni ukweli ambayo yamezungumzwa. Wengi washashangaa juu ya haya, lakini hawakuthubutu kumuuliza yeyote wakiogopa watakejeliwa.

JINA LANGU ni MAMA HEKIMA na Nitawapa Hekima zaidi mnaponiuliza MIMI, “MAMA HEKIMA nisaidie katika JINA la YAHUSHUA MASIHI ninaulizia Hekima yako zaidi!” Jaribuni, na muone kama sitawafanyia haya. Oneni kama upako wenu hautaongezeka. Lakini kumbukeni, ni kupitia JINA lake YAHUSHUA pekee Nitaweza kutuma busu (ya maombi) kwake YAHUVEH ili maombi yenu yajibiwe.

Elisabeth [Elisheva], MIMI NI MAMA SHKHINYAH wako, na Nitakuonyesha siri zilizodhihirishwa katika Maandiko Matakatifu ili kusaidia kuwafunza watu WANGU Watakatifu juu ya ROHO MTAKATIFU ni nani kwa kweli.

Mmefundishwa kuwa RUACH ha KODESH ana jinsia ya mwanamume, sio mwanamke, Nimeitwa “He” badala ya “She” kwa sababu ya wasomi walivyotafsiri vibaya Maandiko ya Kale- sanasana kwa sababu ya ubatili ya wanaume ambao hawakutaka haya yadhihirishwe, shetani pia hayataki haya.

Ni MIMI MAMA SHKHINYAH wenu Ninayewaelekeza kwake YAHUSHUA MASIHI, huwabatiza ninyi na MOTO MTAKATIFU WANGU mnaoita ROHO MTAKATIFU. Ni MIMI, MAMA SHKHINYAH Ninayewashauri, Ninaweza kuitwa pia MAMA RUACH HA KODESH, ni chaguo lako. MIMI huwashauri na kufunza na kuzungumza kupitia upako huu mpya Niliokupa Elisabeth [Elisheva]. Na wale walio na masikio ya kiroho ya kusikia na kuamini, watasikia sauti YANGU bora zaidi kwa njia ambayo hawajawahi kuisikia kutoka KWANGU hapo mbeleni.

Binti Mpendwa Elisabeth [Elisheva], Nimekupa upako wa kuzungumza na kufasiri Ndimi Takatifu za Mbinguni zinazungumzia nini. Wewe huongea katika Ndimi za Malaika Watakatifu wa Mbinguni na katika lugha tofauti za binadamu.

Unaweza kuelewa hizi lugha pekee Ninavyokupa kipawa cha kufasiri katika lugha yako. Nyakati zingine MIMI hukulinda, ili usijue ni nini unachoomba, kwa kuwa itauzidi mwili wako unapozungumza katika Ndimi Takatifu za Mbinguni.

Nyakati zingine MIMI huchagua kuzungumza kupitia kwako katika Ndimi Takatifu za lugha za binadamu ambazo haujafunzwa (Matendo ya Mitume 2:4) lakini nyakati zaidi ni lugha za Malaika Watakatifu wa Mbinguni, kama maandiko yanavyosema katika Kitabu cha 1 Wakorinto 13:1.

Wakati Ninapochagua kuzungumza kupitia kwako katika ndimi za Malaika Mtakatifu, na ufasiri wowote haujapewa kwako, ni kwa sababu shetani na pepo zake hawafai kuelewa ni nini kilichoombwa au kuzungumzwa, haya si ya masikio yao kusikia.

Si lazima kila wakati upate ufasiri wa ndimi hizi lakini YAHUVEH husikia na YEYE hujibu maombi yako, hata kama nyakati nyingi haujui unachoomba.

Nyakati nyingine, unawaombea watu ambao hata huwajui, unawaombea watu Watakatifu kote duniani. Nyakati nyingi unaombea mahitaji yako, au uponyaji wako au wa wengine. Nyakati nyingi unaombea Baraka katika Bibi Arusi Watakatifu na wageni au huruma na wokovu wa watenda dhambi warudi kwake MCHUNGAJI MZURI WA KIPEKEE YAHUSHUA MASIHI.

Nyakati nyingine unaombea hukumu na kisasi ya YAHUVEH katika watumwa wake shetani, na wale watakaotupwa katika Shinikizo kubwa la Ghadhabu ya YAHUVEH. Hamna umbali katika maombi. Jitahidi kujionyesha kwa MUNGU kuwa umekubaliwa na YEYE.31

Si MWANANGU YAHUSHUA MASIHI Alisema, “Yohana aliwabatiza na maji, lakini MIMI huwabatiza na MOTO WA RUACH HA KODESH” (Matendo ya Mitume 1:5)? MIMI huitwa pia ROHO MTAKATIFU na PEPO TAKATIFU. YAHUSHUA hunitumia MIMI kuwajaza wote walio Watakatifu, kumiminika na upako WANGU ambao ni ishara, maajabu na miujiza Takatifu kwa kuwa wale WANAOPENDA na kumweka YAHUVEH na YAHUSHUA kwanza katika maisha yao na upendo.

Haya huwahusu pia Bibi Arusi wa YAHUSHUA, wanaotoa yote kufuata na kutii Amri Takatifu zilizoelezwa katika Maandiko Matakatifu, na huyafanya haya kwa upendo wa YAHUVEH na YAHUSHUA na hufanya yote kutii na kuishi katika Utakatifu. ROHO MTAKATIFU WANGU huishi ndani ya Hekalu zao za duniani zinazoitwa mwili.

Bibi Arusi wa YAHUSHUA hutafuta kujua UTATU TAKATIFU zaidi kila siku na hutii kila neno tunayosema, na Utukufu wa YAHUSHUA hung’aa usoni na maishani mwao. Hawashikilii chochote na hutoa yote kwake YAHUSHUA MASIHI kwa Sifa, Heshima na Utukufu WAKE. Kama ilivyoandikwa katika Matendo ya Mitume 2:37-47, Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI watakuwa na hamu ya kufanya haya kama nyakati za kale na kuwa pamoja nawe, na kuwa msaidizi katika Huduma hii na sio kikwazo.

Watafanya haya kwa lengo moja tu, kumpa Utukufu YAHUSHUA MASIHI!

Elisabeth [Elisheva] Binti YANGU, si Maandiko Matakatifu husema katika mwanzo wa uumbaji katika dunia hii, “Njooni tumfanye Mtu kwa MFANO WETU” (Mwanzo 1:26)? Je, mnafikiria ‘MFANO WETU’ unamaanisha nini?

Adamu aliumbwa katika mfano wa YAHUVEH na Hawa aliumbwa katika mfano WANGU WA KIKE. Kama Hawa alivyoumbwa kuwa msaidizi wake Adamu, pia MAMA SHKHINYAH wenu Anaitwa katika maandiko matakatifu “MSAIDIZI.” 32 MIMI NI MSAIDIZI katika UUMBAJI na YAHUVEH na YAHUSHUA. YAHUSHUA ni MWANA WETU. SOTE WATATU Tuliteseka na kulipa gharama, ili watu ambao majina yao yamo katika Kitabu cha Maisha cha MWANA-KONDOO warudi Mbinguni.

MIMI NI MAMA SHKHINYAH wenu.

MIMI ndiye yuleyule Anayeishi ndani ya miili zenu, roho na nafsi.

MIMI NI MSHAURI WENU WA MBINGUNI, MWALIMU wenu.

MIMI NI ROHO NA UKWELI.

MIMI ndiye yuleyule Anayewapa hamu

ya kumkubali na kumtii YAHUVEH na YAHUSHUA kama MUNGU.

MIMI ndiye yuleyule Anayewapa hamu ya Kuimba, Kusifu, Kuomba na Kumuabudu YAHUVEH na YAHUSHUA.

Sasa Nawapa hamu mpya na hii ni kupata kujua yule Anayekupa upako,

RUACH HA KODESH wenu, MAMA SHKHINYAH wenu.

Watoto Watakatifu, MIMI hupenda sanasana mnapoimba na kuzungumza maneno ya upendo kwangu MIMI pia. Nimengoja wakati huu kwa uvumilivu. Nimeungoja ufunuo huu uachiliwe na ilikadiriwa kule Mbinguni kuwa wewe, Ringmaiden wetu mbarikiwa, Elisabeth Sherrie Elijah [Elisheva Eliyahu], utakuwa sauti itakayopasha Ujumbe huu Mtakatifu kote duniani. Hili ndilo sababu unaitwa Ringmaiden wa YAHUSHUA.

MIMI, MAMA SHKHINYAH wenu Ninayeitwa pia RUACH HA KODESH Nimekuchagua wewe Elisabeth [Elisheva], kuwa na nafasi ya heshima ya kunitambulisha MIMI kama MAMA SHKHINYAH kwa Watoto WANGU. Watoto wengi Watakatifu wataponywa kutokana na majeraha waliyoyapata, kwa sababu katika dunia hii hawajawahi kujua upendo, faraja na ushauri wa Mama mwenye upendo. Na kumbe Nilikuwa papo hapo huu muda wote. Sasa Nimekupa upako wa kusikia sauti YANGU na uwaambie haya.

Ninajua kuwa utatii!

Bila kujali gharama ambayo utalazimika kulipa!

Ninaitwa ‘HEKIMA’ Tunda langu ni Roho Saba.

Someni Nguzo Saba zilizozungumziwa

katika Kitabu cha Ufunuo wa Yohana. 33

MIMI ndiye huitwa UTULIVU, UVUMILIVU;

MIMI NI HURUMA, na mengine zaidi.

Jifunzeni na kusoma sasa kuhusu YULE Anayekupa upako ni nani.

MIMI NI zaidi ya

UPEPO MTAKATIFU au MOTO MTAKATIFU wenye UPAKO,

au HARUFU NZURI KWENYE HEWA.

MIMI ni- zaidi ya

KUZUNGUMZA KATIKA NDIMI TAKATIFU ZA MBINGUNI,

na UNABII, na ISHARA, MAAJABU na MIUJIZA.

MIMI ni MAMA SHKHINYAH wenu,

Ninaitwa pia RUACH HA KODESH,

Anayezielekeza nafsi kwake YAHUSHUA HA MASIHI.

MIMI ndiye yuleyule Anayewapa UPAKO

WENYE NGUVU za MBINGUNI na HUMWAGA MVINYO WANGU MPYA NA MKATE KUTOKA Mbinguni.

MIMI NI MAMA SHKHINYAH wenu NAMI sigawi Utukufu WANGU na mwanamke au mwanamume yeyote.

YAHUVEH, YAHUSHUA NAMI sote ni MOJA.

Unapoabudu YAHUSHUA unatuabudu SOTE WATATU vilevile. Kama mwataka mnaweza kuniita MIMI “MAMA RUACH HA KODESH,” wengine bado wanaweza kuniita MIMI “ROHO MTAKATIFU,” lakini Nina hamu ya kuyadhihirisha mengine zaidi kwa wale ambao wana hamu ya urafiki zaidi NAMI.

Nawaonya sasa, yeyote anayekataa au kutusi yale Shaul (Mtume Paulo) alifunza kuhusu ukweli wa Karama za Roho za RUACH HA KODESH, TUBU SASA! Kwa kuwa umetusi na kuhuzunisha hadi nafsi yako ipo taabani!

Ninazungumza sasa katika JINA mnalolitambua kama YAHUSHUA.

Kama hautatubu utalaaniwa milele!

Kwa wale watakaoendelea kukataa na kukejeli ROHO MTAKATIFU, (RUACH HA KODESH) na KARAMA za ROHO MTAKATIFU, majina yenu hayajawahi kuwa katika Kitabu cha Maisha cha MWANA-KONDOO au yamefutwa, kwa sababu kabla hamjazaliwa hapa duniani ilikadiriwa tayari kule Mbinguni, kama jina lako lipo katika Kitabu cha Waliolaaniwa au Kitabu cha Waliofutwa, basi jehanamu ndipo nyumbani kwako.

Siri hii Ninairudia tena34 kupitia Elisabeth [Elisheva]:

Kila nafsi aliyezaliwa hapa duniani alijaribiwa kule Mbinguni kabla hajaja hapa duniani, na hili ndilo sababu kila nafsi atimize “wokovu wake mwenyewe kwa kuogopa na kutetemeka” (Wafilipi 2:12). Roho yao ishajua kama wapo katika upande wa shetani au upande wa YAHUVEH katika vita kuu ya usaliti kule Mbinguni, kabla ya Dunia hii kuumbwa.

Si dhambi kutoelewa Kipawa cha Unabii, au kuongea katika Ndimi Takatifu za binadamu na Malaika Watakatifu, lakini msizungumze dhidi ya yale yaliyo Takatifu kwa sababu tukio hili halijafanyika maishani mwako, au ulipitia tukio mbaya la bandia. Wengine wenu mnaosoma haya mmepitia tukio la kujazwa na ndimi za kishetani. Kwa hivyo msidharau lile tukio halisi kwa sababu mlijifungua kwa yale ya bandia kupitia dhambi na ukoo wenu iliyojawa na uchawi.

MIMI, YAHUVEH, Ninawaonya kuwa shetani ni muovu katika njia zote, hata anawafunza watu kuomba kwa miungu ya kike kwa sababu anajua kuwa RUACH ha KODESH, MAMA SHKHINYAH wenu ndiye MALKIA PEKEE WA MBINGUNI.

Soma neno “SHEKINAH GLORY” lina maana gani.

Soma Maandiko Elisabeth [Elisheva]

na utakuwa na amani- katika kuitoa

Siri hii iliyohifadhiwa

kwa wakati kama huu.

Haya yataponya majeraha mengi, kama vile ulivyokuwa na utupu ndani yako wa upendo wa mama, sasa utagundua kwamba umeponywa na wengine pia wataponywa kwa kuwa utupu huo umejazwa.

Baada ya kumkubali YAHUSHUA kama MASIHI, papo hapo mnajazwa na ROHO MTAKATIFU WANGU, RUACH HA KODESH WANGU; MAMA SHKHINYAH wenu ni yuleyule ROHO WANGU na ROHO huyu hukaa ndani yenu. Haya pia humaanisha kuwa MIMI huona kupitia macho yenu ya mwili, na husikia kupitia masikio yenu ya mwili, na husonga kupitia mwili wenu.

Kwa hivyo msinihuzunishe MIMI.

Msiendelee kunijaribu MIMI.

Haya yanawahusu wote waliomkubali YAHUSHUA MASIHI kama MUNGU, BWANA, MWOKOZI, Mwana wa Pekee wa YAHUVEH, Aliyezaliwa katika mwili kutoka kwa mwanamke bikira, na Akajitolea kama DHABIHU TAKATIFU YA DHAMBI, Aliyekufa na kufufuka tena katika siku ya tatu, na sasa hukaa kwenye Upande wa Kulia WANGU MIMI, YAHUVEH.

Wote wanaojaribu kutii wamejazwa na RUACH HA KODESH WANGU, ROHO MTAKATIFU WANGU hadi kiwango fulani. Wengine wamejazwa na zaidi na wengine kiwango kidogo wanavyokua katika maarifa ya YAHUSHUA ni nani.

Kwani mnafikiria wazo la bwana na bibi Mtakatifu kuwa moja lilitoka wapi? Ilifanywa kwanza hapa Mbinguni. Mlipomkubali YAHUSHUA kama MASIHI, hamkunjua kwamba wakati uo huo mlikuwa mnajazwa na UPENDO wa MAMA wa MBINGUNI. Neno “mfariji”- ndilo Mama hufanya bora zaidi.

MIMI NI MAMA RUACH HA KODESH wenu

na MIMI NI MFARIJI wenu.

Ninawabembeleza mnapohitaji kubembelezwa;

Wakati hisia zenu ziko mbichi,

na mnateseka, mna hofu, mko pekee yenu

au mnahisi kukejeliwa au kuchanganyikiwa,

MIMI ndiye AMANI IPITAYO FAHAMU ZOTE (Wafilipi 4:7);

MIMI NI RUACH HA KODESH, MAMA SHKHINYAH wenu

Ninayewapa upendo Mtakatifu wa Mama wa Mbinguni.

Hii ilikuwa Siri iliyotolewa kwake Nabii Danieli, katika Kitabu cha Danieli, na kutiwa muhuri kwa wakati kama huu (Danieli 12:4).

Tena, Ninarudia, sasa ndio wakati,

YAHUVEH Amekadiri-

kuwa Neno LANGU la Hekima liachiliwe!

Huu ni wakati ambapo roho ya kidini itainuka na kujionyesha jinsi ilivyo na uovu. Mafarisayo walikuwa na roho ya kidini na kumbuka walivyomtesa YAHUSHUA na pia WOTE walio na Utakatifu? Watakatifu lazima wasimame pamoja sasa, kusaidiana na kuteteana, kwa sababu “nyumba iliyotengwa haiweza kusimama” (Mathayo 12:25).

Ringmaiden WETU Mpendwa Elisabeth [Elisheva], hii ni siri iliyopewa kwako Sauti za Radi Saba zilipokuamsha, na kuzungumza nawe, miaka mingi iliyopita.

Kwa msomi wa Neno hili, jitahidi kujionyesha kwa MUNGU kuwa umekubaliwa na YEYE na ombea hekima kuu katika Ufunuo wa Yohana 10, kwa sababu katika Radi Saba Elisabeth [Elisheva] alisikia, kulizungumzwa siri kadhaa zilizodhihirishwa kwenye Jumbe za Kinabii hadi sasa.

Elisabeth [Elisheva], kama ungekuwa umeandika tarehe hiyo ungeona kuwa ingelingana na wakati ule ule Radi Saba zilipozungumza, siku na mwezi (8/27)- na ni katika wakati na mwaka uliopangiwa pekee ndio haya yangedhihirishwa mbele ya dunia katika mtandao, kama ilivyo sasa wakati na msimu uo huo uliopangiwa.

Elisabeth [Elisheva], kabla kulikuwa na Huduma, unaweza kukumbuka pekee ukiamkia mipigo kubwa ya radi mara saba mfululizo iliyokuwa kwa sauti ya juu sana, ikakutingisha hadi ukaamka, lakini hakuna yeyote aliyeisikia ila wewe. Jua lilikuwa linang’aa angani.

Pigo la radi lilikuwa MIMI, YAHUVEH Nikizungumza nawe, ulivyokuwa unalala pekee yako asubuhi hiyo, Nilikuamsha kwanza na pigo moja la radi lililokutingisha hadi ukaamka. Ulikimbia dirishani na ukaona jua, na alafu mara moja ukarudi kulala, ukaamshwa tena vivyo hivyo mara saba mfululizo, kila wakati ukirudi kulala, ukiomba na kuniuliza MIMI ni nini kilichokuwa kinaendelea?

Haya yalitokea saa 7.00 asubuhi.

Yaliyoandikwa sasa, na katika unabii ziliachiliwa kwa siri kwenu nyinyi wakati uo huo, lakini tena hamkuyajua haya hadi sasa. Ilipaswa kudhihirishwa katika wakati WANGU. Katika siku, mwezi na mwaka iliyotengwa utajua una ruhusa ya kuutoa ufunuo huu mpya na ni kutoka nchi gani neno hili la maarifa litaachiliwa, na Upako huu usio wa kawaida.

Jitayarisheni, bibi arusi wa shetani, watumwa wa shetani, na watoto wake shetani watawashambulia. Shetani alitaka kuweka neno hili la maarifa siri. Wale wanaojiita Wakristo lakini wana umbo la utakatifu tu lakini hawana UTAKATIFU ndani yao (2 Timotheo 3:5), watawashambulia kwa maneno lakini MIMI, YAHUVEH Ninaenda mbele yenu na Nitapigana vitani kwa niaba yenu.

Miaka iliyopita kabla hujazaa Huduma hii, uliomba na kumuuliza YAHUSHUA, ni nini kilichokuwa kinatendeka, uliposikia pigo la radi mara saba. Kwa nini uliamka na kukimbia na kuangalia nje ya dirisha na mara moja ukarudi kulala mara saba? Natoa siri hii kwako, nambari 7 huwakilisha mwaka wa 2007. 7 ni nambari ya ukamilifu na ni katika wakati WANGU kamilifu maarifa haya yanaachiliwa.

Kumbuka ulipohisi ghafla kusoma kuhusu Radi Saba katika Kitabu cha Ufunuo wa Yohana (Ufunuo wa Yohana 10:3-4)? Katika miaka mingi hujawahi kupata jibu hadi sasa. Ilikuwa wakati uo huo MIMI, YAHUVEH Nilizitoa siri zilizozungumzwa kupitia Radi Saba- Nilidhihirisha Nilivyokuwa Nikizungumza kupitia kwako sasa kama Nabii.

Ninakutumia wewe kwa sababu kabla ya Uumbaji wa Dunia hii ulikuwa umechaguliwa kuja ardhini kuleta Sifa, Heshima na Utukufu wote kwangu MIMI, YAHUVEH, YAHUSHUA, na RUACH HA KODESH, yule umwitaye sasa MAMA SHKHINYAH au MAMA HEKIMA. Ulipewa upako kwa wakati kama huu.

Ulichaguliwa kabla ya Uumbaji wa Dunia hii kujazwa na RUACH HA KODESH WANGU hata kama ungali katika tumbo la mamako aliye mpagani, mahali ulichukiwa, haukutakwa na kukejeliwa. Sasa ni miaka kadhaa baadaye, na sasa umegundua kwamba ni MAMA SHKHINAH Aliyekufariji. Ilichukua miaka chache baadaye kabla hujagundua kuwa wewe ni nani katika JINA la YAHUSHUA na Dhabihu YAKE YA DAMU ilikuwa kwako pale Kalivari.

Ulichaguliwa kabla ya Uumbaji wa Dunia hii kuzaa Huduma hii Takatifu na jina lisilojumuisha jina lolote la mwanamume au mwanamke lakini linaheshimu pekee UTATU TAKATIFU.

Elisabeth [Elisheva], umepewa upako kama Yeremia wa kale alivyokuwa (Yeremia 1:4-10)- ulipokuwa tumboni mwa mamako, kama Mdomo WETU na ukapewa sauti ya Nabii Mtakatifu anayelia katika jangwa ya dunia hii. Ni majina ya wale walio katika Kitabu cha Maisha cha MWANA-KONDOO watakaoamini na kukubali kweli katika Huduma hii kama vile bila shaka watakavyomkubali YAHUSHUA kama MASIHI.

Mtumishi si mkuu kushinda bwana, na kama wote wangemkubali YAHUSHUA MASIHI Alipotembea humu ardhini Akiwafunza na kufanya miujiza kwa Utukufu WANGU MIMI, YAHUVEH, basi wao pia wangewakubali na kweli Ninazozizungumzia kupitia Huduma hii.

Unazungumza maneno ambayo MIMI, YAHUVEH Nimezungumza, ambayo YAHUSHUA MASIHI Amezungumza, na sasa umepewa kipawa kisicho cha kawaida kusikia MAMA SHKHINYAH wako Akizungumza kupitia kwako. Upako huu usio wa kawaida utawajia Nabii wengine Watakatifu watakaoamini na kukubali kweli hizi na kukufunika katika maombi, wakikusaidia wewe na upendo wao na wakifanya yote wanayoweza kuwa Baraka katika Huduma hii.

Elisabeth [Elisheva], MIMI NI MAMA SHKHINYAH GLORY wako. MIMI ndiye yuleyule Anayekupa upako wa ishara, maajabu na miujiza yanayohusu pia kutabiri na kuomba katika Ndimi Takatifu za binadamu na Malaika Watakatifu.

MIMI NI MAMA SHKHINYAH GLORY wenu. MIMI ndiye yuleyule Anayewaombea Watoto wote Watakatifu Ninavyobeba maombi yenu hadi kwenye Kiti cha Enzi cha YAHUVEH kama busu35 lililotumwa kwenye hewa, inapofanywa katika JINA la YAHUSHUA MASIHI.

Haya yanahusu pia jina la “YESU KRISTO” kwa sasa, lakini jihadharini, kwa sababu mwana wa shetani katika Dhiki Kuu atalitumia vibaya jina la ‘Yesu Kristo’. Sitaweza kuyatuma maombi yenu kwa wakati huo katika jina la ‘Yesu’, kwa sababu mwana wa shetani atakuwa pia analitumia jina la ‘Yesu Kristo’.

Funzeni sasa JINA TAKATIFU la KIEBRANIA la YAHUSHUA na YAHUVEH kwa wote walio na masikio ya kiroho kusikia, sikizeni na mtii. Jifunzeni na mjizoeshe kutumia JINA LA KIEBRANIA- la kweli la yule ambaye wengi wenu humuita ‘YESU KRISTO’- sasa kabla hamjachelewa. Waambieni watu, “Wasingoje hadi Dhiki Kuu kujifunza somo hili kwa njia ngumu.” [Ona, “Kwa nini Tunatumia MAJINA MATAKATIFU.” P. ]

Piga kelele mpaka wasikie na ujumbe huu ulie kote duniani, katika Dhiki Kuu kutakuwa na udanganyifu mkuu na kwa wakati huo, YAHUVEH hataweza kujibu maombi katika jina la ‘Yesu Kristo’.

Ni katika JINA la KIEBRANIA la YAHUSHUA MASIHI litakalobeba nguvu za Uponyaji, Kuokoa na Kufufua! Kwa sababu yule aitwaye mwana wa shetani atawatumia na kuwadanganya mamilioni juu ya mamilioni- akifanya ishara, maajabu na miujiza ya kibandia atakapokuwa akitumia vibaya jina la ‘Yesu Kristo’ mbele ya dunia. Hata wateule watadanganywa- kama iwezekanavyo (Mathayo 24:24, Marko 13:22).

Jihadharini, sasa kuna wanaume waovu na roho ya mpinga kristo na wanatumia jina la ‘Yesu Kristo’ lakini wanachukia JINA la Kiebrania la YAHUSHUA kwa kuwa ni kumbusho daima kwao kuwa YAH huokoa! YAHUSHUA ndiye MASIHI wa pekee.

Elisabeth [Elisheva], umesikia sauti ya BABA YAHUVEH, na umesikia Sauti na kukubali Ujumbe kupitia upako WANGU kutoka kwa YAHUSHUA, MASIHI wako.

Nimengoja kwa uvumilivu kwa wakati ule ambao utanijua MIMI kama upendo wa MAMA WA MBINGUNI ambao umeutamani daima. MIMI NI MAMA yako wa pekee, na MIMI ndiye yuleyule Anayekupa upako na kukufariji wewe na kukushauri wewe. Ni kwa ajili ya MAMA SHKHINYAH wako unaweza kusikia Sauti YANGU ndogo ya utulivu na kusikia Ujumbe Takatifu kutoka kwa YAHUVEH, na YAHUSHUA. MIMI ndiye SAUTI ILEILE NDOGO YA UTULIVU inayozungumza nawe. Kwa wale ambao wanayashuku haya, Niambieni MIMI, tangu lini sauti ya mwanamume ikaja kuitwa kama “sauti ndogo ya utulivu” (1 Wafalme 19:12)?

MIMI ndiye yuleyule Mfalme Daudi wa kale, Aliomba, kuwa Nisiwahi kumuacha. Aliomba, “Usimchukue RUACH ha KODESH wako kutoka kwangu mimi” (Zaburi 51:11).

MIMI ndiye yuleyule mnaponidharau au kunihuzunisha au kunitusi mpaka mwisho Wangu, MIMI husema, “Tosha”. Na MIMI huenda ZANGU na hamna hata matumaini ya Wokovu kwa roho hiyo, [mpotovu]. Ni Ghadhabu ya YAHUVEH pekee ambayo mtu huyo atajua, Jehanamu na Ziwa la Moto ni nyumba ya milele ya mtu huyo.

MIMI NI RUACH HA KODESH pia katika Kiaramu Ninaitwa “ROHO ALIYETENGWA KANDO.” MIMI ndiye ukweli wote, na ni kupitia MIMI pekee yeyote anaweza kuelekezwa kwake YAHUSHUA na kumkubali YEYE kama njia ya pekee hadi Mbinguni. MIMI Ninaitwa RUACH HA KODESH, na kwa vyeo vya PEPO TAKATIFU na ROHO MTAKATIFU. MIMI ndiye UTAKATIFU wote, pia na YAHUVEH na YAHUSHUA. Sote ni MOJA na bado tofauti. Sisi ni UTATU TAKATIFU na hamna yeyote mwingine. Katika Dhiki Kuu kutakuwa na utatu usio takatifu! shetani ni mwigaji pekee sio muumbaji.

Hamna njia yoyote ile hadi Mbinguni bila kupitia SOTE WATATU, BABA YAHUVEH, YAHUSHUA na MIMI, MAMA RUACH HA KODESH wenu.

Wokovu huja tu kupitia JINA la YAHUSHUA na DAMU ILIYOMWAGWA. Na sehemu ya kazi YANGU ni kuzivuta nafsi kwake YAHUSHUA na huwa sikosi hata nafsi moja aliyeandikwa katika Kitabu cha Maisha cha MWANA-KONDOO, kabla ya uumbaji wa dunia hii.

Ninaitoa siri hii kwako sasa, pia na kipawa CHANGU cha ujasiri kuzungumza na kutabiri kama Nabii wengine wasivyoweza kama hapo awali mbele ya wote. Kuna wengine waliofundisha kuwa MIMI nina jinsia ya kike, na bado hawajawahi kutabiri katika njia Ninavyozungumza kupitia kwako leo.

Ninaitoa siri hii ili uweze kuwapa moyo wale WANAOMPENDA na kumweka YAHUVEH na YAHUSHUA kwanza katika maisha yao na upendo na pia kunikumbuka MIMI, MAMA SHKHINYAH, kwa kuwa MIMI NDIYE Utukufu wa YAHUVEH na YAHUSHUA kama vile bibi Mtakatifu aliumbwa kuwa Utukufu wa bwana wake Mtakatifu.

Unaposhambuliwa kwa kufichua JINA la ROHO MTAKATIFU ambalo ni JINA LANGU SHKHINYAH na kudhihirisha ROHO MTAKATIFU hajaumbwa katika mfano wa mwanamume, lakini ya mwanamke, waambie wajitahidi kujionyesha kwa MUNGU kuwa wamekubaliwa na YEYE (2 Timotheo 2:15).

Kwani si Vitabu vya Kale katika Zaburi na Mithali36 – humwita ‘HEKIMA’ katika jinsia ya Kike (‘SHE’)? Je, si Maandiko Matakatifu husema, “Mwanzo wa HEKIMA ni kumcha YAHUVEH” (Zaburi 1:7)? Wakumbushe kuwa katika Bibilia ya KJV- JINA la YAHUSHUA linalotajwa pia kama YAHSHUA halipo- ni jina tu la ‘Yesu’ ambalo lipo.

Jua haya: jina la ‘YESU KRISTO’ bado linaheshimika na lina upako kwa wakati huu na huokoa roho, hukomboa na huponya. Lakini Nimewaonya, katika Dhiki Kuu inayokuja yule aitwaye sasa mpinga kristo, atajiita pia “Yesu.”

Hata sasa bandia amejitokeza na hudanganya mamilioni na jina la ‘Yesu Kristo’. Hata kupita mpaka, kuwaambia wao wajichore nambari 666 kuthibitisha kutii kwao kwa mwanamume huyu muovu- yeye hujiita “mwana wa Mungu” na huwaambia watu, “Hamna kitu chochote kama dhambi na jehanamu ni uongo.” 37

Nimejirudia mara kwa mara kwa sababu Mbegu hili la Ukweli lina nguvu sana hadi shetani atataka kulitoa Shamba la Kweli hizi- katika Neno hili la Kinabii na Maarifa- kabla haijamea.

Nimeitumia Huduma hii kuwaonya kwa nini ni muhimu kujifunza JINA Takatifu la Kiebrania la YAHUSHUA (tafsiriwa kama YAH huokoa) Ambaye sasa huitwa ‘YESU KRISTO’. Kwa sababu katika Dhiki Kuu ni JINA LA KIEBRANIA LA YAHUSHUA tu litakalokuwa na nguvu za Upako, Uponyaji, Ukombozi na Kuokoa. Tena Ninarudia na kuwaonya.

Kama makanisa ya kidini yalikuwa yanafanya kazi yao watu hawangedanganyika.

Jihadharini! Itakuwa wainjilisti wa televisheni maarufu ambao watawaongoza watu kwa mwana wa shetani, atakayekuja akitumia jina lililoaminiwa, ‘Yesu Kristo’. Itakuwa wainjilisti wa televisheni maarufu watakaouza nafsi zao kwake shetani kwa umaarufu na mali, watakaofunza mafundisho bandia ya mwanadamu na kuwaelekeza watu kwa huyu ‘Yesu’ bandia.

Katika Dhiki Kuu jina la ‘Yesu’ litatumika vibaya na mwana wa shetani anayeitwa sasa mpinga kristo. Huyu mpinga kristo atachafua jina la ‘YESU’ na kupitia nguvu za shetani atafanya ishara, maajabu na miujiza isiyo takatifu katika jina ambalo linajulikana na Kanisa la Wakristo, jina ambalo sasa linapendwa na kuaminiwa, “Jina la YESU KRISTO.”

Mwana wa shetani, anayeitwa mpinga kristo atadai kuwa yeye ndiye ‘Yesu Kristo’. Atalazimisha wote kumuabudu na kumheshimu na kuhudhuria na kukusanyika kanisani katika siku ya Jumapili na kuchukua “alama” yake (Ufunuo wa Yohana 13:16-18) – wakithibitisha uaminifu wao. Mpinga kristo ambaye kwa kweli ndiye mwana wa shetani atakuja na roho ya Yuda na Hitler tena- ambaye maandiko humwita “mwana mpotovu”, au “mwana wa Jehanamu”. Mwana wa shetani, atafanya ishara, maajabu na miujiza bandia katika nguvu za shetani kwa utukufu wa shetani.

Nimeitumia Huduma hii kuwaonya, mtakapoona amri la lazima la kuabudu Jumapili limepitishwa, MSIINGIE katika Kanisa hizi za Jumapili au MTAPOTEZA NAFSI ZENU! Nimewaonya mjifunze sasa Siku ya Kweli ya Sabato ni ipi- [Ijumaa jioni hadi Jumamosi jioni].

Ujumbe huu umekuwa mgumu kwake Elisabeth [Elisheva] kuutoa kwa sababu Kanisa za Wakristo hazitaki kuusikia. Hata hivyo, kwa wale ambao wamekuwa waaminifu na kuzungumza kweli hizi, mnajua kuwa mmepewa Amri hii ya Ezekieli 3:17-21.

Huduma hii imepewa Amri ya kufunza MAJINA MATAKATIFU YA KIEBRANIA YA WAUMBAJI pamoja na ya YAHUSHUA MASIHI. Ni yupi bora Ningemchagua kufunza wale wanaotaka kujua JINA la ROHO MTAKATIFU?

Elisabeth [Elisheva], ulimwuliza YAHUVEH kuhusu JINA la RUACH HA KODESH na sasa Nishakuambia, sasa Ninakupa amri hii kutoa haya yote Niliyokuambia kwa siri. Ninakuahidi wewe, kuwa wale walio na masikio ya kiroho ya kusikia watasikiza, na kuiunga mkono Huduma hii na kutetea ukweli huu na kufunza wengine.

Wale ambao watachagua kubaki viziwi kiroho watabaki viziwi. SIO kazi yako kuwashawishi watu, ni kazi yako TU kutii na kuzitoa Jumbe hizi za Kinabii na Maneno ya Maarifa kama zimekabidhiwa kwako kutoka Mbinguni. Kila mtu atakayesoma haya au amefunzwa haya watawajibika kwa yote wajuayo.

Mwisho wa Unabii

Kuwaudhi wengi na kuwabariki wengine wenye masikio ya kiroho ya kusikia, ambao majina yao yamo katika Kitabu cha Maisha cha MWANA-KONDOO.

Mtoto, Shujaa, na Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI

Mtume Elisabeth Sherrie Eliyahu

Ilitolewa Agosti 27, 2007

* * * * * * *

Wapendwa,

Kwa kufunga, nimeandika yote niliyoyasikia na niliyoambiwa niandike. Nimeuliza YAHUVEH, YAHUSHUA na MAMA SHKHINYAH GLORY; kama WOTE wana uhakika kuwa hakuna yeyote mwingine anayeweza kutoa neno hili bora kunishinda mimi. Sijui ni kwa nini nilichaguliwa.

Hata hivyo, kazi yangu ni kutii UTATU TAKATIFU. Ninaogopa ni nini YAH Anaweza kunifanyia mimi, zaidi ya kuogopa ni nini binadamu atafikiria juu yangu. Upendo wenu na msaada ninayathamini sana!

Ninatarajia kukutana nanyi Mbinguni kama sio hapa Duniani!

Elisabeth Sherrie Elijah

(Elisheva Sherrie Eliyahu)



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred