Prophecy 88
MIMI, YAHUVEH, Nachezea Maadui WANGU!
Imepewa kwake Mtume Elisheva Eliyahu Oktoba 16, 2006
Haya ni kutoka Unabii 105, YAHUVEH Alisema kuweka haya kwa Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)
Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya kila Unabii:
2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”
* * * * * * *
[Unabii huu ulirekodiwa kwenye kinaza sauti na iliandikwa vilevile ilivyorekodiwa. Dakika 15 za ndimi za vita zilitangulia kabla neno hili halijakuja.]
* * * * * * *
Na hii ni onyo kwa maadui! Mnaingia kisirisiri kwake (Elisheva) wakati analala. Mnafikiria kuwa sitamuamsha. Hata kama hamuezi kuonekana, MIMI Ninaweza kuwaona! Hazungumzi lugha yenu; o lakini MIMI, YAHUVEH, Ninazungumza lugha yenu. Mnataka kumuua pale ambapo mikono ya binadamu haiwezi kuwaguza.
O lakini MIMI, YAHUVEH, Ninaweza kuwaguza. Mtalipa gharama kwa haya. Ninawakejeli, Ninawatesa, kwa kuwa mtasikia lugha yenu kwa sauti yenu na ndimi yenu kwenye hewa na mtasema, “Je, Anajuaje lugha yetu? Anajuaje ni mimi niliyemshambulia?” Sio yeye anayejua, ni Muumbaji wa YOTE Anayejua!
Hauwezi fanya lolote, o maadui WANGU, ambalo sijui na yeye hujua tu yale Ninayomuambia, hamna lingine, mtoto tu asiye na hatia na MIMI Ndiye Baba Afunzaye. Yeye ana Masihi, ana mwombezi, ana Shinikizo la Damu, ni Mwana WANGU YAHUSHUA! Je, Yako ipo wapi?
Nyote mwaenda jehanamu! Nyote mwaenda katika Ziwa la Moto! Mnaingia kisirisiri, katika dunia ya kiroho, mnaingia kisirisiri kuua huyu asiye na hatia kama amelala. Ni MIMI, HA, HA, HA, Ninayewakejeli! Anapolala pale, ni MIMI Niliyemuezesha kuwasikia mkiingia kisirisiri. Ni MIMi Niliyesema, “Elisheva, sikiliza,” hata kama alikuwa usingizini, ni MIMI Niliyesema, “Muda ujao utakapofungua mdomo wako, utazungumza katika lugha usioijua, ndimi hujasikia, lakini itakuwa ni MIMI Ninayezungumza hukumu kwa maadui wasioonekana wanaotaka kukuua.”
Ninawachezea nyinyi (maadui) kuwaonyesha, ni MIMI, YAHUVEH, Ninayejua yote, ili Niwape tu kamba iliyotosha kwa nyinyi kunyinyonga. Kwa kuwa mtakufa mahali pa kuanguka pa hamani! Nimeongeza ulinzi, yeye hana [maisha] ya kawaida. O, wanalia, wanataka kuwa ‘kawaida’ lakini hakuna kitu kawaida kuhusu huduma hii, hakuna kitu kawaida kuhusu hawa ambao Nimewaamuru kulinda na kutetea.
Kwa hivyo kimbieni, kimbieni, kimbieni! Wengine wenu mtaishi na wengine wenu mtakufa usiku huu, lakini ujumbe huu utarudishwa, kama ndimi yenu inasikika kote hewani. Na Nitawapa manabii wengine tafsiri ya ndimi hii, kwa hofu yenu.
Mwaona, kila wakati mnapomshambulia, kila wakati mnaposhambulia wale 5 wa hekima, inayoashiria bikira 5 wa hekima, kila wakati mnaposhambulia Bibi Arusi WANGU (Ufunuo ya Yohana 14 na 7), hamna popote kwa nyinyi kujificha. Ninawacheka nyinyi (Katah, katah, katah, Ndimi takatifu inasikika) mliohifadhiwa kwa hukumu, mliohifadhiwa kwa uharibifu. Nyinyi ambao ni maadui wa huyu Ringmaiden, wa huduma hii, wa Bibi arusi WANGU, mmehifadhiwa kwa uharibifu WANGU na itakuwa Jehanamu, katika Ziwa la Moto mtaishi!
Mwisho wa Onyo.
* * * * * * *
Maoni ya Elisheva kwenye kinaza sauti: “Nilikuwa na usiku-nilitaka tu wakati na nafasi” kwa hivyo nikawa na usiku wa amani. Wakati spesheli na YAHUSHUA na wakati tu wa kucheka na kucheza na kitu ambalo [mimi] sikuwa nimefanya kwa muda mrefu, tukiwa tu kwa mambo yetu-nikalala. Kwa hivyo, kama nimelala kabisa na ghafla nikasikia mtu anafungua mlango wetu, sauti ya mlango ukifunguliwa, mlango ukifunguliwa. Nakumbuka nikiamka nikasema, ‘Mtu ameingia. Mtu amefungua mlango,’ lakini nilikuwa nimelala hata nilipokuwa Ninasema hayo.
Hata kama nilikuwa nimelala nikaanza kusikia YAHUVEH. Na YAHUVEH Akasema, “Ataanza kuzungumza kwa ndimi ya adui aliyefungua mlango”, ningoje. Na bado nilikuwa nimelala na Akasema, “Ngoja tu, wakati ujao utakapofungua mdomo wako itakuwa kwa ndimi ambayo haujawahi kusikia” na vivyo hivyo ndivyo ilivyofanyika. Hayo tu ndio ninayojua na niliweza kuona (kwa maono) watu wakikimbia na niliona hukumu na moto na walishtuka kwa sababu walijua kuwa wameonekana na walijua kuwa sikuwa nijue kuwa walikuwa pale.
Na hayo tu ndio ninayokumbuka isipokuwa najua kuwa kuna kitu muhimu sana kuhusu neno ‘katah’ na Aliniambia kuwa mtu atatambua hizi ndimi au mtu ambaye atakuwa na uwezo wa kutafsiri kwa sababu kuna mengi zaidi juu ya tunayojua na haya ndiyo ninayotaka kusema. Ninachotaka kuongezea ni, kabla hata sijazungumza kwa sauti na mdomo wangu, na hizo ndimi, ilikuwa jambo la ajabu. YAHUVEH Alikuwa Amenifanya nipigie hao maadui kelele katika Kiroho na ndimi hizo. Nilisikia ndimi hizo katika dunia ya kiroho nikipigia maadui kelele kabla sijaweza kuyaachilia kwa mdomo wangu. YEYE (YAHUVEH) Alikuwa na hasira na wakati mmoja, Alichukua mkono wangu na ninakumbuka haya kwa sababu nilikuwa nimeifanya katika kiroho hapo awali hata kabla sijaifanya kimwili, na nikauchukua mkono wangu na kuukoroga kama kimbunga, “haraka, haraka, haraka, haraka, haraka.” Na Akasema, “Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa maadui wanaoshambulia huduma hii.” Wameshambulia hela zetu na bado, YAHUVEH Anasema, (Elisheva anaanza kuomba katika ndimi tena na neno hili likaja).
* * * * * * *
JE, UTAENDA MAILI ZAIDI?
Baraka, baraka, baraka, kwa kila mtu ambaye amekuwa akiifunika huduma hii kwa maombi. Mmeshangaa ni nini kimekuwa kikiendelea. Kwa kuwa sauti ya Elisheva imekuwa kimya tangu Unabii wa mwisho. Ni wachache sana waliandika kuwa walikuwa wanaogopa. Barua zingine ziliibwa, ndio asipate kutiwa moyo. Je, ni wangapi waliosikia sauti YANGU na mkajaribu kutoa kwa huduma hii? Lakini kadi zenu zikazuiliwa lakini mbona hamkuuliza maswali, kwa nini?
Hamjaweza kusaidia huduma hii kama mlivyofanya miaka iliyopita. Je, mbona hamkuenda maili zaidi? Mbona hamkusema, “lazima kuwe na njia ingine?” Kwa kuwa amekataa kuchukua hali ya msamaha wa kodi, amekataa kunyamazishwa kama nabii.
Mnasema kuwa huduma hii ni ya maana kwenu. Mnangojea neno lijao na mbona hakuna yeyote, isipokuwa tu wachache, hamjaenda maili zaidi kusema, “Je, kuna njia ingine ya kumtumia hizi pesa?”
Sasa Ninazungumza na wale ambao Niliwaambia watoe na hela zao zikarudishwa. Sasa mtatoa tena, kwa kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, wote watamjazia mali hadi kifuani. Kwa kuwa ni MIMI, YAHUVEH, Niliotoa amri kuwa utakuwa msaidizi na wakati mlango mmoja unafungwa, tafuta kujua kama kuna njia nyingine kwa kuwa unajua maneno haya yanayotolewa ni ya KWANGU.
Wajua kuwa huduma hii ni ya ‘Hatimaye ya Mara ya Mwisho.’ Mnapokuwa baraka kwa huduma hii, pia MIMI Nitakuwa baraka kwako. Kwa nyinyi ambao ni laana kwa huduma hii, ambao mmesikiliza na hamjafanya chochote kusaidia, mmekula, mkanona kiroho na bado hamjasaidia. Nazungumza sasa ujumbe huu, mtawajibika.
Kuna njia zaidi ya moja kumtumia hela. Mnawaona kwa nchi geni. Mnawaona wakifanya yale ambayo mlifaa kufanya. Lakini hamkutaka kutoa faraja ya nyumba zenu, na za familia zenu, kwa hivyo Nikainua mwingine. Hamjui na hata hamuezi kuelewa gharama wanayolipa kwa upako unaosikia leo.
Sababu ya pekee kuwa sijamtuma mwana WANGU YAHUSHUA kuja bado kuwachukua Bibi Arusi WAKE, ni kuna vitu bado lazima zifanyike. Bado kuna kazi ya kufanywa. Ndio sababu nguvu zilizomo, serikali ya Marekani, wanataka kutoa huduma hii kwenye mtandao, kufinyilia hela. Lakini mahali mlango mmoja unafunga, Nafungua nyingine. Je, Ni wangapi watasikia na wangapi watasikiliza? Ni wangapi ambao humtumia barua pepe na hawakomi tu kwa barua moja lakini wanaendelea kuzituma mpaka wamfikie na kusema, “Lazima nikusaidie, Nina amri kukusaidia.
[Barua pepe nyingi zilizotumwa kwetu zimeibwa. Endeleeni kutuandikia hadi msikie kutoka kwetu.]
Waona, huduma hii ni ya wale watakatifu wote. Haibebi jina la mwanamume, au mwanamke. Haya maneno sio yake. Upako huu sio kama mwingine. Kama wataka kupata upako huu pia, kama wataka kupata baraka hizi pia, kama wataka kujua kwamba umelindwa kama Ninavyomlinda yeye na Bibi Arusi wengine, basi msiendelee kusimama kando mkizubaa. Kwa kuwa makanisa ya babiloni ni washerati; wamechukua hali ya msamaha wa kodi. Wamekubali kunyamazishwa. Wanakataa kuzungumza juu ya kuavya mimba, ushoga, wanakataa kuzungumza dhidi ya serikali zao zinazofanya, lakini sio huduma hii. Hakuna bei juu yake, kwa kuwa ni ya Mbinguni na ni nani atajaribu kunyamazisha MIMI, YAHUVEH? Je, Ni nani atajaribu kunyamazisha MWANA WANGU YAHUSHUA? Je, Ni nani atajaribu kunyamazisha RUACH HA KODESH? Kwa kweli mtalipa.
Si Neno LANGU husema, “Unapotoa maji ya kunywa kwa nabii utapata zawadi ya nabii?” Ninamsababisha kumwaga Maji ya Uzima. Na ni wachache sana ambao hurudisha kwake. Wanailipia (gharama ya huduma), na gharama hushinda ikipanda. Ni wachache sana wanaojali? Kwa hivyo, Ninazungumza kupitia kwake.
Na wakati uu huu pia, Ninawaonya maadui. Pia Ninatoa baraka kwa wote ambao ni baraka kwa huduma hii na wote ambao humfunika kwa maombi na wanaofunika huduma hii na wanaoenda maili zaidi. Ujumbe kwa Watakatifu, ujumbe kwa Bibi Arusi WANGU, kwa kuwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA ni Bibi Arusi wa YAHUVEH, furahieni! Mpo siku moja karibu na kukuja KWAKE. Mpo siku moja karibu na kukuja kwa YAHUSHUA! Mpo siku moja na Mbinguni, nyumbani kwenu, na makuu, makuu, makuu yatakuwa zawadi zenu kwa yote mliotoa.
Ninatamka baraka ZANGU kwa waaminifu, kwa wale wanaokataa kupuuza ukweli. Hamna chochote ambacho umepitia kitapotea, au bure. Kumbukeni haya, Bibi Arusi, mnahitaji kila mmoja, kwa hivyo msitingize vichwa vyenu na kusema, “O, Sijaweza kupata mahali pa kutoa.” Enda maili zaidi. Pitia mlango ulio wazi. Mtumie barua pepe. Bisha mlangoni mwa Mbinguni kwa kuwa vitabu vinachapishwa. Vingine vinaandikwa sasa hivi na vitabu hivi vitapeanwa (na wengine) wakati wa Dhiki Kuu. Ulizeni mnaweza saidia vipi kwa kuwa gharama za kuchapisha ni kuu.
Je, Ni wangapi wanajali gharama ya kuishi inayotumika kuenda Ninaposema enda na kufanya Ninachosema kifanywe? Ninaweza kuimwaga kutoka Mbinguni, hela, lakini haya yatakuwa baraka kwenu kivipi? Mavuno ni makuu sana na wafanyikazi wachache. Wale na masikio ya kiroho kusikiliza jua Ninazungumza nanyi. Nyinyi wengine-nyinyi ni maadui WANGU, mbaki viziwi. Hakuna sehemu ya ujumbe huu isipokuwa ya hukumu, ambayo ni ya kwenu.
* * * * * * *
[Neno hili lifuatalo lilipeanwa usiku ufuatao wa Oktoba 17, 2006 baada ya mfumo wa kengele uliacha kufanya kazi na wanawake walikuwa kwa maombi. Esnart ni mjakazi anayefanya uchawi na huja kwa nyumba mara mbili kwa wiki kuosha nguo kwa gereji.]
* * * * * * *
Nimekupa ulimi wa shujaa usio kama mwingine. Unapozungumza Neno LANGU katika lugha YANGU, hauisemi tu katika lugha moja, unaizungumza katika lugha nyingi. Ninajua mahali maadui walipo. Ninajua ni nchi gani wapo na ndimi hii huwakata na usahihi.
Katherine, unanipa MIMI heshima Unapochukua wakati kufanya unachofanya (kuandika Ndimi Takatifu). Ili Nikuonyeshe vile mambo haya ni kweli na yale ambayo hayawezi kutafsiriwa ni ndimi za malaika. Hii ni ulinzi ulioongezwa. Kama mngeweza kuona ni maadui wangapi waliozunguka dunia hii, mngeshangaa. O’, lakini Ninasimama mbele ya maadui. Ninasimama kati ya maadui na Bibi Arusi WANGU. Lazima wapite KWANGU ili wawafikie, na ni nani wanaoweza kupitia KWANGU?
[Elisheva Anaomba: Takatifu, Takatifu, Takatifu, Takatifu, Takatifu, Takatifu, Takatifu.] [Katika kinaza sauti Katherine anauliza kama tutaona kifo cha Esnart. Elisheva anauliza, ni yeye amesababisha (nguvu za usalama kuenda) au sio Baba YAHUVEH? Amekata kengele yetu.]
Usiku huu sikuwapa [nyote katika nyumba hiyo] amani ya kulala, na Ninakuonya Elisheva, katika ndoto yako. Katherine [Kathrynyah], yule ambaye anaashiria amani, ulinzi na upendo aliingia chumbani mwako kukuonyesha kuwa kila kitu kitakuwa sawa. Je, Wafikiria kuwa ulikuwa unafanya kazi kwa ndimi hiyo kuu ya vita kwa bahati, usiku ule ule haya yote yalifanyika? Haikuwa kwa bahati.
Elisheva, ni ukweli kuwa Nimebadilisha ndimi yako kwa ile ya shujaa mkuu zaidi. Kila wakati unapoomba, wakati maovu yanajaribu kuingia kwa nyumba yako, hata maombi ya vita inaiweka nje, kwa kuwa ipo katika upako WANGU.
Katherine, ulizungumza maneno haya tena na tena na tena, uliyasikia tena na tena na tena, yaliingia ndani ya roho yako. Ni kama ngome ilipandishwa, na maovu hayakuweza kuingia ndani. Nimeaibisha adui usiku huu. MIMI ni usahihi, MIMI ni kamili. Ole kwa yeyote anayejaribu kuwaguza Watoto WANGU. Ole kwa yeyote anayejaribu kuwaumiza Manabii WANGU. Wanaweza kujaribu mara moja lakini hawataishi kujaribu tena.
Hamjui ni wangapi Nimewaua kwa ajili yako. Mahali fulani wakiwa katikati ya kumuita shetani kwa uharibifu wako, Elisheva, walishika nyoyo zao na kufa walipokuwa katikati ya ombi hilo. Mahali fulani katika dunia isiyoonekana, walipokuja kukushambulia, kitu ya mwisho waliyoisikia ni ndimi hii, nafsi zao zikipelekwa jehanamu, lakini miili yao ipo sakafuni katika nchi nyingine. Wengine walipotea na hawatawahi kupatikana.
Njia zangu ni kuu kushinda njia zenu. Hamuezi hata kuanza kuelewa ni nini Ninachosema. Akili zenu haziwezi kuyaelewa yote. Hata sasa mnasumbuka na mnataka kujua zaidi. Sio ya kwenu kujua. Ni ya kwenu kuelewa. Jueni tu MIMI ni YAHUVEH na itakuwa vilevile, kwa usahihi Nilivyoipanga.
Hata maadui wanaingia katika mtego WANGU. Kwa kuwa Ninasema, “Ndio hawa, njoo na mwashike.” Je, hamjui kuwa Nilijua mbeleni kuwa hiyo kengele itazimwa? Kwani siwezi kuwachunga wale ambao ni WANGU? Ndio, ni vizuri hamjalala. Ni vizuri kujua kuwa mko makini, kwa kuwa adui anawatazama kwa mbali. Wanajua hawawezi kuja karibu na Malaika WANGU watakatifu wanawachunga. Tazameni Esnart, msimuone hivyo tu, kwa kuwa maovu huingia kisirisiri. Mmekuwa na heshima sana, anapotaka kuwaguza na kwa haraka mnajipaka mafuta ya upako juu yenu. Lakini kutoka sasa, mjulishe kwa uwazi, kuwa mmemruhusu kuwaguza mpaka sasa kwa kuwa hamkutaka kumkwaza lakini hakuna yeyote anayeruhusiwa kuwaguza bila ruhusa yenu. Ninawapa amri hii kwa kuwa Nimewafunika mara kwa mara.
Sasa zungumzeni na kumjulisha. Atapata ujumbe na hatataka kuifanya tena mara ya pili. Kuna njia ya kuisema na mtajua ni kwa sauti gani ya kuzungumza, kwa kuwa yeye ni kama kifo kinachotembea. Lakini mtamjulisha, hakuna yeyote anayewaguza bila ruhusa yenu. Haya ni kwa kila mmoja wenu. Ni lazima mjue ni roho gani mnayoguza. Je, Si Neno LANGU husema, “Msiweke mikono yenu juu ya mtu ghafla?” Sanasana hapa Afrika, chukueni haya kwa uzito.
Mwisho wa neno iliyopewa Oktoba 17, 2006.
* * * * * * *
Hili ni neno la onyo kwa maadui wa YAHUVEH. YAHUVEH Aliingilia kati na Akawafukuza maadui. SIFA kwake YAHUVEH na YAHUSHUA! Mambo haya ni ya kweli watu, yachukueni kwa uzito!
Bibi Arusi wa YAHUSHUA wataanza sasa kuona maadui wao wakianguka na mnaweza kuona adui akianguka na macho yako, lakini kuwa na imani YAHUVEH na YAHUSHUA wanapolipiza kisasi kwa niaba yetu.
Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!