Unabii 87
Israeli, O Israeli, Sikieni O Israeli, Yerusalemu Na Dunia Nzima, Nini MIMI, YAHUVEH, Ninalosema!
Imepewa kwake Mtume Elisheva Eliyahu Agosti 27, 2006
Haya ni kutoka Unabii 105, YAHUVEH Alisema kuweka haya kwa Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)
Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya kila Unabii:
2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”
* * * * * * *
Sh’ma Yisrael Kumbukumbu la Torati 6:4
“Sikieni O Israeli, Bwana ni Elohim YAHUVEH, Bwana ni Mmoja, Baraka ni kwa Ufalme WAKE wenye Utukufu milele na milele.
* * * * * * *
UNABII UNAANZA
Sikieni O Israeli Wapendwa, Yerusalemu na Dunia nzima. Je, hamuezi kusikia Muumbaji wenu akilia jinsi mlivyopotea njia mbali na Utakatifu WANGU? Hamuezi kusema kuwa hamjui ni nini sawa na mbaya kwa kuwa o Israeli na Yerusalemu si Niliandika Torati YANGU kwenye nyoyo zenu na si Niliamuru kufunza amri za Torati kwa watoto wenu? Je, Nyinyi sio mbegu ya Abrahamu, Isaka na Yakobo? Je, hamjajifunza chochote kutoka kwake Mfalme Daudi na kwa Yoshua? Kisingizio chenu ni nini?
Je, mna defense gani kuruhusu machukizo kama ajenda ya ushoga inayosukumwa kwa vijana wenu kuwaharibu? Mbona mnakaribisha ninachoita machukizo na kejeli ya ndoa? Je, mnajifanya hamjui Tanakh YANGU? Hamuelewi kuwa mnaleta aibu kwa yote yaliyo Takatifu kwa kuruhusu uchafu huu kuingia katika pale palipoitwa hapo zamani Mji Mtakatifu?
Kwa nyinyi mlio Israeli na Yerusalemu mnaolia kwa maovu yaliyoletwa kule Israeli na mmefanya vile iwezekanavyo kupinga, jueni kuwa Nitawatoza katika kile kiwango ambacho mlipinga pepo hii ya ushoga na pepo ya Molech inayoitwa kuavya mimba. Kwa nini o Israeli, shujaa wenu wanawake wanaua watoto wao wasio na hatia katika tumbo zao badala ya kubaki bikira? Je, hamuelewi kuwa sitawabariki mpaka mtii na kutubu na kuacha njia zenu ovu na muwe Takatifu kwa MIMI, YAHUVEH?
O Israeli na Yerusalemu, wapi hofu, kutii, heshima na Utakatifu ambayo baba zenu Musa, Abrahamu, Isaka, Yakobo, Yosefu, Daudi na Yoshua walikuwa nayo? Niendelee? O wanaume wa Israeli, mbona Mnafikiria kuwa nguvu ya jeshi lenu linawafanya kuwa shujaa? Je, hamuelewi kuwa utakatifu wenu kupitia MWANA WANGU YAHUSHUA ndio itakayonifanya MIMI kupigana kwenye vita zenu na mtashinda?
O Wanawake wa Israeli na Yerusalemu, wapi vyombo Vitakatifu wanaoogopa MIMI, YAHUVEH, kushinda mnavyoogopa ni nini wanaume wanasema? Wapi wanawake wa Israeli na Utakatifu na kutii na imani kama Sarai, Debora, Ruth, Esta au Miriamu? Mbona pepo za Delila na Yezebeli zimeruhusiwa kuchafua kile ambacho kinafaa kuwa Kitakatifu? Je, hamjui kuwa mmoja wa Mashihidi WANGU Wawili watakuwa na roho kama ya Debora ambaye alikuwa Jaji wa Israeli nzima.
Mnaweza kuthubutu kuniuliza MIMI kubariki Israeli na Yerusalemu mpaka msimamie Utakatifu? Hamuezi kuona kuwa MIMI nina haki kwa njia zote; MIMI ni mkuu kwa upendo na kwa vita. Ninabariki wale ambao hutii MIMI, YAHUVEH, na Ninawalaani wale ambao wanatotii. Hamuezi kuona imeandikwa katika Torati yenu na Tanakh kuwa kuna upako takatifu katika Jina LANGU ambalo ni YAHUVEH? Je, si Neno LANGU katika Zaburi 91 lasema “Nitamueka juu kwa sababu anajua Jina LANGU?” Mbona hamusomi na kuhesabu ni mara ngapi Nimenena baraka juu ya wale wanaotumia Jina LANGU TAKATIFU LA KIEBRANIA? Mbona mmeruhusu Marabi kuiba baraka hii kutoka kwenu? Vitu havikuwa hivi hapo awali. Ni Baba mgani aliye na upendo huficha jina lake kutoka kwa mtoto wake?
Jina LANGU ni YAHUVEH na haijalishi KWANGU vile mtakavyoinena bali tu mtambue Jina LANGU ina YAH ndani yake na pia MWANA WANGU MASIHI wa kipekee Jina lake ni YAHUSHUA. Haijalishi mtakavyoinena bali tu muweke Jina LANGU YAH ndani yake. Jina letu sio tu cheo kama HaShem au Bwana, au Adonai. Jina LANGU ni jina juu ya majina yote na ni YAHUVEH. Chukueni kile ambacho Marabi wamewaibia. Mnakosea Jina LANGU heshima mnapoitamka kama G-D au kuifupisha kama YHVH au YHWH kwa kuwa mnazitamka vipi? Nyinyi mna jina, ni nini kinawafanya mfikirie kuwa MIMI Muumbaji wenu sina jina? Mnapoomba niiteni MIMI kwa Jina LANGU, YAHUVEH. Wale walio na masikio ya kiroho watasikia na wengine watabaki viziwi.
O Israeli, mbona hamtii amri zilizopewa kwenu nyinyi kule Mlimani Sinai. Je, si Niliwatenga kwa utukufu WANGU? Si Niliwalinda kwa upendo kutokana na vipigo na laana zilizowajia adui zenu? Si niliwavusha salama salmini kule kwa Bahari ya Shamu kwa kuigawa na kuwazamisha majini maadui wenu Wanamisri? Mnathubutu hata kuhesabu ni miujiza ngapi nimefanya kwa sababu yenu? O Israeli na Yerusalemu, Mnafikiria Ninapenda kuwapiga ili mnisikie. Hakuna nchi kama yenu katika dunia hii. Nimewabariki sana, lakini mmenibariki na kunitii MIMI Muumbaji wenu? Rudini KWANGU o Israeli ili niweze tena kuwabariki zaidi. Siwezi kubariki yeyote aliye katika uasi. Chagueni siku hii ni Elohim mgani mtamtumikia!
O Israeli, moyo WANGU umehuzunika, MIMI ni YAHUVEH, MIMI ni Elohimu wa Israeli hata kama mmekuwa kama bibi wa uasi. Mnafanya kinyume na kile Nilichowaamuru baba zenu wa kale Musa, Abrahamu, Isaka, Yakobo, Daudi na Yoshua ambao waliweka mapenzi YANGU kwanza kuzitii amri ZANGU zilizopewa kwa Musa pale Mlimani Sinai. Mfalme wenu Daudi alikuwa na ushindi katika vita, pia Yoshua kwa ajili alijua ya kwamba sio kwa uwezo, wala kwa Nambari na nguvu za mashujaa wao au silaha. Ushindi ulikuja kwa sababu waliweka mapenzi YANGU MIMI, YAHUVEH kwanza. Walikuja KWANGU na nyoyo za kutubu, kufunga, na maombi yaliyo na upako, ibada na sifa. Walijua ya kwamba maadui wao wamewekwa kwenye mikono YANGU. Walijua wametumika kupigana katika hizo vita lakini ilikuwa ni MIMI, YAHUVEH, Niliyeshinda hizo vita kwa Sifa, Heshima na Utukufu WANGU pekee!
O Israeli, mna haki ya kujikinga lakini kwa aibu yenu, hamtegemei tena mikono YANGU ya vita. Mtazungukwa upande zote kwa sababu mnategemea yudasi anayeitwa Marekani kwa kuwa Mkono wenu. Lazima muelewe MIMI ni YAHUVEH na sitakejeliwa hata na Israeli. Ndio, Nilitengeneza agano na Abrahamu kuwalinda na kuwabariki Israeli lakini kwanza lazima muwe baraka KWANGU. Lazima mfanye sehemu yenu na kunitii MIMI kabla ya kutembea katika baraka za Kumbukumbu la Torati 28.
MIMI, YAHUVEH, Nabariki wale ambao ni baraka KWANGU MIMI, YAHUVEH, na YAHUSHUA. Siwezi kuwabariki waasi. Lazima Niwaadhibu wale Ninaowapenda au siwezi kusema kuwa Ninawapenda. Nina huzuni kwa yale Nitakayolazimishwa kufanya kwa kuwa ni wachache hapa Israeli watakaookolewa. O Israeli, mnaadhibu maadui wenu zaidi ya yale Niliopanga, kwa kuwa Mnasahau kuwa Abrahamu yupo mbele ya uso WANGU akinikumbusha MIMI kuwa maadui wenu pia ni mbegu ya Abrahamu kupitia Ishmaeli. Mnakataa Damu Inayookoa ya MWANANGU YAHUSHUA iliyoloweka kwenye mchanga wa Israeli, kama wao wanavyofanya.
Hata miaka elfu baadaye tone moja la Damu ya YAHUSHUA Inayookoa imefunika dunia yote, lakini mnakataa kukubali zawadi Niliowapa kama Dhabihu yenu ya Damu, zaidi ya dhabihu ya damu ya mnyama. Sikukubali tu MWANANGU mpendwa YAHUSHUA kusulubishwa kwa dhambi za dunia hii na kufa na kuzikwa katika wafu. Nilimfufua YAHUSHUA kutoka kwa kifo kama ishara kwa Israeli, kuwa kuna maisha baada ya kifo lakini MIMI, YAHUVEH, Nilichagua Yerusalemu kwa YAHUSHUA kufa na kuzikwa kwa mchanga wenu na kufufuka tena. O Yerusalemu, wakati unawadia ambapo dunia itasema, “Mtakufa na hamtafufuka tena” lakini wakati Israeli WATAKAPOTUBU, na kutii, Nitafufua Israeli tena.
Sikieni o Israeli, Yerusalemu na Dunia nzima. MIMI, YAHUVEH, Niliyafanya haya kwa sababu zaidi ya moja. YAHUSHUA Anaashiria miujiza wa kuzaliwa kwenu kama taifa kama vile YAHUSHUA Ametengwa kwa utukufu WANGU. Israeli mlipaswa kujitenga kuniletea MIMI, YAHUVEH, Utukufu sanasana katika nyakati hizi za mwisho. Nilimwaga Maji ya Uzima kupitia ukuta wenu wa kuomboleza inayoashiria machozi ya YAHUSHUA alipokuwa pale Bustani ya Gethsemane. Alililia Yerusalemu na Israeli kama MIMI, YAHUVEH, Ninavofanya sasa.
Sikieni Israeli, Ninawatayarisha Mashahidi WANGU Wawili wanaoishi hapa duniani na ambao watanyakuliwa Mbinguni na kurudi tena wakiwa wana Nguvu mpya za upako kutoka Mbinguni na Mwili wa Utukufu, ambao hautazuiliwa na vifungo vya mwili wa nyama. Mashahidi WANGU Wawili watakuja kwenu tena na ishara, maajabu na miujiza wakitamka Jina LANGU MIMI, YAHUVEH na Utukufu na Jina la Mfalme wa Amani ambaye ni MASIHI wa pekee, YAHUSHUA. Mashahidi WANGU Wawili watakuja tena kuwakemea nyinyi Israeli na kuwaonya mtubu.
Sikieni o Israeli na Yerusalemu, kwa sababu mlikataa Damu ya YAHUSHUA pale Kalivari kuosha dhambi zenu zote, sasa mtakuwa na damu imejaa mpaka kwenye uso ya farasi na itatiririka kwenye ardhi yenu. (Ufunuo 14:20)
Siizeni Israeli na Yerusalemu, Yakobo alipigana NAMI, YAHUVEH, na kwa sababu ya haya akawa kilema na kutembea akichechemea (Mwanzo 32:24-26). Mmekuwa mkipigana NAMI o Israeli na mtakuwa vilema, hamtajua amani ya kweli mpaka mtakapolia BARAKA KWA YULE AJAYE KATIKA Jina LA YAHUSHUA MASIHI! Alafu mtabarikiwa kweli na zaidi ya ndoto zenu au mtakachouliza.
YAHUSHUA Alifungua macho ya vipofu na magamba yakaangua kutoka kwa macho yao na wakamsifu YAHUSHUA kwa kuona kwao wakimpa Sifa na Utukufu KWANGU MIMI, YAHUVEH. Lakini nyinyi Israeli na Yerusalemu, mmekataa hii miujiza zimetoka mbinguni na sasa nyinyi ni vipofu na mna magamba kwenye macho yenu na ndio sababu mtadanganywa na mwana wa shetani ambao wengine humuita mpinga kristo kwa miaka mitatu na nusu mtadanganywa na kuamini amani ya uongo.
YAHUSHUA MASIHI Alithibitisha kuwa YEYE ni MWANA wa MIMI, YAHUVEH, Alipofanya ishara, maajabu na miujiza kote Yerusalemu na Israeli. Lakini mlimtesa YEYE kwa haya na kuita miujiza hiyo, kazi za shetani. Katika Dhiki Kuu mwana wa shetani (mpinga kristo) atakuja kwenu na kuwadanganya na ishara, maajabu na miujiza bandia kwa sababu mlikataa ya kweli, mtadangaynywa na ishara, maajabu na miujiza bandia. (Ufunuo 13:11)
Mashahidi WANGU Wawili watahubiri tena kama YAHUHUSHA Alivyofanya. Vivuli vya Mashahidi WANGU Wawili vitaponya, kurejesha na kuokoa na hata Watakatifu waliouwawa watafufuka. Chakula kitaongezeka mara elfu kama ile mikate na samaki ilivyokuwa wakati YAHUSHUA Aliomba. Yale yaliyofanywa hapo mwanzoni yatafanywa tena pale Yerusalemu na kwa yeyote au popote Mashahidi WANGU Wawili watatumwa na kupokewa na kuaminiwa, miujiza hii itafanywa katika Jina la YAHUSHUA tena. Watahubiri kama YAHUSHUA Alivyofanya na kuita hukumu juu ya mafarisayo. Kama YAHUSHUA Alivyotolewa, Mashahidi WANGU Wawili watajitoa wenyewe na kuuwawa lakini siku tatu na nusu baadaye watafufuka kutoka kwa kifo kama ishara kuwa YAHUSHUA ANAISHI na HUONGOZA na HUTAWALA kutoka Mbinguni na YEYE kwa kweli ni MWANA wa MIMI, YAHUVEH. (Ufunuo 11:3-13)
Sikieni o Israeli, Yerusalemu na Dunia nzima, kama YAHUSHUA Alivyoogopwa na wapagani, kudharauliwa, kukejeliwa, kuchukiwa, kuteswa na mipango ya kumchukua maisha YAKE iliyofeli, pia Mashahidi WANGU Wawili watateseka vivyo hivyo. Kama YAHUSHUA Alivyolaani mtini usio na matunda na ukanyauka na kufa kwa sababu haukuzaa matunda, vilevile Mashahidi WANGU Wawili watalaani kazi za uovu na dhambi za binadamu. (Mathayo 21:18-20) Ule mtini usio na matunda unaoashiria wapagani, binadamu pia watanyauka na kufa Maneno ya Moto yanapotoka mdomoni mwa Mashahidi WANGU Wawili. Maadui wanachukia YAHUSHUA, Utakatifu na Mashahidi WANGU Wawili na itakuwa kama nyakati za Eliya wa Zamani (Katika Kiebrania, Eliyahu) na maadui WANGU wataangamia kwa moto.
Sikieni o Israeli, Yerusalemu na Dunia nzima, kama YAHUSHUA Alivyomkuta yule mwanamke pale kisimani samaria na kumpa Maji ya Uzima kisimani na akapokea ukweli na kurudi kwenye mji wake na kuwapa habari njema na akawapa wengine maji ya uzima ya ukweli. (Yohana 4) Kama YAHUSHUA Alivyosema kwa yule mwanamke pale kisimani aende na kunywa hayo Maji ya Uzima na hatawahi kupata kiu tena. MWANA WANGU YAHUSHUA ni Chemchemi ya Maisha, YAHUSHUA Ndiye Kisima cha maji ya Uzima na hakuna yeyote Anayeweza kuja kwa MIMI, YAHUVEH, bila kunywa kutoka kwa Chemchemi ya Maisha na bila kukubali Dhabihu ya Damu pale Kalivari.
Sikieni o Israeli, Yerusalemu na Dunia nzima, Ninatuma Maji ya Uzima tena na tena kupitia vyombo VYANGU venye upako lakini mmetupa maji ya Uzima kwa nyuso zao. Mmewatesa, kuwachapa, kuwafukuza, kuwafunga gerezani na kuwaua Manabii WANGU. Kwa sababu hii Nitatuma Mashahidi WANGU Wawili Yerusalemu na watatabiri dhidi ya maovu yenu o Israeli mliofanya, mnayofanya na mtakayofanya. Mashahidi WANGU Wawili watafunga anga na hakuna mvua yoyote itakayoanguka kwa sababu mnakataa na kukataa Maji ya uzima kutoka YAHUSHUA. Mashahidi WANGU Wawili wataachilia laana za Kumbukumbu la Torati 28 kwa wale wanaototii na kwa wale wanaokana uungu wa MWANA WANGU Mpendwa YAHUSHUA. Ghadhabu ZANGU zitaangukia yeyote anayelaani Jina la YAHUSHUA. Ghadhabu ZANGU zisizo na kipimo zitaangamiza kila mtu anayebeba alama ya mnyama na kuabudu mnyama. (Ufunuo 13:16-18)
Sikieni o Israeli, Yerusalemu na Dunia nzima, kwa sababu mnakataa kusikiza manabii WANGU Watakatifu na walio na upako na kunitumikia MIMI, YAHUVEH, Ninawatuma hawa Mashahidi WANGU Wawili ambao watakuwa na upako wa Musa na Eliya wa Kale (Katika Kiebrania Eliyahu). Watatumwa kumtesa yule aitwaye mpinga kristo ambaye ni mwana wa shetani, nabii bandia na watumishi wake wote wanaobeba alama ya mnyama kama vile Musa alitumiwa kumtesa Farao muovu, pia Nitawatumia Mashahidi WANGU Wawili.
Kama Musa alivyotamka laana na hukumu juu ya Wanamisri akithibitisha nguvu ya MIMI, YAHUVEH, itakuwa vivyo hivyo tena, kama vile Musa alivyogawa Bahari ya Shamu ili Wanaisraeli waweze kupita kuwaepuka maadui wao, itakuwa vivyo hivyo tena. Ni mabaki waaminifu ambao wataokolewa kule Israeli na kwa sababu walirudi kwa Utakatifu wakiziweka kwanza amri MIMI, YAHUVEH, Nilizoziandika na mkono WANGU wa mamalaka na wamekubali na kumuabudu MWANA WANGU YAHUSHUA kama MASIHI wao na kutubu dhambi zao. Nitawalinda wale tu wanaobariki Jina la YAHUSHUA. Alizaliwa kwenye dunia hii kutoka kwa mwanamke bikira Muebrania bila mbegu ya mwanamume. Akithibitisha YAHUSHUA ni MWANA wa pekee wa YAHUVEH Aliyetumwa duniani na Maneno YANGU na mamlaka. YAHUSHUA Ndiye Torati ya uhai na mlimkataa o Israeli, mnapomkataa YEYE mnanikataa MIMI, YAHUVEH. Nilimtuma YAHUSHUA kwanza kwa Wayahudi alafu kwa Mataifa kuonyesha Mamlaka YANGU na Utukufu.
Nitawatuma Mashahidi WANGU Wawili mmoja mwanamume na mmoja mwanamke kuonyesha mamlaka YANGU MIMI, YAHUVEH na kuita chini hukumu za YAHUVEH na laana na kuongea maneno yenye upako na kuonyesha Nguvu katika Majina matakatifu ya MIMI, YAHUVEH, na YAHUSHUA. Sikilizeni kwa makini na sikieni o Israeli na Yerusalemu, sitabariki Israeli mpaka mbariki Majina ya YAHUVEH na YAHUSHUA na mpaka mbariki Wale Watakatifu wanaokuja na kuwahubiria kwa Majina yetu.
Sikieni o Israeli, Yerusalemu na watu wa ulimwengu, kuna njia moja tu ya kurudi Mbinguni na ni kupitia Dhabihu Takatifu iliyopewa kwa ulimwengu huu inayofunika dhambi za watu na ni kupitia Jina na Damu ya YAHUSHUA. Lazima mmkubali kama MWANA wa Pekee WANGU MIMI, YAHUVEH na dhambi zenu zitasamehewa na kuoshwa kupitia Damu ya kuokoa ya YAHUSHUA lakini lazima mtubu na kuachana na dhambi zenu na kutii. (Yohana 14:6)
Sikieni o Israeli, huu ndio ujumbe Mashahidi WANGU Wawili watazungumza. Maadui wowote wa YAHUSHUA ni adui WANGU MIMI, YAHUVEH, na kama hawatatubu hamna msamaha kwa dhambi hii. Jehanamu itakuwa nyumbani kwao.
Sikieni o Israeli, Yerusalemu na Dunia nzima, hakuna damu ya kiufalme hapa duniani ila tu kupitia damu ya YAHUSHUA MASIHI Iliyomwagwa. Ni wale tu majina yao tayari yamo kwenye Kitabu cha Maisha cha mwanakondoo (Ufunuo 17:8) kabla ya msingi wa dunia hii, wanaweza kudai damu ya kiufalme kupitia damu ya kiufalme ya MFALME wa ULIMWENGU, MFALME wa WAFALME, MFALME wa Wayahudi! Wale wengine wanaojiita damu ya kiufalme ya ulimwengu ni bandia na hakuna chochote kifalme ndani yao. Ni Watu WANGU waliounganishwa kupitia damu ya kiufalme ya YAHUSHUA MASIHI ambao ni Kifalme katika macho YAKE. Ni Bibi Arusi wa YAHUSHUA pekee ambao watavikwa taji Mbinguni.
Mashahidi WANGU Wawili ni sehemu ya Bibi Arusi wa YAHUSHUA wa Ufunuo 14. Mwili ambao wataupokea utakuwa Mwili Mtukufu. Kama vile YAHUSHUA Alivyotembea bila kuonekana katika umati adui alipotafuta kumuua pia Mashahidi WANGU Wawili watafanya vivyo hivyo. (Luke 4:28-30)
Sikizeni o Israeli, Yerusalemu na dunia nzima, vile shetani hakuweza kumueka YAHUSHUA kifoni na katika siku ya tatu YAHUSHUA Alifufuka, vivyo hivyo haijalishi watakachofanya shetani, nabii bandia na mwana wa shetani mpinga kristo, hawawezi kuzuia Ufufuaji wa Mashahidi WANGU Wawili kutoka kifoni siku tatu na nusu baada ya vifo vyao. Shetani hawezi kuzuia watu kote duniani kuona haya na kusikia juu ya haya na kutoa maisha yao na nafsi zao na kumkubali YAHUSHUA kama MASIHI wa kweli, MWANA wa MIMI, YAHUVEH.
Sikieni o Israeli, Yerusalemu na Dunia nzima, kama vile YAHUSHUA Alivyopaa Mbinguni mbele ya Mashahidi vilevile Mashahidi WANGU Wawili watapaa Mbinguni mbele ya Mashahidi wa dunia hii. Kwenye hewa zenu kote duniani, haya yataonekana. Kama ilivyoandikwa na waliokufa katika (Masihi) YAHUSHUA MASIHI Atafufuka kwanza, hii imekuwa siri na imetolewa kupitia huyu nabii tayari. Mashahidi WANGU Wawili pamoja na watoto WANGU wengine Watakatifu waliouwawa wakati uo huo, hawa ndio wale waliokufa watakaofufuka kwanza kuonyesha nguvu ya upako iliyofufua YAHUSHUA kwa mkono WANGU. MIMI, YAHUVEH, Nitafanya haya tena kwa dunia kuona.
Kama ilivyoandikwa, “Wale ambao bado wako hai na wamebaki watanyakuliwa na kukutana na YAHUSHUA hewani,” na hii itawahusu Bibi Arusi wa Ufunuo 7. Wakati wa ushuhuda ni miaka mitatu na nusu iliyoashiriwa katika siku tatu na nusu na miili ya Mashahidi WANGU Wawili itakapokuwa imelala pale bila uhai ingawa Roho zao zitakuwa Mbinguni. Siku tatu na nusu baadaye Roho zao zitaitwa kurudi kwa miili yao kama YAHUSHUA na kufufuka na wengi watainama, kutubu na kuabudu YAHUSHUA kama MWANA WANGU na MASIHI wa ukweli. (Ufunuo 11)
Sikieni o Israeli, Yerusalemu na Dunia nzima, kama ilivyoandikwa, yule mliyemuita Yohana mbatizaji alitengeneza njia kwa MWANA WANGU YAHUSHUA ndivyo itakavyokuwa tena kama Eliya WANGU Mpya (katika Kiebrania, Eliyahu) anatengeneza njia kwa kurudi kwa YAHUSHUA kuongoza na kutawala hapa ulimwenguni kama YEYE Alivyofanya Mbinguni.
Sikieni o Israeli, Yerusalemu na Dunia nzima, Mashahidi WANGU Wawili wanakuja na upako na Roho kama ya Musa lakini pia wanakuja na upako na Roho kama ya Eliya (katika Kiebrania, Eliyahu). Hakuna silaha ambayo itawazuia ikiwa ni ya kiroho, ya mwanadamu, ya kibiologia au ya kemikali. Lakini, silaha yoyote itakayotumika dhidi yao, silaha hiyo itawarudia hao maadui. Hakuna maangamizi ambayo yatawaguza hadi mwisho wa miaka mitatu na minusu ya kuwashuhudia na ni mpaka Nitakaporuhusu wao kuuwawa kwa utukufu WANGU kuthibitisha kuwa Nitawafufua tena katika siku tatu na nusu.
Sikieni o Israeli, Yerusalemu na Dunia nzima, kama vile tu MIMI, YAHUVEH, Nilimpa Eliya wa Kale (katika Kiebrania, Eliyahu) upako wa kuwaangamiza maadui wake na moto vivyo hivyo ndivyo Mashahidi WANGU Wawili watakavyofanya. Vile tu YAHUSHUA Alivyodhibiti na alikuwa na mamlaka juu ya upepo na mawimbi, vivyo hivyo ndivyo Mashahidi WANGU Wawili watakavyofanya. MIMI, YAHUVEH, Nitawapea Mashahidi WANGU Wawili nguvu ya kusafiri kokote duniani. MIMI, YAHUVEH, Nitawapea mamlaka katika dunia hii. MIMI, YAHUVEH, nitawapea mamlaka ya kuwalinda Kondoo na Wanakondoo WANGU Watakatifu, Bibi Arusi wa Ufunuo 7 na kuwahamasisha wageni wa Karamu ya Mwanakondoo walio duniani kwa wakati huu.
Sikieni o Israeli, Yerusalemu na Dunia nzima, vile mtakavyosaga meno yenu kwa hasira o maadui wanaomkataa YAHUSHUA kama MASIHI wa Kweli. Jueni haya, Mashahidi WANGU Wawili hamtaweza kuwaweka nje ya Sinagogi, Hekalu, na Makanisa yenu kama vile tu hamkuweza kumueka YAHUSHUA nje ya Sinagogi zenu katika nyakati za kale. Mashahidi WANGU Wawili watajitokeza kwa maadui wa YAHUSHUA wakionyesha ghadhabu ya YAHUVEH. Mashahidi WANGU Wawili wataingia hadi kwa chumba cha mpinga kristo, wakimtesa katika nyumba yake na katika nyumba ya nabii bandia na yeye pia hataepuka mateso haya ya Mashahidi WANGU Wawili.
Mashahidi WANGU Wawili wataenda kokote na kwa yeyote kama nitakavyowatuma. Hakuna adui yeyote atakayeweza kuwaweka nje au kuwazuia kwa kuwatesa na kumtusi mwana wa shetani na nabii bandia mpaka miaka mitatu na minusu ya kushuhudia iishe. Nitawatuma ndani ya vyumba vyao wanapolala na wanapojaribu kulala na kula. MIMI, YAHUVEH, Nitawatesa maadui kama Musa alivyofanya na hakuna chochote kitakachowazuia, hamna kengele, hamna askari na hamna silaha itakayoshinda dhidi ya Mashahidi WANGU Wawili mpaka miaka mitatu na minusu ya kushuhudia itakapoisha na wakati kazi yao itakapokuwa imekwisha. Adui hakuweza kumzuia YAHUSHUA kwa kuhubiri na kwa watu kukubali ukweli na hakuna yeyote atakayeweza kuwazuia Mashahidi WANGU Wawili.
Sikieni o Israeli, Yerusalemu na dunia nzima, hamkuweza kufunga mdomo wa Yohana Mbatizaji mpaka MIMI, YAHUVEH, Niliiruhusu na kwa sababu kazi yake hapa duniani ya ushuhuda ilikuwa imemalizika. Kama tu vile hamuezi kufunga mdomo wa Mashahidi WANGU Wawili ambao wataendelea kuzungumza na upako kama wa Yohana Mbatizaji. Mashahidi WANGU Wawili watatabiri Hukumu ZANGU na wataita laana chini na kuzungumza juu ya yajayo. Watakemea na jumbe zilizojawa na thibitisho na toba na upako hata zaidi ya Yohana Mbatizaji.
MWANA WANGU hawezi kuja kama Mfalme wa Amani wa Israeli mpaka maovu mengi zifanyike na sio hadi masihi bandia hajaja. Mnapoomba Mfalme wa Amani aje Israeli sasa, hamjui vitisho ambavyo lazima zifanyike kwanza, lakini itafanyika. Tayari imeanza kufanyika. Kwa kuwa gari la moshi limeanzishwa ambalo haliwezi kusimamishwa.
(Elisheva anaonyeshwa ufunuo, Ninaona gari mbili za moshi zikija na hazijui kuwa zitagongana kwa kuwa wako kwa reli moja!)
Ninawaadhibu Israeli kwa sababu Ninawapenda Israeli lakini hizo gari za moshi zitagongana kwa sababu zote ziko kwa reli isio sawa. Bibi Arusi wa YAHUSHUA wanahisi yote yanayofanyika kule nchini Israeli. Kwa kuwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA ndio Israeli ya kiroho. Nchi ya Israeli mtabarikiwa na baraka za Kumbukumbu la Torati 28 mtakaporudi kwa Utakatifu na kuabudu MIMI, YAHUVEH, na njia ya pekee ya kufanya haya ni kumkubali YAHUSHUA kama MASIHI na kukiri YEYE Ndiye Dhabihu ya Damu ya pekee iliyopewa pale Kalivari. Baraka Nilizozihifadhi ni za Israeli ya Kiroho na kwa wale wanaonipenda MIMI, kuniabudu MIMI na kuniweka MIMI kwanza katika upendo wao na katika maisha yao, wale wanaotii Torati YANGU, wale wanaoheshimu utakatifu wa JINA LANGU Takatifu na wale wanaompokea YAHUSHUA kama MASIHI.
Hii ndiyo sababu mna huzuni mnapoona na kuhisi kinachofanyika kule Israeli. Abrahamu yupo mbele ya Uso WANGU kila wakati na husema, “Utafanya nini na watoto wa Ishmaeli, haupendi mbegu ya yule mwana wangu mwingine? Tuma mtumishi wako kwa mbegu yangu na kuwapea nafasi ya kuamini.” Hii ndiyo sababu mnalilia Lebanon kwa kuwa, si wao ni mbegu ya Abrahamu? Nina Israeli ya kiroho ambao wamo kule Lebanon waliomkubali YAHUSHUA kama MASIHI.
Nina Bibi Arusi WANGU wa YAHUSHUA kule Lebanon. Nina Bibi Arusi WANGU kule Iraq na Iran. Nina Bibi Arusi WANGU kule Syria. Kumbukeni kuombea Bibi Arusi wa YAHUSHUA haijalishi wako wapi duniani humu. Nina Bibi Arusi WANGU kule Uchina, nina Bibi Arusi WANGU kule Urusi, nina Bibi Arusi WANGU kule Hong Kong, nina Bibi Arusi WANGU Australia, nina Bibi Arusi WANGU kule Marekani, Canada, Ujerumani, Ufaransa na Ulaya, Ninao kote duniani. Nina Bibi Arusi WANGU kule India, Indonesia, Afrika, Marekani Kusini na kote duniani.
Kwa sababu nchi zenu zimewabandika nchi nyingine adui, msiifanye adui wenu, kwa kuwa serikali nyingi za dunia hii sio za KWANGU. Hawazungumzi kwa niaba YANGU, hawaniheshimu MIMI na hawanitaki MIMI. Maadui wenu ni wale ambao Ninaamuru kuwa ni maadui wako. Mbegu ya shetani ndio maadui wenu. Mbegu ya shetani ni nani, ni yeyote ambaye majina yao HAYAMO katika Kitabu cha Maisha cha Mwanakondoo. Hawajawahi kuwa WANGU walipozaliwa hapa duniani.
(Anaomba kwa sauti ya juu katika Kiingereza Mtakatifu, mtakatifu, Mtakatifu)
O Israeli, o Yerusalemu, Ninawalilia nyinyi. Mna umbo la Utakatifu lakini Utakatifu upo wapi ndani? Mnataka dunia iwaonee huruma, lakini wapi huruma yenu Israeli? Mna haki ya kujilinda lakini mmepita mpaka mnapochukua silaha za kibiologia na kemikali. Mimi sipo katika vita hizo, hamuniiti MIMI, YAHUVEH, kwa usaidizi, mnajaribu kuyafanya haya kwa mikono yenu wenyewe mkitumia silaha za nchi nyingine. Mnapotumia silaha za kibiologia na kemikali mnawaadhibu maadui wenu zaidi ya yale Niliyoruhusu. Jihadharini, kwa kuwa mtavuna kimbunga ya ghadhabu ya MIMI, YAHUVEH kama mnachotuma inarudi usoni mwenu. Mataifa yanayowapea hizi silaha pia watapata hatima sawa.
Nitakapotuma Mashahidi WANGU Wawili, Nitawatuma kwa mbegu wote wa Abrahamu. Nitawatuma sio tu kwa Kabila ya Yuda lakini kwa Wanaisraeli wote, Waarabu na Mataifa watasikia. Watakachozungumza pale Israeli itapeperushwa kwenye hewa na magazeti kote duniani. Nimechagua wakati huu na teknolojia yake, kwa kuwa Maneno YANGU yatasikizwa kote duniani kwa kuwa hamna wakati kama huu.
Shetani ametumia teknolojia kujenga ajenda yake lakini Ninatumia teknolojia kuharakisha ajenda YANGU. O, wapi malalamiko? Wapi mlio na mayowe? Mbona watu wanatingiza tu vichwa vyao na kusema,”haya ni mabaya?” Mbona Israeli ya kiroho haiinuki? Mbona hawaombi kwa kuwa nina mabaki kule Lebanon? Je, hao wangekuwa watoto wenu? Je, hao wangekuwa bibi zenu, bwana zenu, wapendwa wenu, familia zenu na jirani zenu? Je, hizo zingekuwa nyumba zenu? Wazimu umechukua kiti kwenye serikali zenu.
Oh Israeli, o Yeruslaemu, watu wako wanalia na kupiga mayowe, wanakimbia kwa kuchanginyikiwa, Ninawalilia nyote. Itakuwa tu venye MIMI, YAHUSHUA, Nitakuja, ndio kutakuwa na amani kati ya Ndugu, amani kati ya mbegu ya Abrahamu. Mpaka wakati huo, kama ilivyokuwa daima, mtaendelea kujaribu kumalizana. Wakati amani bandia itakapokuja, hasira na chuki bado itakuwepo. Hakuna amani mpaka MFALME WA AMANI AJE (Isaya 9:6) na ni MIMI, YAHUSHUA MASIHI!
* * * * * * *
Imezungumzwa, na imeandikwa na kupewa kwa Mtoto huyu wa YAHUSHUA
Mtume Elisheva Eliyahu tarehe 8/27/06
Kulikuwa na shida ya kibinafsi ambayo ilikuja maishani mwangu adui alipoigonga familia yangu kwa njia tofauti. Hii ilikuwa ili nilisitoe Unabii huu. Unabii huu ulikuja kwangu katika sehemu mbili lakini bado sitatoa sehemu ya pili bado, YAHUVEH Anasema kuwa kuna nyama ya kiroho hapa ya kumeza, yaani, ufunuo kutoka Mbinguni. Sina habari kwa nini neno hili linatolewa kupitia mimi, na maelezo ya kazi ya Mashahidi Wawili.
Kuna gharama ya kulipa kwa nabii kupokea ufunuo kama hizi kutoka Mbinguni, na vita vya kiroho vimezidi kwa wakati huu, lakini tuna USHINDI katika jina la YAHUSHUA.
Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!