Unabii 85

Lieni Kutoka Kwenye Paa za Nyumba. Lieni Kwa Dunia! Bibi Arusi wa Kimataifa wa YAHUSHUA, Njooni!

Imepewa kwake Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu) Mei 5, 2006

Haya ni kutoka Unabii 105, YAHUVEH Alisema kuweka haya kwa Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH Alisema kuongezwe yafuatayo kuonya wale ambao wanakejeli:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

Jambo Familia Wapendwa,

Tunayaandika haya kwa sababu kuna vitu vimetajwa katika unabii na YAHUVEH ambayo hamtaelewa tusipoelezea maneno kadhaa. Kwa sababu hamkuwa tutawaelezea yaliyotokea.

Sisi (Uongozi wa Amightywind) tunawashukuru kila mtu anayetuandikia na kusema wanatufunika kwa maombi, na wengine pia waliongozwa kufunga na hawakujua ni kwa nini. Sasa mnajua kwa nini. Hatuwaambii yeyote ila tu wale wanaoaminika sana mahali tupo hadi tufike pale, au wakati mwingi baada tushaondoka. Hivi, shetani hatakuwa na watu wanaotungoja.

Cha ajabu zaidi ni tulidhani tunaenda nchi nyingine, tukijitayarisha kununua tikiti ya ndege ya nchi nyingine ambapo nabii mwingine anaishi na bado anatungoja. Na mimi, (Elisabeth [Elisheva], niliamka na kusikia, “YAHUVEH Alinizungumzia usingizini na kusema, “Nendeni Uswizi.” Hakuna yeyote kati yetu alijua chochote kuhusu Uswizi na tuliambiwa lazima iwe tikiti ya first class, hata kama hatujawahi kusafiri first class. Nilikuwa na shida za afya kwa hivyo tukafikiria hiyo ndiyo sababu. Sasa tunaelewa umuhimu wa kutii na kununua tikiti ya first class. Kwa sababu utakaposoma hapo chini utaelewa kulikuwa na sababu nyingine na umuhimu wake. Asante kwa wote waliosababisha hii exodus kufanyika.

Unabii huu ulikuja asubuhi wa kwanza baada ya sisi kuwasili Zurich, Uswizi. Ninataka kueleza kuwa Baba YAHUVEH Anataja kuhusu Homeland Security na wakati mgumu tuliokuwa nao kuondoka Marekani. Kwenye uwanja wa ndege wa Seattle, tulikuwa tunatembea kwenye handaki kuingia ndege ya kuenda Zurich.

Njiani, tuliona maafisa wa Homeland wakisimama kwenye handaki kabla ya sisi kuingia kwenye ndege. Afisa alikaa ni kama alikuwa anatungoja sisi, kwa sababu alikuwa anawaruhusu wengine kumpita na akaendelea tu kutuangalia. Alitusimamisha na kutuuliza, “Mnaenda wapi na kwa nini tunaenda kule.” Akaanza kuongea juu ya pesa na kusema kuwa tumeruhusiwa kubeba pesa kiasi fulani kama $10,000 nje ya nchi. Aliuliza tulikuwa na pesa ngapi, na ilikuwa kiwango kikubwa, lakini tulikuwa chini ya kikomo kinachokubalika kisheria. Tulifikiria kwa muda na tukampa takwimu niliyodhani ni sahihi.

Akaanza kusema kuwa kama hatuna uhakika hata kwa dola kadhaa, kuwa Homeland Security itachukua pesa zetu na akatuambia tuweke saini kwenye karatasi fulani na kusema tuna pesa ngapi nasi. Nilikuwa na wasiwasi lakini nikajaribu kuhakikisha kuwa tuna takwimu sahihi. Niliamini kuwa ilikuwa sawa.

Baada ya kujaza ile fomu na kutia saini na nikagundua ni nini kilichokuwa kinafanyika, tulidhani kuwa ni heri tuhesabu kila peni tuliyokuwa nayo kwenye mkoba wangu kwa sababu Homeland Security wanaitaka. Tulipoanza kuhesabu pesa, nilijua tulikuwa shidani kwa kuwa nilikuwa na pesa zaidi na nilyodhania kwa sababu tulipewa pesa za Kanada $500 wakati wa Pasaka na Adam, kwenye Uwanja wa Ndege wa Seattle alipokuwa anatuaga kwaheri, akatupa $500 nyingine kwa dola ya Kanada.

Nilikuwa nikiweka pesa hizi kwenye bahasha na sikuwahi hata kuhesabu. Nilikuwa ninataka kushangaa vile YAHUSHUA Alivyoifanya kuongezeka tutakapowasili kule Uswizi. Kulikuwa na Euros zilizotumwa kwetu kwa zawadi za Pasaka, hata pia pound za Uingereza. Pia nilikuwa nimeweka kwenye boxi ya bati la kijani dola za USA zilizopewa kwetu wakati wa Hanukkah na siku yangu ya kuzaliwa, pia Purim. Niliziweka iwapo tuwe tunahitaji pesa ya dharura. Hesabu yake ilikuwa chini ya $500 tu. Nilikuwa nayo kwenye mkoba wangu lakini nikaisahau kabisa. Kulikuwa na maafisa 7 wakichunguza vitu vyetu vyote na wakitafuta pesa zozote zile walizoweza kupata. Walipokuwa wanachunguza vitu vyetu, afisa aliyeanzisha haya yote akauliza pasipoti zetu na kuangalia kama tulikuwa na shida yoyote na sheria. O, kwenye uso wake hakuwa amefurahia, alipata kuwa hatukuwa na shida yeyote na sheria, hata tikiti ya kuegesha gari! Sifa kwake YAHUSHUA! Tikiti zetu zilinunuliwa na zawadi ya pesa na zilikuwa first class, au tuna uhakika ndege hiyo ingetuacha sisi na hizo tikiti za first class haziwezi kurudishwa. Wengine tayari walikuwa kwenye ndege na kama ndege hiyo ingetuacha, tungekuwa Uropa bila pesa na tungekuwa Seattle pekee yetu. Na kama pesa zetu zingechukuliwa, tungekuwa bila pesa. Hii ilikuwa kionjo tu kwa jinsi vile Homeland Security, ambao tunawaita Polisi Gestapo, walivyowafanyia Wayahudi walipokuwa wanaiba kila kitu walicho nacho. Lakini, YAHUVEH Alikuwa ana udhibiti.

Asubuhi ii hii mapema Niliamka kutoka kwa ndoto na onyo juu ya Homeland Security. Niliamka, nikipiga mayowe na kulia, nikisema “Hatuwezi kupanda ndege hiyo, kutakuwa na shida na serikali yetu. Hawatatuacha tutoke Marekani”

Nilijua YAHUSHUA Alikuwa Anatupa onyo kuhusu kile shetani aliyokuwa anapanga kufanya na lazima tuombe dhidi ya haya sasa ili isifanyike. Tuliomba kwa masaa mengi, tukimkemea shetani, tukipigana kwa vita vya kiroho na kupambana kwenye Kiroho na tukapata amani na kuzungumza neno kutoka kwake YAHUVEH. Alisema, “shetani anajaribu kukutega, lakini hakuna lolote litakachofanyika ambayo sijaruhusu na sitairuhusu. Bahari ya Shamu itafunguka kwako.”

Tena nilipata amani na nikarudi kulala. Kwa hivyo kwa kusema haya, hatuwezi kusema kuwa hatukuambiwa mbele ya wakati juu ya mtego uliowekwa kwetu sisi. Hatukujua huo mtego utakuwa wapi. Sasa, tuliweza kuuona. Nilikuwa ninatingika katika upako wakati huo. Ilikuwa ni unabii huu uliokuwa umefungwa ndani ya mifupa [yangu], kwa kuwa YAHUVEH Alikuwa Amekasirika jinsi tulivyokuwa tunafanyiwa kama wahalifu. Hata hivyo, pesa hizi zilikuwa zetu, hata kama hatukuchukua muda wa kuhesabu kila kitu. Haya yanasikitisha sana kuwa Wamarekani wameruhusu faragha yao kuibwa namna hii. Sisi sio nchi ya uhuru tena na wajasiri kama Unabii 84 unaosema “JIHADHARINI NA UDANGANYIFU.”

Sasa ndege ilikuwa imejaa ila tu sisi na walikuwa wanatungoja ili waende. Walipokuwa wanahesabu pesa zetu, afisa mmoja akawa ameshinda akiuliza mahali tulipotoa pesa hizi, na tulikuwa tunafanya kazi ipi, nk. Tukawaambia kuwa sisi ni wahudumu. Na walipomaliza, tulikuwa na pesa zaidi ya tuliyokuwa tumetaja na wakasema lazima waite mkubwa wao pale, kuona kama watachukua pesa zile. Tulikuwa katika maombi ya ajabu kama mnavyoweza kufikiria sasa.

Kulikuwa na afisa 7 wa Homeland Security wamesimama pale wakijaribu kuamua watafanya nini kwa sababu hawakuweza kumpata mkubwa wao. Alafu mmoja wao akasema, “Acha tuwaachilie na kuamini kuwa hawakujua ni pesa ngapi waliyokuwa nayo na tuwaache waingie kwenye ndege.” Sasa, kama tungekuwa na kiwango kikubwa cha pesa tungeona ni kwa nini haya yalikuwa yanafanyika. Lakini kidogo tu juu ya tuliyokuwa tumeandika chini, ni ujinga.

Tulisema ‘Amina’ kwa hayo, tukafunganya virago vyetu na tukapanda ndege, kamwe kutoona Marekani tena. O ndio, kuna kitu kimoja nimesahau kutaja. Tulikuwa na sarafu za dhahabu kwenye mkoba wangu, zilizopewa kwetu kutoka kwa sehemu ya Bibi Arusi wa Australia anayeitwa John. Alikuwa amezituma mwaka uliopita kwa sababu YAHUSHUA Alimwambia azitume haraka iwapo tutazihitaji kwa pesa za dharura au kwa kubadilishana kwa safari. Huwa hatujui ni nini kitakachofanyika. Niliziweka hizi kwenye mkoba wangu kwenye begi kama la make-up.

Mmoja wa afisa hao alizipata na alikuwa anaziangalia na tulikuwa tunamwangalia na kuomba kwa kimya alipoangalia juu na plastiki iliyokuwa na sarafu ya dhahabu mkononi mwake, na kusema, “Hizi ni nini, zawadi?” Tukasema, “Ndio, waweza kusema hivyo” na tabasamu kubwa usoni mwetu. Tunajua wangeweka kila kitu kama hii dhahabu pia ingehesabiwa, na wangeiweka yote kama YAHUVEH na YAHUSHUA hawangekuwa kwenye kona yetu. Tunajua haya, tulijihisi kama wahalifu kwa sababu ilibidi tuwe na pesa ili tuweze kuenda nchi nyingine, na hata kama Baba yetu wa Mbinguni Alikuwa na udhibiti, bado tulikuwa na wasiwasi. Shetani alikuwa anajaribu kutumia chochote kile alichoweza kutusimamisha kutoka kwa misheni hii ya kuwakusanya Bibi Arusi wa YAHUSHUA na kuleta upako mpya kwa [nchi] tutakazotembelea. Tutakapoenda, ishara, ajabu, na miujiza zinafuata, yote kwa Utukufu wa YAHUVEH na YAHUSHUA MASIHI.

Baada ya tukio hili, tulishinda tukimwuliza YAHUVEH mbona walitutenga sisi tu kwa sababu tulijua tunatafutwa na YEYE Alitupa ndoto hii.

Kwenye ndoto hii, ndugu fulani alikuwa anasimama nyuma ya watu wakiangalia mashine ya x-ray na alikuwa anaangalia skrini. Alafu akajiona yeye mwenyewe akipitia ndani ya mashine hiyo ya x-ray lakini bado alikuwa nyuma ya hawa watu wanaotazama skrini. Skrini ikaanza kuonyesha kiwango sahihi cha pesa aliyokuwa nayo. Na sasa kwa sababu wana mashine hii na wanaweza kuona kwa uwazi kiwango cha pesa ulicho nacho, haya yote yalikuwa tu ni unyanyasaji kwa sababu moja tu kwa sababu Homeland Security ni njia nyingine ya kuchukua uhuru na faragha ya wananchi wa Marekani.

Tunajuta sana kuwa sisi tunaitwa Wamarekani kwa sababu kwa ukweli tulikaribishwa na heshima na haki kwa faragha yetu kule Uropa na ndio, hata Afrika. Homeland Security haina bajeti, ni shimo la fedha lililotengenezwa na Rais Bush na itatumika tena, na inatumika, dhidi ya wananchi wa marekani wasiokuwa na hatia, kuiba, kuua, na kuchukua uhuru zetu na haki yetu ya faragha. Someni hapo chini na oneni vile YAHUVEH Anavyosema juu ya Homeland Security na mashirika mengine katika nchi nyingine wanaofanya vivi hivi lakini chini ya jina tofauti.

Ilibidi tupate mahali salama ili tuweze kutoa unabii huu na zingine ambazo hazijatolewa bado. Pole sana kwa kuwa imechukua muda mrefu, lakini hatukuweza kuyaepuka haya. Tunajua kuwa hata kama tunafikiria kuwa tumechelewa, kwa kweli ni wakati mzuri, kwa sababu ni wakati wake YAHUVEH. Labda tukio hili litamsaidia mtu mwingine.

Kwa kumalizia, tunaamini kwa kweli zawadi hizi za pesa kwa Huduma hii zimepewa na Watu Watakatifu, sanasana zawadi za pesa za Bibi Arusi wa YAHUSHUA na shetani alikomeshwa siku iyo hiyo. Wakati unabii huu unanakiliwa na kupeanwa, tafadhali hakikisha kuwa maelezo yamo ndani ili wengine waelewe.

* * * * * * *

Unabii 85

Lieni Kutoka Kwenye Paa za Nyumba! Lieni Kwa Dunia! Bibi Arusi wa Kimataifa wa YAHUSHUA, Njooni!

Haukujua haya hapo mbeleni, lakini Nilikuonyesha, Elisabeth [Elisheva], kwa maono. Ulipokanyaga Zurich, Uswizi, Nilithibitisha kuwa Niliweza kukutoa Marekani salama. Ingawa haukuvunja sheria, shetani hakuwa anataka utoke kwa sababu hakuwa anataka upako huu uachiliwe na wewe kutembelea nchi zingine. shetani hataki uwakusanye Bibi Arusi wa Kimataifa wa YAHUSHUA.

Hata baada ya yote adui alijaribu kufanya, Mbinguni mzima ilifurahia, Malaika walifurahia, kule Mbinguni mlio wa pembe za shofar ulisikika, kwa kuwa kule Marekani walisema kuwa hakuna chochote kilicho na nguvu kushinda Homeland Security. Lakini Nilithibitisha na Nitathibitisha kwa wote wanaojaribu na kuniamini MIMI, wanaonitii MIMI, wanaojua NGUVU ya Majina YANGU Takatifu. MIMI, YAHUVEH, Naapa ya kwamba: Wale wanaofuata hizi kweli Nilizowapa na kuzungumza katika Huduma hii watakuwa na ushindi uu huu juu ya Homeland Security au kwa jina lingine lile linavyoitwa katika nchi zingine. Kwa kuwa kuna shirika kama hizi zilizowekwa kuwashika wahalifu lakini pia wale wasio na hatia.

Na katika siku zijazo za giza, itakuwa ni Watakatifu ambao watasakwa. Kama vile Nilivyowaonyesha kuwa hakuna nguvu zaidi kushinda MIMI, “MIMI NIKO” Mkuu mnapokuja KWANGU katika Jina la YAHUSHUA MASIHI, Nitafungua Bahari ya Shamu. Nitawakomesha wale wanaojaribu na kuwasaka. Nyinyi ambao ni Watakatifu WANGU mnaolia katika jina la YAHUSHUA MASIHI kama vile nyakati za kale, Nitawakomboa.

Kwa hivyo mwaona Watoto WANGU, kulikuwa na sababu nyingine Nilikutuma kule Uropa na ni kuthibitisha Nitakapofungua Bahari ya Shamu wale wengine pia watapita. O Marekani, mnaweka ulinzi wenu katika kitu kinachoitwa Homeland? Nitawaonyesha, Homeland Security, kuwa mpo tu kwa sababu ya kitu kimoja na ni hiki, uharibifu wa MIMI, YAHUVEH. MIMI, YAHUVEH, Ninazungumza haya sasa. Mnajaribu kuwazuia Watoto WANGU, mnajaribu na kuwachelewesha Watoto WANGU, Nasema hapana. Mlikuwa mnajaribu kufanya waachwe na lile ndege. Mlikuwa mnataka kuwaibia Watoto WANGU, mlikuwa mnataka kuwaweka jela Watoto WANGU na kuwa hamkuwa na hata tikiti ya kuegesha gari dhidi yao na hamkuweza kupita Damu iliyomwagwa kwa niaba yao pale Kalivari. Hamkuweza kunipitia MIMI, YAHUVEH, kwa sababu wameweka usalama wao katika YAHUSHUA na MIMI. Walinitii MIMI na wakatoroka kabla ya siku za uharibifu zije.

Sasa Ninazungumza haya. Lieni kutoka paa za nyumba, lieni kwa dunia. Nilikuletea ishara kuwa Nitakomboa wengine vivi hivi. Nilikutuma nje ya Marekani, kutoka kwako, usirudi huko tena. Kwa hivyo, pia Nilivyozungumza nawe, pia Nimezungumza na wengine na hawajasikiza na hawajajifunza na wanaitwa kwa Jina LANGU kwa hivyo wengi wao watajifunza kwa njia ngumu. Wanaamini kweli unazoamini na bado wamebaki. Lakini Nilikutuma katika Huduma hii ya Nafasi ya Mwisho cha Wayahudi Masihi kuambia watu wa Marekani na Kanada Ninapowaambia wakimbie, ni afadhali wakimbie. Au wasije kunililia MIMI. Kumbukeni kuwa kamwe huwa kuna amani ndani ya macho ya kimbunga. Kanada, Niliwaonya msifuate nyayo za dada yenu Marekani kupitia huyu nabii miaka iliyopita, lakini, je, mlisikiza? Hapana, kejeli yenu ilizidi kukua.

Wakati nchi hizi zilikuwa zimefinywa kama Nilivyokuonyesha, Elisabeth [Elisheva], maono haya tena na tena. Kikombe kikubwa nyekundu cha kutupwa kilichotengenezwa kwa plastiki nzito na mkono mkubwa ulichukua kikombe hicho, juu ya panya mdogo aliyeogopa, panya mdogo mweupe, na kuifunika na presha ya mkono ule, na panya anakimbia huku na kule chini ya kikombe hicho akijua kuwa hakuna kutoroka, huyo ni nyinyi. Wale mnaosema kuwa nyinyi ni Watakatifu, mnaolia katika Jina LANGU, na bado wamebaki. Ninatabiri sasa huyu ni nyinyi. Msipokimbia na kufanya Ninachowaambia mfanye Ninapowaambia kukimbia, lazima mtii. Au, huyo ni wewe, wewe ni yule panya aliyeogopa na serikali zenu ni mkono ule unaowazuia kukimbia.

Ninapowaambia muuze kile mlicho nacho, torokeni kama bado mwaweza kukimbia. Wengi wenu bado mnaniuliza MIMI maswali. Je, mnafikiria ni kwa nini Niliwaambia mfanye Pasaka? Hata kama hamjawahi kuifanya hapo awali, Niliwaonya kuifanya ili malaika wa kifo awapite na asiguse familia zenu au nyumba na laana zisije juu yenu. Je, ni wangapai walisikia haya Nilipozungumza haya kutoka kwa Ringmaiden huyu na kuwapa amri kufanya haya. Baada ya Pasaka huja exodus. Elisabeth [Elisheva] hakujua kuwa kutoka kwao kutakuja bila onyo. Nimewaonya nyinyi. Wanaenda mbele yenu.

Wananchi wa Marekani na Kanada kimbieni, kimbieni kama bado mwaweza, kama mwajua kuwa mwajua Nimewaambia. Kumbukeni, Niliwaambia kuwa nchi mnazoziita third world, ingawa maskini, ndipo kutakapokuwa salama kutoka kwa serikali zenu zilizo fisadi na zenye pesa, watakaomkaribisha mpinga kristo, na MIMI, YAHUVEH, Ninamwita mtoto wa shetani, mwana mpotevu, anayeleta Alama ya Mnyama. Msiamini serikali yoyote kuwalinda katika nyakati za giza zijazo, kwa kuwa Ninatuma Amightywind kutumika kama njia dhidi ya maovu katika dunia hii na maovu yajayo duniani humu. Jifunzeni maandiko yatakayowatia moyo kama bado mwaweza kuisoma kwa huru. Wakati unakuja wakati neno litafichwa kwa njia mpya.

Lakini nyinyi, ambao mnapaswa kubaki kule Marekani na Kanada, Ninawapa amani YANGU inayozidi maarifa yote na Ninao Watakatifu WANGU ambao watabaki, hapa ndipo imani yako lazima ibaki imara. Lakini ni lazima mjue kwamba wajua kwa kweli Nimewaambia mbaki na msiende. Ninawashukuru kwa kuniruhusu MIMI kuwatumia kama tuzo kuu kwa huduma hii. Na wanapotembea kwa upako mkuu na kubarikiwa na kulindwa, pia nyinyi mna upako, mnabarikiwa na kulindwa. Vipande vya chess vipo kwenye ubao sasa, kila kitu kipo kinapofaa. Kwa maadui WANGU na maadui wa huduma hii, sasa hivi karibuni MIMI, YAHUVEH, Nitasema, “CHECKMATE!”

Kanada, hatima yako ni kama ile ya Marekani. Ninapoangalia Marekani na Ninapoangalia Kanada, hamna tofauti. Nyinyi ni dhambi, nyinyi ni uvundo, nyinyi ni mavi machoni MWANGU. O, Nitaanza kutabiri kwa [nchi] zingine, lakini sana jicho LANGU lipo kwa yule aliyefanya wengi kupotoka. Marekani, mtalipa. Sasa nabii huyu anaweza kuzungumza maneno haya ya moto Niliyoiweka. Kwa siku zijazo, mnapokaribia siku ya Penetekoste, kila mtu aliye WANGU, kila mtu anayeita Jina LANGU Takatifu ni heri waanze kutamka Zaburi 91 tena na tena, kwa sababu amejua Jina LANGU, ataniita MIMI wakati wa shida na Nitamjibu na Nitamuokoa, Sitadanganya.

Wale wanaoheshimu Siku YANGU ya Sabato, wale ambao Torati YANGU wanaitii kwa kweli, wale wanaoabudu YAHUSHUA, Nitawajibu, Nitawaokoa. Wale ambao wameipenda Huduma hii, kwa kuwa Maneno YANGU pekee yamezungumzwa, Nitawajibu, Nitawaokoa, kama tu mtatii. Kama mtabaki kwa sababu mwasema, “O lakini bwana yangu hajaokoka,” mtakapobaki nyuma na kusema, “O lakini mke wangu hajaokoka,” mtakapobaki na kusema, “O lakini watoto wangu hawajaokoka” lazima Niwakumbushe nini kilichomfanyikia mke wa Lutu? Na itakuwa vivyo hivyo tena.

Hamwezi hata kufikiria ni nini nilichowapangia o Marekani na Kanada. Wale ambao wamekimbia Marekani wanadhani kuwa wamepata usalama pale Kanada, wale walio Kanada wamekimbia pale ambapo wanadhani ni salama kule Marekani lakini wote ni sawa, hamna tofauti, wote wanalikejeli Jina LANGU Takatifu. Nyinyi mnaofikiria kuwa mnaepuka umaskini kuja kwa nchi tajiri; hamjui ni nini watakachowafanyia. Nina watoto wengi zaidi walio na upako na Watakatifu katika nchi maskini kushinda wale walio katika nchi tajiri zikiweka zote pamoja. Bibi Arusi WANGU wengi ndio Ninaowaita Bibi Arusi wa YAHUSHUA wa Kimataifa, ni wachache walio katika nchi tajiri. Bibi Arusi wa YAHUSHUA wa Afrika, njooni. Jitambulishe kwa huyu Ringmaiden. Maombi yenu ndiyo Nuru inayozuia giza kwa kufunika Afrika mzima.

O, Ninajua kanisa nyingi kule Ulaya ni vuguvugu. Mnafaa tu kutemwa nje ya mdomo WANGU na bado sijawafikia. Lakini MIMI, YAHUVEH, Ninaamuru Bibi Arusi wa YAHUSHUA wa Ulaya njooni. Jitambulisheni kwa huyu Ringmaiden; ni maombi yenu ambayo yamesaidia kuizuia ghadhabu ZANGU juu ya Ulaya.

Mnapoona bei ya mafuta ikizidi kuenda juu kule Marekani, mtaona hofu ikija juu ya watu ambayo hawajawahi kuona. Kwa kuwa mwaona, kampuni za mafuta wanasema nyinyi ni wao. Na watawakanyaga. Je, mwafikiria kuwa hela zenu zitaharibiwa vipi? Kama mnavyoona bei ya kila kitu ikienda juu. Ni kile tu ulichomfanyia YAHUSHUA ndicho kitakachosimama, hii ndiyo njia ya pekee MIMI, YAHUVEH, Nitaongezea baraka zako za kifedha. Kwa wale ambao wanaweka imani yao kwa kile kinachoitwa mafuta, mafuta meusi badala ya kuweka imani yao kwa MIMI, YAHUVEH, kwa Jina la MWANA WANGU YAHUSHUA MASIHI, mtajua hofu kama vile hamjawahi hapo awali. Ninazungumza kwa wale wanaojiita Wakristo. Mlikuwa mnafaa muombe na kuniuliza MIMI kwa ulinzi. Badala ya haya, mnaweka imani yenu kuwalinda kwa kitu kinachoitwa Homeland Security badala ya kumuamini Mungu YAHUVEH. Sasa, o marekani, sasa, o Kanada, sasa mnafaa kwa MIMI kuwakanyaga.

O, lakini wale ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha uzima cha Mwana Kondoo kabla ya dunia hii kuumbwa. Wale wanaolia kwa MIMI, wale wanaolia katika Jina la MWANA WANGU YAHUSHUA, endeleeni kuweka imani yenu na kushikilia kwenye pindo la vazi la YAHUSHUA na msiiachilie. Hata nini kifanyike, msiiachilie. Kama Nimewaambia mbaki basi Nitawalinda pale mlipo. Lakini kama Nimewaambia muende, kumbukeni mnatotii kama bado hamjaondoka.

Sasa Elisabeth [Elisheva], mna anwani mpya ya kuweka. Hamhitaji tena kupata barua zenu kutoka Oregon. Hamhitaji hii gharama sasa. Mna ruhusa YANGU kuweka anwani ya Alaska.

Upako mpya umekuja juu ya Ulaya ulipokanyaga mahala hapo. Sasa jeshi la nuru na giza watapigana kwa njia kuu. Kwa kuwa Bibi Arusi wa Ulaya watajua ya kwamba hawapo pekee yao. O, daima walikuwa NAMI lakini wamekuwa wakiuliza, “O wapi, o wapi wengine?” Sasa ndio wakati Nitaanza kuwaleta pamoja. Yale ambayo yalitabiriwa miaka mingi iliyopita na upako mpya na mkuu zaidi. Bibi Arusi WANGU watajitokeza na kupigana na pepo chafu kote duniani.

Elisabeth [Elisheva], utapata njia ya kuingia kwenye intaneti. Kuna mmoja ambaye alikuandikia na lazima umfikie, kwa sababu ni kwa Jina LANGU yeye huomba kila wakati. Kuna Bibi Arusi wa Ujerumani unapaswa kuwaita; walikutafuta hapo awali na sasa lazima uwatafute tena. YAHUSHUA ana Bibi Arusi wa Kiitaliano na Ninapozungumza juu ya Bibi Arusi, Ninazungumzia zaidi ya mmoja. Bibi Arusi wa YAHUSHUA wa Kiitaliano njooni. Tuma mwaliko sasa na jitambulisheni kwa huyu Ringmaiden. Je, mko tayari kupeana mlicho nacho kwa Huduma hii? Je, mtawafunika kwa maombi na upendo?

Kote katika nchi zote kule Ulaya MIMI, YAHUVEH, Ninawaita. Njooni na mkusanyike na huyu Ringmaiden, kwa kuwa kuna upako mpya ambao utawajia wakati nyote mwaleta taa zenu pamoja, itazuia giza kote Ulaya. Fikirieni haya. Kukiwa na nuru zaidi, giza itapunguka, Ulaya, kwa kuwa mmefunikwa na giza. Lakini Ninaleta nuru kufukuza giza. Bibi Arusi wa Ulaya, je, mko tayari kupa hii Huduma kile mlicho nacho? Je, mko tayari kuleta upako zenu pamoja?

Katika siku zijazo, unabii zitakuja kwa Ulaya na mataifa mengine. Marekani, mlikataa kusikiliza. Kanada, milikataa kusikiliza. Walipoondoka, walipiga vumbi itoke miguuni mwao na Nikawapa maagizo yao. Wasiingie tena, kwa kuwa itakuwa ni kama Lutu alirudi tena kuingia Sodoma na Gomora Nilipowaambia wakimbie. Nitawakumbuka kwa upendo nyote mliokuwa Baraka kwa Huduma hii, nyote mliofanya hii njia kuwezekana kukusanyika na Bibi Arusi wa Kimataifa. Yale mliyoyafanya, Ndivyo Nitakavyowalinda, ndivyo Nitakavyowahurumia kwa kuwa mtapata Baraka sawa na huyu Ringmaiden anayezungumza.

Wale wanaokataa kuhamasisha Huduma hii, hamjui, lakini mnajiibia Baraka nyinyi wenyewe, baraka ambazo Nimewawekea. Haya ndiyo maneno, Watoto WANGU ambayo mnafaa kuyaweka pamoja na yale maneno Niliyowapa kule kwenye Uwanja wa Ndege wa Seattle kabla hamjaenda Ulaya.

O Elisabeth [Elisheva], mmenipendeza MIMI sana, kwa kuwa mnatembea kwa imani na sio kwa kuona. Nilipokuambia uondoke, haukuniuliza MIMI maswali, ulitii. Ninapokutuma kwa nchi geni, ulisema, “Lakini sizungumzi lugha yao,” na bado ulitii. O unavyonipendeza MIMI; je, wafikiria kuwa Ninaweza kukuacha ubaki njaa? Ulisema, “O, lakini bei ni ghali hapa.” Je, MIMI, YAHUVEH, ni maskini na mtu hajaniambia? Je, hamjui kuwa dhahabu yote na fedha Mbinguni iko tayari kwenu nyinyi Nitakavyokadiri?

Ninapowaambia mtafute pahali Patakatifu pa kukusanyika na muwe tayari kwa wengine kuja, Ninajua mtatii. Ninafurahia kuwabariki kwa njia hii. Na Makuu, Makuu, Makuu, yatakuwa Baraka [ya wale] waliofanya juu chini, kutoa Baraka sawa, kwa kuwa nyinyi ni kitu kimoja. Mliwakumbatia na kuwapa busu na mnajua kuwa ni MIMI Niliyekuwa kwenye hizo busu na kumbatio. Mbele ya dunia mzima, Ninawashukuru. Ninawabariki kwa sababu Mlitii.

Adam, tena Nilikutuma, ulitoka Vancouver kuenda Seattle kwa gharama kuu. Ulikuja kwa upako WANGU, ulikuja kwa upendo WANGU. Nilijua Ninaweza kukuamini, kwa kuwa wewe ndiye Nilituma walipoondoka Seattle na kuenda Alaska. Kwa hivyo Nilijua Ninaweza kukuamini tena, na Adam M. huwa haunikosei na o, Ninavyokubariki. Na kuna Kathy wawili. Mnajua majina yenu ya mwisho. Vile mlivyo Baraka kwa huyu Ringmaiden, nyinyi ni Baraka kwa MIMI, YAHUVEH na MWANA WANGU YAHUSHUA. Binti YANGU mpendwa Kathy A., wewe hufanya juu chini kuhakikisha unabii zote Nilizompa Elisabeth [Elisheva] zinatolewa kwa vitabu ambazo zitakuwa hazina yenye dhamana ya juu, nyumba ya imani, wakati wa Dhiki Kuu. Kathy A., wewe uliyefanya juu chini na kujitolea kwa kila njia, tena Ninasema mbele ya dunia, wewe ni Baraka kuu. Ninakadiri kuwa jina lako linaheshimiwa huku Mbinguni pamoja na maombi yako na zaka na sadaka.

Watakatifu WANGU wanaotoa pesa ili niweze kuitumia Huduma hii kuhudumia kote duniani majina yenu imeandikwa katika kitabu cha Baraka pamoja na Adam na Joseph W. pale Hong Kong waliokuwa watakatifu kwa muda mrefu. Ninataja majina yenu kuwapa moyo. Makuu, Makuu, Makuu, Makuu, yatakuwa Baraka zenu kwa kuwa kila miguu yao itakapoenda, kwa kiroho nyinyi pia. Kule mbinguni, wakati tuzo zitakapopewa kwa nafsi zilizoletwa kwa YAHUSHUA na huduma hii, nyote mtasimama nao. Bila nyinyi kuwa Baraka kwao, Ningetumia nani kuwa jibu kwa maombi yenu? Nitatumia watu kubariki wengine, kwa kuwa unapobariki wengine MIMI, YAHUVEH, Nitawabariki.

Kuna wale ambao sijataja majina yenu na mmetoa pesa kwa ajili ya Huduma hii. Ninawaahidi kuwa Baraka zilezile zimewekwa kwenu nyinyi pia, watoto wapendwa, kwa kuwa Ninajua nyinyi ni nani. O binti mpendwa Sharon M., kwa miaka hii yote umekuwa Baraka tena na tena. Wewe ni kama yule Mjane wa Sarepta na unatoa kile ulicho nacho kutengeneza nafasi ya Baraka zaidi. Imani yako na kutii kwako kunanifurahisha MIMI.

Nimetuma matajiri kwa Huduma hii na mnajua sauti YANGU na bado mnasimama mbali, hamjitambui, na ni upako wa RUACH ha KODESH uliowaleta hapa. Je, mko tayari kupeana Nilichowabiriki nacho kusaidia Huduma hii kwa kazi yao kwenye shamba la mavuno? Je, hamjaelewa ya kwamba mali yenu haitawaponya wala kuwasaidia wakati wa Dhiki Kuu? Je, hamjaelewa ya kwamba kweli mnazojifunza hapa zitawalisha na kuwasaidia? Na wakati mtakapohitaji imani au mnashangaa nini kitakachofuata, Nimetabiri tayari. Je, sijawathibitishia mara kwa mara, muwe Baraka kwa Huduma hii, ili Niweze kuwa Baraka kuu kwenu?

Je, hamjui ya kwamba mnapobariki wengine wanaotumika kama mdomo wa YAHUVEH. Mnanibariki MIMI na YAHUSHUA na mnajiwekea baraka na hazina kule mbinguni? Si Neno LANGU husema, “Unapompa nabii maji ya kunywa, utapokea zawadi ya nabii?” Ni kwa nini Ninawaambia haya katikati ya unabii? Kwa sababu wengi wenu mnataka kujua ni kwa nini maombi yenu hayajibiwi? Mbona upako haukui? Kuna gharama ya kulipa kwa Baraka ZANGU na inaitwa KUTII.

Inahuzunisha kusema lakini kuna Watoto WANGU wanaosoma haya au kuisikia na kusema, “Ninatambua sauti ya YAHUVEH. Ninakuja hapa na kuona anachosema YEYE lakini nakataa kuhamasisha au kuwatia moyo Huduma hii kwa njia yoyote.” Ni wangapi mlianza kama Baraka alafu mkabadilika kuwa laana, mkipuuza mnachojua kuwa ukweli? Mmenililia MIMI na kusema, “majibu ya maombi yangu yako wapi, wapi ukombozi wangu na uponyaji wangu? Mbona mpenzi wangu anachelewa?” Hii ndiyo nafasi yako ya mwisho kuwa Baraka na kutii!

Je, kwani hamjalishwa kwa hizi malisho kijani kibichi ya upako, kiroho na hamjakuwa kwa hekima na ufunuo? Kwa sababu wengine wanalipa gharama ya kulisha wengine maneno YANGU kwa wanakondoo na kondoo WANGU na kwa wote wanaojali kusikia kote duniani. Je, hamfikirii kuwa hamna gharama ambayo huyu nabii Ninayemtumia kuzungumza halipi pamoja na wale wanaosimama naye na kumuombea kiroho katika vita na maombi, na bado wanaendelea kufanya matakwa YANGU na njia. Ni wachache sana wanaosoma haya wanaokiri upendo wao kwa YAHUSHUA walio tayari kulipa gharama inayochukua kuzungumza maneno haya ambayo sio ya masikio inayowasha, kuhamasisha Huduma hii inayokataa kupuuza ukweli.

Kila mahali hawa walio na upako wanapopanda miguu yao, ni aidha Baraka ZANGU au laana zinazofuata, katika kila taifa, aidha wokovu au hukumu itafuata. Hivyo ndivyo itakavyokuwa na Bibi Arusi wa YAHUSHUA. Bibi Arusi wa YAHUSHUA anzeni kuita na kuuliza dowry, ile Niliyowahifadhia na kuwawekea kando. Ninavyompa Ringmaiden pia Ninawapa nyinyi pia. Kwa kuwa mali ya waovu imewekwa kwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI na ni nyinyi. Kwa kuwa Ninajua ni nani ataitumia kwa utukufu WANGU na utukufu WANGU pekee.

MIMI, YAHUVEH, Nina onyo hii ila tu kwa wale waliokuja kama rafiki, wakileta zawadi za pesa na tena wakamruhusu shetani kuingia na kukubadilisha kuwa Yudasi. Ingekuwa ni afadhali kama haungewahi kusikia jina la huyu Ringmaiden, kwa kuwa Nitahakikisha mtateseka kwa kila huzuni aliyohisi kwa sababu ya usaliti wenu na kwa kila chozi aliyolia kwa ajili yenu. Mlipomsaliti, mmesaliti yule aliyewatuma kuwa baraka na sio laana. Wakati maombi yenu hayapati majibu kabisa na mnashangaa kama nimekana kilio chenu, wakati mlichoogopa kinakuja kufanyika, kwa sababu ya shetani, mliamini uongo na mkapuuza ukweli. Wakati mtakuwa hapa wakati wa Dhiki Kuu na kuteseka bila huruma, hamtashangaa ni kwa nini. Si Niliwaonya, “Msiwaguse Watakatifu WANGU na kuwaumiza Manabii WANGU?” Je, ni lini mtajifunza kuwa rafiki kukusaliti ndiyo uongo mbaya zaidi? Msipotubu na kurekebisha mlichofanya, mtapitia njia sawa na Yudasi na yule unayempenda atafariki.

Elisabeth [Elisheva], kila kitu Nilichokupa, uliachia wengine. Ulichochukua tu ni begi zako na hata sio gari Nilizokupa. Unapoacha zawadi ya gari ya ndoto yako, o, lakini Nitakubariki. Hakuna kitu kizuri ambacho Nitakunyima. Nitazungumza kwa nyoyo za watu Watakatifu na wanaosoma haya na kusikia haya, ni nyinyi mnaojua kuwa mmeitwa na mmechaguliwa kusimama naye kwa Huduma hii. Mmepewa zawadi ya kuwa wasaidizi. Nimewabariki kwa kazi yenu. Pamoja mmeitwa kufanya kazi kwa uwanja huu na kupeleka kweli ZANGU katika mataifa kote duniani. Ninazungumza baraka sawa juu yenu. Hakuna chochote kizuri ambacho Nitawanyima na mtakuwa invisible kwa maadui wanaotaka kuwaangamiza.

Kwa hivyo, Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI, Ninazungumza na Ulaya sasa. Je, mko tayari kutoa kile mlicho nacho kwa Huduma hii? Leteni taa zenu za kiroho zinazong’aa pamoja na muwe baraka na mzilete kama binti bikira watano walivyofanya. Taa hizi zitakua kama taa ya lighthouse na upako zenu zitakua na pamoja mtakuwa moja KWANGU MIMI. O ishara, maajabu na miujiza mtakayoona katika Jina Takatifu la YAHUSHUA kama mtakuwa tu na imani na kuamini. MIMI, YAHUVEH, Nitatukuka, kwa Utukufu wa MWANA WANGU WA YAHUSHUA MASIHI.

Ninazungumza maneno haya sasa. Msiogope, o Bibi Arusi pale Israeli na kufikiria kuwa sijali kwa kuwa Nitawatuma wao kwenu pia. Hili tu ni hatua nyingine kuwafikisha pale. Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI pale Israeli, njooni. Jitambulishe kwa huyu Ringmaiden, kwa kuwa ni mojawapo ya kazi ya Huduma hii kuombea Baraka na usalama juu ya Bibi Arusi wa Israeli. Nyinyi ni kitu kimoja naye- naye nanyi. Je, mko tayari kutoa kile mlicho nacho kwa Huduma hii? Sasa ndio wakati wa kuanza kumualika na kuanza kuombea Huduma hii kuja na kubariki Watakatifu kule Israeli, kuomba maadui wakimbie katika njia saba tofauti. Hukumu itawaangukia maadui na wataanguka katika shinikizo kubwa la ghadhabu ya MIMI, YAHUVEH. Ombeni, o Bibi Arusi wa Israeli na Bibi Arusi wa Middle East, walio wa YAHUSHUA kuwa upako kwa Huduma hii izidi kukua ili upako wenu uongezeke pia.

MIMI, YAHUVEH, Ninazungumza kwa Bibi Arusi wa Kimataifa wa YAHUSHUA. Ninawapa amri hii. Saidieni huyu Ringmaiden kufikia dunia hii kwa Utukufu wa YAHUSHUA. Jitoleeni na kutafsiri hizi unabii kwa lugha tofauti. Kuna mfasiri Mwebrania ambaye ni mmoja wa Bibi Arusi wa YAHUSHUA anayesoma haya sasa na anajua kuwa anafaa kutafsiri unabii hizi katika Kiebrania. Mwingine anajua kuwa anafaa kutafsiri unabii hizi katika Kiafrika na Kiarabu. Je, mbona hamjakuja na kujitambulisha kwa Huduma hii? Je, mbona Bibi Arusi wa Kimataifa wa YAHUSHUA hawatii na kutumia Baraka, zawadi na talanta MIMI, YAHUVEH Nimewapa? Je, mbona mmezizika pale ambapo hazina thamani kwa yeyote?

Kwa wale walioanza kazi kwa kutafsiri unabii katika lugha zenu, Nina swali hili kwenu. Je, Mbona hammalizi kazi mliyoanza, kazi kwenye ukuta, kwani hamjali nchi yenu hata kidogo? Kwa wale mliofanya haya, Nitawauliza swali hili siku moja mbele ya Kiti CHANGU cha Enzi. Kaeni tayari kunipa jibu, kwa kuwa mliitwa na kupewa kazi hii, na bado hamjamaliza kazi hii. Hii inachelewesha kukuja kwa YAHUSHUA kuwachukua Bibi Arusi WAKE, kwa kuwa unabii hizi na jumbe hizi lazima ziwe katika lugha nyingi kabla YEYE hajarudi. Bibi Arusi wa YAHUSHUA katika Mataifa kote duniani, Nilisababisha hawa kutoka manyumbani kwao, wakaacha mali yao nyuma, kuja kuwa baraka na kutoa kile walicho nacho. Je, haya ni makubwa kwenu? Mko tayari kutoa mlicho nacho kwa Huduma hii ya Mitume Wayahudi na Pentekoste? Njooni waombezi kuwaombea kila mara, kwa kuwa vita ni vikali lakini Ushindi tayari umepatikana kwa Sifa, Heshima na Utukufu wa YAHUSHUA!

* * * * * * *

Ndivyo ilivyozungumzwa, ndivyo ilivyoandikwa katika upako wa RUACH ha KODESH.

Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu) kwa Utukufu wa YAHUVEH na YAHUSHUA!

* * * * * * *

Neno Lilipewa katika Uwanja wa Ndege wa Seattle, May 3 2006.

Neno hili lilikuja kwake Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu) katika Uwanja wa Ndege wa Seattle, kabla hawajaenda Ulaya.

Nimekuonya tena na tena, na hawasikii. Elisabeth [Elisheva], unavaa rangi nyeusi kwa sababu Nina huzuni. Sio kwa mapenzi YANGU lazima Nifanye Ninachotaka kufanya, lakini Nimelazimishwa kufanya. Kwa kuwa kuna gharama ya kulipa kwa kutotii. O, wale waliosikia, kwa kweli siku ya uharibifu imeanza tayari.

Kutakuwa na nguvu, upako na yale ambayo mpendwa Adam na Luigi wameitwa kufanya. Sio kwa makosa huduma hii itakuwa Ulaya na mnafanya hayo. Ombeni kwa usalama, ombeni wafichwe. Ombeni kuwa mali ya waovu, iachiliwe kupitia Mikono ya Bibi Arusi, kwa kuwa sasa ndio wakati, sasa ndio wakati uliokadiriwa.

Adam, wakati utakapofika Niwaambie muondoke, Ninawaambia sasa, Tengezeni begi! Niulize MIMI ni nini utakachoweka ndani, msichelewe. Waona vile Nilivyomtoa Elisabeth [Elisheva] kwa haraka, kwa sababu Kanada haikumsikiliza. Nimetuma onyo baada ya onyo. Walikataa kusikia! Kwa hivyo, hao sio afadhali ukiwafaninisha na Marekani. Kwa wale, wanaoona Kanada kuna usalama, wamedanganywa.

Sasa, Nimekutuma Elisabeth [Elisheva], kutoa Hukumu YANGU juu ya Ulaya, kwa wale vuguvugu. Waambie kuwa Nitawatema nje ya mdomo WANGU. Kuna wale wanaosema kuwa ni WANGU na kumbe hawanijui MIMI. Mtajua mengi mtakapopata? Upako mpya utawajia. Ni hayo tu kwa sasa.

Lakini Adam jua haya, hamna hata nywele moja kwenye kichwa chako itakayoguzwa, kwa kweli wewe ni WANGU na Nina wivu juu yako. Yeyote atakayekuumiza wewe, ni kama

Wameniumiza MIMI, na hata hivyo, wasinijaribu MIMI. Nitakaposema, tengeneza begi, itengeneze, kwa kweli machungu ya kuzaa ya Siku ya Uharibifu tayari ishaanza. Hakuna chochote kitakachosimamisha Dhiki Kuu, kuzaliwa kwa Ghadhabu ZANGU!

Lakini, wale walio WANGU, wale wanaonitafuta MIMI msijali!

Je, Unahitaji maombi au Wokovu? Una maswali? Tafadhali mtafute Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred