Unabii 81

O Israeli! MIMI, YAHUVEH, Ninawakemea!

Imendikwa/Kuzungumzwa katika upako wa RUACH ha KODESH Kupitia Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu) Januari 24, 2006 Saa 7:00 usiku (Sehemu ya kwanza ya unabii) YAHUVEH Alisema nisiitoe bado, haijakamilika Sehemu ya pili ilitolewa Februari 7, 2006 – Saa 5:00 jioni

Haya ni kutoka Unabii 105, YAHUVEH Alisema kuweka haya kwa Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH Alisema kuongezwe yafuatayo kuonya wale ambao wanakejeli:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

O Israeli, O Israeli, Nina huzuni. Nitafanya nini zaidi, kwa kuwa Nilimtuma Mwana WANGU YAHUSHUA kwenu.

* * * * * * *

[Kwenye kinaza sauti]

Elisabeth [Elisheva] anasema “Hmmm.”

“Ngoja, Ngoja, Ngoja!” [Aliambiwa na YAHUVEH kusimama na kuchukua mamlaka ya kiroho, kwanza kumfunga shetani na pepo zake mbali na eneo hilo ambapo wanapoishi, akiwafunga wakuu, nguvu, falme na wakuu kwenye sehemu za juu, juu ya eneo hili, katika Jina la YAHUSHUA, ili neno hili lisizuiwe.] Elisabeth (Elisheva) aliendelea kuomba katika Ndimi Takatifu na hili ndilo ombi lililotoka katika upako.]

“Hili ndilo neno lililopewa kwa Israeli baada ya ndoto iliyokoroga upako ndani yangu. Kwa hivyo ninakuomba Baba YAHUVEH, kwa sababu Unanipenda, kwa sababu Uliniumba, Uliumba mdomo huu na ulimi huu, ni heri haungeniumba kuliko kuniacha mimi kutabiri neno la uongo katika Jina LAKO. Kwa hivyo kama haya ni ya kwako kwa kweli, acha Neno hili litoke. Kama sivyo, Maneno haya yaende.

Katika Jina la YAHUSHUA MASIHI, ninaomba. Ninakuuliza Baba YAHUVEH, katika Jina la YAHUSHUA, kuweka makaa yako ya mbinguni kwenye mdomo wangu. Acha maneno yako yatoke kama vile hayajawahi kutoka hapo awali (Ndimi Takatifu) Takatifu, Takatifu, Takatifu, tunakusifu ewe Baba YAHUVEH na YAHUSHUA.”

[Nilikomesha Neno hilo kutoka mpaka nilipochukua mamlaka ya Kiroho.] O Takatifu, Takatifu, Takatifu Baba YAHUVEH, ni nini Unachotaka kusema?

* * * * * * *

Unabii 81

Oh Israeli! MIMI YAHUVEH, Ninawakemea!

O Israeli, O Israeli, wale ambao ni mboni la jicho LANGU ambao lina mdudu ndani yake, Ninawakemea! MIMI, YAHUVEH, yule Ambaye Abrahamu, Isaka na Yakobo wanamuabudu na walimtii,

MIMI, YAHUVEH, NINAWAKEMEA!

Mnasema ni kwa nini mmelazimishwa kupeana ardhi yenu ya baba zenu wa kale waliowapa? Ninawauliza haya: Je, mnatembea katika Torati? Je, mnaishi katika Torati? Kama baba zenu wa kale walivyofanya?

O, Israeli, kama vile tu Mwana WANGU YAHUSHUA Alikuwa na Yudasi ambaye alimsaliti YEYE kwa fedha 30, pia nyinyi mna Yudasi, yule ambaye anawapa ramani ya amani ambayo itaisha kwa kuangamizwa kwenu, kutayarisha njia kwa yule aitwaye mpinga kristo, mpinga Masihi.

Watu wanasema kuwa nyinyi ni Nchi Takatifu, lakini MIMI, YAHUVEH, Ninasema kuwa hakuna utakatifu wowote. Ni wachache tu Ninao ambao wanatembea katika Torati na kuishi katika Torati. Nyinyi mna pepo ya Kifarisayo. Na Ninawaambia haya: ingawa sio MIMI Ninaogawa ardhi yenu, lakini Nitamruhusu adui kufanya vivyo hivyo kwa sababu ya kutotii kwenu.

Lakini Ninawaambia haya; Ninaapa kwa haya, kwa JINA LANGU LENYEWE MIMI, YAHUVEH, Naapa kwa haya. Nitalipiza kisasi kwa maadui wenu kwa kuwa ni MIMI, na mamlaka YANGU pekee kuwaadhibu kwa njia ambayo Nimekadiri. Maadui hawa wanaokuja dhidi yenu watakuwa na hatima sawa kama Yudasi. MIMI, YAHUVEH, Nitakuwa na huruma kwa wale wanaolia na kuomboleza na kupiga mayowe mnapoona usaliti wa Yudasi, kwa Yerusalemu, wale kati yenu mnaochukia na kumkemea mwanamume wa dhambi. Wale ambao huita Jina LANGU katika Jina la Mwana WANGU YAHUSHUA, Nitawahurumia na Nitawabariki. Hamjahifadhiwa kwa ghadhabu YANGU.

Lakini nyinyi o Marekani na mataifa mengine wanaowaunga, wanaothubutu kugusa yale ambayo Nilisema msiguse, kugawa yale ambayo Nilisema msigawe, mtapata hatima ya Yudasi. Mtajuta siku ambayo mlitupa fedha 30 njia ya Israeli. Kwa kuwa mnapogawa ardhi hiyo, mnapowapa hongo kugawa ardhi hiyo vivyo hivyo Nitawagawa kwa kila njia. Mwaka wa 2005 ulikuwa tu mfano. Hamjui, wala hata kufahamu, hofu Ninayoleta kwenye njia yenu kutoka Mbinguni ambayo binadamu yoyote hajatuma. O Israeli, O Israeli, mtapigana NAMI hadi lini? Ninajua siku ile ile ambayo mtaniachia MIMI matakwa yenu. O, lakini itakuwa njia yenye damu ambayo lazima mtasafiria hadi MWANA WANGU YAHUSHUA Aje na mtalia, “Baraka kwa yule ajaye katika Jina la YAHUSHUA MASIHI.”

Lakini hadi siku hiyo, o ni njia ya damu ambayo mtasafiria. Waliokufa wamewazunguka, kushoto na kulia, kulia na huzuni kwa hofu ijayo usiku. Mnajua bora, mnajua bora, na bado mlifanya yale ambayo Niliwaambia msifanye. Mlikubali hongo, inayoashiria fedha 30.ninafunia uso WANGU kwa aibu kila wakati Ninasikia Israeli ikiitwa, Israeli ikiitwa Nchi Takatifu. Ninatafuta mbali na karibu na kuna tu mabaki ambayo yanaweza kuitwa Takatifu mbele YANGU na kuna wale ambao wanalia na kuhuzunika, kwa kuwa wanaona ni nini kinachofanyika kwa ardhi yao.

Kuavya mimba na ushoga, ponografia, usherati, ibada ya sanamu haifai kuwa kati yenu. Tena na tena Ninaona pepo ya Kifarisayo ikiwaongoza. Nyinyi o Israeli, mna umbo la utakatifu na je, ni Utakatifu upi upo ndani yenu? MIMI, YAHUVEH, Ninawakemea na Ninawaadhibu na yameanza tu.

Rabi waovu ambao sio Rabi, lakini bado wanathubutu kujiita Rabi, wako na umbo la utakatifu lakini hawana Utakatifu wowote ndani yao. Hawana hofu ya MIMI, YAHUVEH, au mwana WANGU YAHUSHUA au gharama Aliyolipa pale Kalivari. Wao watatupwa kwenye moto wa uangamizaji WANGU. Nina mabaki, mabaki wachache. Wanatingika kwa jina la Rabi, kwa kuwa wao ni wanyenyekevu mbele YANGU na hawa ndio wale wanaonifurahisha MIMI wanaosema kuwa kuna Rabi mmoja tu, na Jina LAKE ni YAHUSHUA MASIHI.

O Israeli, Ninaangalia ardhi yenu na ni sehemu kubwa ambao haitii Torati. Maovu yamezidi na mnashangaa ni kwa nini? Mnaogopa maadui wenu wa dunia hii kushinda MIMI, MIMI YAHUVEH. Mmeruhusu hawa mnaowaita Rabi kuiba Jina LANGU Takatifu, kuwafunza, “Msiite hilo Jina, hamfai kuita Jina la Muumba!” Mmeamini uongo zao lakini Ninawatumia Handmaiden na Nabii WANGU KUWAAMBIA SASA, “Msiamini uongo hizi!” Iteni Jina LANGU, YAHUVEH tena na tumieni Jina la YAHUSHUA, kufika kwenye Kiti CHANGU cha Enzi. Mmeruhusiwa kujua Jina LANGU. Je, ni mtoto mgani hajui Jina la Baba yake? Msiamini uongo hizi. Kuna Nguvu za upako katika Jina LANGU na Nitasikia na kujibu vilio vyenu mnapokuja KWANGU katika Jina la MWANA WANGU Mtakatifu YAHUSHUA!

Someni maandiko yenu. Je, ni mara ngapi Nimewaambia muite Jina LANGU na Nitawakomboa? Jiulizeni, ni nani ambaye angefunza kuwa hamna thamani ya kuita Jina la Muumba? Hili ndilo limekuwa funzo la uongo la shetani lililofunzwa kwenu na Rabi wenu. Kemea uongo hizi. Mimi sio G-D. Mimi sio L-rd. wakati mmefuta Jina LANGU, mmetenda dhambi na kuchukua Jina LANGU bure. Mimi ni YAHUVEH. Lakini, mnaitamka kama (YAHVEH, YAHWEH), angalau mnatambua Jina LANGU. Ninawakaribisha mniambie MIMI ni wapi Nimewaambia katika Maandiko yenu Matakatifu kuwa hamna thamani kuliita Jina LANGU? Jina LANGU sio Ha Shem (jina lile). Jina LANGU sio tu Adonai (Bwana)!

Mimi ni YAHUVEH, Muumba wa yote. Jina LANGU sio Mungu. Hizi ni lebo na majina tu Niliyopewa na Rabi wenu na wafasiri wa maandiko wanao hamu ya kuliondoa Jina LANGU, wakiitaja kama YHVH au YHWH. Nimempa kila mtu jina. Mimi ni YAHUVEH, Mimi nina Jina. Jionyesheni kuwa mnanipenda MIMI na mniamini MIMI kwa kutumia Jina LANGU Takatifu. Je, si Mfalme Daudi aliita Jina LANGU kwa ukombozi? Je, kwani hamsomi kitabu cha Zaburi? Je, Zaburi 91 inawaahidi nini mnapoliita Jina LANGU? O Israeli, mengi sana imeibiwa kutoka kwenu, hata kama Vitabu Vitakatifu vilivyoandikwa tena kufuta Jina LANGU. Chukueni yale ambayo yameibwa, na muone mnapoita Jina la MIMI, YAHUVEH, katika Jina la MWANA WANGU YAHUSHUA, kama sitawakomboa kwa haraka kutoka kwa maadui wenu.

O Israeli, O Yerusalemu, YAHUSHUA MASIHI MWANA WANGU Alitumwa kutoka Mbinguni, kuzaliwa kutoka kwa binti bikira wa Kiebrania. YAHUSHUA ni Myahudi na YEYE Alitabiri katika nchi yenu, na Akafanya miujiza na vipofu wakaona, vilema wakatembea, viziwi wakasikia, bubu wakaongea, wakoma wakasafishwa, wagonjwa wakaponywa, waliofariki wakafufuliwa, yote katika nchi yenu, o Israeli. YAHUSHUA Alifunza katika Hekalu zenu Sabato, Alisherehekea Sherehe Takatifu, kwa kuwa hamuoni kuwa YAHUSHUA yupo katika Sherehe hizi zote Takatifu?

YAHUSHUA Alifanya miujiza nyingi katika nchi yenu. Alifunza na ndiye Torati iliyo Hai kama Alivyotabiri. YAHUSHUA Aliishi na kuuwawa hata kama yeye Alikuwa hana dhambi, kwa minajili ya dunia hii. YAHUSHUA Alifufuka kutoka wafu kwenye kaburi pale Israeli baada ya kumwaga Damu YAKE Takatifu kwenye ardhi yenu wakati watu walipokuwa wanalia, “Msulubishe” pale Kalivari. YAHUSHUA Aliwaombea na pumzi yake ya mwisho, “Baba, wasamehe, hawajui wanachofanya.” Kwa hiyo, Nitakuwa na huruma kwa nchi yenu, o Israeli, o Yerusalemu. Kama Mikono ya YAHUSHUA ilivyogongwa misumari kwenye mti, alivumilia mateso zaidi na sononeko zaidi ya vile mwanadamu kawaida angeweza.

MIMI, YAHUVEH, Nilichagua nchi yenu Israeli, kumzaa MASIHI wa pekee wa dunia hii. Hivi ndivyo MIMI, YAHUVEH, Ninavyowapenda na kuwabariki nyinyi o Israeli. Damu ya YAHUSHUA itawalinda Israeli kwa kuangamizwa kabisa na kuondolewa kwenye ramani ingawa hata Jina la YAHUSHUA wengi wa Wayahudi wanachukia Jina hilo na wanakataa Uungu WAKE. Mishipa na ateri za YAHUSHUA zimeenea kote Israeli. YAHUSHUA Alimwaga Damu YAKE iliyopenya kwenye ardhi pale Kalivari na kiroho imefika kona zote za dunia hii. MIMI, YAHUVEH, Niliwachagua nyinyi Israeli, kati ya mataifa mengine ya dunia hii kufanya haya. Kwa yeyote atakayeamini na atakayemkubali Mwana WANGU YAHUSHUA kama Dhabihu ya Damu ya pekee kwa ondoleo la dhambi. YAHUSHUA Ndiye Mwombezi wa pekee mbele YANGU YAHUVEH.

YAHUSHUA Ndiye upatanisho wa Damu Takatifu wa pekee Nitakaokubali. Kwa wale ambao wamekataa Damu hii iliyomwagwa kuosha dhambi zenu, wale wanaokataa Damu ya YAHUSHUA isiyo na dhambi kama alivyouwawa kwa nafasi ya mtenda dhambi, mtahukumiwa na Moshe (Musa) ambaye hatakuwa na huruma kwenu mnaposema kuwa YAHUSHUA hastahili kuitwa Mwana wa YAHUVEH na kuwa Masihi wenu na mnadhani kuwa kuitwa Myahudi na kufuata Torati ni tosha kuokoa nafsi yenu. Wanadamu wajinga, hamjui kuwa hakuna yeyote aliye kamili aliyetembea dunia hii ila tu Mwana WANGU YAHUSHUA. Mpaka Israeli ilie ‘Hosanna’ kwa YAHUSHUA tena na Atawale kama Mfalme wa Wafalme, hakutakuwa na amani ya kweli mpaka Israeli ikubali YAHUSHUA ni Mwana wa Pekee wa YAHUVEH, Aliyezaliwa kutoka kwa binti bikira wa Kiyahudi, bila dhambi. Na YAHUSHUA ndicho Alichotabiri na yote yaliyotabiriwa na manabii wa kale wakizungumzia kuja KWAKE.

Mdundo wa moyo wa YAHUSHUA unapiga kote Israeli, mishipa YAKE na ateri inabeba dhabihu ya Damu inayoosha uvundo wa dhambi kote duniani, kwa wale watakaotambua kuwa Nilimtuma YAHUSHUA katika Jina LANGU, YAHUVEH kuwa MASIHI wa pekee.

O Israeli, hakuna ondoleo la dhambi bila dhabihu ya damu. Je, dhabihu yenu ya damu iko wapi? Je, kwa kweli mwafikiria kuwa mnyama atatosha tena? O Israeli, o Yerusalemu, hamuezi kuona kuwa hakutakuwa na amani ya kweli. Hofu, maombolezo na damu itaendelea kumwagika kutoka kwa nchi yenu mpaka mkemee Yudasi ambao wanakuja katika mfano wa wanasiasa na Mafarisayo waovu, Rabi waovu, walio na umbo la utakatifu lakini hawana Utakatifu ndani yao. Israeli, jihadharini na kuja kwa mwana wa shetani, yeye ni mwana wa uharibifu atakayekuja na amani yake bandia, na atawadanganya, mkifikiria kuwa amani imekuja, sasa mnaweza kupumzika. Badala ya haya amini Mfalme wa Amani wa pekee na kubali upatanisho wa damu isiyo na dhambi wa pekee Niliyowapa kupitia MWANA WANGU YAHUSHUA pale Kalivari.

Hakuna wokovu, wala amani ya kweli kwenu Israeli, mpaka muache kuikataa Agano jipya la Damu Niliyowapa kupitia YAHUSHUA, kama YAHUSHUA Alivyo MASIHI Mtakatifu wa pekee! Agano la damu la kale haliwezi kuokoa nafsi zenu kutoka Jehanamu. Agano la damu la kale lilikuwa pale hadi wakati uliokadiriwa ambapo kutakuwa na bora, agano la damu jipya linalofunika. O Israeli, acheni kujiunga na mataifa mengine, kwa mfano wao wa dhambi ni nini. Badala ya haya kuwa kama Mfalme Daudi tena. Nisifuni MIMI, YAHUVEH, na mnyenyekee na kutubu dhambi zenu katika Jina la MWANA WANGU YAHUSHUA. Msitegemee nchi nyingine kuwaokoa kutoka kwa uharibifu, kwa kuwa mtakasirishwa.

Kwa sababu ya agano Niliyofanya na Abrahamu na MWANA WANGU YAHUSHUA, Nitaiponya nchi yenu mtakapotubu mbele ya MIMI, YAHUVEH, na kurudi tena kufuata amri

Za Torati ambazo Moshe (Musa) aliyowapa pale Mlima Sinai. Simameni kwa Utakatifu hata kama dunia itawakejeli. O Israeli, msiwagonge mawe Manabii, wala kuwaweka jela, au kuwaua Manabii Ninaowatuma kuwakemea. Badala ya haya furahieni kuwa Ninawapenda kuwaadhibu na kuwaonya kabla sijaachilia ghadhabu ZANGU kwa wale wanaokataa kutii na walio maadui WANGU.

Ukuta wenu wa vilio imeloweka kwa machozi na maombi mkiombea huruma. Maadui wenu wamewazunguka pande zote. Sasa wale ambao wamewadanganya wamewashawishi kuweka Myahudi dhidi ya Myahudi, hata kuuana, kufurushana kutoka kwa manyumba zenu na ardhi, mkisaliti wenzenu. Mnakimbia Goliathi wenu badala ya kuja KWANGU kama Mfalme Daudi alivyofanya kama kijana mchungaji. Siwezi kuwabariki hadi msimamie Utakatifu. O Israeli, Ninawaahidi haya na kuwakumbusha kupitia huyu handmaiden WANGU. Mtarushwa chini, lakini hamtaharibiwa kabisa. O Israeli na Yerusalemu, mtashangaa lakini hamtaachwa. MIMI, YAHUVEH, Nitawatumia tumaini pale ambapo panakaa ni kama hamna kutoroka. MIMI, YAHUVEH, Nitawaadhibu lakini sitawaacha. Mtakanyagwa na wapagani, lakini mtainuka tena kwa utukufu mkuu. Kama wakati ule wa Musa, Nitawabariki wale wanaonitii na kunibariki, na Nitawalaani wale wanaototii na kunilaani MIMI, YAHUVEH.

Dunia hii itaona wakati ghadhabu ZANGU zitakapomwagwa katika nyakati hizi za mwisho, vile Nitakavyowaficha wale ambao wamefichwa katika MWANA WANGU YAHUSHUA. Mapigo yote yaliyomwagwa katika wakati wa Musa itamwagwa katika kipimo kikuu juu ya maadui WANGU kutoka kwa Mikono YANGU, YAHUVEH. Bado kutakuwa na mashahidi tena kama mitume na manabii wa kale, na wote ambao ni Watakatifu, ambao damu yao ilimwagika wakati uleule na hata kama sasa bado inamwagika katika sehemu fulani za dunia hii, kwa sababu Watakatifu WANGU hawatawahi kupuuza wala kukataa kuwa YAHUSHUA Ndiye MASIHI wa pekee na mwana WANGU wa Pekee Aliyetumwa kutoka Mbinguni kutawala. O Israeli nimewafanya kuwa kikombe cha hofu ya kutetemesha kwa dunia na wataikunywa. Maadui wanasaga meno yao kwenu na kutoa kucha zao, wakiona wivu kwa yote MIMI, YAHUVEH, Niliyobariki nchi yenu nayo. Maadui wenu wanahesabu siku kabla ya wao kujaribu kuwaibia na kuwaua wanaume, wanawake, na watoto wenu bila huruma.

Tena Ninasema Nimeapa kiapo kuwa sitawahi kuwaacha wala kuwabwaga, Nitaanza na Nimeanza kuwaadhibu nyinyi hadi msimamie Utakatifu na kusema, “Baraka kwa YEYE Anayekuja katika Jina la Bwana YAHUSHUA MASIHI.” Alafu MIMI, YAHUVEH, Nitawalinda enyi Israeli kutoka Mbinguni, na dunia itaona tu kama wakati ule wa Moshe (Musa) hakuna yeyote ila MIMI, YAHUVEH, angeweza kuwakomboa kutoka kwa Mikono ya adui na tena itakuwa vivyo hivyo. Kuna boxi la dhahabu la ajabu linaitwa Safina ya Agano ambayo ina maajabu ya kale ya nchi yenu, o Israeli. Safina hii hakuna yeyote atakayeigusa ila tu wale ambao Nimekadiri walio Watakatifu kwa kweli mbele ya MIMI, YAHUVEH. Shetani anataka kuharibu kilicho ndani ya boxi hiyo ya dhahabu, kwa kuwa kuna nguvu za upako iliyoko kwenye vitu hivyo katika boxi hiyo ya dhahabu. Shetani anatuma mwana wake yule anayeitwa mpinga kristo kutafuta na kuharibu Safina.

Kati ya mataifa yote duniani Niliwachagua nyinyi o Israeli kuficha kile ambacho kimekuwa kikilindwa mpaka wakati itakapohitajika. Kati ya dunia mzima Niliwachagua nyinyi o Israeli na Yerusalemu, kuniletea Sifa, Heshima na Utukufu. MIMI, YAHUVEH, Nilichagua Damu Takatifu ya YAHUSHUA MASIHI kumwagika kwenye ardhi na juu ya Kiti cha Rehema na itakuwa pale Israeli ambapo Nitampa shetani kipigo chake cha mwisho. Boxi hii ya ajabu ina fimbo iliyogawa Bahari ya Shamu kati ikiwa moja ya vitu vingine vya miujiza kama Mana kutoka Mbinguni. Safina ya Agano ni mfano wa yale yaliyo Mbinguni. Ninawaambia haya sasa kama onyo kama nyakati za kale, msifikirie kuwa yeyote ataishi ambaye hushika boxi hii ya ajabu inayoitwa Safina ya Agano, isipokuwa wale waliokadiriwa kustahimili kuigusa na kuifungua.

Someni Maandiko yenu na oneni tu ni kwa maombi na sifa na Mikono Takatifu iliyooshwa katika Damu ya Mwana WANGU YAHUSHUA ndipo Safina ya Agano yaweza kufunguliwa na itatumika tena kwa wakati fulani uliopangwa na kukadiriwa. Na kama wakati ule wa Moshe, itatumika kuwakomboa watu wa YAHUVEH kwa njia, kwa wakati ambao hamfikirii itakayoleta MIMI, YAHUVEH, na YAHUSHUA Sifa, Heshima, na Utukufu. O Israeli, je, hamjui kuwa wakati askari wa kirumi walipovua nguo za YAHUSHUA na kugawa mavazi YAKE kama ilivyotajwa kwenye Tanakh, “Waligawa mavazi YANGU kati yao na kwa vazi LANGU walipiga kura.” (Yohana 19:24)

Walisema haya kati yao wenyewe, “Tusirarue vazi lake lakini tupige kura, kuona itakuwa ya nani.” O Israeli, je hamuoni kuwa kama tu hawa askari wa kirumi walivyogawa nguo za YAHUSHUA, hivyo pia ardhi yenu wanaigawa na Roma imehusika kwa siri. Kama vile tu vazi la YAHUSHUA lilichezewa kamari, yule aliye na kiulizio kikuu kugawa ardhi yenu atawafunua na kuwasaliti kwa dunia yote kuona.

O Israeli, MIMI daima huwatuma Manabii WANGU kuwaonya kabla Hukumu haijaja. Mmeonywa siku hii lakini ni Mabaki Watakatifu tu watakaosikiza na kutii. Kwa yeyote anayeita MIMI, YAHUVEH, katika Jina la YAHUSHUA MASIHI, yeyote atakayetubu, atakayeacha dhambi zake akiniuliza MIMI, YAHUVEH, kwa msamaha, wanaonipenda na kunitii MIMI, kuamini na kunipokea MIMI na Uungu Wa MWANA WANGU ili YAHUSHUA Aweze kuwa mwombezi wenu wa pekee mbele YANGU. Kwa kuwa ni YEYE pekee Anayestahimili kuja mbele YANGU katika Jina LAKE. Msijaribu kukaribia Kiti CHANGU cha Mbinguni bila jina la YAHUSHUA. Msije katika utakatifu wenu lakini njooni kama mmevaa mavazi ya utakatifu ZAKE. Basi Nitawasikia na kujibu maombi yenu na mtaokolewa kutoka kwa moto wa Jehanamu.

O Israeli na o Yerusalemu, nyinyi ambao mnapendelea kubaki viziwi MIMI, YAHUVEH, Ninajirudia tena na tena kwa niaba yenu. Amkeni sasa, kwa kuwa wakati ni wa kuchelewa. Siwaambii mbadilike kuwa Wakristo kwa kuwa hata wao huona YAHUSHUA tu kwa sehemu ndogo. Wamekataa umuhimu wa kufunza Uyahudi wa YAHUSHUA. Wamekataa upako kwa kuzungumza Jina la YAHUSHUA na Majina YANGU Takatifu. Wamekataa Sabato ZANGU, Sherehe ZANGU Takatifu na Siku Takatifu, wale wanaojiita Wakristo Takatifu na lazima wajifunze kukubali Uyahudi Niliyoiweka ndani yenu na kupitia mbegu ya Abrahamu, Yakobo na Isaka.

O Israeli na Yerusalemu, amkeni sasa kutoka kwa usingizi wenu. Ilikuwa kwa sababu ya ukaidi wenu, na kwa ajili ya Mataifa, Nilifunga macho yenu, lakini wakati umekuja sasa, fungueni macho yenu wazi, funua wale wanaozungumza hizi uongo.

Nikiwakera wengine, Nikiwasaidia wengine katika Jina la YAHUSHUA MASIHI.

* * * * * * *

Familia wapendwa, Tafadhali sikieni huru kunakili hizi unabii na tusaidie kufika mataifa ya dunia hii, sanasana Israeli na Yerusalemu. Mataifa yote ya dunia hii inaathirika na yale yanayofanyika pale Israeli. Elisabeth [Elisheva] anachouliza ni tafadhali acha ujumbe ilivyo, hata nakala zake za kibinafsi.

Elisabeth [Elisheva] anajua kuwa kwa kawaida majina hayaandikwi kwa herufi kubwa, lakini RUACH ha KODESH Alimuambia kuwa majina ya MUUMBA wetu na MASIHI inapaswa kutengwa na kuandikwa tofauti, ikionyesha utakatifu na heshima kwa jina zao. Kwa heshima kwa yale aliyoambiwa, tafadhali mnapofasiri unabii, fanyeni vivyo hivyo.

Elisabeth [Elisheva] anaomba msamaha kwa muda uliochukua kuweka hizi unabii kwenye tovuti, lakini kulikuwa na gharama ya kulipa kwa unabii 80 na 81. Ilikuwa vita dhidi ya shetani lakini kwa sababu ya maombi yenu na msaada katika jina la YAHUSHUA, tulipata ushindi juu ya vita hiyo. Sifa, Heshima na Utukufu wote kwa YAHUVEH na YAHUSHUA MASIHI.

Kwa sababu mimi ni Myahudi wa kuzaliwa kutoka kwa mama yangu wa kuzaliwa na baba na Myahudi wa Kiroho kupitia Damu iliyomwagwa ya YAHUSHUA. Nina upendo kwa Israeli na Yerusalemu na watu Wayahudi, hata ingawa ninajua wengi kule Israeli watanichukia kwa neno hili. Mimi tu ni Nabii aliyetumwa na YAHUVEH kuzungumza maneno YAKE na ninafanya haya kwa hofu na kutetemeka. Nabii yeyote wa kweli ambaye hafanyi haya, nina swali… wanawezaje kuwa Nabii Takatifu?

Ninaomba kuwa sijaacha hata neno moja nje wala kuongeza moja, na sasa ninawapa ujumbe huu wa kinabii na kuuliza wote wanaopenda Israeli na Yerusalemu kunakili haya na kuweka kwenye mitandao yao. Tumekuwa na Wayahudi halisi na Waislamu wakimkubali YAHUSHUA kama MASIHI na hautajua wakati tunapopanda mbegu itakayokua kuwa tunda nzuri la Wokovu. Ujumbe huu wa kinabii ulikuja baada ya ndoto juu yangu na kabila 12 za Israeli. Itawekwa kwenye tovuti hivi karibuni. Ujumbe huu ulikuja mnamo Januari 24, 2006 lakini YAHUVEH Akasema isitolewe kwa kuwa hakuwa Amemaliza. Februari 7, 2006 YAHUVEH tena Alianza kutabiri na ilikuwa mfulizo wa unabii huu.

P.S. Muhimu. Nabii, ndugu katika YAHUSHUA aliniandikia mimi kutoka Yerusalemu mwaka uliopita na kuniambia mimi alikuwa anachukua unabii hizi nilizopewa kote Israeli na kuwaonya watu. Sikupata fursa ya kumshukuru mwanamume huyu, na ninataka kufanya hivyo sasa. Pole sana sikuweza kukujibu kwa sababu nimepoteza anwani ya barua pepe yako. Sijui jina lako, lakini ninataka ujue kuwa nimeshukuru kwa kweli na upo kwa maombi yangu na utaniandikia tena.

Nimekuwa nikiombea mfasiri Mwebrania kufasiri jumbe hizi za kinabii za kiingereza hadi kiebrania. Nikiwa kwa maombi, YAHUSHUA Aliniambia kuwa tayari Ametuma mfasiri anayeweza kufanya haya, na YAHUSHUA Akanikumbusha wewe. Tafadhali niandikie tena. Sina shaka kuwa Ndugu huyu ni sehemu ya Bibi Arusi wa YAHUSHUA. Kama yeyote anayesoma haya anajua yeyote anayeweza kuandika Kiebrania na kuizungumza vizuri ili unabii hizi zipewe kwa Israeli, na zinaweza kurekodiwa katika Kiebrania, tafadhali niandikie mimi pale Wasiliana Nasi, sina shaka kuwa kuna wale walio Bibi Arusi wa YAHUSHUA wanaoishi Israeli na sanasana Yerusalemu.

Tafadhali njooni, kwa kuwa muda ni mfupi sana sasa kwa kufikia Israeli. Tuko pumzi moja tu kufikia Dhiki Kuu. Tafadhali, sehemu ya Bibi Arusi wa YAHUSHUA, kubaliana na mimi katika maombi kuwa huyu mwanamume ataniandikia mimi tena, na kuwa Mfasiri Mwebrania atajitokeza. Mwaka huu macho yetu yafai kuwa kwetu sisi lakini kwa Israeli. Bibi Arusi wa YAHUSHUA tafadhali ombeni kwa amani ya Israeli na Yerusalemu kwa njia mpya. Ombeni kuwa Mfalme wa Amani YAHUSHUA MASIHI Aje tena.

Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu)

Februari 7, 2006 Saa 5:00 Jioni

* * * * * * *

BARUA PEPE ZILIZOPOKEWA KUHUSU UNABII 80 NA 81:

* * * * * * *

Habari dada,

Nilichukua bibilia, na nikataka kutenga maneno mengine kumpa mtu. Na nikafungua kwenye Kitabu cha Ufunuo wa Yohana 14:14-20. Hapa inazungumzia ulichosikia. Shinikizo kubwa la ghadhabu ya Mungu. Pamoja na mavuno makuu. Na kabla ya hapo kuwa YAHUSHUA yupo na Bibi Arusi WAKE walio tayari na wamewekewa muhuri. Kwa hivyo tupo tayari kuona mapigo yakija duniani humu, bila kipimo. Yote yanajifunua, kwa sababu mpinga kristo hayupo mbali.

L

* * * * * * *

Baraka kwa nyumba yako,

Nataka kukuambia niliomba kwa upako mkuu asubuhi hii kutoka kwa unabii 81 na nilipokuwa nikimwombea mwingine mchana huu upako ulikuja juu yangu kwa nguvu ikawa ni kama sauti nyingine ilikuwa inatoka ndani yangu na machozi! Wow, ilikuwa imenizidi lakini niliikaribisha na niko tayari kufanya kile ambacho Yahu’weh na YAHUSHUA wanataka nifanye. Sabato Njema.

Michelle

* * * * * * *

Dada Mpendwa,

Nimesoma unabii 81 na 80 na ninataka na lazima nikueleze kuwa hii ni uthibitisho kwako. Wiki mbili iliyopita katika Mkutano wetu wa Sabato tulikuwa tunaomba na tulipokuwa tunaomba tulihisi upako kama vile hatujawahi kuhisi kwa muda. Na nilikuwa ninaomba kwa bidii kuhusu yote niliyokuwa ninaona kwa kiroho. Na ilikuwa kuhusu Israeli na Yerusalemu na Hamani (S). Wao ni adui sawa lakini umbo tofauti. Lakini jina hilo linasimamia jambo sawa. Na nilijua kuwa Sherehe hii ya Purim ijayo inafaa kuwa sherehe kama tu vile Hamani hakufaulu, pia Hamas hawatafaulu.

L… … Mmoja wa Bibi Arusi (Uholanzi)

* * * * * * *

Dada Mpendwa Elisabeth (Elisheva),

Ninaombea afya yako na ustawi wako. Nilisoma unabii zilizotoka juzi kutoka kwenye tovuti yako. Unabii 80 inatupa moyo na tuombee amani ya Israeli! Ninaposoma unabii, ninahisi uwepo wa baba wetu wa mbinguni YAHUVEH! Ninajihisi vizuri sana.

Upendo mwingi katika YAHUSHUA,

Stephen

* * * * * * *

Shalom katika Yeshua!!!

Mwili wa 80 na 81, RUACH Ha Kodesh tayari Amenifanya kuomba!!! HalleluYAH!!!

Ndugu Tito

* * * * * * *

Sabato Njema katika Yeshua!!!

Wow!!! Nilipiga Shofar kama nilivyosema kwako na kwa familia yako, na kwa YHVH kuwa Adui kwa maadui wetu. Sijui kama nilizimia au kama YHVH kupitia RUACH Alinigonga kwenye sakafu, lakini kwa kweli nilikuwa chini!!! HalleluYAH!!!

* * * * * * *

Shalom Elisabeth (Elisheva),

Asante kwa kutuambia ndoto yako “Elisabeth (Elisheva) na Wok” kuhusu zeituni kwenye mchakato wa kupika. Yote yanapatana pale chini. Bibi Arusi waaminifu wanaitwa “Israeli”.

Kilichokuja akilini mwangu kuhusu zeituni, ndio, ninakubali kuwa zeituni inawakilisha kabila 12 za Israeli.

Kabila 12 ndio mabaki ya YAHUVEH walio waaminifu na hutii amri zake, na wana ushuhuda wa Yahushua. Sio Israeli (kidunia) tunavyoifikiria leo. Israeli ya kweli ni wale waumini wanaotembea na kusikia sauti yake. Wao ndio bibi arusi waaminifu wasio na kasoro wala madoa. Wakati hizi kabila 12 wanapokutana pamoja kama moja. Kutakuwa na upako mkuu na mkubwa zaidi katika nyakati hizi za mwisho kabla Yahushua arudi. Yahushua hatarudi hadi kabila hizi 12 zije pamoja. Kuna kutakaswa kwingi lazima kufanyike kati ya waumini. O tuondoe hizi kasoro na madoa kwetu kujitayarisha kwa kuja kwa bwana arusi, Yahushua.

John Davies

* * * * * * *

Habari Elisabeth (Elisheva),

Labda ni wakati kwa Mashahidi Wawili kutambuliwa au kuitwa na Yahuveh. Tunahitaji kuomba kwa kuwa upako unaweza kuwa waja juu ya hawa watu na Shetani anaweza kuwa amekasirika sana. Tunahitaji watakatifu kuombea ulinzi wa Mashahidi. Kwa sababu baadaye wanakadiriwa kuuwawa lakini watafufuliwa tena baada ya siku tatu.

Ni wakati sasa wa kukutumia makala ya Eliya na Manabii wa Baali. Haya yanasema mengi. Sikuiandika, lakini iliugusa moyo wangu kwa miaka sasa. Huwa ninaituma mara kwa mara kwa vikundi vya habari.

Nimekubaliana na Yahushua kuleta hizi kabila 12 pamoja kupitia Elisabeth (Elisheva). Kutakuwa na wasaidizi katika haya. Nimekuwa nikiwa na kugumia katika roho yangu kuwaleta ‘Kabila 10 zilizopotea’ na tovuti iitwayo Kosher kwa Mataifa ambayo yatengenezwa. Nimekuwa nikingoja thibitisho kwa tovuti yangu, na kwa Yahushua kunisaidia mimi kuijenga. Imekuwa sasa zaidi ya mwaka mmoja kwa kuwa nangoja ‘Wakati wake.’ Ninaamini kuwa ninahitaji kutakaswa kabla haya yafanyike. Lazima sote tuwe watulivu na kama Mfalme Dausi husema, “ngojeni wakati wa Yahuveh.”

Kemeo linaweza kuwa Yuda hajaruhusu wale kabila kumi kurudi kwa sababu wao kama fumbo la Mwana Mpotevu (kabila 10) wamewafuata miungu mingine (Ukristo) na wamekuwa Mataifa, na wapo katika mchakato wa kurudi nyumbani kwa nyumba ya Baba (Torati) na mwana mwaminifu (Yuda) aliye nyumbani ana wivu kwa kurudi kwa mwana aliyerudi na humkataa kama sehemu ya Familia (Israeli). Yuda amekuwa akikataa kumruhusu Efraimu kurudi Nyumbani. Kila jaribio la Efraimu kurudi limeangaliwa na Yuda kama jaribio lingine la theolojia mbadala au imani inayofuata bibilia kwa kina.

Secondly, wakifananishwa kwa wakuu 12 wa kabila hizi (ndugu) walimuuza Yosefu (Efraimu) katika utumwa (dhambi) na Yosefu akawa mtu mkubwa, kiongozi wa ufalme mkubwa (Marekani) alipojionyesha kwa ndugu yake (Yuda) hawakumtambua (Efraimu) mpaka alipojidhihirisha kwao.Yahuveh alifungua macho yao na Familia ikaunganishwa tena.

Nitahitaji kuwajumuisha Wayahudi, kwa kuwa watataka kujua kuhusu Mataifa na Kosher.

Michelle

* * * * * * *

Mpendwa Elisabeth (Elisheva),

Kulikuwa na pepo iliyokuwa imenifunga kwa kutosifu na kutoomba na polepole ikafika mahali sikuweza kuongea jina la YAHUVEH au YAHUSHUA. Nilikuwa ninangoja wakati WAKE mzuri kukombolewa kutoka kwa haya, na niliposoma unabii 80 na 81, Niko HURU!!!!! Sifa kwa YAHUVEH, YAHUSHUA na RUACH HA KODESH!!!!!

* * * * * * *

Wahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali Wasiliana na Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred