Unabii 53

MIMI Nimewapa Nyinyi Ushindi!

Imezungumzwa katika Upako wa RUACH HA KODESH Kupitia Mtume, Nabii Elisheva Eliyahu mnamo Machi 28, 2002

Unabii wa Pasaka

* * * * * * *

Yafuatayo ni Unabii ulivyokuja

—na Nabii Elisheva, akizungumza katika "Ndimi Takatifu," kama ROHO wa MUNGU alivyomjalia kutamka (Matendo ya Mitume 2:3-4) kwa lugha za wanadamu na malaika (1 Wakorintho 13:1). Elisheva anazungumza katika ndimi Unabii ukitokea (1 Wakorintho 14:6).

Tunatumia Majina ya Kiebrania ya MUNGU:

YAH/YAHU יה ni JINA TAKATIFU la MUNGU, kama vile “Alleluia” au “Hallelu YAH” הללו–יה ambayo humaanisha “Msifu YAH”: YAHUVEH/YAHWEH י-ה-ו-ה MUNGU BABA; YAHUSHUA/YAHSHUA יהושוע MWANA WA PEKEE WA MUNGU—(HA MASHIACH המשיח inamaanisha “MASIHI”; ELOHIM אלוהים inamaanisha “MUNGU.”) Ufunuo wa “SH’KHINYAH GLORY” שכניה תפארה —kama Jina la Kibinafsi la RUACH HA KODESH רוח הקדש, (katika Kiingereza “ROHO MTAKATIFU”) —upo kwenye tovuti hii. (HA SH’KHINAH {SHEKINAH} ni Kiebrania ya UWEPO WA MUNGU, UWEPO MTAKATIFU.)

Zaidi ya hayo, ABBA YAH אבא יה humaanisha “BABA YAH” na IMMA YAH אמא יה humaanisha “MAMA YAH.” Katika Kiebrania, ROHO WA MUNGU ni kike, Anatajwa kama “SHE,” na Ametajwa vivi hivi katika Unabii na Maandiko pale chini. Pale MUNGU Anapotajwa tunatumia herufi kubwa.

Maandiko yaliyotajwa yametoka KJV/NKJV au CJB, isipokuwa pale palipotajwa vinginevyo.

* * * * * * *

Onyo la YAHUVEH Mbele ya Unabii:

Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako.

Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha.

Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo.

Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. ‘‘Mimi Ndimi BWANA YAHUVEH: hilo ndilo JINA LANGU! Sitampa mwingine UTUKUFU WANGU, wala sanamu SIFA ZANGU” (Isaya 42:8).

(Unabii 105)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH Alisema kuongezwe yafuatayo kuonya wale ambao wanakejeli:

“Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.” —2 Mambo ya Nyakati 36:16

* * * * * * *

Unabii 53 Unaanza

Kwa kweli watoto WANGU mnaangalia Bahari ya Shamu.

Kwa kweli watoto WANGU Farao muovu

na jeshi wapo nyuma yenu,

lakini watoto WANGU kama vile Nilivyowapa njia ya kutoroka

kwa Musa na Watoto wa Israeli,

Nitayafanya yaya haya tena.

Watoto WANGU, katika siku zifuatazo mtaona vitu vikija juu ya dunia hii

ambavyo vitawafanya kutingiza vichwa vyenu. Na mtashangaa na mtasema,

“Je, YAHUVEH & YAHUSHUA wetu wako wapi leo?”

Lakini wekeni imani yenu na wekeni macho yenu KWANGU MIMI

na mtaona- Bahari ya Shamu

ikigawanyika tena

na mtavuka kwa usalama-

na maadui wenu wataangamizwa.

Wote ambao wanakuandama!

Wote ambao wanakukimbiza! Wataangamizwa.

Kwa kuwa MIMI ni YAHUVEH na MIMI sibadiliki.

MIMI ni YAHUVEH, na MIMI ni yuleyule-

leo, jana na milele.

Na kupitia Damu ya MWANA WANGU YAHUSHUA,

mnakuja kwa ujasiri mbele ya Kiti cha Enzi, mnaniambia MIMI kwa ujasiri

kile mnachohitaji.

Ninawaambia haya leo hii,

Nimewapa ushindi.

Ninawaambia siku hii!

Ninawaambia haya leo hii

Kuwa hakuna chochote ambacho adui alitaka kufanya

Niliruhusu kifanyike.

Ninawaambia,

Nimewapa ushindi

-ingawa mmepigana kwa masaa

Na upanga wa ROHO WANGU mkononi.

Tena, watoto WANGU,

Mmeona ushindi.

Haikuwa ushindi wa rahisi.

Sijawahi kuwaahidi kuwa itakuwa ushindi wa rahisi.

Ninapowaambia itakuwa ushindi,

Hakuna yeyote aliyewaahidi kuwa itakuwa rahisi.

Ni ukweli kuwa nira YANGU ni rahisi

Na mzigo WANGU ni mwepesi,

Lakini watoto WANGU kuna gharama ya kulipa

Kwa Upako Niliouweka

Kwa maisha yenu nyote.

Kwa hivyo kuleni sherehe hii ya Pasaka-mkule

na hata

“msinung’unike wala kuwa na tamaa

Kwa sababu ni heri muifanye

Na moyo wa shukrani na kumbuka kilichofanyika

Na Watoto wa Israeli.

Kumbukeni Watoto wa Israeli

Waliozunguka miaka 40.

Haingekuwa vile

Kama hawangenung’unika,

Kupiga kelele na kuwa na tamaa,

Lakini Nikawafanya watembee kule mara kwa mara

Kama wengine wanavyosema, kwa duara.

Niliwafanya watembee kule mara kwa mara

Na kuwajaribu wao tena na tena.

Ninawaambia nyinyi watoto WANGU, Ninawaambia ukweli.

Msinung’unike, msipige kelele, msiwe na tamaa

Hata Niruhusu nini kifanyike – kwenu.

Badala ya haya inueni macho yenu KWANGU.

Badala ya haya peeni YAHUVEH & YAHUSHUA utukufu.

Na jueni kuwa MIMI pekee Ndiye MKOMBOZI wenu!

Na jueni kuwa pekee

Kupitia Damu ya MWANA WANGU YAHUSHUA Iliyomwagwa

Kuwa mna ushindi;

Kupitia Jina Takatifu la YAHUSHUA

Pekee mna ushindi.

Nimewaahidi haya

Na kama tu mtatii,

Kama mtatega sikio

Kwa kila Ninachosema,

Ninawaambia haya watoto WANGU,

Mtakuwa na ushindi.

Kumbukeni, kuwa ushindi huja na gharama.

Kumbukeni, hakuna askari yeyote

Anayeenda kwenye vita

Na hahisi kuchoka.

Hakuna askari yeyote ambaye

Kwa wakati mmoja hutaka kukimbia.

Lakini kumbukeni watoto WANGU, kumbukeni haya

Kuwa Nimewaahidi ushindi

Kama tu mtatii.

Kama mtatega sikio kwa kila neno Ninalosema,

Kama mtabaki katika Utakatifu na kuishi

Kama mfano kwa wote kuona

-Ninawaambia haya- watoto WANGU,

Nyinyi na Huduma hii mtaona

ushindi kamili.

Mtaona maadui wenu wakifa

-kwa Mkono WANGU pekee.

Mtaona maadui wenu wakikimbia

-kwa Mkono WANGU pekee.

Mtaona maadui wenu wakiinama na kupiga magoti

-na kuungama YAHUSHUA kama BWANA & MASIHI.

Na itakuwa, tu, kama Nilivyokadiri:

Ushindi katika JINA la MWANA WANGU YAHUSHUA-

Na mtajua kuwa gharama mliyolipa

Haikuwa bure.

Kwa kuwa Nimewapa nafasi kuu

Ya kuniletea MIMI utukufu kupitia mateso yenu

-kama vile Manabii wa Kale-

Wakati watu watakuona ukisimama,

Watajua kuwa ni kwa Mkono WANGU

Unaokulinda na kukuongoza

-kwa njia zote.

Watoto WANGU, furahieni sherehe hii ya Pasaka

Niliyowapa leo hii.

Asante kwa kunitii MIMI.

Asante kwa kusikiliza.

Kwa kuwa baraka za Unabii huu wa Pasaka

zilikuwa kwa wengine na sio wewe pekee yako.

Waambie kama walikosa kufanya maelekezo ya pasaka,

Hata tu wanavyoweza- ila tu wanitambue MIMI,

(kuwa MIMI Ndiye yuleyule YAHUVEH Aliyewakomboa

Watoto wa Israeli

Kutoka kwa wenyeji wa Misri na kutoka kwa laana

Na mapigo yaliyokuja);

Waambie, kama tu watoto WANGU watayafanya haya

Wanavyoweza- na kunitambua MIMI,

Haijalishi ni siku gani kwenye kalenda:

Palipo Pasaka yao, ndipo imani yao ipo

-na pale imani yao ipo, ndipo Pasaka yao ilipo.

Mwisho wa Rekodi.

Nikiwakera Baadhi ya watu; Nikiwabariki Wengine

Kwa Upendo & Kutii & Utukufu

Wa YAHUVEH & YAHUSHUA MASIHI

Siku ya Kwanza ya Pasaka – Machi 28, 2002

Ilipewa kwake Mtume, Nabii Elisheva Eliyahu

* * * * * * *

Je, Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una mchango au maswali? Tafadhali wasiliana na Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred