Unabii 44

Inukeni Wachungaji Kwenye Ukuta!

Imezungumzwa katika upako wa Mtume Elisheva Eliyahu Oktoba 8, 1998.

Haya yanatoka kwenye Unabii 105, YAHUVEH Alisema iwekwe mbele ya Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya kila Unabii:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii Wake, hata ilipozidi Ghadhabu ya Bwana juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

Kwa kuwa Ninawaita wengi sasa, Ndivyo Asemavyo YAHUVEH. Hawa ndio viombo WANGU waliojitolea, vyombo vilivyojitolea katika jeshi LANGU la kiroho ambao wataleta umoja katika mwili WANGU. Wataleta mpango. Kwa kuwa sasa ndio wakati, Ndivyo Asemavyo YAHUVEH, sasa ndio wakati wa wachungaji WANGU. Sasa ndio wakati wa wale ambao waliotembea masaa ya usiku wa manane. Inukeni, inukeni, inukeni, enyi watu mnaolala. Inukeni sasa, inukeni sasa, inukeni sasa, na kutangaza ushindi. Jeshi la kutisha na lenye nguvu, jeshi ambalo litasababisha adui kutingika na kutetemeka kwa hofu wanaposikia sauti ya mkusanyiko na wa kutembea kwenu kwenye ardhi. Endeleeni kulia na kutangaza na kuhubiri injili ya wokovu.

Kuleni chakula chenu cha kiroho na fukuza usingizi kutoka machoni mwenu na sikieni sauti za wachungaji WANGU. Kwa kuwa ni kwa wao ambao Nimewapa haya, Neno LANGU, kwa nyinyi kuinuka, inuka, inuka, Ndivyo Asemavyo YAHUVEH fanyeni yale ambayo yanafurahisha machoni MWANGU. Fanyeni yale ambayo yananiletea MIMI Utukufu na yale ambayo yataleta mavuno makuu ya nafsi na Nitajua kwa kweli mnanipenda. Inukeni, inukeni, inukeni na amkeni kwa ukweli na mjifunike na ukweli na kusimama katika ukweli huo na kutembea katika ukweli huo kwa kuwa mpango WANGU wa milele umejitokeza kati yenu na bado kuna matayarisho mengi ya kufanywa na fanyeni kile ambacho Nimewaumba kufanya.

(Baba YANGU wa Mbinguni Alizungumza haya kwangu leo na kusema vitu hivi kwangu leo, kwa uwazi, kwa uwazi. Kwa kuwa kuna mawingu ya dhoruba ndani ya nyoyo za wanadamu ambayo haionekani katika ulimwengu huu na mawingu ya vita inapokusanyika kwa upeo wa macho, na tmgurumo na radi kutoka kwa nguvu ya mawingu hiyo ya vita inayoendelea kujitokeza ndani yao.)

Mnasikia na mnaona, msiogope, Ndivyo Asemavyo YAHUVEH, kwa vitu hivi ambavyo ni vya KWANGU. Kwa hivyo tayarisheni nyoyo zenu, vitu hivi ambavyo vimekadiriwa vitajitokeza vyenyewe, Ndivyo Asemavyo Mwenyezi YAHUVEH. Nimewatayarisha vyema wale WANGU Niliowaita. Sio wajibu wenu wa kujua chanzo cha ukweli ni kipi. Ni wajibu wenu tu kuukubali ukweli WANGU, Ndivyo Asemavyo Bwana Mungu wenu. Kwa kuwa mtatambua yale ambayo ni kweli kutoka kwa yale ambayo ni uongo na mtakuwa na amani katika nyoyo zenu kuwa vitu vile ambavyo ni vya KWANGU ni kwa uzuri wenu na mtatambua vile vya uongo na vilivyotumwa na adui na wafuasi wake kuwadanganya. Kueni waangalifu; na kaeni macho.

Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!

Tuma Barua Pepe Kwa Nabii Elisheva Eliyahu



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred