Unabii 41

Bibi Arusi WANGU wa Kweli Simameni!

Imepewa kupitia Mtume Elisheva Eliyahu Septemba 17, 2000

Unabii 41 ulipokuwa unazungumzwa na kuandikwa siku ya Septemba 17, 2000, kulikuwa na polisi 3 waliozunguka nyumba yangu na gari nyeupe ambalo halina alama waliposimama mbele ya nyumba yangu. Mwana wangu aliona mwingine nyuma ya nyumba na mwingine kando ya nyumba. Akasema alikuwa amekuja kwa sababu ya simu za 911 zilizotoka kwenye anwani hii. Nikamuambia kuwa hayo sio kweli, kwa sababu hakukuwa na yeyote mwingine hapa ila tu mwanangu na nilikuwa kwa simu wakati huo nikiongelesha rafiki mwingine. Haya yalifanyika dakika kadhaa baada ya mimi kukata simu baada ya kusoma Unabii wa “Msiwe Sehemu ya Bibi Arusi Bandia”. Tafadhali Ombeeni usalama wangu.

Elisheva Eliyahu

* * * * * * *

Haya yanatoka kwenye Unabii 105, YAHUVEH Alisema iwekwe mbele ya Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya kila Unabii:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii Wake, hata ilipozidi Ghadhabu ya Bwana juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

Bibi Arusi WANGU hawawezi kuingia bila harufu nzuri ya upako WANGU. Hauwezi kuzidisha harufu hiyo nzuri ya upako WANGU. Mnafaa kutafuta upako mkuu. Acha ijulikane kuwa hakuna mwanamume au mwanamke yeyote anayeweza kukupa upako huu; Ni RUACH HA KODESH WANGU Mpendwa tu Anayeweza kukusafisha na manukato hii ya upako WANGU iliyotengwa kwa Bibi Arusi WANGU. Jitayarisheni kuenda nyumbani na kuloweka na nguvu, upako wa RUACH HA KODESH. Vaeni nguo zenu za arusi. Ni vazi LANGU la utakatifu. Nilivaa taji la miba. Mtavaa taji za Utukufu WANGU ambazo zimewekwa juu ya vichwa vyenu. Kama Esta alivyojitayarisha kwa mfalme, mnajitayarisha kwa MFALME wa WAFALME, BWANA wa MABWANA, BWANA MUNGU MWENYEZI YAHUSHUA NDILO JINA LANGU NA MIMI NDIYE BWANA ARUSI AMBAYE YUAJA!

Kama vile tangazo la arusi linapotoka, na mialiko inatumwa, MIMI pia hutuma tangazo LANGU Gabrieli anapopiga tarumbeta, na ni wale tu ambao ni Bibi Arusi WANGU wataisikia tangazo hilo kwa Bibi Arusi WANGU. Mtakuwa mmechelewa kufikiria kujitayarisha wakati huo, kwa hivyo kaeni tayari kwa tangazo lijalo, mtaifanya nyinyi wenyewe au kupitia Mitume na Manabii WANGU. Sikizeni onyo LANGU! Sikizeni onyo LANGU ambalo lasema kuwa Naja. Ni elopement, kwa sababu BWANA ARUSI Anajua kwa uhakika. Sasa endeni, msiaibike na mpeane mwaliko. Msishangae na wengi ambao wataikataa. Lakini msihuzunike, kwa kuwa hawakufaa wala kupita mtihani wa swali, au uaminifu, au mtihani wa upendo, au mtihani wa dhabihu au mtihani wa kutii. Kwa hivyo, wao hawafai kuitwa Bibi Arusi WANGU. Kutakuwa na wale ambao watauchukua mwaliko huu na kuurarua, kutakuwa na wale ambao watauchukua na kuuweka kwenye rafu kwa muda mrefu na hawatautumia. Hawa wote sitawaita WANGU.

Bibi Arusi WANGU wameningoja sana na Ninakuja kuwachukua Bibi Arusi WANGU. MIMI sioni rangi wala dini. Haijalishi wewe ni rangi gani au wa dini gani, MIMI hutafuta uhusiano NAMI na Ninatafuta kitu kimoja, ambacho ni rangi nyekundu ambayo ni Damu YANGU iliyomwagwa pale Kalivari. Kwa hivyo Ninasema tena nyumbani KWANGU ambayo ni Mbinguni itakuwa nyumbani kwenu hivi karibuni. Mtanyakuliwa hewani kukutana NAMI kuletwa kando YANGU kama bado mko hai. Miguu YANGU haitakanyaga ardhi hii ya dunia hii ya waovu ilivyo sasa, kwa hivyo jitayarisheni Bibi Arusi WANGU kunyakuliwa kama bado mpo hai. Acha wakejeli. Ninasimama kwenye mlango na Nitaugonga. Kile wanachofaa kufanya ni kuufungua mlango wa moyo wao na kutubu na kunialika MIMI ndani na MIMI ni mwaminifu na Nitawasemehe dhambi zao zote.

Waulize, mbona wanataka kuteseka kule Jehanamu au kuchomwa katika Ziwa la Moto? Haikuumbwa kwa wao. Iliumbwa kwa wale waovu. Nililipa gharama pale Kalivari na kuwachukua kutoka mikononi mwa shetani ili wanadamu wote wapate kuwa huru. Lakini MIMi ni muungwana. Sitauvunja mlango. Ninaubisha tu na kungoja Nialikwe ndani. Kwa hivyo mara nyingine, Ninawaambia kuwa YAHUSHUA MASIHI ambaye wengine wananiita MIMI Bwana Yesu Kristo, Anarudi. Waambie Bibi Arusi WANGU kuwa Ninarudi tena kuwapeleka nyumbani. Jitayarisheni kuenda nyumbani kwa kuwa Nyumbani KWANGU ni nyumbani kwenu. Jitayarisheni kuja nyumbani, kwa sababu Naja kuwapeleka Bibi Arusi WANGU nyumbani! Hivi karibuni mtaisikia sauti ya tarumbeta ya Gabrieli, na mtanyakuliwa kando YANGU Ninavyowaita kama Bibi Arusi WANGU. Mtayasikia maneno Njooni hapa kama sauti ya malaika mkuu anavyopiga tarumbeta. Jitayarisheni kuenda nyumbani kwa kuwa Ninawajia Bibi Arusi WANGU! Mmoja atachukuliwa na mwingine kuachwa.

* * * * * * *

Imeandikwa Septemba 17, 200 Saa 6:15 Jioni.

Imezungumzwa, imeandikwa.

Imepewa kwake huyu handmaiden Elisheva Eliyahu.

Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!

Tuma barua Pepe Kwa Nabii Elisheva Eliyahu



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred