Unabii 40

Usiwe Sehemu ya Bibi Arusi Bandia! Kama ndivyo… KIMBIA!

Imepewa kupitia Mtume Elisheva Eliyahu Septemba 17,2000

(Tafadhali ombeeni handmaiden huyu Elisheva Eliyahu. Ambaye Mungu amemchagua kutoa ujumbe huu mkali ambao utawakasirisha mamilioni, lakini yeye ni mjumbe tu. Tafadhali msimpige mawe mjumbe, Anarudia tu yale ambayo RUACH HA KODESH anasema kwa sababu moja tu: kuleta nafsi katika Ufalme wa Mbinguni. Kwa sababu ya urefu wa ujumbe huu, tumeugawa katika sehemu 1 na 2.)

* * * * * * *

Haya yanatoka kwenye Unabii 105, YAHUVEH Alisema iwekwe mbele ya Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya kila Unabii:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii Wake, hata ilipozidi Ghadhabu ya Bwana juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

Jitayarishe kuenda nyumbani. Kuenda nyumbani. Kurudi nyumbani kwako kwakungoja. Bibi Arusi WANGU lazima wawe tayari kurudi nyumbani. Ambieni Bibi Arusi WANGU wajitayarishe kurudi nyumbani. NINAWATAYARISHA Bibi Arusi WANGU kuenda nyumbani kunyakuliwa kando YANGU kama bado wako hai. Waambie mbali na karibu; waonye kwenye ardhi, anga na bahari. Jitayarisheni kuenda nyumbani NAMI. Ninawajia Bibi Arusi WANGU. Jitayarisheni kuenda nyumbani, kuja kwenye Sherehe ya Mwanakondoo. Siwezi kungoja Bibi Arusi WANGU kuja nyumbani pale Mbinguni kwa kuwa Nimengoja kwa muda mrefu. Waambie kuwa Nawajia Bibi Arusi WANGU. Naja, waambie mbali na karibu. Msiangalie hata gharama. Wekeni kiburi chenu chini, toa ujumbe, na waambie Bibi Arusi WANGU kuwa tayari wajitayarishe kurudi nyumbani.

Ni Bibi Arusi mgani ambaye hajui siku ya arusi inapowadia. Ni Bibi Arusi mgani ambaye hajui kuvaa nguo yake ya arusi. Jiwekeni, jisafisheni, ogeni na kujirusha katika Damu YANGU iliyomwagwa pale Kalivari. Jitayarisheni kuenda nyumbani. Ni Bibi Arusi mgani hataki harufu yake kuwa manukato kama harufu ya maua na viungo? Harufu ya Bibi Arusi WANGU sio ya kutengenezwa na binadamu au kupatikana mkebeni. Harufu ya Bibi Arusi WANGU ni ya kutoka Mbinguni. Ni upako wa RUACH HA KODESH Anayekupa harufu nzuri. Sio ya kutengenezwa na binadamu. Haipatikani mkebeni, upako wa RUACH HA KODESH WANGU ndiyo inayowafanya kunukia kama manukato. Wale ambao hawana upako huu ni kama uvundo kwa pua LANGU na hawatakuwa wanaenda nyumbani NAMI. Harufu ya upako WANGU ni Takatifu.

Kuna wengine wanaojiita Bibi Arusi WANGU, lakini wao sio Bibi Arusi WANGU. Wao ni Kanisa la Wanaojifanya wanaodai kunijua MIMI na kumbe hawanijui MIMI. Harufu yao ni bandia na ni uvundo kwenye pua LANGU. Bibi Arusi bandia huvaa rangi nyeupe

isiyo ya kiasili. Johari zake ni glasi. Tiara yake ni la bati. Anadai kunipenda MIMI, na kumbe hamna upendo pale. Je, Mbona hawa Bibi Arusi bandia wanasema kuwa wananipenda MIMI lakini hawanitii MIMI? Wanasema wanafanya miujiza katika Jina LANGU, lakini moto wao bandia unaniletea MIMI aibu.

Wao ni bikira watano wapumbavu waliopatikana bila mafuta kwenye taa zao. Utambi wa taa yao haijakatwa. Wanakataa Neno LANGU, hata Amri ZANGU kuibadilisha katika umbo lao wenyewe, sio kwa “MIMI NIKO” ni nani. Wanahamasisha dhambi hata kama Nimeiita dhambi. Wanapita mpaka hadi kujiita mungu. Wanaziandika tena upya Amri ZANGU. Wanaiandika tena upya Neno la “MIMI NIKO.” Kiongozi wao wa kiroho anaketi kwenye kiti cha enzi. Anatoa amri katika jina lake. Anakejeli gongo LANGU la chuma na kuiita fimbo. Anakejeli vazi LANGU la utakatifu na kuvaa vazi lililo na johari ndani yake.

Analikejeli vazi LANGU ambalo hujaza Hekalu na vazi lake ni ndefu sana. Hata anakejeli Neno LANGU Takatifu na anawafanya Watu WANGU kumuita mtakatifu. Yeye, kiongozi huyu wa kiroho anajulikana kote duniani. Kuna viongozi wengine wa kiroho katika makanisa mengine ambao wamefunzwa kuabudu binadamu aliyezaliwa kutoka tu kwa mwanamke na sio kuzaliwa kutoka kwa bikira. Hawa viongozi wa kiroho bandia wanawalazimisha watu kuinama miguuni mwao, wakikejeli Neno LANGU ambalo lasema kila goti litainama na kila ulimi kuungama kuwa YAHUSHUA MASIHI ni Bwana.

Kiongozi mwingine wa kiroho anajaribu kuongeza mwingine kwenye Utatu Mkuu. Huyu kiongozi wa kiroho anapeana ushirika LANGU na kamwe hataki kuwaambia watu watubu dhambi zao. Ni kipindi tu. Wale wanaofuata kiongozi huyu wa kiroho watamfuata hadi jehanamu na katika Ziwa la Moto. Hakuna chochote takatifu kwake kwa sababu anataka kuichukua nafasi YANGU. Hii ndiyo sehemu ya Bibi Arusi bandia ambao ni uvundo katika pua LANGU. Huyu kiongozi wa kiroho hawezi kujishusha katika macho yake au macho ya wengine kuosha miguu ya wengine. Kanisa hili ndilo lina pesa zaidi katika dunia hii, lakini wao ndio maskini zaidi katika imani. Huyu anawapotosha wengi na hata anawafanya kuungama dhambi zao kwake.

Huyu anathubutu kukejeli yule wa pekee ambaye ana haki ya kuwa hakimu wa wanadamu wote, na bado makuhani wanafunzwa kuwa wako na haki ya kutoa hukumu. Wanahukumu dhambi za wengine na makuhani wanapitisha sentensi. Hakuna yeyote anayefanya haya ni sehemu ya Bibi Arusi WANGU. Wao ni uvundo katika pua LANGU. Hata mbinu ya kusafiri inanikejeli vile Nilivyosafiri kwa punda. Wanakejeli pia msalaba. Hawa ndio sehemu ya Bibi Arusi bandia. Wanazungumza katika lugha ya kale inayojulikana tu na wasomi. Mmeonywa, Kimbieni kama nyinyi ni sehemu ya hawa Bibi Arusi bandia. Kwa kuwa wao ni uvundo katika pua LANGU. Kumbukeni kuwa Mimi Ndiye Bwana Mungu WENU na hamfai kuwa na Miungu wengine mbele YANGU. Msidanganyike kwa kuwa MIMI sikejeliwi virahisi. Kutakuwa na gharama ya kulipa.

* * * * * * *

Kwa kuwa imezungumzwa na imeandikwa chini ya upako wa RUACH HA KODESH. Imepewa kwake huyu handmaiden mnyenyekevu Elisheva Eliyahu.

Saa 6:15 Jioni Sepetemba 17, 2000.

Sehemu ya 2 – Unabii 41 – Bibi Arusi wa Kweli Simameni!

Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!

Tuma Barua Pepe Kwake Nabii Elisheva Eliyahu



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred