Unabii 38

NDOTO YA PIGO NYEKUNDU!

Imepewa kupitia Mtume Elisheva Eliyahu 8 Juni 2000

Haya yanatoka kwenye Unabii 105, YAHUVEH Alisema iwekwe mbele ya Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya kila Unabii:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii Wake, hata ilipozidi Ghadhabu ya Bwana juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

Mungu huzungumza na kuonya kupitia maono, ndoto, funuo baadhi ya njia zingine.

Niliona angani ukungu mzito wa rangi nyekundu ukija na nilipoangalia juu na ulipokaribia na upepo ukavuma uliwaangukia watu. ngozi yao ilifunikwa katika hii vumbi nyekundu (nyekundu kabisa) na watu wakawa wagonjwa SANA na kulikuwa na polisi aliyekuwa ananilinda na alikuwa na huu ukungu wa rangi nyekundu umemjia na akaruka kwenye bwawa la kuogelea nje niliposimama pale. Nilijua bwawa hilo litakuwa limechafuka lakini alitaka kuondoa hiyo vumbi nyekundu imtoke. Polisi huyu alikuwa mtu ambaye ninamthamini sana. Nilihuzunika kwa sababu haya hayakuwa ya kutosha.

Dakika ambapo UKUNGU huu wa rangi NYEKUNDU unagusa ngozi yako unaifunika na magonjwa makuu yaja na ngozi hiyo yaanza kukosa hewa. Nilitazama huyu polisi wangu mpendwa aliyekuwa mlinzi wangu, nikawa sijui la kufanya kumsaidia. Alafu nikaona ukija angani. Kwa sababu nisiyoijua sikuiogopa lakini niliweza kuuona ukija kutoka mbali. Ulianza kama giza kwa umbali kule juu angani na alafu ulipokuja karibu ukawa rangi nyekundu. Watu walijaribu kukimbia kutokana na haya lakini hawakuweza kuuepuka. Watu walijaribu kuuosha lakini wakati unapogusa ngozi basi hakuna la kufanya. Hii ndiyo sababu shetani anajaribu kunyamazisha sauti yangu katika kila njia awezayo. Acha wanaokejeli wakejeli, mimi nina wajibu kwa yale ninayosema na kutosema! (Ezekieli 3:17-21)

Haya ndiyo Nabii mwingine aitwaye Gary alisema nilipompigia na kumuuliza utambuzi wa ndoto hii. Ninajua ni kwa nini nililindwa na kwa nini Bibi Arusi wa YAHUSHUA watalindwa pia.

Elisheva,

Nilipofunga macho yangu niliona kidole cha Mungu ikishikilia nyumba ndani ya bubble ni kama nyumba hiyo imelindwa kutoka kwa dunia ya nje na ilikuwa salama ndani ya bubble hiyo.

Akili yangu ikaenda kwenye Pasaka ambapo agano la damu iliwafunika watu waliokaa ndani ya nyumba zao baada ya kujitayarisha na kuweka damu ya mwanakondoo kwenye milango yao. Kama haya ndiyo hayo, basi kwa kweli tunahitaji kuwaonya wengi.

Gary, tutangojea Ushahidi WAKATI tunafaa kupiga tarumbeta ya kuonya.

“Mahali Imani Yako Ipo, Ndipo Pasaka Yako Ilipo”

JUNI 8, 2000

UJUMBE MPYA KUTOKA KWA

Mtume Elisheva Eliyahu

Leo nilipomuuliza YAHUSHUA kuwa na RUACH HA KODESH WAKE Afungue Bibilia na kujibu swali langu kama Yeye yuaja hivi karibuni na labda hata mwaka huu, ikafunguka hapa

Ufunuo wa Yohana 3:7-21

Kazi tuliyo nayo lazima ifanywe kwa haraka kwa Utukufu wa YAHUSHUA MASIHI. Hakuna lolote ambalo litakalokuwa la umuhimu tunapotoka duniani ila tu tulichomfanyia YAHUSHUA na ni nini tulichomfanyia YAHUSHUA na ni nafsi ngapi tuliwaongoza kwa YAHUSHUA! Je, Kama sasa, umemfanyia nini YAHUSHUA ?

Ufunuo wa Yohana 3:10

Kwa kuwa umelishika neno la saburi Yangu nitakulinda hata utoke katika saa ya kujaribiwa inayokuja ulimwenguni pote ili kuwajaribu wote wakaao duniani.

OMBA kuwa hautakuwa hapa kuiona hii NDOTO ya PIGO NYEKUNDU ikija kutendeka!

Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!

Contact Prophet Elisheva Eliyahu



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred