Unabii 29

Ole Wenu Mbwa Mwitu Mliojivalia Ngozi ya Kondoo!

Imepewa kwake Mtume Elisheva Eliyahu Februari 4, 1999 2:12 Mchana

Haya yanatoka kwenye Unabii 105, YAHUVEH Alisema iwekwe mbele ya Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo kama onyo kwa wale wanaokejeli:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii Wake, hata ilipozidi Ghadhabu ya Bwana juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

(Maelezo) Ole wenu mbwa mwitu mliojivalia ngozi ya kondoo! Msiwaguse masihi WANGU wala kuwaumiza Manabii WANGU. Ingawa Unabii huu ulipewa kwa mwingine aliyenidanganya kama meneja wa tovuti, aliipa huduma yake jina sawa na yetu. Lakini huduma hiyo inawapotosha wengi kwa kupenda mali, na mafunzo ya uongo. Hawa akina Engle waliipa huduma yao jina HOLY GHOST FIRE, wakijaribu kuifananisha na kile ambacho Mungu alinipa na iliyo Takatifu. Ninapaswa kutoa Unabii huu kutia moyo wahudumu wengine na huduma ambapo mbwa mwitu wanaharibu au kuwauma kwa meno yao. Kama Mungu Anavyonilinda mimi, YEYE hana ubaguzi kwa watu na Atawasababisha maadui wenu kukimbia katika njia saba tofauti!

Mwanamke huyu anayejiita mchungaji alikuwa meneja wangu wa tovuti kwa usiku mmoja na akawapotosha watu mbali na YAHUSHUA! Sina budi ila kuacha jina lake pale kwa sababu hajabadilisha jina la huduma yake. Alipata faida kutoka kwa NABII huyu kwa usiku mmoja! Ninamuuliza, gharama ya nafsi ni nini na wale ambao hufanya vitu hivi? Wahudumu jihadharini na wale ambao huchukua hali ya kutolipa ushuru na kuhongwa na Serikali ili wasionye watu dhidi ya yale yanayofanywa katika nchi hii. RUACH ha KODESH Aliniambia kuwa kwa kweli hiyo hali ya kutolipa ushuru ndio itakuwa zawadi yako ya pekee! Hivi karibuni hakutakuwa na zawadi kutoka kwa Serikali, mtafanya nini? Mhudumu huyu aliyetajwa kwa unabii huu ningependa kutoa jina lake lakini SINA ruhusa ya kutoa jina lake kwa kuwa hili ni neno la Mungu na onyo kwa wengine wanaofanya yaya haya. Kumbukeni YAHUSHUA na Alivyorarua pesa pale kwenye Hekalu ya wanabiashara! Huduma hii ni mfano mdogo wa vile alivyohisi. Ninamsamehe na kuomba kuwa aache Kumtumikia Mungu wa mali.

Niliondoa Unabii huu kwa muda mrefu sana mpaka watu walipoanza kuiulizia. Sipendi kuzungumza laana za Mungu YAHUVEH na sio baraka. Mungu ni Mungu wa usawa kwa kila kitu. Someni Kumbukumbu la Torati 28 laana za Mungu kwa wale wanaototii na Baraka za Mungu kwa wale wanaotii! Februari 4 1999

* * * * * * *

Maadui wa mhudumu huyu na huduma hii waliokuja kama kondoo na mkaonyesha meno yenu ya mbwa mwitu na nia zenu za kuua huduma hii na mhudumu huyu na inayosimamia, mtajuta (Ndivyo ASEMAVYO YAHUVEH, YAHUSHUA na RUACH ha KODESH) kuiba jina la huduma hii ili kuwachanganya Watoto, Bibi Arusi, Wachaguliwa na Wateule. Hauna haki yoyote wala MIMI Bwana YAHUVEH au YAHUSHUA, hatujakupa haki ya kuita huduma yako “Huduma ya HOLY GHOST FIRE!” Tubu leo Barbara Engle kwa kuiba kile ambacho ni Takatifu na kujiwekea ghadhabu ZANGU juu yako na nia zao na huduma sio takatifu! Wewe ni Yudasi Niliyemuonya binti YANGU Elisheva Eliyahu juu yake kitambo. Rudisha mara saba yale ambayo umeiba. Ondoa jina hilo uliloliiba au utapoteza nafsi yako ukiendelea katika njia hii ya uharibifu unayoifuata. Hakuna yeyote ambaye anafanya vitu hivi ataepuka na moto wa jehanamu itakuramba uso na mwili wako daima. Rudisha. Achana na yote uliyoiba.

Jihadhari kwa kuwa MIMI ni Mungu ambaye hatakejeliwa. Nilimtumia handmaiden WANGU, mtumishi WANGU mpendwa kukujaribu wewe, kukuonya lakini hautaki kusikiliza. Ulisoma na ukaandika Unabii hizi, ukasikia hukumu ZANGU zikitajwa kwa wapagani na wale wanaotaka kuharibu huduma hii ambayo haijajengwa kwa mikono ya mwanamke tu. Lakini kwa mikono ya Mungu Mwenyezi YAHUVEH, YAHUSHUA na RUACH ha KODESH WANGU! Unathubutu kuiba jina la huduma inayozungumzia moto WANGU wa ROHO MTAKATIFU. Kwa kuyafanya haya kama hautatubu leo na kuacha maovu haya utapoteza nafsi yako. Hii ni onyo YANGU ya mwisho kwako Barb na Paul. Mtakuwa mnafaa tu kwa uharibifu WANGU, acheni njia zenu za uovu. Kumbukeni kuwa Yakobo Nilimpenda! Esau Nilimchukia. Ikabodi ni jina lako.

Usifikirie kuwa huyu ni Elisheva Eliyahu anayezungumza kwa kuwa ni MIMI Ninayetabiri uharibifu wako katika njia zote kama hautaachana na njia zako za uovu. Kitambo Nilikuonya na sasa Ninakuonya tena. Mbwa wako alikuwa ishara. MIMI Bwana Mungu Ninawapa maisha na MIMI Bwana Mungu Ninaichukua. Haujui vile ulivyo taabani, TUBU leo! Ondoa jina Huduma ya HOLY GHOST FIRE kwa huduma ambayo sikukupa. Unajiita dreamseeker lakini MIMI Bwana Mungu Nitakuwa ndoto mbaya kwako kama hautamsikiliza Nabii WANGU ambaye anazungumza sasa. Rudisha mara saba kifedha yote ambayo umeiba. Rudisha jina takatifu la huduma ambalo umeiba kutoka kwake. Ni moto tu wa jehanamu ambao utaona usipofanya haya leo ii hii. Nijaribu MIMI na uone kama sitaleta uharibifu kwa yote uliyojenga kwa mikono yako. Je, Haujajifunza bado kwa yale ya kale? Kwa ajili sitaki yeyote kuangamia Nimekuonya tena.

Msiziweke hazina zenu hapa ulimwenguni lakini zijenge kule mbinguni! Ndivyo ilivyozungumzwa, ndivyo ilivyoandikwa, na vivyo hivyo ndivyo itakavyotendeka kwa kuwa maneno haya ni ya Mungu mmoja wa pekee, “MIMI NIKO.” “MIMI NIKO” Nitakuwa adui wako hatari kutoka siku hii kama hautaachana na, na kurudisha yote uliyoiba mara saba. Usimlaumu bwana yako Paul, kama hawa, ulijua ulichokuwa unakifanya sio sawa. Ulihisi huzuni YANGU katika mfano wa depression na bado haukutubu. Nilikuonyesha hasira ZANGU kwa kugusa maisha ya mbwa wako na kukuonyesha vile maisha ni tete, lakini pia ukaona vile Ninavyoweza kupa maisha pale ambapo pana kifo. Magonjwa pale ambapo kuna afya. Umaskini pale ambapo kuna utajiri. Huzuni pale palipo na furaha.

Tumbo lako litabaki tasa na yale ambayo unafikiria hayatakuja kufanyika kama hautarudisha yote uliyoiba kutoka kwa Elisheva Eliyahu na kuondoa HOLY GHOST FIRE kutoka kwa jina la huduma yako. Sikukuambia kuyafanya maovu haya. Kuchafua huduma hii Takatifu ambayo inasimamia utakatifu tu na kukejeli kile Nilichompa Elisheva Eliyahu. Kama hautatii baraka zako zote hata zile ndogo zitabadilika kuwa laana. Kila wakati utaandika au kuona jina Huduma ya HOLY GHOST FIRE uliyoiba kwa binafsi yako na umaarufu. Utapata laana nyingine mpaka hatima yako itakapokuwa kama ya farao. Tokeni kwenye kanisa la wanaojifanya Barbara na Paul Engle. Elisheva Eliyahu hakujua kwa uwazi ulichokuwa ukifanya, lakini Nilionyesha wengine. Ulipokuwa unafanya kazi Nilikupa ishara kuacha ulichokuwa unafanya na bado ulipuuza ishara hizi. Tena Ninasema tubu kwa yale uliyoyafanya. Rudisha jina la huduma hii. Ondoa kila maovu na Damu ya Mwana WANGU iliyomwagwa; achana na mafunzo maovu, na Miungu wengine wa faida. Umeonywa siku hii na YAHUVEH, YAHUSHUA na RUACH ha KODESH, wale unaojidai kuwatumikia.

Februari 4 1999 2:12 Mchana gharama ya nafsi yako ni ipi? Umeonywa na jihadhari, Nitachukua baraka ambazo Nilikupa kama HAUTATUBU leo! Nilikutuma kwa Elisheva Eliyahu kuruhusu ujaribiwe Nikijua kuwa atazungumza maneno YANGU Nitakapozizungumza. Hauwezi kusema kuwa haukuambiwa. Ndivyo Asemavyo Bwana Mungu wa Majeshi. TUBU kwa mafunzo ya uongo unayoamini na kufunza. Masikio yanayowasha na macho ya huku na kule, na tamaa ya dhahabu imekuongoza mbali na Kalivari.

* * * * * * *

Imezungumzwa na kuandikwa kupitia handmaiden WANGU, Elisheva Eliyahu 2-4-99 2:12 Mchana

Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred