Unabii 28
Je, Wewe Ni Mmoja Wa Watu WANGU Waliofichwa?
Imepewa Kwake Mtume Elisheva Eliyahu Januari 25, 1999
Haya yanatoka kwenye Unabii 105, YAHUVEH Alisema iwekwe mbele ya Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)
Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo kama onyo kwa wale wanaokejeli:
2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii Wake, hata ilipozidi Ghadhabu ya Bwana juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”
* * * * * * *
Silaha zenu za vita sio za mwili lakini ni kuu za kuangusha ngome za shetani. Kompyuta itakuwa mojawapo ya hizi silaha zitakazotumika kumfunua adui, zitakazotumika kuonya adui, zitakazotumika kukomesha adui kutoharibu Watu WANGU kwa sababu ya ukosefu wa maarifa. Ambieni Watu WANGU kutafuta chombo hiki cha kisasa kwa kuwa wakati watakapotakikana kukimbia hawawezi kusafiri na kompyuta kubwa. Niliumba kompyuta kwa wakati huu na sababu hii. Haya ndiyo maarifa yanayoongezeka yakikimbia huku na kule. Hivi ndivyo mnaweza kuwa mahali moja na pia kwingine mkizungumza na Watu WANGU kote duniani. Msifikirie hata kidogo kuwa silaha hii haina nguvu. Shetani anatafuta kutawala intaneti, kuwanyamazisha Watu WANGU. Lakini hawezi kufanya yale ambayo siruhusu.
Wakati wenu ni mfupi lakini Nitawapatanisha na wale ambao wana maarifa ya kompyuta. Mkusanyiko wa Watu WANGU utakuwa sauti kubwa katika nyakati hizi za mwisho. Geniuses WANGU wa Kompyuta wamefichwa kwa wakati kama sasa. Wale walio na hekima ya YAHUVEH na YAHUSHUA wamefichwa kwa wakati kama sasa. Wanafanya kazi duniani kujifunza njia za wapagani, ili waweze kutumika dhidi ya wapagani na njia zao kwa wakati unaofaa. Nina Watu WANGU katika kila sehemu haijalishi mlipoogopa, kutoka kwa polisi, jeshi, IRS, serikali, wauzaji wa mazao ya shamba, watoa huduma ya intaneti, tafuteni Watu WANGU. Mtawapata. Sasa ndio wakati ambao watainuka na kung’aa. Kama jua watang’aa.
Maarifa ambayo yamepatikana kule mashuleni ikipewa na adui itatumika dhidi ya adui kulinda wale Ninaowaita WANGU. Watajua njia kando za sheria ambazo mnafikiria haiwezekani. Nina mawakili, madakitari; Nina walimu katika sehemu zote. Msifikirie kuwa wapagani wana hekima zaidi. Geniuses WANGU wamefichwa hadi wakati uliopangwa. Geniuses WANGU wana hekima ya MIMI, YAHUVEH, na YAHUSHUA na wanaweza kujifunza chochote haraka, hata kama hawakufikiria kamwe kujifunza haya hapo awali. Mawasiliano itakuwa chombo cha maana katika nyakati hizi za mwisho.
Njia kando ya kile ambacho dunia inapanga kufanya kuwanyamazisha Watu WANGU, zipo. Sitawaambia njia hizi sasa, lakini mtazitambua mtakapozisikia. Ninawaambia haya wanaweza kujenga minara yao ya Babeli; Nitatoa njia kwa Watoto WANGU ili kamwe muweze kuwasiliana. Niamini MIMI na kujifunza njia ZANGU, jihadharini Watu WANGU wamefichwa, wana karama zilizofichwa za RUACH ha KODESH, wametembea pekee yao bila ushauri ya wengine, kufunzwa, na bado wamefunzwa juu na RUACH ha KODESH WANGU.
Kusafiri itakuwa vigumu zaidi kutoka nchi moja hadi nyingine bila ruhusa kutoka kwa nchi hiyo. Lakini Ninawaambia Nina Watu WANGU tayari wanafanya kazi katika sehemu hizi na Watu WANGU wataepuka wakati wa kukimbia ukija. Nina ndege, marubani, na stewardesses. Nina mpango WANGU tayari. MIMI ni Mungu Ambaye hawezi kushtuliwa hata kama hivyo ndivyo adui anafikiria. Nina mpango na mpango WANGU kwenu ni mzuri na sio wa maovu. Mpango WANGU kwa Watoto, Bibi Arusi, Wachaguliwa na Wateule ni za baraka, baraka tele ambazo hamtaweza kuzitaja zote.
Mipango YANGU kwa maadui WANGU ni laana, nyingi sana ambazo hawataweza kuzitaja zote! Jitayarisheni maadui, laana zinakuja kwenu! Wataziita janga za kiasili, lakini hakuna chochote kiasili katika janga hizi ambazo zinakuja kutoka kwa mkono wa YAHUVEH ALIYEKASIRIKA! Mnajigamba eti mna surplus lakini hakutakuwa na surplus kwa sababu ghadhabu ZANGU zitaanguka bila kipimo, lakini hazitawaumiza Watu WANGU! Nitawalinda Watu WANGU kama Nilivyofanya wakati wa Nuhu, kama vile wakati wa Lutu, kama vile wakati wa Moshe.
Maadui watasaga meno yao katika hasira kwa kuwa wataona kuwa hakuna chochote ambacho kinaweza kuwakomesha wala kuwazuia wote wanaotii na kuamini YAHUSHUA kama Mchungaji Bora. Hakuna mbwa mwitu wanaoweza kuwashtua kondoo WANGU. MIMI huenda mbele ya mbwa mwitu na kuzungumza maneno kwa Manabii WANGU na Mitume Nikiwaonya mapema ni wapi na wakati upi mbwa mwitu watashambulia. Mnaona hawa mbwa mwitu na meno makali, ni hatari na wakikuuma hata mara moja, umo lao ni la mauti. Kwa hivyo sio umo tu lakini nafsi yako na maisha yako yamo hatarini.
Nyoka wanaotumwa kuwazunguka sio moja tu, lakini wengi, nyoka hawa watajaribu kuwazunguka na umo lao sio tu umo la nyoka lakini kuna cobras ambao hudunga sumu katika Roho zenu wakiwaambia kuwa YAHUVEH na YAHUSHUA hawawezi kuwalinda kondoo, kuwa haijalishi, watawadunga na sumu ya kudanganya wakisema, “Amini serikali lakini sio Mungu wenu!” Alafu watatumia boa kujaribu kuwafinya katika kila njia wanayoweza. Kifedha, kiroho, kimwili, kiakili, serikali itawafinya kama boa wakati uo huo, wakitumia cobra kuwadunga sumu ya uongo kuwafanya hata wale walio na imani kuu kutetemeka kwa hofu.
Lakini sasa Ninazumgumza kupitia huyu handmaiden sasa kuwaambia nyinyi wapendwa WANGU kuwa hamuhitaji kuwaogopa hawa mbwa mwitu wala nyoka! Nimewaambia kuwa kamwe Nimekuwa na watu ambao huniabudu, kunitumikia, na kunitii Mungu Mkuu “MIMi NIKO” na Nitakuwa nao daima! MIMI, YAHUVEH, na Mwanangu YAHUSHUA tunatazama kimya na kufuatilia kile ambacho adui anafanya na tunairipoti kupitia manabii wetu na wao pia hawawaonyi tu lakini pia kuwatia moyo kama sasa, kuwajulisha katika wakati WANGU Nitawaambia lini kuondoka, kile cha kufanya, vile ya kuwaepuka hawa boa, na cobra wa mauti!
Ningojeni MIMI tu, kwa kuwa MIMI Bwana Mungu wenu siji mapema wala kuchelewa. Nitawaokoa Watu WANGU kwa njia ambayo mtaipata kuwa ya miujiza. Ndio, kutakuwa na wale watauawa na wanauawa lakini damu yao inaanguka chini na kuwainua wengine ambao watazungumza na kufanya mambo makuu katika Jina la Mwanangu YAHUSHUA. Msihuzunike kwa sababu ya wale ambao Nimeruhusu wauawe kwa binafsi YANGU. Lakini Kueni na huzuni kwa yule ambaye alifanya hayo mauaji na mateso. Watakuwa katika mateso milele kwa sababu ya kile walichofanya, kwa kile walichofanyia Watoto WANGU ambao waliweka maisha yao chini KWANGU. Watateswa vivyo hivyo walivyowatesa kule jehanamu milele. Wale ambao watauawa waliteseka maishani lakini milele hawatawahi kuteseka tena. Tuzo zao ni kuu kule Mbinguni.
Naja kwa Bibi Arusi WANGU bila doa wala kunyanzi. Jifunzeni sasa vile ya kunifurahisha MIMI. Jifunzeni sasa jinsi ya kunitii MIMI. Jifunzeni sasa kuweka yote kwenye madhabahu YANGU ya dhabihu. Kile Nitakachorudisha kwako kitakuwa baraka kwako, kile Nitakachoondoa haukufaa kuwa nayo, kwa kuwa itakuumiza. MIMI ni Mungu mzuri. MIMI ni Baba yenu wa Mbinguni na Ninatazama kwa makini wale wanaonililia MIMI na kuwazungumzia, kuwaonyesha cha kufanya, wakati wa kuifanya, pahali pa kuenda. Msifikirie hata kwa wakati mmoja kuwa maombi yenu hayajasikika. Ni vile tu sio wakati bado wa kuzungumza majibu.
Ninangoja, kama tu nyinyi mnavyongoja, kwa utulivu Ninangoja kama kila siku nafsi zaidi wanamsogea YAHUSHUA kama mkombozi wao. Siwezi kungoja zaidi kwa sababu adui anapanga kuachilia shambulizi kote duniani mara moja. Sitawaruhusu Watoto WANGU wanaosikia sauti YANGU kudanganywa. Sikilizeni kwa makini kwa sauti za maadui na mtaona mnapozisikia kote hewani kuwa hii sio sauti ya Muumbaji wenu na Mwokozi! Sikilizeni kwa makini na kutazama macho wanapoongea, msisikilize na masikio yenu ya kimwili, lakini tumieni masikio yenu ya kiroho, na msitazame na macho yenu ya kimwili, lakini ulizeni RUACH ha KODESH kuwaonyesha na macho yenu ya kiroho.
Katika dunia hii kila kitu hakipo unavyokiona. Katika dunia hii mungu wa uongo na uharibifu anaongoza mataifa mengi. Lakini Mungu wa Ukweli ni YAHUVEH na YAHUSHUA na Nimeweka ndani ya wote wanaoniabudu, kunitumikia na kunitii MIMI RUACH ha KODESH na RUACH ha KODESH Atatenga ukweli kwa uongo. RUACH ha KODESH Atawalinda kutoka kwa uharibifu ujao. Msiruhusu macho yenu kubaki tu kwenye giza, kwa mabaya ya dunia hii, lakini fikirieni fikra nzuri, ulinzi, miujiza Nitakayofanya kuwaokoa Watoto WANGU. Kama tu ilivyokuwa wakati wa Moshe, ndivyo Nitakavyofanya tena. Katika njia mpya, na vifaa vipya vya kisasa, lakini hata hivyo Nitawalinda Watoto, Bibi Arusi, Wachaguliwa na Wateule WANGU. Sitawalinda tu lakini Nitawabariki Bibi Arusi wapendwa katika njia ambazo hawajawahi kuota. NIAMINI MIMI tu!
Sio wote ambao wanajiita Bibi Arusi WANGU na wanaoningoja Nitawachukua nyumbani NAMI katika siku hiyo. Mwanangu YAHUSHUA Atakubali tu Bibi Arusi bila doa wala kunyanzi. Je, Mnaishi bila kujali, katika dhambi na bado mnaifunika na Damu iliyomwagwa ya YAHUSHUA? Je, Mnafikiria kuwa sio lazima kutii Amri ZANGU na kiulizo cha utakatifu kwa kuwa ilimalizwa pale msalabani wa YAHUSHUA? Kama ndivyo, basi wewe sio Bibi Arusi WANGU. Kwa kuwa Bibi Arusi wanajua kuwa kunipenda mimi ni kunitii MIMI. Bibi Arusi WANGU hawanijaribu MIMI kuona ni mpaka wapi kule jehanamu wanaweza kufika na bado kufika Mbinguni. Bibi Arusi WANGU hawangoji kuona kama Nitawaadhibu kujua wametenda dhambi. Wanathibitishwa na RUACH ha KODESH WANGU na kutubu kabla sijawaadhibu.
Kwa wale wanaojiita kwa Jina la Mwanangu YAHUSHUA na kusema kuwa wameokolewa na bado wanaishi maisha ya dhambi. Hamdanganyi yeyote ila tu nyinyi wenyewe. TUBUNI LEO! Bibi Arusi WANGU, Nitawalinda kutokana na hofu ijayo, lakini sio nyinyi mnaocheza michezo na Damu ya Kalivari ya YAHUSHUA MASIHI! Mnafikiria inafunika dhambi zenu mnapotenda dhambi kimaksudi? Mnafikiria kuenda kanisa inafuta dhambi hizo kwa sababu mnafanana watakatifu kwa wengine, haimaanishi kuwa nyinyi ni watakatifu KWANGU. TUBUNI! Siku za hofu zijazo zitathibitisha nani kweli ananitafuta MIMI na ni nani amekuwa akijificha kutoka KWANGU. Msisahau kuwa Ninajua mioyo yenu, Ninajua akili zenu; Ninajua nia zenu bila hata nyinyi kuzungumza neno. MIMI, YAHUVEH, Niliyewaumba, Ninawajua kwa njia zote. Hakuna chochote kilichofichwa kutoka KWANGU. Kumbukeni Anania na Safira, walidhani kuwa wanaweza kudanganya RUACH ha KODESH. Kama vile ilivyokuwa katika siku za Anania na Safira ndivyo itakavyokuwa tena. Wale watakaojaribu kunikejeli MIMI watakejeliwa! (Mitume 5:1-11)
Damu ya YAHUSHUA MASIHI wa Kalivari itawaokoa au kwa kukataa ile tuzo pale Kalivari mtalaaniwa. Ni moja ya hili au lingine, kwa wengine tuzo hili lililopewa Kalivari ni baraka na watajua milele Mbinguni. Kwa wengine, tuzo LANGU Nililotoa pale Kalivari litakuwa kama laana kwa kuwa waliokataa njia ya pekee Mbinguni, njia ya pekee ya msamaha. Kwa kuyafanya haya walimkubali shetani na jehanamu na vyote ilivyonavyo. Ole kwa wale katika nyakati hizi za mwisho wanaokubali njia za shetani na kuishi maisha ya upagani, kwa kuwa maisha yenu yatakuwa bila tunda na kila baraka mlio nayo itakatwa. Lakini kwa wale wanaojaribu kuweka Amri ZANGU, hawana Mungu mwingine ila YAHUVEH na YAHUSHUA na wana sikiliza sauti ya RUACH ha KODESH na sio kufuatana na pepo za seduction. Maisha yenu yatajaa na baraka hapa ulimwenguni na Mbinguni. Kamwe sitawaacha wala kuwapungukia. Amini tu. Msitupe imani yenu mkiona siku ya Hukumu ikija.
* * * * * * *
Imeandikwa, na kuzungumzwa Januari 25, 1999 12:00 Mchana.
Imeandikwa, kuzungumzwa kupitia huyu Handmaiden, Mtoto, Shujaa, Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI
Mtume Elisheva Eliyahu
Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!