Unabii 27
YAHUSHUA Atarudi Sabato! Inukeni Wanawake Mitume na Manabii!
Imepewa kupitia Nabii Elisheva Eliyahu Januari 4, 1999
Haya yanatoka kwenye Unabii 105, YAHUVEH Alisema iwekwe mbele ya Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)
Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo kama onyo kwa wale wanaokejeli:
2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii Wake, hata ilipozidi Ghadhabu ya Bwana juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”
* * * * * * *
MIMI, YAHUSHUA, Ninarudi siku ya sabato, hamjui ni ipi. Njooni Mitume na Manabii WANGU Wanawake! Inukeni SASA! Msiruhusu yeyote tena kuwaambia kuwa sijawaita kuwa Mitume na Manabii, Walimu, Wainjilisti au Wachungaji! MIMI ndiye Mfinyanzi na nyinyi ndio Udongo. Je, Kwa nini mnasikiliza mwanadamu au wale na pepo za kifarisayo? Zungumzeni ujumbe huu ambao Nimempa huyu Mtume kuzungumza. Jiungeni na sauti yake, wanawake na wanaume ambao wanatambua sauti YANGU ikizungumza kutoka kwa yale ninayoandika kupitia kwake. Mjitie moyo nyinyi kwa nyinyi. Shetani amewanyamazisha kwa muda mrefu sana. Mashujaa walio Mitume na Manabii mnajijua nyinyi ni akina nani. Andikieni handmaiden WANGU na mjitie moyo nyinyi kwa nyinyi. Ninarudi tena hivi karibuni. Shikaneni mikono nyinyi kwa nyinyi. Hampo pekee yenu. Nimewaweka kote duniani, lakini mtajuana kwa wakati.
Mnahitajiana. Mtaungana na wanaume wale walio na mwito sawa. Lakini, wale ambao watakataa kuwakubali niachie MIMI. Msigombane na wale ambao wana masikio yaliyo viziwi wanaotaka kutenda mema, lakini wamewaumiza sana wale wanawake ambao wameambiwa kuwa hawawezi kuwa na upako wa mtume, hata huyu anayeandika sasa alikatishwa tamaa na kuambiwa haya. Alisema, “O, nitaendelea kufanya kile ambacho nimeitwa kufanya na ile jina unaloiita”. Lakini mwanamume aliyesema haya alidanganywa na sauti nyingine, ambayo sio YANGU. Lazima ATUBU kwa kuyafanya haya. Je, Mtakuwa tayari? YAHUSHUA ANARUDI SIKU YA SABATO! Ambieni kila mtu atakayesikia, lakini tarajia kuwa hakuna yeyote atakayeamini. Hili si shida lako, lakini lao. Wewe wafaa kutii.
Pamoja, wale ambao nimewaweka pamoja mtakuwa kama jigsaw puzzle na hakuna vipande vingine ambavyo vitatosha kamili. Macho yenu yawe wazi kwa wengine. Ninaleta jeshi la Manabii, Mitume, Wainjilisti, Walimu na Wachungaji na bado watafanya kazi kama kikundi kimoja. Kamwe hawatajifikiria kuwa zaidi ya vile walivyo. Wakijua kusimama pamoja watafaulu kuyafanya yale uliyoamuru kufanywa. Kutakuwa na mavuno makubwa ya nafsi ambao watafikiwa na hii itakuwa mojawapo ya huduma itakayoleta nafsi wengi, ambayo ipo hapa duniani. Kwa Utukufu wa MIMI Baba YAHUVEH, Mwana WANGU YAHUSHUA na RUACH HA KODESH WANGU! Wengi hawangeokolewa kama singeinua huduma hii.
Mtume WANGU ambaye wanaume wanamkataa kama Mtume, anajua sauti YANGU na huandika anachosikia. Wanawake wengine Nimewaita kama Mitume na wameambiwa kuwa hawawezi kutumika katika ofisi hii, lakini Ninasema kwenu kama Nilivyomuambia huyu mtume, haya sio ya wanaume kuchagua, vile Ninavyowatumia handmaidens WANGU ni biashara YANGU MIMI mwenyewe. Hawa ni udongo WANGU na ni MIMI pekee Ninayewaunda na kuwajaribu kupitia majaribio vile Ninavyochagua. Mwanadamu ni nani kusema ni nini MIMI, YAHUVEH, Ninaweza na siwezi kufanya. Wanaume wengi wanadharau Roho za Daudi, Nilizoziweka ndani ya handmaidens WANGU.
Wanaume wanapopigana dhidi ya haya, ndivyo Nitakavyowainua zaidi Roho za Daudi ndani ya handmaidens WANGU. Ni kiburi tu kitakachofanya mwanadamu kuongea namna hii. TUBUNI LEO! Nimemuamuru yeye kuwatia moyo wanawake Manabii na wanawake Mitume, walimu, wainjilisti, na wachungaji. Anajua moto wa mateso kwa mwito mkuu ulio juu ya maisha yake Niliyoiweka maishani mwake na katika wote Niliowaita kuwa mashujaa WANGU Manabii na Mitume wa nyakati hizi za mwisho. Wengi ni wanawake! Msiruhusu wanaume au mafarisayo KUWAZUIA! Haya ndiyo MIMI, YAHUVEH, Nimefanya na Ninafanya. Je, Ni nani atajaribu kumuambia YAHUVEH Amekosa?
Nimekuleta wewe na wanaume na wanawake wote pamoja kuwa kitu kimoja katika RUACH HA KODESH, mtasonga kwa umoja katika RUACH HA KODESH WANGU na mtazungumza kwa umoja katika RUACH HA KODESH WANGU. Mtawafikia wengi ambao hawajafikiwa na watu wengi ambao wamekataliwa na kutupwa kando kama wale ambao hawawezi kuokolewa na bado Nitawatuma na upako na maneno ya upendo ambayo sio ya kwenu, Ndio, Ninasema muwafikie watu ambao mtaogopa kuwakasirisha, lakini kwa kutozungumza ndio itakuwa kosa kuu. Ninawaamini wafanyikazi WANGU Ninaowatuma, kwa kuwa MIMI ndiye Mfinyanzi na nyinyi ndio udongo. Ninajua ni nini Nimeweka ndani ya kila mfanyikazi kujiunga na yeye. Ninajua alichotengenezwa nacho na udhaifu wake. Mahali ambapo yeye ni dhaifu, wengine wamefanywa kuwa na nguvu. Mahali wale ambao watakuja ni wadhaifu, yeye amefanywa kuwa na nguvu, kama chuma ambayo imepitishwa motoni ndivyo Nilivyofanya na wale ambao wanafaa kukuunga. Haufai kuogopa ni nani watakaokuunga, kwa kuwa Ninakuambia sio chaguo lako lakini LANGU!
Yudasi yeyote atakayetafuta kuunga huduma hii atapata hatma sawa kama Yudasi! Sitaruhusu yeyote kuharibu kile Nilichojenga mwenyewe na Ninaendelea kujenga. Huduma hii itakumbatia dunia hii. Msidharau mwanzo mdogo kwa kuwa Nilianza kama mtoto kwenye manger, au sio? Katika dunia hii, pale mwanzoni, hayo tu ndiyo dunia iliweza kuona. Na bado katika miaka mitatu, angalia ni wangapi Niliwagusa, na kuwaokoa. Vitabu vyote katika dunia hii haiwezi kushikilia kile Nilichofanya kwa huo muda mfupi. Msidharau nguvu za Upako WANGU! Nimewapa upako wote na Nitaendelea kuimwaga Upako WANGU katika njia kuu. Mtajua katika nyinyi wenyewe hamuezi kufanya lolote lakini na YAHUVEH vitu vyote vyawezekana kama Mnaamini.
Sasa mpo katika majimbo tofauti, lakini haya tu ni kwa sasa, kwa kuwa mwaka huu mtakuwa pamoja, karibu kwa kugusa. Mtasafiri na kufunza pamoja. Msijaribu kuyafanya haya, nitazameni MIMI Nikiyafanya haya. Msijaribu na kusema ni wakati upi na msimu gani, jueni tu itakuwa kwa wakati na msimu WANGU. Ombeni na kufunikana katika maombi. Fanyeni kazi pamoja; toa yale ambayo mmejifunza pamoja. Ninapochagua washirikas kumuunga binti YANGU, Nilichagua kwa makini na Nikawajaribu. Ninakupenda sana. Ninakuamini sana. Ninajua hamtaumiza mtumishi WANGU lakini mtamlinda na yeye hatawaumiza lakini atawalinda. Wale wote ambao wanajiunga ni kama mnyororo spesheli uliotengenezwa na dhahabu. Siweki chuma yoyote kama tin, au silver, au lead pamoja na mnyororo WANGU wa dhahabu lakini ni ile chuma inayofaa ambayo Nimepata kuwa imepitizwa kwenye kizimba cha moto na kutoka kama dhahabu, iliyoboreshwa mara saba.
* * * * * * *
Update iliongezwa 1/22/2016. Maandiko haya yafuatayo inaonyesha kuwa YAHUVEH Anawaamini watumishi WAKE. Manabii WAKE wa kale. Kama tu Yeremia alivyojulikana hata kabla hajawekwa kwenye tumbo la mamake.
Yeremia 1:4-5
4Neno la BWANA lilinijia kusema, 5“Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako nilikujua, kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalumu,
nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.’’
Hesabu 12:6-7
6BWANA akasema, “Sikilizeni maneno yangu: “Akiwapo nabii wa BWANA miongoni mwenu,
ninajifunua kwake kwa maono,
ninanena naye katika ndoto.
7Lakini sivyo kwa mtumishi wangu Mose, yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote.
* * * * * * *
Msijifikirie nyinyi wenyewe zaidi ya vile mlivyo. Wewe ni chombo cha udongo kilichothaminiwa, ambayo Nimemwaga neema YANGU na huruma na karama za RUACH HA KODESH. Wewe ni chombo kilicho tayari ambacho hakipigani na mikono ya Mfinyanzi. Umeniruhusu MIMI na utaendelea kuniruhusu MIMI kukuunda vile Ninavyotaka uwe na sio vile unavyochagua kuwa. Kila kitu ulicho nacho lazima uiweke kwenye dhabahu na kuniruhusu MIMI kuondoa kile ambacho sitaki uwe nacho, na kurudisha kile ambacho Ninataka uwe nayo. Usishikilie chochote na uniamini MIMI, Nitarudisha na sio tu kile ambacho ulitoa lakini Nitakupa zaidi ya yale ambayo utanipa. Nijaribu MIMI na kuona kama sitafanya Ninavyosema.
Mtume WANGU, wekeni yote mliyo nayo katika dhabahu hii pia huduma hii, tazama Nitakachofanya. Kuwa tayari kwa MIMI kuondoa chochote au yeyote katika maisha yenu ambayo haiwasaidii, lakini huwazuia kwa kuwa na kufanya yote Niliyowaamuru kufanya katika Jina LANGU. Fanyeni haya na kila kitu, hata watoto wenu. Kama Abrahamu, lazima muamini kuwa MIMI ni Mungu mzuri na Nitawarudishia yote ambayo yanafaa kuwa baraka, na kuchukua chochote ambacho shetani Aliweka mbele yako kuwa kizuizi! Je, Mtathubutu kuyafanya haya, Watoto WANGU?
Pesa pia. Msishikilie chochote kwa kuwa ni yangu haya hivyo. “Kilicho chenu ni CHANGU, na kilicho CHANGU ni chenu!” Nipe MIMI ili Niweze kuirudisha katika njia kuu. Ambia watu WANGU. Andika haya, sio tu kwa washirika kukuunga, lakini pia kwa Watu WANGU kwa kuwa amri ii hii yaenda kote katika nyakati hizi za mwisho. Waambie, “WEKENI KILA KITU ULICHO NACHO KATIKA DHABAHU.” Sema, “THUBUTUNI KUMUAMINI BABA YENU YAHUVEH, YAHUSHUA na RUACH HA KODESH!” Thubutuni kuwa tayari kwa MIMI kuondoa kile ambacho hakifai kuwa maishani mwenu! Thubutuni kuniamini MIMI kuwa Nitaongezea baraka Ninazokupa. Fanyeni haya sasa, kabla Niichukue bila ruhusa yenu! Fanyeni haya, iwe bwana, bibi, watoto, pesa, nyumba, gari, huduma na orodha yaendelea. Fanyeni haya na chochote Mnachothamini iwe biashara, ushirikiano, makanisa. Utajua ni ipi.
Chochote ambacho unajua siruhusu kama sigara, au dhambi nyingine unayoitumia kukuletea amani, lakini kwa kweli, ni bandia tu, kwa kuwa MIMI ndiye Mfalme wa Amani! Hauhitaji chochote kingine. Nipe MIMI, itoe KWANGU na kama inafaa kukubariki, Nitairudisha. Kama haifai kukubariki, NITAIONDOA! Kwa sababu nyinyi, mnaojiita WANGU, nina haki ya kuchukua kile Nilichowapa, na pia mlichopewa na shetani au nyinyi wenyewe, chochote kinachozuia uhusiano wako NAMI. Je, Mnataka Niwaokoe katika siku zijazo? Basi NITII MIMI na fanyeni haya. Ombeni kama hamjui maana ya haya. Wekeni hata ndoa zenu kwenye Dhabahu hii ya Dhabihu. Wacha Mungu watasimama. Kwanza, Nitawabariki katika njia ambayo hata hamtaamini.
Nyinyi Watoto WANGU mnasema mnataka matakwa YANGU kamili? Je, Hii ni kweli? Mtanipa MIMI siku moja ya wiki? Sabato, Ijumaa jioni hadi Jumamosi jioni mnafaa kupumzika ndani YANGU, kufurahia ndani YANGU, kujifunza juu YANGU. Wekeni kazi zenu kando na kufanya tu kazi YANGU, kama kazi yoyote yafaa kufanywa. Ombeni na Nitawaonyesha yale ya kufanya na kutofanya. Mimi ni mungu wa usawa kamili. Ninachukia chochote ambacho hakina usawa. Hata Sabato lazima iwekwe katika usawa! Siku hii ni ya kufurahia ndani YANGU, sio laana; hii ni siku ya kuwa baraka kwako na sio ya kuogopwa lakini ya kufurahia. Sabato sio siku ya utumwa lakini ni siku ya uhuru katika MIMI, YAHUSHUA! Wanafunzi WANGU na MIMI ni mfano wa kile cha kufanya Sabato. Msijifunze haya kutoka kwa Mafarisayo ambao wanasema siku hii ya utumwa. Wanaosema kuwa siku hii ni ya mateso. Ndio, Ninasema makuu yatakuwa baraka ya kuweka Sabato YANGU na kuiweka Takatifu.
HII NDIYO SIKU NITAKAYORUDI TENA! Ndio, Nimesema wekeni Sabato kutoka leo hii kwa wale wanaojidai kuwa Bibi Arusi WANGU! Jitayarisheni kwa kuwa BWANA ARUSI wenu yuaja na atawasili Sabato. Hamjui ni ipi. Lakini wale ambao hawaningoji MIMI WATANIKOSA SABATO. Ndio, Ninasema tena, kukuja KWANGU ulimwenguni kunapokaribia, katika siku hii acha MIMI niwe katika fikra zenu, maneno na matendo. Jivinjari siku hii NAMI. Je, Hamuezi kuachana na mambo ya dunia KWANGU kwa siku moja ya wiki? Fanyeni mazoezi kwa haya sasa hivi. Wakati unakuja ambapo wale waovu watatambua ni nani kwa kweli ni WANGU na ni wagani ambao sio WANGU. Watajua kwa ISHARA ya kama unaiangalia na kuiweka Sabato au kuitambua siku hii kama Sabato. Kumbukeni Ijumaa Jioni hadi Jumamosi Jioni. Hii ndiyo SABATO. Iwekeni iwe TAKATIFU na siku ya wewe NAMI kukumbatiana na kujuana. Wewe ni mpendwa WANGU. Wale wanaofanya haya watajua baraka kushinda yale ambao wamejua hapo awali.
Sasa Nimezungumza vitu hivi kwa watumishi WANGU na Nimeleta ujumbe huu kwa nyinyi watu katikati ya Unabii wa kibinafsi ikipewa kwa wale katika huduma hii. Na bado Ninawaachia maneno haya kwa wale wanaodai kuwa WANGU, na wale ambao huongoza nafsi KWANGU, funzeni Watoto WANGU, Bibi Arusi, Wachaguliwa, na Wateule kuwa Waweka Sabato ni sio Wavunja Sabato. Kwa haya, binadamu wote watawajua! Kwa haya mtakuwa tayari kwa kukuja KWANGU. Wale walio na masikio wasikie, wote wengine wabaki viziwi. Waache viziwi, kwa kuwa ni pepo ya uasi iliyoingia mioyo na nafsi zao. Waacheni! Tena Ninasema msijaribu hata kubadilisha akili zao. Maandiko YANGU yanazungumza ukweli, haibadiliki.
MIMI, YAHUSHUA Nilikuja kutimiza sheria na sio kufuta sheria za YAHUVEH! Waambie na kama wataka kusikia, msimalize pumzi yenu. Kumbukeni kama ilivyokuwa katika nyakati zilizopita wengi walikuwa kwa kutofuata Sabato YANGU. Wakati unakuja ambapo mtaona maafa makuu na zitafanyika Sabato. Watu watatingiza vichwa vyao na kushangaa ni kwa nini? Mtajua sababu ni nini. Nimewaambia tu sasa hivi. Lakini hawa wengine watajuaje kuwa wananikasirisha MIMI msipowaambia? Wote mnaosoma haya, na kuitambua sauti YANGU, mtawajibika kwa kuwaambia wale ambao hawajui. Wanafikiria kwa kuenda kanisa Jumapili kuwa wanaheshimu Sabato YANGU. Lakini Sabato YANGU inapitwa tu na wawa hawa. Sijali kuwa mnakutana kila siku na kuniabudu MIMI. Lakini Sabato, hii ndiyo siku YANGU na siku yenu tunatenga kuwa spesheli kushinda zingine. Mkila kumbukeni kuwa mna mgeni ambaye haonekani. Kumbukeni kuwa kila kitu mnachofanya siku hiyo, MIMI niko pale naifanya nanyi.
Kama unatubu dhambi siku hii Nitaona sanasana kwa siku hii. Mmeonywa tena ili Watu WANGU wasiseme kuwa hawakupata onyo kabla Nitume hukumu kwa wale ambao wanatotii kimaksudi. MIMI ni Mungu wa Upendo na Ghadhabu kwa maadui WANGU. Nyinyi ni maadui WANGU tu kama mtachugua vivyo hivyo. Nilifariki kwa wote, Damu YANGU ilimwagwa kwa wote; Mimi sina upendeleo, lakini Ninajua ni wagani ni WANGU na nani ni wa kanisa ya wanaojifanya. JIHADHARINI kujaribu kunikejeli MIMI kwa kusema maneno ambayo wengine wanataka useme, na kumbe Hamsikii sauti YANGU. Jihadharini na kuzungumza na kutofanya. Nimezungumza kupitia handmaiden huyu, wakati hakuwa anatarajia MIMI kutabiri kwa watu tena. Kwa hivyo hamuezi kusema kuwa wale wanaonikejeli MIMI kwa maneno ya mwisho ya onyo Niliyompa NISIKIENI MIMI! NIOGOPENI MIMI! NIAMINI MIMI! Je, Si ilikuwa MIMI Bwana wenu Mungu YAHUVEH na YAHUSHUA walioizungumza kumpitia? Jihadharini na kumfanya yeye awe adui wenu kwa kuwa hatawajibika kwa maneno ambayo atazungumza. Atawajibika tu kama ataogopa kuzungumza katika ujasiri. Amenitii MIMI hadi sasa.
Je, Mtakuwa wavunja Sabato au waweka Sabato? Msitarajie kuwa Bibi Arusi WANGU kama hampo tayari KWANGU katika siku hii. Jitayarisheni sasa Bibi Arusi WANGU kwa kuwa NAJA KWA HARAKA! Maafa makuu yatatendeka katika siku ya Sabato YANGU kama ishara kuwa hii ni amri ambayo haijabadilika. Mtajua mtakapoyasikia haya. Sibadiliki kwa mwanamume wala mwanamke yeyote, wakati au msimu, MIMI ni Mungu yule yule jana, leo na milele. Amri ZANGU zimeandikwa kwenye jiwe na kidole cha MIMI Mungu Mkuu “MIMI NIKO” na sitasema pole kwa yeyote.
Ninasamehe kwa urahisi wote ambao hawakujua bora. Handmaiden huyu Ninayezungumzia sasa ndivyo anavyojifunza maana YANGU ya Sabato ya kweli. Ilikuwa kwa wakati na msimu. Yeye sio bora au mbaya kuwashinda nyinyi wengine Ninaowafunza sasa. Kumbukeni sasa mtawajibika kwa yale mnayoyajua. Yale ambayo mtafanya na haya tayari Ninajua. Niulize MIMI katika siku hii ni nini kinachonikasirisha MIMI na nini kisichonikasirisha. Omba katika siku hii na toa yote kama dhabihu KWANGU, Nitaibariki na kuiongeza yale ambayo ni baraka KWANGU. Je, Ni wangapi wanaosema haya watathubutu kumuamini Mungu wao? Tayari Ninajua chaguo lako.
Imezungumzwa, Imeandikwa, katika upako WANGU kupitia Mtume WANGU Elisheva Eliyahu, Januari 4, 1999, 9:49 Usiku.
Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!