Unabii 22

Wapendwa, Msiwe Maadui Wenu Wenyewe!

Imezungumzwa na kuandikwa katika upako wa RUACH HA KODESH kupitia Mtume Elisheva Eliyahu

Agosti 7, 1998

Haya yanatoka kwenye Unabii 105, YAHUVEH Alisema iwekwe mbele ya Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo kama onyo kwa wale wanaokejeli:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii Wake, hata ilipozidi Ghadhabu ya Bwana juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

Elisheva: Sisi wote ni watenda dhambi tuliookolewa kwa neema na huruma na kama haingekuwa hivyo, basi tungehitaji Mwokozi kweli? Ni yule mshtaki wa akina ndugu ambaye hutushtaki na kutusumbua akili. Ninasikia Bwana Akisema kwenu;

Wana na Binti ZANGU mmekuwa maadui wenu wenyewe! Kujihukumu sio kazi yenu lakini ni kazi ya Baba yenu Aliye Mbinguni! Acheni kuniambia MIMI ni nini Nilichosamehe na ni nini Nisichoweza kusamehe, Tubuni kwa mambo ya kale, lakini dhambi hizo zimetupwa kwenye bahari la sahau. Damu YANGU iliosha dhambi hizo kitambo sana. Ziko mbali kama vile mashariki ilivyo na kaskazini.

Kati ya fikra zenu za hivi karibuni na dhambi, makuu zaidi yamekuwa kile kichapo ambacho mmempa mtu ambaye Ninampenda kushinda mnavyoota wala kuelewa. Mtu ambaye Nilimmwagia Damu YANGU na kumtolea Maisha YANGU na Ningefanya vivyo hivyo hata kama ingekuwa mtu huyo pekee. Mtu ambaye kwa binafsi yake Nilichapwa hata sikuweza kutambulika. Mtu huyo ni wewe. Sasa acheni kujaribu kuniambia MIMI kuwa Nimefanya makosa kwa kukuchagua wewe. Je, Mnajaribu kunielezea MIMI kazi YANGU? Je, Mnajaribu kuniambia kuwa Niliumba viumbe bure? Je, Mnajaribu kuniambia MIMI mnajua zaidi ya Mungu MWENYEZI, Bwana wenu na Mwokozi? Je, Mnajaribu kuniambia MIMI Nafanya makosa? Je, Mnajaribu kuniambia MIMI kuwa Damu Niliyomwaga haitoshi kukuosha hadi uwe msafi. Kwa nini mnachukua maisha yenu kama sio yenu ya kuchukua? Mbona mtathubutu kuniibia MIMI raha ya kuthibitisha kuwa sio wale ambao walio na kiburi MIMI huzungumza kupitia kwao katika dunia hii, lakini ni wale wanyenyekevu. Ni wale ambao wanajiona hawafai ambao huwa wanafaa kwa kuyajua haya. Siwachagui wale ambao wamejawa na nguvu zao, lakini wale wanyonge kwa kuwa wanyonge wanapata nguvu kupitia YAHUSHUA MASIHI pekee. Mnaweza kufanya yote kupitia jina la YAHUSHUA. Sikufanya makosa Nilipowachagua kuzungumza katika Jina LANGU, Mimi ni Mungu MWENYEZI na sifanyi makosa.

Je, Nitasema haya mpaka lini kwenu? Mtanisikiliza MIMI lini? Niliwachagua nyinyi na Nilijua ni kifaa gani kilichowatengeneza nayo na ndio pia dhambi zitakazowajaribu hata kabla hamjazaliwa. Nilijua ni pepo gani mtapigana nazo hata kabla shetani azitume. Pia Nilijua neema YANGU itatosha kwa yote. Ninajua pia, kama Shaul (Paulo) Alivyosema, “Unapojaribu zaidi kunifurahisha MIMI ndivyo shetani anavyotuma pepo zake kukushambulia.” Lakini kaeni makini dhidi ya mashambulizi haya. Msijiweke katika nafasi ya kushindwa na mashambulizi haya. Tumia hekima ya Bwana Niliyowapa. Mnajua ni nini Ninachozungumzia, kama sivyo Niulizeni MIMI, kwa kuwa nabii huyu anayezungumza nanyi amehisi vitu hivi vyote katika njia tofauti. Manabii WANGU wote wa kweli, hata katika nyakati za bibilia, walijiona hawafai. Kama hauhisi hivyo, basi haukufaa kutumika kama wafikiria unaweza bila MIMI.

Nisikizeni MIMI Wana na Binti ZANGU wapendwa. Acheni kuua yale ambayo Nimeyapa maisha na maisha ya kudumu. Acheni kupokea pepo ya wazimu. Wale ambao wanawahukumu kuwa nyinyi ni wazimu hawaelewi ni nini Nilichozungumza wala kuwaonyesha. Kwa kusudi KWANGU Nimekuchagua. Hii sio vita. NITASHINDA na utashindwa ukiendelea kuwa na shaka kuhusu yale ambayo ni kweli. Mmeonywa kwa sababu NINAWAPENDA! Nimewaita na kuna wale ambao wanafikiria kuwa wewe ni wazimu kwa kuamini kuwa Ninazungumza nawe na kukuonyesha vitu ambavyo wengine hawaoni. Kitu cha wazimu tu juu yako ni, kuamini kuwa Ninakuadhibu kwa dhambi zako ambazo zimesahaulika na kusamehewa zamani. Ni shetani tu na wewe mnaoenda kutafuta kule, sio Mwokozi wenu. Acheni kujaribu kuosha nguo zenu ambazo tayari ni safi. Je, Mnafikiria DAMU YANGU haitoshi? Mnaihubiri, sasa YAAMINI!

Nina mambo mengi zaidi ya kuwaambia na Nitafanya vivyo hivyo, lakini kwa sasa fikirieni haya Niliyoyazungumza kwa kuwa ni ukweli. Nimewapa vazi LANGU la vita la kusimama, Neno LANGU la kusimama, Damu YANGU ya kuosha na Jina LANGU na Damu ya kuponya na kufukuza mapepo yanayosumbua akili na miili yenu na Roho. Sasa shetani anaogopa nguvu hii kwa kuwa Nimewapa upako wa kuomba. Je, Mbona hamuamini kile mnachoomba? Je, Mnafikiria kuwa MIMI ni kiziwi? Je, Mnafikiria kuwa mikono YANGU ni mifupi kuwakomboa? Je, Mnafikiria Damu YANGU, Jina, Neno na vazi la vita HAZITOSHI? Nyinyi, wapendwa WANGU, Mmenikasirisha MIMI kwa kutoamini kile Nilichokizungumza.

Sasa mnayajua haya kuwa kweli, kwa hivyo zishikilieni na acheni kuyatazama mawimbi katika bahari za maisha yenu, kwa kuwa hii ndiyo sababu mnazama katika depression na fikra za dhambi wakati mwingine. Badala ya haya wekeni macho yenu KWANGU Bwana na Mwokozi YAHUSHUA MASIHI na Njooni na tutembee majini pamoja. Nyinyi ni waerevu kujua kuwa simaanishi kimwili bali kiroho. Njooni mchukue mkono WANGU na kuamini na msiwe na shaka. Acheni mambo yenu ya kale nyuma yenu mara moja. Wekeni mikono yenu kwenye panda na kufanya kazi katika shamba LANGU la mavuno na msiangalie nyuma. Kitu kimoja cha mwisho, mnatafuta uhakikisho kutoka kwa wengine mliowatafuta na wanawezaje kuwasaidia?

Kwa kutoa kibanzi kutoka kwa jicho lako kwanza lazima watoe boriti kutoka maishani mwao. Katika dunia hii mtakuwa na shida. NDIO, lakini Nimeshinda dunia hii. SASA YAAMINI! Kama Nilivyoyazungumza maneno haya kwa handmaiden WANGU Elisheva Eliyahu Ninasema kwenu nyinyi sasa tena, ihubiri, ifunze na kuiamini. Nahitaji kusema mengine? Acheni kujizunguka na wanafariji wa AYUBU, kwa kuwa kama AYUBU hawakumsaidia na walimzuia na kumfanya kupigania ile imani ambayo anaamini na kumfanya amtetee Mungu wake. Haya yanawafanyikia pia. Ninawapa onyo moja na muichukue ilivyo; mkifa kwa mikono yenu wenyewe mtajipata mbele ya JEHOVAH (YAHUVEH) Aliyekasirika. Kwa hivyo acheni kujaribu kuua na kuharibu yale Niliyoyabariki. Mmeonywa; acheni kuwa maadui wenu wenyewe.

Kwa kuwa mmekuwa mkiifanya kazi yake shetani na anaketi tu na kuwacheka. Sasa ni wakati wenu wa kumcheka tena shetani. Sio katika nguvu yenu, sio katika upako wenu wala jina, lakini katika upako au jina, lakini katika Jina juu ya Majina yote, YAHUSHUA MASIHI wa Kalivari na Nazareti na Mungu Mwenyezi YAHUVEH Ambaye Ana ulimwengu huu kama kiti cha kuweka miguu. Nyinyi ni watoto WANGU wapendwa Ninaowathamini sana kama wana na binti, mashujaa na Bibi Arusi. Ninarudi tena. Je, Mtaamini haya tena? Je, Mtaamini kuwa Mimi huwatuza wale ambao wametoa yote KWANGU? Nina tuzo ZANGU NAMI na zina majina yenu. Je, Mnataka Nichague kuwapa wengine? Nimewachagua nyinyi lakini wakati ni mfupi sana, hamna wakati wa kujionea huruma. Wahurumie wale ambao hawako tayari kwa kuja KWANGU.

Wahurumie wale ambao hawaamini kuwa Nitawashughulikia kwenye Dihiki Kuu na kuwaokoa kutoka kwa ghadhabu kuu ijayo. Wahurumie wale ambao wanafikiria kuwa wameokolewa kwa sababu ya dini na sio uhusiano NAMI. Kujihurumia ni mojawapo ya maadui wenu; ikemee leo katika Jina LANGU. Rudini kwa kuwalisha kondoo WANGU kama Nilivyowaamuru kufanya. Siku hii mmesikia sauti YANGU, sasa itii. Imezungumzwa siku hii na nabii mwingine, Elisheva Eliyahu, ambaye amehisi mambo haya yote mwenyewe. Lakini anajua kuwa imani ni ukweli sio hisia. Nyinyi wote chapeni kazi na kuwalisha kondoo WANGU. TAYARISHENI BIBI ARUSI WANGU! Msaidie kuwa bila doa wala kunyanzi kwa kutangaza yale ambayo yanayomfanya shetani kutetemeka na hofu.

Kwa ukweli ni Jina la YAHUSHUA MASIHI NI USHINDI na Ninarudi tena kuyathibitisha haya! PIGENI KELELEKWENYE INTANETI; PIGENI KELELE KWENYE PAA ZA NYUMBA! Itangazeni kwenye mitaa na makanisa, redio na televisheni kuwa YAHUSHUA MASIHI YUPO NJIANI! Gabrieli AMEPULIZA TARUMBETA yake! Yale mwaimbi ya sauti yamezuiliwa na vita kali inayoendelea kule Mbinguni sasa. Mikaeli na shetani na malaika wanapigana, mazuri dhidi ya maovu, lakini mazuri hushinda kamwe. Kuna wale ambao wameisikia tarumbeta na wale ambao hawajaisikia.

Lakini Ninawaambia kuwa Nimewapa onyo kwa wale ambao wamesikia ile tarumbeta, ingawa tarumbeta ya Gabrieli imesikika tu na wachache, hivi sasa, ilikuwa tu kuwatayarishia Bibi Arusi WANGU kwa Bwana Arusi WAKE YUAJA! Msijali kuwa hamjaisikia tarumbeta ya Gabrieli bado lakini ni ya wakati uliokadiriwa. Hata mawimbi ya sauti zile zinazuiliwa tu kwa wakati ulioakadiriwa. Je, Si ni MIMI Ndiye Nijuaye umbali kati ya Mbinguni na ulimwengu? Hata mahesabu ya haya yamekadiriwa hapo mbeleni. Kwa haraka fanyeni yale Niliyowakadiri na kuwaita kufanya.

Upendo mwingi katika YAHUSHUA, handmaiden, mtoto, shujaa, Bibi Arusi

Nabii Elisheva Eliyahu

Agosti 7, 1998

Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred