Unabii 19
Vueni Pazia Zenu Nyeusi Za Uchungu, Watoto WANGU, Hazina ZANGU!
Imepewa kwake Mtume Elisheva Eliyahu Aprili 10, 1998
Haya yanatoka kwenye Unabii 105, YAHUVEH Alisema iwekwe mbele ya Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], Kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)
Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo kama onyo kwa wale wanaokejeli:
2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii Wake, hata ilipozidi Ghadhabu ya Bwana juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”
* * * * * * *
Maoni ya Elisheva Eliyahu: Unabii huu ulipewa kwangu, lakini BABA Ameniambia kuwa inafaa kwa watoto wengine wa YAH walio na upako na karama za RUACH ha KODESH wanaomtumikia BABA YAHUVEH, YAHUSHUA, IMMAYAH.
* * * * * * *
Unabii unaanza:
Hivi Ndivyo Asemavyo YAHUVEH; mpendwa WANGU Ninayekuthamini kushinda hazina nyingine hapa ulimwenguni. Ninaona uchungu wako. Ni uchungu wa ajabu sana kwa kuwa watu hawakuelewi. Je, Watu ambao si wa Roho YANGU wanawezaje kuhisi uchungu wako au kuona Nilichokuonyesha au kukuambia? Je, Si wangekuwa pia wamemuita Yohana Mbatizaji wazimu pia? Je, Si wangekuwa wamefikiria kumkamata kwa ajili ya tabia yake na Eliya, Yeremia na Manabii WANGU wote? Fikiria ni nini dunia hii ya kisasa inayonyamazisha sauti ya YAHUVEH Mwenyezi ingefanya nini na hawa manabii wa kale?
Wewe ni kama Yona anayetumwa kule Ninawi na ni wachache sana ambao wamesikia na kusikiliza onyo ZANGU. Lakini wataona kama vile yale Niliyoyazungumza kupitia kwako yakija kutendeka. Usiyafikirie haya ni ya ajabu kwa kuwa wale unaofikiria wameokoka, wameokoka kweli? Je, Unajua nyoyo zao kwa kweli, wale ambao wanakujeruhi vikali nafsini mwako? Sijawatuma kukutesa kwa kuwa wewe ni hazina YANGU mpendwa.
Usisimame tu kwenye ufahamu wako lakini Nitegemee MIMI na Nitaongoza njia zako. Usimuamini yeyote ila tu wale unajua waweza kusikia sauti YANGU yatoka kwao. Usifanye lolote hadi Nikupe amani kamili ambayo yazidi ufahamu wote. Sijakuacha na wala sitawahi. Mimi ni kipenzi chako cha kwanza; wengine wote ni wa pili kwa MUNGU YAHUVEH MWENYEZI unayemtumikia. Endelea kuzungumzia juu ya huruma ZANGU na upendo lakini onya juu ya ghadhabu ZANGU na kisasi na adhabu ijayo kama hawataachana na njia zao za uovu na kujipaka Damu iliyomwagwa kwao pale Kalivari, ikiosha uvundo wa dhambi na kuachana nazo.
Mabaya haya mmeyatumia kama gongo lakini Nitawakomboa kutokana na lolote ambalo mnahisi mnahitaji kuwaletea amani na faraja kwa kuwa MIMI tu NdiyeYote mnayohitaji. MIMI, YAHUVEH, Ninatosha kwa vitu vyote. Lakini kila kitu kina wakati na msimu na sitawawekea zaidi ya yale msioweza kubeba. Ndio mpendwa WANGU umeteseka kwa ajili ya Jina LANGU. Ndio umeitwa mgonjwa wa akili lakini wale wanaokuita majina haya ni wangonjwa rohoni! Unalia lakini ni machozi YANGU. Unashangaa lakini ni mshangao WANGU. Unahuzunika lakini huzuni ni YANGU. Wale wanaosema wanakupenda hawajui maana kamili ya upendo au wangeyaelewa haya. Usiwahukumu vikali kwa kuwa wanafanya vile wawezavyo na roho zilizo ndani mwao.
Haya pia yatapita na ingawa mito ya huzuni yafurika Mpendwa WANGU. Haya pia yatapita. Utafurahia tena. Maisha yako haijaisha. Imeanza tu. Miujiza ipo kwenye kona. Je, Wafikiria ni kwa nini shetani anakuambia ufe moyo sasa. Umepigana kwa muda mrefu, usife moyo.
* * * * * * *
Imepewa kwake Mtume Elisheva Eliyahu
Aprili 10, 1998
Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!