Unabii 16

Msiwanyamazishe Manabii WANGU!

Unabii umepewa kwake Mtume Elisheva Eliyahu Februari 6, 1998

Haya yanatoka kwenye Unabii 105, YAHUVEH Alisema iwekwe mbele ya Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo kama onyo kwa wale wanaokejeli:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii Wake, hata ilipozidi Ghadhabu ya Bwana juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

Wanapowashambulia Manabii WANGU, wananishambulia MIMI. Wanadunga kidole kwenye jicho LANGU. Wanashambulia na kutangaza vita dhidi ya Mkuu, “MIMI NIKO,” YAHUVEH, YAHWEH yote yana maana sawa. Kuna Mungu mmoja tu, Baba. Wanaposhambulia Manabii WANGU wanashambulia yule aliyewatuma na kuwapa upako. JIHADHARINI kwa kuwa Ninajua ni Roho ipi Manabii WANGU wa kweli wanayo na ni ya RUACH ha KODESH (Roho Mtakatifu). Nimeweka ROHO MTAKATIFU WANGU ndani yenu; Nitazikoroga zile karama za utambuzi. Mtatumika kuwafichua mbwa mwitu waliojivalia ngozi za kondoo wanaotaka kuwadanganya, kuwashusha moyo na kuwanyamazisha Manabii WANGU. Wanasema msisikie maovu yoyote, msizungumze maovu yoyote, msiyaone maovu yoyote. Lakini mnajua sauti YANGU. Kemea laana ya tumbili 3. Oneni hawa mbwa mwitu kwa rangi yao kamili.

Nimemtuma dada yenu kusafisha vidonda vyenu ambavyo sikuwatia. Kwa kuwa Ninawapenda wapendwa WANGU. Mnatafuta tu kuwa karibu NAMI, lakini jichungeni ni nani anayewafunza, tambua roho zao. Dada yenu Elisheva anayezungumza nanyi ananijua MIMI na Ninamjua, na Nimewaonyesha Roho yake na matunda. Kueni wakaguzi wa matunda kutoka sasa. Ombeeni na kuwaonya wale ambao maadui anawaumiza kama wewe ulivyoumizwa. Niliiruhusu kukuonyesha vile inavyohisi ili uweze kutambua uchungu wao. Kemea mbwa mwitu hawa wanaowakemea, Nitafuteni MIMI na Nitathibitisha yale yanayoandikwa sasa hivi. Nitafuteni MIMI na Nitawapa maneno ya kuyafanya yaya haya. Nimewaelekeza hadi mahali hapa kuwahudumia wale mlio na masikio ya kusikia na macho ya kuona. Wengine wote wabaki viziwi. Nimewapa jumbe nyingi. Toa yale ambayo Nimekupa ambayo utajua ni yapi ya kutoa kwa dada huyu atajua ni ya KWANGU.

Shetani anaogopa karama zenu za kinabii. Lakini ombeni na Nitazungumza maneno na atapiga kelele kutoka kwenye paa za nyumba na intaneti. Pamoja mtawarudisha Manabii WANGU waliopotezwa njia, wamefunga midomo, kufungwa macho, kufungwa masikio, kunyamazishwa, kufungwa, kushushwa moyo na wamekata tamaa. Ninamtuma nabii huyu kuzungumza maneno YANGU na kuwapa moyo na kuwarudisha kwa yale ambayo Niliwaita mfanye. Wengi watasikia sauti YANGU na wamepata thibitisho katika Roho zao Ninavyozungumza maneno haya. Zungumzeni yale ambayo Nimewapa. Msinyamazishwe tena. Kwa utukufu WANGU zungumzeni na kupiga tarumbeta. Kama watachagua kusikia au la, Ninawaita mrudi kwenye ofisi ya nabii. Fungueni masikio yenu, toeni vizuizi kwenye macho yenu na mtoe vizuizi midomoni mwenu. Jitoeni pingu. Na myafanye yaya haya kwa wengine. Mwasaidie kama nyinyi mtakavyosaidika. Muwape moyo. Na kwa laana za tumbili 3 zitafichuliwa na wale ambao wamekuwa wakiziweka juu ya Manabii WANGU, wakawaambia wasizungumze juu ya kisasi au hukumu ya YAHUVEH. Msizungumze juu ya toba. YAHUVEH Anatia moyo tu sio kukemea! Uongo, uongo, na uongo mtupu!

Ninawatuma Manabii WANGU kabla sijatuma baraka ZANGU, au ghadhabu za Mungu Mwenyezi YAHUVEH! Nimezungumza haya kuwatia moyo na kuwaambia mrudi na kufanya yale ambayo Nimewapa upako ya kusema na kufanya. Kuna wakati mdogo sana wa kuonya watu. Pigeni kelele kwa ujasiri ndio hawataweza kusema kuwa hawakuonywa. Waonye juu ya manabii wanaoanzisha shule za kinabii, wakifunza yale ambayo hawawezi kufunza. Ni RUACH ha KODESH tu Anayempa mwanamume au mwanamke au ndio, hata mtoto kuzungumza maneno YANGU ya moto.

Onya juu ya Craig martin (Vanguard), Andrew Strom (Revival Ministry), na Pam Clark Prohecy Site), waonye. Kwa hivi vikundi vya kinabii vinazungumza uongo na kuwalaani Manabii WANGU kwa kutumia hizi laana za tumbili 3. Jihadharini na vitabu vilivyoandikwa na mbwa mwitu wanatafuta kuwapotosha Manabii WANGU. Ninawaonya kwa wengi tayari wameanguka katika mitego wakifunzwa mafunzo ya uongo. Lazima watubu kwa kufurukuta na kuharibu Neno LANGU. Kuna hivi ndivyo Asemavyo Bwana na wanaipokea sasa hivi.

Wakiwaambia Manabii WANGU wanyamaze kuwa YAHUVEH haongei hivyo. Wakiwaambia Manabii WANGU wawe vipofu, kwa kuwa YAHUVEH hapeani maono kama haya. Wakiwaambia Manabii WANGU kunyamaza kwa kuwa YAHUVEH hazungumzi juu ya ghadhabu ya YAHUVEH au toba au hukumu. Wakiwaambia Manabii WANGU kuzungumza tu mambo mazuri na sio chochote cha kuwakasirisha watu. Uongo na uongo mtupu! Wakisema kuwa wao ndio wanapaswa kufunza manabii na kumbe “MIMI NIKO” Ndiye wa pekee Anayewapa upako na kuwafunza na RUACH ha KODESH WANGU. Jihadharini na wale wanaochukua pesa wakiandika vitabu na kuuza maarifa ambayo sijawapa. Jihadharini Manabii WANGU, na mdanganyifu anayetafuta kufunga midomo ya manabii.JIHADHARINI kwa kuwa mtafanya nini bila manabii wa kweli kuzungumza Maneno YANGU? Katika nyakati hizi za mwisho midomo ya manabii haiwezi kunyamazishwa kama mbwa. Lazima wawe huru kuzungumza kwa ujasiri na yale Niliyoyakadiri yatakuja kutendeka.

Jihadharini nyinyi mnaotafuta kunyamazisha manabii WANGU wapendwa na Mitume na wachungaji, walimu, wainjilisti. Jihadharini kwa kuwa ghadhabu ya Mungu Mwenyezi YAHUVEH itawajia na malaika wa YAHUVEH watawakimbiza. Acheni manabii WANGU Ninaowathamini. Kazi yao sio ya kwao lakini ni MIMI Ninaowatuma kama zawadi kwa dunia hii. Nikizungumza kwa sauti inayosikika, hata mnong’ono tu, nguvu itakuwa katika ile mnong’ono hadi hakuna chochote kinachoweza kushindana na nguvu za upepo huo. Hasira YANGU imewaka juu ya wale ambao wanaumiza Manabii WANGU Wapendwa. OLE, OLE, OLE kwenu kwa kuwa mtanijibu MIMI na mtavuna mlichopanda.

Msiwanyamazishe Manabii WANGU tena. Wao sio mbwa wa kunyamazishwa. Umo la moto walilowauma nalo kwa kuzungumza maneno YANGU sio maneno yao na umo lao sio umo lao lakini LANGU. Ghadhabu zilizoitwa chini sio hasira yao, sio ghadhabu yao, sio hukumu yao, lakini YANGU! Msisikize yeyote anayesema kama hawa waliotajwa kwa ujumbe huu kuwa hakuna kitu kama “Hivi ndivyo Asemavyo Bwana” ya ukweli. Wanafunza kuwa kuna mwili pia. Kama neno limetoka kwa RUACH ha KODESH WANGU basi ni vivyo hivyo. Imenenwa na upako wa RUACH ha KODESH na yote ni Roho na hakuna mwili pale. Mwili ni nabii bandia.

Nimempa upako huyu nabii Ninayemtumia kuzungumza sasa kuwaita manabii WANGU warudi waliofukuzwa, wakaambiwa wao ni bandia. Lakini siku hii, mtaamini nani, binadamu au Mungu Mwenyezi YAHUVEH? Nimempa upako wa kusafisha vidonda vyenu, acheni awahudumie kwa upendo, faraja na ukweli WANGU. Rudini! O mashujaa Niliowapa upako wa kuzungumza na sauti kuu na ya ujasiri. Mruhusu huyu Niliyempa upako kuwa kama mama kwa manabii wachanga na manabii walioteswa. Nimemuita Elisheva kuwachunga, kuwatia moyo, na kusafisha vidonda vyenu, kuwafunza, kuwapenda na kuenda vitani kwa binafsi yenu kama mama simba anavyowapigania watoto wake walio hatarini. Nitaweka mgurumo kwenye mdomo wake, mgurumo WANGU, na adui atakimbia katika njia 7 tofauti.

Ameshambuliwa kama vile ilivyotabiriwa, midomo 500,000 YANGU itainuka na kupiga kelele wote pamoja. Manabii WANGU watakusanyika pamoja na kupiga kelele kwa umoja na kama tu siku za kale itakuwa kwa Sifa, Heshima na Utukufu WANGU, ushuhuda kuwa MIMI ni yule yule na sibadiliki. Kama kuta za Yeriko zilivyoanguka na kuwa vumbi. Kama Daudi alivyomuua Goliathi. Msijaribu kuyaelewa, amini tu kuwa yale Niliyoyazungumza yatakuja kutendeka. Nitawaweka kwenye ukuta kama Nehemia lakini stesheni zenu zitakuwa kote duniani na hamtashuka na kuacha kujenga Hekalu mpaka Nitakaposema kazi imemalizika. Kazi yenu itamalizika wakati Nitakapokuja tena, sio kwa sababu ya chochote alichofanya, lakini kwa sababu anazungumza kwa mgurumo WANGU wa Simba wa Yuda.

Kueni tayari kukimbia maadui, mbwa mwitu mliojivalia ngozi ya kondoo lakini mnawala kondoo WANGU. LAKINI TOSHA! Nimemuinua mmoja ambaye atawafichue nyie na sababu zenu fiche. Sio katika nguvu yake lakini katika nguvu ya Mungu Mwenyezi pekee watakimbia. Atawatunza na kuwatii moyo tena ili mtakuwa na imani tena kuwa mumeitwa kuwa shujaa kwenye ukuta mkitoa jumbe ZANGU kama tarumbeta kwa wote. Jipangeni kwenye ukuta na kuzungumza yale Ninayowaambia kuzungumza.

Msishuke na kutoka pale kwa sababu ya yeyote iwe mwanamume wala mwanamke wala shetani. Msiogope nyuso zao! Msiogope ghadhabu yao. OGOPENI GHADHABU YANGU! Kwa kuwa msipofanya Ninachowaamuru kufanya basi mpo katika uasi dhidi ya Mungu mnayemtumikia. Kwa kuwa Ninahitaji mzungumze. Kama dada yenu anavyozungumza ujumbe mwingine ambao utakuwa mgurumo unaosikika kote duniani. Kwa kuwa tena Ninamtumia yeye kuzungumza yale wengine waliokataa. Wanaona mabaya, na kusema sio shughuli yangu. Acha mtu mwingine azungumze. Adui na watoto WANGU watasikia mlio huu wa tarumbeta kama wanataka kusikia au la. Wataisikia! Msiwazuie Manabii WANGU kwa kutozungumza.

Makanisa acheni kuwanyamazisha. Acheni kuwatupa nje. Kubali kuwa kwa kweli hamtaki dhambi zenu kufichuliwa na kutubu! Msiwanyamazishe au kufikiria kuwa mnaweza kuchagua ni yupi anazungumza na yupi hawezi. Wachungaji mmemhuzunisha RUACH ha KODESH WANGU. Je, Nyinyi ni nani kuwanyamazisha wale Ninaowatuma? Mnasema ni kwa sababu hamtaki kuruhusu tu yeyote kuzungumza kama Nabii WANGU. Lakini kama sio wa KWANGU Nitawafichua. Nitawaonyesha ishara kama wanazungumza maneno YANGU ya Moto Mtakatifu au kama ni moto bandia au moto wa kishetani. Acheni wazungumze! Hapana, sio lazima mpitie maneno yale watakayoyazungumza kwanza. Wachungaji mmepita mipaka yenu. TUBUNI LEO! Je, Kwani RUACH ha KODESH hawezi kuwapa utambuzit kujua ni yapi ni ya KWANGU au sio. Jihadharini, kwa kuwa mnamhuzunisha RUACH ha KODESH! Mtawajibika. Mtajua kama wao ni nabii bandia.

Ishara za nabii bandia ni matunda yao yatakuwa yameoza na ni mbaya, na neno la YAHUVEH litafurukutwa kufanana na umbo lao, sio umbo LANGU. Watakuwa wamejawa na kiburi. Watakuwa wanauza karama za RUACH ha KODESH kwa yule aliye na pesa zaidi. Watawaelekeza kwa YAHUSHUA tofauti (Yesu Kristo); hata wale waovu wanatumia Jina LANGU. Waovu wengi wamejitokeza katika jina LANGU wakitafuta kuwaharibu manabii WANGU. Lakini wao hao ndio Nitakaowaharibu. Maadui WANGU, ingawa mnafanana vizuri, mimi tu ndiye Nijuaye mioyo zenu. TUBUNI siku hii kwa kuwa mmeonywa! Imezungumzwa siku hii kupitia Mchungaji Nabii WANGU Elisheva Eliyahu Saa 4:00 Jioni 2/6/1998, tena Ninapoiweka siku jihadharini kwa kuwa sasa mtawajibika kwa yale mnayoyajua. Je, Mtafanya nini nayo? Ninajua tayari!

Tafadhali wekeni nakala ya kibinafsi ifuatayo mnapotoa neno hili kwa kuwa inaonyesha vile shetani alivyokasirika kwa kutoa neno hili kutoka kwa YAHUVEH.

* * * * * * *

Nakala ya kibinafsi: Imekuwa sasa kila wakati ninapewa Unabii, YAHUVEH Anathibitisha yale Yaliyozungumzwa. Hii ilimalizwa Saa 4:00 Jioni na Saa 5:25 Jioni nikashambuliwa kwa maneno. Moja kwa mhudumu nilimuita rafiki na hata nikawaelekeza kwa tovuti yake na nitakuwa ninaitoa jina lake hivi karibuni, kwa kuwa amemhuzunisha RUACH ha KODESH. Aliniandikia na kusema nitoe jina lake kwenye orodha ya barua pepe yangu wakati ninapozituma Unabii. Anafikiria kuwa mimi ninamlazimisha na kufanya haya bila ruhusa yake. Pole Mchungaji Steve C. Nilidhani kuwa tulikuwa wa Roho moja. Inakaa sivyo. YAHUVEH ndiye Atakayekuwa Wakili wako. Alijua ni nini utakachofanya, ukijaribu kuniaibisha mbele ya mashujaa wengine wa YAHUSHUA. Nilidhani kuwa utabarikiwa na utataka kujua ni nini YAHUVEH Anachozungumza. Ninatoa jina lako kabisa kutoka kwenye kitabu cha anwani changu. Hautawahi kusikia lolote kutoka kwangu tena.

Lakini nina uhakika siku moja YAHUVEH Atakukumbusha yale uliyoyafanya leo hii. Kwa haya utawajua kwa upendo walio nao kwa ndugu. Tunda lako linajionyesha. Ninaomba utubu. Na pia, ulipojaribu kunikemea, sikuona ukiuliza ruhusa ya watu wengine kuwatumia barua pepe. Fuata unayoyafunza. Hata hivyo, katika Bibilia tangu lini nabii anahitaji ruhusa ya kuzungumza Unabii za Mwenyezi YAHUVEH? Sehemu kubwa ya Bibilia haingekuwa imeandikwa. Nabii huyu anakataa kunyamazishwa, kufungwa, wala kupofushwa na

Mwanamume au mwanamke au shetani anayewatuma. Nabii huyu anatafuta tu kuona vizuri na kusikia vizuri kile RUACH ha KODESH Anachozungumza. Tafadhali YAHUSHUA usiwahi kuruhusu chochote kizungumzwe au kuandikwa kupitia chombo hiki ambacho sio “Hivi ndivyo Asemavyo YAHUVEH’ ya kweli.

Ninawakasirisha wengine wasiotaka kusikia, na kuwafunza wengine wanaotaka kusikia. Nabii Elisheva Eliyahu, Alpha & Omega Almightywind, Kanisa la Moto wa ROHO MTAKATIFU. Upendo, dada yenu, chombo cha udongo kilichovunjwa lakini shujaa mkuu na Bibi Arusi wa YAHUSHUA. 2-6-98 Saa 4:00 Jioni

* * * * * * *

Update mpya kuhusu Unabii huu iliyoandikwa Disemba 24, 2015:

Ninajuta kutotumia jina kamili ya yule Mchungaji pale kwa footnote ambaye katika mwaka wa 1998 alifanya kila kitu kujaribu kunyamazisha nabii huyu. Mchungaji Steve C. alikuwa Mchungaji wa Kanisa la Jumapili na alijaribu kunishawishi mimi kuwa YESU KRISTO (YESU KRISTO ndilo jina alilolitumia wakati huo), haiti Wanawake kuwa viongozi wa kiroho wala Nabii. Alifanya maisha yangu kuwa tata, akinishambulia na pepo ya dini na mafunzo ya binadamu. Mchungaji Steve C. aliandika kwenye tovuti yake miezi iliyofuata, kuwa alikuwa amepata habari kuwa ana saratani, aliacha kunishambulia, na baadaye nikasema kuwa alikuwa amefariki kwa sababu ya saratani inayoenea haraka! YAH Alinithibitishia “msiwaguse masihi wangu, wala kuwaumiza Manabii wangu”.

Sina shaka yoyote kuwa marehemu Mchungaji Steve C. atajibu kwa ukatili aliyonifanyia katika Siku ya Hukumu! Je, Alienda jehanamu kwa yale aliyonifanyia mimi, nitaona nitakapofika Mbinguni.

Ufunuo mpya baada ya miaka hii mingi kuhusu jeshi la 500,000 kwenye ukuta, wao ni midomo! Jasmine, binti yangu ninayemthamini aliona kipande siri cha fumbo ambacho hakuna mtu yeyote aliyekiona! Hawa 500,000 ni Manabii wenye upako! Sasa Nabii anaweza kuwa na Unabii moja tu kama Stephen katika Kitabu cha Mitume (Mitumu Sura ya 7), au Unabii nyingi! Sifa kwake YAHUSHUA! Tafadhali mnaposoma Unabii hizi na YAHUVEH Anathibitisha maneno haya kwa roho yako kama ukweli tuandikie sisi na kutujulisha ili tuweze kusaidiana na kutiana moyo kama Bibilia inavyotuambia tufanye. Inaongezea upako katika sisi sote tunapotoa utambuzi ambao RUACH ha KODESH Anatupa kutoka kusoma Unabii hizi.

Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred