Unabii 156

Je, Mko Tayari?

Unabii huu ulikuja Septemba 11, 2026 Siku ya Rosh HaShana kama tulivyokuwa tunasifu na kuabudu.

Onyo la YAHUVEH Kabla ya Unabii kutoka Unabii 105:

Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako.

Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha!

Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo.

Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

“MIMI ni BWANA YAHUVEH: hili ndilo JINA LANGU: Na UTUKUFU WANGU sitampa yeyote, Wala Sifa YANGU kwa sanamu” (Isaya 42:8).

Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo kama onyo kwa wale wanaokejeli:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii Wake, hata ilipozidi Ghadhabu ya Bwana juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

Tulikuwa tunasifu BABA YAHUVEH, YAHUSHUA MASIHI na MPENDWA RUACH HA KODESH na tukitoa asante na kungojea YAHUSHUA MASIHI. Tulipoanza kuomba, Unabii huu mfupi lakini wa maana ulikuja kama kumbusho kwa sisi sote. Kwa kuwa ingawa YAHUSHUA MASIHI wetu MPENDWA hakuja kuwachukua Bibi Arusi WAKE Rosh HaShana hii, swali bado linabaki, je tuko tayari kwa kurudi KWAKE? Je, Tumejitayarisha na Mioyo yetu yote kukutana na MWOKOZI wetu mpendwa? Je, Atatupata tukiwa tayari na bado tukimngojea YEYE? YAHUSHUA MASIHI Awabariki wote na endeleeni kuomba, ili tuwe kati ya wale waliohesabiwa kuthaminiwa kama Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI na kuwa na ushuhuda wa Enoki. Kueni na Rosh HaShana iliyo na baraka,

katika Upendo na shalom wa YAHUSHUA MASIHI.

Mpendwa Nabii na Dada Grace na Viongozi wengine wa Huduma ya Amightywind.

* * * * * * * * *

Nabii Grace: Asante BABA YAHUVEH, asante YAHUSHUA MASIHI, asante MAMA IMMAYAH, SHKHINYAH GLORY kwa Sherehe YAKO ya Tarumbeta, L’shanah Tovah (inamaanisha, kwa mwaka mpya mzuri)! Tunakungojea WEWE, YAHUSHUA MASIHI! Tunakungojea! Tunaomba tuwe wale ambao waliothaminiwa kuwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI!

Asante kwa kutusafisha. Ninaomba BABA YAHUVEH, kuwa tutakufurahisha WEWE katika kila kitu tulichoitwa kufanya. Ninaomba, BABA YAHUVEH, Unapoangalia chini, kuwa utaona umbo LAKO. Kuwa hautatuona sisi, bali tu umbo LAKO. Maisha yetu yote, BABA YAHUVEH, yatolewe KWAKO. Tukuishie WEWE, BABA YAHUVEH, Maandiko YAKO na Neno LAKO, tulitumie maishani mwetu katika Jina na Damu ya YAHUSHUA MASIHI. Tusiwe tu wasomaji na wasikilizaji wa Neno lakini tuwe wafanya Neno na kuwafunza wengine kufanya vivyo hivyo, BABA YAHUVEH!

Ninakushukuru sana, sana, sana, sana, kwa familia hii walionizunguka iliyobarikiwa na inayo upako. Ninawapenda sana. Asante YAHUSHUA MASIHI. Kwa kweli uzuri na huruma itatufuata siku zote za maisha yetu na tutaishi katika Nyumba ya YAHUVEH. Ninakushukuru WEWE, BABA YAHUVEH. Ninakushukuru na moyo wangu wote. Moyo wangu umejaa furaha. Ninakushukuru BABA YAHUVEH. Ninakushuru wewe, YAHUSHUA MASIHI. Ninakushuru WEWE, MAMA IMMAYAH SHKHINYAH GLORY! Asanteni kwa Upako WENU! Asanteni kwa karama ZENU! Asanteni kwa Ukweli WENU!

Asanteni kuwa nimekuwa katika Huduma hii tangu niwe na miaka 12! Siwezi kuamini kuwa imekuwa miaka 20. O, BWANA nihurumie! Wow! Asante EWE, BABA YAHUVEH! Kweli, kweli, kweli, WEWE ni MUNGU Anayeokoa! WEWE ni MUNGU Anayeokoa! WEWE ni MUNGU Anayekomboa! Na WEWE ni MUNGU Anayefanya miujiza. Ninakushukuru EWE, BABA YAHUVEH. Ninakushuru EWE, YAHUSHUA. Ninakushukuru EWE, IMMAYAH!

Na asante hazitakoma, BABA YAHUVEH. WEWE ni wa ajabu! Na Ninakushukuru EWE, BABA, kwa uzuri WAKO. Ninakushukuru kwa kutimiza ahadi ZAKO. Na ninakushukuru EWE, BABA YAHUVEH, kwa kuwa yote uliyotabiri itakuja kutendeka! Katika Jina na Damu ya YAHUSHUA MASIHI!

Chunguza mioyo yetu. Tusafishe sisi wote kutokana na uovu. Tuvute karibu na WEWE. Ninaomba kuwa tuchukue muda mbele ya Kiti CHAKO cha enzi, BABA YAHUVEH. Wale ambao wanataka kukujua WEWE, wachukue muda mbele ya Kiti CHAKO cha enzi, pale miguuni PAKO BABA YAHUVEH! Wale ambao wanataka kujua sauti YAKO, wanaohitaji kukujua WEWE, BABA YAHUVEH!

Ninakushukuru WEWE kwa baraka ZAKO! Ninakushuru WEWE! Ninakushukuru WEWE na ninajua kuwa una jambo la kusema, ndio maana mimi nimekuwa wa mwisho, Kwa hivyo BABA YAHUVEH. Ninafunga mwili wangu katika Jina na Damu ya YAHUSHUA MASIHI. Ninafunga macho yangu, masikio na mdomo kwa Damu ya YAHUSHUA MASIHI iliyomwagwa. Usiache hata neno moja la mwili litoke katika Jina na Damu ya YAHUSHUA MASIHI! Masikio yangu yasikie sauti YAKO BABA YAHUVEH. Niweze kusikia kila Neno vizuri katika Jina na damu ya YAHUSHUA MASIHI na ninajifunika kwa Damu ya YAHUSHUA MASIHI kwenye kinywa changu na sauti yangu. Ninaombea ulinzi katika Jina la YAHUSHUA MASIHI Naomba. Amina. Sawa.

Nabii Grace anaomba katika Ndimi Takatifu:

Unabii Unaanza:

Siku takatifu! Siku takatifu! Hizi ni Siku Kuu Takatifu! Watoto WANGU wapendwa, kazeni mishipi kwa kuwa vitu vitaanza kuenda kwa haraka! Rosh HaShana, ni wakati Mtakatifu sana! Na Ninauliza watoto WANGU tena, je, Itakuaje kama Rosh HaShana ndiyo siku Nitakayorudi?

Je, Mko tayari? Je, Mmejitayarisha? Je, Nitampata Bibi Arusi ambaye hana doa, na mafuta kwenye taa yake? Ninauliza, je, mko tayari?

Ninawaita Bibi Arusi WANGU, jitayarisheni! Je, Nitapata utakatifu? Je, Nitapata Bibi Arusi anayengoja kwa uvumulivu kusikia mlio, kusikia mlio?

Je, wewe ni Bibi Arusi mwenye hekima au wewe ni yule mjinga? Je, mko tayari kwa kweli, mnaposikia Maneno haya? Chukua nafasi hii kuchunguza moyo wako na kujiuliza, je, MIMI ni wa kwanza katika maisha yako? Au MIMI ni wa pili? Au wa tatu? Au wa nne? Au MIMI ni wa mwisho?

Wakati unapungua!

Kathrynyah, Adam, mtatayarisha neno hili. Liwe tayari kutolewa. Mada yake ni rahisi na Neno ni fupi. Ni rahisi, “Je, Mko tayari?”

Mwisho wa Neno.

Wote: Amina! Sifa kwa YAHUVEH, YAHUSHUA MASIHI, MAMA SHKHINYAH GLORY IMMAYAH!

Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred