Unabii 152
Sikilizeni & Kueni Huru Kutokana na Pepo ya Hofu!
Uso kwa Uso na Nabii Elisheva Eliyahu!
Unabii 152 Mpya, Hapo Awali Iliitwa MIMI, BABA YAHUVEH, Nitawakomboa Tena!
Imeandikwa/Imezungumzwa katika Upako wa RUACH HA KODESH Mnamo Novemba 2, 2001 kupitia Mtume, Nabii Elisheva Eliyahu Imezungumzwa Upya Machi 20, 2020 Wakati wa Janga la Virusi ya Korona Ikatolewa tena Aprili 4 | Sherehe ya 26 ya Amightywind kuwa Mtandaoni!
Unabii huu, chini ya jumbe za Sabato, ilitolewa kwanza & kuwekwa mtandaoni kama miaka ishirini iliyopita, na ina maana sana leo hii na yenyewe, ni “Ushahidi wa Kuthibitisha Unabii”-Nabii Elisheva alioongozwa kuisoma tena, wakati huu akiizungumza na Upako mkuu, na kuhakikisha video mpya imetengenezwa.
* * * * * * *
Yafuatayo ni Unabii ulivyokuja
—na Nabii Elisheva, akizungumza katika "Ndimi Takatifu," kama ROHO wa MUNGU Alivyomjalia kutamka (Matendo ya Mitume 2:3-4) kwa lugha za wanadamu na malaika (1 Wakorintho 13:1). Elisheva anazungumza katika ndimi zinazoleta Unabii (1 Wakorintho 14:6).
Tunatumia Majina ya Kiebrania ya MUNGU:
YAH/YAHU יה ni JINA TAKATIFU la MUNGU, kama vile “Alleluia” au “Hallelu YAH” הללו–יה ambayo humaanisha “Msifu YAH”: YAHUVEH/YAHWEH י-ה-ו-ה MUNGU BABA; YAHUSHUA/YAHSHUA יהושוע MWANA WA PEKEE WA MUNGU—(HA MASHIACH המשיח inamaanisha “MASIHI”; ELOHIM אלוהים INAMAANISHA “MUNGU.”)
Ufunuo wa “SH’KHINYAH GLORY” שכניה תפארה —kama JINA la KIBINAFSI la RUACH HA KODESH רוח הקדש, (katika Kiiengereza “ROHO MTAKATIFU”) —upo kwenye tovuti hii. (HA SH’KHINAH {SHEKINAH} ni Kiebrania inamaanisha UWEPO WA MUNGU.)
Zaidi ya hayo, ABBA YAH אבא יה humaanisha “BABA YAH” na IMMA YAH אמא יה humaanisha “MAMA YAH.” Katika Kiebrania, ROHO WA MUNGU ni kike, Anajulikana kama “SHE” na kuonyeshwa katika njia hii katika Unabii & Maandiko yafuatayo. Kila mbapo kuna jina la MUNGU ipo katika herufi kubwa.
Maandiko yaliyotajwa yametoka KJV au NKJV, au CJB, isipokuwa pale palipotajwa vinginevyo.
* * * * * * *
Onyo ya YAHUVEH iliyoongezwa mbele ya Unabii zote:
Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako.
Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha.
Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo.
Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli.
Isaya 42:8
8‘‘Mimi ndimi BWANA,
hilo ndilo jina langu!
Sitampa mwingine utukufu wangu
wala sanamu sifa zangu.
(Unabii 105)
Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo kwa wale wanaokejeli:
“Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA YAHUVEH juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”
—2 Mambo ya Nyakati 36:16
+ + + + + + +
Sherehe ya 26 ya Amightywind Kuwa Mtandaoni!
Nakala ya Ujumbe wa Elisheva wa Sabato |Jumamosi, Aprili 4, 2020
O BABA YAHUVEH-Ninakushukuru na kukusifu-MPENDWA YAHUSHUA MASIHI & RUACH HA KODESH-kwa kunipa mimi HESHIMA kwa kuchaguliwa kuzalisha Huduma hii miaka 26 iliyopita mtandaoni (na kwa kweli ina miaka kushinda haya, lakini haya ni mtandaoni), ilianza 1994: na hakuna hata rekodi ya kitambo vile kwa sababu kwa wakati huo ilikuwa “America Online” [AOL]; na hakukuwa na World-Wide-Web [vile ilivyo sasa].
Je, waweza kuamini?
Lakini BABA YAHUVEH, YAHUSHUA & MPENDWA RUACH HA KODESH, tunawaabudu, tunawapenda! (Na haya YOTE ndiyo ninayotaka kuwafunza watu, kuwaongoza kusikia Maneno YENU-kusikia Mjumbe WAKO-kuwaongoza wao kwa YAHUSHUA MASIHI, kuwapa ufunuo ambazo umenipa mimi, na ziara za Mbinguni kuwa nimeona YAHUSHUA Uso kwa Uso).
Na picha hii iliyoko karibu nami, ndiyo mfano wa karibu sana ambayo niliweza kupata hapa duniani, kama vile msichana mdogo alivyoichora na kwa kweli WEWE una Macho ya samawati.
Na siku moja wale [ambao watakuwa] Mbinguni wataona ni kwa nini picha hiyo ilichaguliwa.
Na ninataka kila mtu kujua-asante, asante Kongamano la Amightywind! BABA YAHUVEH, umenipa kongamano nzuri sana KOTE duniani katika lugha 52 tofauti sasa, na Hindi imeongezwa.
Na tamanio la moyo wangu ni kwa huyo mwanamume kutoka Judah kujitokeza na kunisaidia kufikia Israeli. Mimi ni Myahudi na ingawa sikuzaliwa kule Israeli na ninahitaji mwanamume huyu kutoka Judah. Ninahitaji mfasiri wa Kiebrania, BABA YAH-na hii ndiyo tamanio la moyo wangu, BABA wa MBINGUNI-kufanya Israeli wajue YAHUSHUA MASIHI ni NANI. YEYE ni Isaya 53.
Tunawashukuru na kuwasifu, BABA YAHUVEH, katika mwaka huu wa 26 ambapo Sherehe hii imefanyika: Ulichagua 4/4/20 [siku hii kwa Huduma hii miaka 26 iliyopita] pia kuzalishwa kwenye Intaneti katika siku yangu ya kuzaliwa. Na-kwa siku 30! Ulitupa amri mwaka uliopita.
Na WEWE Ukasema unataka tusherehekee [siku 30] na kuwapa watu nafasi ya kuweza kutuma video zao na-kama wanataka tuziweke kando-waniambie kama hawataki tuiweke kwenye video kuu, zote zikiwa mahali pamoja. (Wana siku 30 kuweza kuyafanya haya.) na kwa njia hii, mambo yao ya siri itabaki vivyo hivyo, kwa sababu itakuwa tu video za walichosema na vile Huduma hii ina maana kwao na vile wanavyotaka kukupa utukufu, na vile walivyookolewa au kile ambacho wataongozwa [kusema].
Kwa hivyo YAHUSHUA MASIHI, ninakushukuuru kuwa hata katika Sabato, wakati huu Takatifu [Aprili 4, 2020] ya kusherehekea ipo hapa.
Ninataka kukushukuru kwa kuwa huyo Mfasiri wa Kiebrania yuaja. Ninataka kukushukuru kwa ndugu zangu Watakatifu katika YAHUSHUA walio na upako na waliozaliwa na kulelewa kule Israeli, lakini wanaojua historia ya Kiebrania ambayo ni muhimu na kuambatana na Bibilia.
Ninataka kukushukuru na kukusifu, BABA YAHUVEH, kwa kila kitu unachokifanya.
O BABA YAHUVEH, tafadhali, bariki kongamano la Amightywind na wageni waliokuja kusherehekea sana na kwa wingi-kwa wale waliokupa maisha yao WEWE, YAHUSHUA-na wanajua sasa kuwa kuna Huduma ambayo haitoi visingizio kwa dhambi.
Tunawafunza kuwa, YAHUSHUA, WEWE utawasamehe kama kwa kweli watatubu kwa huzuni mkuu na kuungama dhambi zao. Kuungama huongoza katika kutubu na kutubu katika wokovu-na YAHUSHUA, tunakushukuru na tunakusifu.
Ninakusifu kwa kila mmoja katika timu yangu, kwa kila mmoja wa wahudumu. Ninakushukuru kwa wanaotengeneza video. Ninakushukuru kwa kupata meneja wa tovuti ambao wanaaminika!-ambapo wale wengine walikuwa Mayudasi.
Na ninakushukuru na kukusifu WEWE, BABA YAHUVEH-watu hata hawajui kuwa mara 5 Huduma hii karibu iibiwe kutoka kwangu lakini-hii nii [Huduma] ya UTATU MTAKATIFU na hauwezi kuibia BWANA MUNGU MWENYEZI ambaye NI & ALIKUWA na ni MUUMBAJI WA YOTE.
Sabato Njema!
Ninapenda, penda, penda, penda, penda, kila mtu anayeabudu YAHUSHUA MASIHI, na ninatarajia kusikia kutoka kwenu. Kwa kweli.
Katika Jina la YAHUSHUA, Amina.
Kuogopa ni Kinyume cha Imani! |Zaburi 91
Nakala ya Ujumbe wa Kinabii wa Sabato wa Elisheva
Ijumaa, Machi 20, 2020
Kueni na Imani!
Sabato Njema! Kwa kongamano wapendwa wa Amightywind! Na karibuni kila mtu ambaye ni mgeni hapa kwa mara ya kwanza!
Ninataka kuzungumza kwa kongamano la Amightywind. Ninataka kuwaambia kuwa nimetengeneza upya ukurasa wa mbele na nimewauliza meneja wa tovuti kutoa habari za kinachoendelea na hii virusi ya Wuhan na-kwa sababu nimetambua kuwa wengi wenu mnapambana na hofu.
YAHUSHUA Alinionyesha wangapi kati yenu wanapambana na hofu sasa-na kuwa ni ukweli dhidi ya hofu-lakini YAH hakutupa roho ya hofu, lakini ya nguvu, upendo na akili timamu.
Kuogopa ni sononeko ambalo YAHUVEH & YAHUSHUA hawajatuma! Na upendo kamili-upendo wa YAHUSHUA MASIHI, upendo ambao unajua BABA yako MTAKATIFU aliyo nayo kwako kule Mbinguni, BABA YAHUVEH na upendo wa RUACH HA KODESH, ROHO MTAKATIFU, aliyo nayo kwako-upendo kamili hutupilia mbali hofu, kwa nini? Tunawaamini WAO!
Tunajua kuwa Mkono WAO sio mfupi. Tunajua kuwa Macho YAO sio kipofu, na tunajua kuwa Masikio YAO sio kiziwi. Na tunajua kuwa WAO wanajua Hamani wa kweli hapa ulimwenguni ni akina nani ambao waliumba, kwenye maabara, virusi hii iliyoumbwa kwa nia nyingine-na sitaenda katika hayo kwa sasa.
Lakini ninataka mjue-salamu kubwa ya upendo kwa kongamano la Asia, salamu kubwa ya upendo kwa wale walioko Italia. Na Ninawaambia kuwa YAHUSHUA Ananipa onyo na kutukumbusha sote-mitandao kama tu kila stesheni za habari ni za Hamani. Kumbukeni haya.
Pia ninataka kusema kuwa hofu ni kinyume cha imani, imani ndiyo sababu pekee itakayokufikisha Mbinguni: Imani ya kwamba DAMU YA YAHUSHUA MASIHI inaweza kuosha kila dhambi unaposema pole KWAKE, na kuungama dhambi zako-kwa huzuni mkuu-unauliza msamaha, na kuamini kwa imani kuwa YEYE Atakusaidia kushindana pale ambapo unashindwa na dhambi.
Kuwa na imani! Hii ndiyo fedha tu iliyoko Mbinguni! Je, mnajua haya? Hakuna chochote ambacho kitakufanya kuingia Mbinguni ila tu imani. Bila imani, itakuwa vigumu sana kumfurahisha BABA wa MBINGUNI, BABA YAHUVEH WETU.
Kwa hivyo lazima uitumie hiyo imani sasa, kwa sababu kama hautaweza kuwa na imani sasa-na hivi vitu hata havijakuguza-unavisikia tu juu yake, utafanyeje vitu vikizidi kuharibika?
Kuwa na imani!-katika zaburi 91 kuwa Ataziweka hizi pigo mbali na kwako.
Kuwa na imani!-kuamini kile Daudi alichosema, “Sijawahi kuona waaminifu
wakiachwa, wala wana wao wakiomba mkate” (Zaburi 37:25).
Kuwa na imani!-kuamini kuwa hakuna chochote kitakachokufanyikia ambacho YAHUVEH hajaruhusu!
Na kuwa na imani ya kuamini kuwa vitu vyote huenda vizuri! Ndio, hata kama Hamani wanawatafuta akina Esta sasa, na sisi ndio Esta, sisi ndio Modekai.
Na sasa tunangoja Bahari ya Shamu kufunguka na kuwazamisha majini Farao muovu wanapotukimbiza sisi sasa, sanasana kila mtu ambaye ni mwaminifu kwa YAHUSHUA MASIHI.
Kuwa na imani kuamini kuwa WAO wanakupenda sana mpaka shetani hataweza kukuangamiza ijapokuwa tu pale tu mazuri yatatokea. Hii ndiyo sababu nasema siku hii ya Machi 20, 2020-na ninataka kuwakumbusha tena, 20 ni Nambari ya waliokombolewa, (katika Kiebrania [Bibilia & Unabii]-nambari ya ukombozi).
Sisi tumekombolewa! Huu ndio mwaka wetu! Wanapofikiria kuwa tumeogopa kabisa, PIGANA! Na mseme hapana hata kama “habari” zasema, hata kama ni wangapi wanasema-katika mamilioni au mabilioni-watakufa, IMANI YANGU inaniambia hamuezi kufanya lolote dhidi yangu isipokuwa pale YAH Atairuhusu na basi lazima mazuri yatokee.
Kuwa na imani ya kuamini.
Kumbukeni mjane za Zarepta? Kumbukeni chupa ya mafuta ambayo hayakuisha? Kumbukeni alivyompa Nabii Eliya (Eliya wa kale), mafuta yake ya mwisho na unga wake wa mwisho kutengeneza mkate ule? Na Kumbukeni kuwa ilikuwa chakula chake cha mwisho ambacho yeye na mwanawe wangekula, na bado alikuwa na imani kuwa YEYE Ataongezea kila kitu. YEYE Aliiongeza.
YAHUSHUA & BABA YAHUVEH ni WAUMBAJI WA KUZIDISHA!
LAKINI OLE KWA WALE HAMANI NA OLE KWA MAADUI WA HUDUMA HII! Kwa sababu YEYE pia ni [MLETAJI wa] kuzidisha ole zitakazowajia! Na o, YEYE ana njia nyingi sasa na za kuwafanya mteseke! Haya ndiyo ninayo ya kusema kuhusu-kuzidisha.
Tunangoja! Tunangoja BABA YAHUVEH! Tunangoja YAHUSHUA wetu! Tunangoja YAHUSHUA kusema, “Njooni Nilipo!” kwa sababu tunajua tukiangalia juu, UKOMBOZI wetu wakaribia (Luka 21:28).
O kama tu ningeweza kuwakumbatia na kuweka mikono yangu juu yenu na kuwabusu kwenye shavu, ningefanya vivyo hivyo sasa. Wale wanaoona Huduma hii kama baraka, na kuhamasisha Huduma hii na kunitia mimi moyo!
Ingawa sijakuwa na bwana na kiongozi msaidizi sasa kwa miaka miwili na kupita, ninawashukuru sana kwa maombi ya mashujaa wakuu, ambao ni wanaume wa Uyahudi wa Kimasihi ambao wamekuwa wakija kama ndugu na kunitia mimi moyo. Tafadhali, tafuteni Ukurasa wa kunitumia ujumbe. Nitajibu.
YAHUSHUA MASIHI awabariki! Ninawapenda zaidi ya maneno inavyoweza kueleza!
Na o, asante MPENDWA WANGU YAHUSHUA MASIHI! Ishara, maajabu na miujiza imefuata Huduma hii, kwa sababu hatutafuti hizi ishara, maajabu na miujiza, lakini tunajua kuwa MUNGU WA MIUJIZA ni nani, na YAHUSHUA MASIHI ndilo Jina LAKE.
YAHUSHUA Ameniambia niwape surprise spesheli na hii ni kusoma tena Unabii 52. Ambao [hapo awali] mwaka wa 2001-ilikuwa “Ushahidi wa Kuthibitisha Unabii” kwa yote mnayoona sasa-ilikuwa ishatabiriwa, siri hizi, zilipewa Nabii huyu.
Ninaitengeza iwe kwenye video sasa na-lakini, ninataka-mtakapoona bar, bonyeza pale [play] kidude na sikiza Upako mpya juu ya sauti yangu: Uhakikisho ya vile YAH & YAHUSHUA WANAVYOPENDA watoto WAO.
Sabato njema!
Zaburi 91 | Iandikeni & Kuikariri!
Haya ndiyo Maandiko unayofaa kuandika. Na kwa wale ambao wapo [mahali] ambapo hamuezi kufanya haya kwa uwazi, tafuteni njia kuweza kuifanya.
Zaburi 91. Andikeni.
Maneno ya Elisheva ya Psalms 91
Yeye akaaye mahali pa salama pake YEYE ALIYE JUU SANA atadumu chini ya uvuli wa MUNGU mwenye nguvu zote- YAHUVEH, pia YAHUSHUA MASIHI.
Nitasema kuhusu YAHUVEH, “'YEYE ndiye KIMBILIO langu na NGOME yangu, MUNGU wangu, ambaye ninamtumaini.’’
Hakika YEYE atakuokoa na mtego wa mwindaji na maradhi ya kuambukiza ya kufisha.
Atakufunika kwa manyoya YAKE, chini ya mbawa ZAKE utapata kimbilio, uaminifu WAKE utakuwa ngao na kinga yako.
Hutaogopa vitisho vya usiku, wala mshale urukao mchana,
Wala maradhi ya kuambukiza yanayonyemelea gizani, wala tauni iharibuyo adhuhuri.
Ijapo watu elfu wataangukia kando yako, kumi elfu mkono wako wa kuume, lakini haitakukaribia wewe.
Utatazama tu kwa macho yako na kuona adhabu ya waovu.
Kwa sababu WEWE, O YAHUVEH-(ADONAI, ELOHIM, EL SHADDDAI, ABBA YAH, YAHUSHUA, WEWE unayeitwa “BWANA”)-WEWE ni makao yako, hata BWANA ambaye ni KIMBILIO langu,
Basi hakuna madhara yatakayokupata wewe, wala maafa hayataikaribia hema yako.
Kwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako, wakulinde katika njia zako zote.
Mikononi mwao atakuinua juu, ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.
Utawakanyaga simba na nyoka wakali, simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu.
“Kwa kuwa Ananipenda Nitamwokoa, Nitamlinda kwa kuwa amelikubali Jina LANGU.’’
Ataniita,-hii ni ahadi ya YAH, YAHUVEH Anasema- Ataniita NAMI Nitamjibu, Nitakuwa pamoja naye katika taabu, Nitamwokoa na kumheshimu.
Kwa siku nyingi Nitamshibisha na kumwonyesha WOKOVU WANGU.
Na WOKOVU wako ni NANI? Kuna MMOJA tu, ambaye ni UKWELI, na NJIA na MAISHA, ambalo Jina LAKE ni WOKOVU, Jina LAKE ni YAHUSHUA MASIHI.
Na YAHUSHUA katika Kiebrania inamaanisha “YAH AOKOA.” Jifunze Jina hilo.
Shalom.
Utangulizi wa Elisheva:
MSIOGOPE!
Usomaji wa Unabii 152 (52 upya) ilirekodiwa kupitia kinaza sauti. Hii ndio nakala.
Sabato Njema! HalleluYAH!
Utukufu kwa BABA YAHUVEH, YAHUSHUA MASIHI na MPENDWA RUACH HA KODESH!
Leo ni Machi 20, 2020-kumbukeni, Nambari 20 ni Nambari [ya] waliokombolewa katika Kiebrania [Unabii & Bibilia]. Kumbukeni kuwa hiyo ni 20 mara mbili, wakati uliopita-nilikuwa na unabii-Januari 20 2020, ambayo ni [Unabii] 150.
Na sasa ninataka mjue, huu ni Mwaka wa Waliokombolewa! Msiogope!
Hofu ni mateso ambayo YAHUVEH hajatuma. Nimetoa [kilichokuwa] pale kwenye ukurasa wa mbele-ya habari ya kinachotendeka kote duniani-na nimeiweka kwenye YAHSTube (ili mueze kuiona pale unapobonyeza ile banner au unapoenda kunapoitwa media [pale kwenye menu ya tovuti]), lakini sasa ninasikia, nataka kujenga imani yako!
Kuna habari nyingi kote kwenye intaneti sasa. Haujui nini ya kuamini.
Na chochote mtakachofanya-kama nabii anasema wao ni “Nabii” na kudai kuwa na Unabii, waulize Ushahidi wa “Unabii” zao zipo wapi, kwa sababu Ninawaambia haya: nina “Ushahidi wa Unabii,” na itakuwa miaka 26 [mtandaoni] Aprili 4, 2020.
Sasa tupo katika mwaka “20”, Nambari ya waliokombolewa! Je, Hamtaki kuwa kati ya wale waliokombolewa? Hii inamaanisha kuwa umeokolewa na DAMU YA YAHUSHUA MASIHI WETU! Hii inamaanisha kuwa hauna chochote cha kuogopa. Kwa kuwa YAHUVEH anasema YEYE hakutupa roho ya hofu, lakini ya nguvu, upendo na akili timamu!
O kongamano langu la Amightywind-nyinyi mnaoniita mimi mchungaji wenu, na Mtume na Nabii, nitawasomea Unabii 52, na mtaona, kinachofanyika sasa kilishatabiriwa.
Usiamini “Nabii” ambaye anachukua tu habari alafu kutengeneza Unabii nazo. Oneni ni miaka ngapi kitambo ilitabiriwa na mtaona hata hii virusi ya Wuhan-mnajua tayari ilitengenezwa kwenye maabara, mnajua ni kazi ya mikono ya mwanadamu, na nina Unabii inayozungumzia haya.
Nitawasomea Unabii-lazima niharakishe lakini.
Ninataka mjue vile ninavyowapenda kila mmoja wenu, na mmefunikwa kwa maombi yangu-yeyote ambaye anafahamu-Huduma hii ya Amightywind kama baraka na huniweka mimi katika maombi yao na Huduma hii ikilindwa na maombi yenu!
Nimeomba kuwa utaendelea kutii! Na usipotii YAHUSHUA MASIHI, hauwezi kudai ahadi.
Kwa hivyo, mtii! Amka na kukimbia katika Mikono YAKE! Na kusema, “YAHUSHUA nisamehe, nimetenda dhambi!”
Na YEYE Atakuwa mwaminifu na kukusamehe tena na waweza kudai ahadi kuwa hamna pigo zitakazokuja karibu na nyumba yako, kama tu Zaburi 91 husema!
Kwa hivyo Unabii 52 MIMI, YAHUVEH, Nitawakomboa Tena! Na haya ndiyo Niliyopewa mnamo Novemba 2, 2001. Miaka mingi iliyopita!
2 Mambo ya Nyakati 36:16 “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA YAHUVEH juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”
Jihadharini kuwagusa Nabii wa kweli wa YAH na kuwaumiza (Zaburi 105:15)-na hii sio ujumbe kwa kongamano la Amightywind: Ni kwa maadui wanaopenda kuja hapa. Na kuona kama bado niko hai! [anacheka] Na kama bado Huduma inasimama! [anacheka] O! Sio Huduma yangu; ni ya UTATU MTAKATIFU. Mimi ni kiongozi tu na ninapata amri kutoka Mbinguni.
* * * * * * *
Unabii 152 Unaanza
Imepokewa Novemba 2, 2001 |Upya Machi 20, 2020
Watoto WANGU wapendwa, ni wangapi wenu ambao mnanililia MIMI kwa mayowe na machozi na kujaribu kuficha hofu kutoka kwa dunia na marafiki zenu, lakini mnaniaminia BABA YAHUVEH na MASIHI wenu YAHUSHUA! Mnakuja KWETU na nyuso zenu zilizojawa na machozi mkasema, “Tufanye nini sasa? Tuende wapi sasa?”
O wapendwa WANGU, o Mimi sijakasirika nanyi wakati huu. Ni wale waovu-ambao MIMI Nimewakasirikia.
Ninaona wale waovu wakipanga. Na ni kama nyakati za kale za yule nyoka katika Shamba la Edeni, akitafuta kuwadanganya Adamu & Hawa, na sasa wanawafanya kufikiria kuwa hamuezi kushinda bila maarifa ya kidunia.
MIMI, BABA yenu YAHUVEH, Ndiye MAARIFA YOTE na unaponitafuta MIMI, YAHUVEH & YAHUSHUA MASIHI (pia huitwa “Yesu Kristo”) na RUACH HA KODESH (ROHO MTAKATIFU), mnatafuta UKWELI & MAARIFA. Kwa uhakika-kama mnatafuta, mtapata majibu wakati unapofika. Kama haujui la kufanya, kuwa na uhakika: bado sio wakati wa wewe kujua utakapoenda, wala utakachofanya.
MIMI, YAHUVEH, sitakupa tiketi ya kusafiri mpaka ni wakati wa kutoka. MIMI, YAHUVEH, siji mapema sana wala kuchelewa, lakini MIMI huwa papo hapo. Kwa wakati unaofaa-hata sekunde moja haipiti, lakini MIMI, YAHUVEH, sitawahi kukuacha, wala kukutupa. MIMI, YAHUVEH, NDIYE MUUMBAJI WA WANADAMU WOTE.
Msiogope ni nini maadui hawa watafanya. Kwa kuwa MIMI, YAHUVEH, Ninatumia vitu rahisi kama maombi yenu, kuwashangaza hawa wanaojiona “wenye hekima” (waovu) wa dunia hii.
MIMI, YAHUVEH, Naweza hata badilisha DNA yenu. Je, Mlijua haya? Ndio, Nikiamua. MIMI, YAHUVEH, Ninaweza badili hata rangi ya ngozi yako na macho yako. Msishangae. MIMI, YAHUVEH, NI MUUMBAJI, Kumbukeni? MIMI, YAHUVEH, Ninaweza kuwafanya mkose kuonekana kama MIMI, YAHUVEH, Nitakavyoamua. Hamna FAHAMU ya kiwango ambayo Nitainua dhidi ya waovu!
Utumwa, magonjwa & pigo ambazo wale waovu, wanaoitwa watoto wa shetani, wanatafuta kuziachilia juu yenu, itawajia wao wenyewe. Wengi wa watoto WANGU hawataumia. Lakini, familia za wale waovu ndio watakaopata hizi magonjwa na pigo, na hawatakuwa na majibu kuhusu sababu yake. Itawabidi kutambua kuwa MIMI, YAHUVEH, Ndiye Nilioifanya.
Wale waovu huwa wanafanya lolote kujilinda, na wanajifikiria wao wenyewe kama wenye hekima mpaka wanawapa familia zao, wapendwa wao na marafiki zao chanjo. Na bado MIMI, YAHUVEH, Nitafuta ulinzi huo. Kile kiwango ambacho hawa waovu-wanaojigamba-wanataka kuumiza watoto WANGU, hii ndiyo kiwango ambacho uharibifu huo utawajia.
Anzeni kuomba haya. Kuna nguvu nyingi katika maombi iliyosemwa kwa MIMI, YAHUVEH katika Jina la YAHUSHUA MASIHI, MWANA WANGU WA KIPEKEE.
Ombeni kuwa MIMI, YAHUVEH, Nitawapa silaha kuu za kiroho kutumia dhidi ya hawa wanadunia wanaojiinua dhidi ya wapendwa WANGU, wanaotafuta Uso WANGU na mapenzi YANGU kila siku. Ombeni kuwa kama Elisha alivyoona nguo ikianguka kutoka kwake Eliya wa kale, itakuwa vivyo hivyo tena-na tutajawa na nguvu, Upako zaidi wa RUACH HA KODESH.
Haya yatakapofanyika, hamna haja tena ya kuwa na wasiwasi-ni vipi utakapofika nchini kwingine? Wakati MIMI, YAHUVEH, Nitakutuma, Utatokezea tu. Je, Mnadhani haya si ya kawaidia? Someni Maandiko yenu na muone ni nyakati ngapi tayari, walikuwa na nguvu za kusafiri kiroho [yaani, miujiza wa kusafiri] na kujua kuwa wale waovu tayari wanatumia hizi nguvu kwa nia mbaya.
Wale waovu wanaweka siri za giza, na bado, MIMI, YAHUVEH, Nitawaambia siri ZANGU wale wanaofuata NURU INAYOWAONGOZA, AMBAYE ni YAHUSHUA MASIHI. MIMI, YAHUVEH, Nitawalinda Watoto, Bibi Arusi, Waliochaguliwa & Wateule WANGU! YAHUSHUA MASIHI Ndiye Taa miguuni mwenu.
Waovu wanapochukua nuru yenu, niangalieni MIMI, YAHUVEH, na Nitawatuma malaika WANGU kuwapa nuru njiani.
Waovu hawa wanataka kuchukua imani, tumaini, ukweli, faragha, uhuru, furaha-isiyo na kifani-na pesa zenu kutoka kwenu! Hii ni rahisi kwa wao kufanya KAMA utasikiliza pepo ya hofu, na ripoti zote mbaya zilizopo kwenye habari kushinda unavyo sikiliza na kusoma ripoti nzuri zilizoandikwa katika Maandiko.
Angalau watoto WANGU hupata haya kwa usawa. Je, Wawezaje kushinda hofu kama kile ambacho wafanya ni kusikiliza hofu?
Wale WANGU Niliowaficha wana maarifa, na njia ya kuzungukua KILA silaha ya maadui wanaotaka uharibifu wa watoto WANGU. Na huu ndio uharibifu wa dunia hii. Msisimame kwa kuelewa kwenu tu, bali katika njia zenu zote Nitambue MIMI, YAHUVEH na MIMI, YAHUVEH Nitaongoza njia zenu katika YAHUSHUA MASIHI. Kuelewa kwako kutawafanya muogope msiyoyajua.
MIMI, YAHUVEH, silali. MIMI, YAHUVEH, sitalala. Macho YANGU yapo kwenye mataifa ambapo watu WANGU wananililia MIMI katika maombi, “Tuokoe!”-kuwaokoa!
Msisikilize wale ambao wana ripoti za hofu na kutisha. Wanazungumza na kuandika kuwa MIMI, YAHUVEH, sitatoa mahali pa usalama kwa wapendwa WANGU wanaofuata YAHUSHUA MASIHI na kufanya vile iwezekanavyo kutii amri ZANGU.
Je, Ni kwa nini watoto WANGU wanataka kunitii MIMI, YAHUVEH? Kwa sababu wanapenda BABA yao WA MBINGUNI!
Wadanganyifu wamejiingiza katika ofisi tano za kanisa, na wanasiasa, na wanahabari. Wanazungumza vitu vya hofu kwa watoto WANGU. Wanazungumzia kushindwa na sio ushindi. Wanapanda fikra za kutoamini katika akili zenu [kama] MIMI, YAHUVEH, Nitawaokoa watoto WANGU. Wanaonya kuwa kila mtu lazima ajiandae kushambuliwa, “Kila mtu atakufa au atapata majeraha makubwa!”-bila MIMI YAHUVEH & YAHUSHUA MASIHI kando yenu, haya ni kweli.
Kile ambacho wanahabari na wanasiaisa wengi na wadanganyifu husahau ni kuwa MIMI, YAHUVEH, sijawatupa watoto WANGU.
Je, Haya yatanilitea vipi MIMI utukufu? Ndio watoto WANGU, siku moja mtaniunga MIMI kule Mbinguni. Haya ni kweli, lakini kama singetaka kuwapa njia ya kuepuka, mbona Niliyasema katika Maandiko YANGU (Luka 21:36, 1 Wathesalonike 5:9)? Neno LANGU halitarudi KWANGU bure. Litafanya yale ambayo Nimekadiri lifanye.
MIMI NI YAHUVEH! Na sijabadilika.
MIMI, YAHUVEH, Nilichowafanyia Israeli katika wakati wa Moshe, Nitafanya tena! MIMI, YAHUVEH, Nilichofanyia Lutu, Nitafanya tena! MIMI, YAHUVEH, Nilichofanyia Yosefu & Miriamu, Nitafanya tena! MIMI, YAHUVEH, Nilichofanyia Nuhu, Nitafanya tena. MIMI, YAHUVEH, Nilichowafanyia watoto watatu Waebrania, Nitafanya tena! MIMI, YAHUVEH, Nilichofanyia Eliya wa kale, Nitafanya tena! MIMI, YAHUVEH, Nilichofanyia Enoki, Nitafanya tena! MIMI, YAHUVEH, Nilichofanyia Elisha, Nitafanya tena.
Pale mahali pa kuanguka watu ambayo Hamani alijenga, MIMI, YAHUVEH Nitawaangika pale! Nina Esta na kama tu katika nyakati za kale, MIMI YAHUVEH Nitawakomboa watu WANGU tena. Nina Mfalme Daudi [wale na roho kama] na watatumia muziki na sifa kuwashinda maadui kama Zaburi tena zinainuliwa KWANGU katika imani kuwa MIMI, YAHUVEH, Nitakomboa tena!
Nionyesheni MIMI katika Maandiko mahali ambapo sikuwakomboa watu WANGU-waliofuata amri ZANGU na kunipenda na kuniweka MIMI, YAHUVEH, kwanza katika maisha yao? MIMI, YAHUVEH, Nitawakomboa watoto WANGU kutoka kwa mtego wa mwindaji! Kile unachotakikana kufanya ni kuomba na kuwa na imani na kuamini kuwa MIMI ni mkuu kushinda hivi vitu vya kutisha vinavyojaribu kuja juu ya watoto WANGU! MIMI, YAHUVEH, Nitajibu maombi yenu mnaponililia MIMI katika Jina la YAHUSHUA MASIHI.
Njooni na ujasiri mbele ya Kiti CHANGU cha Enzi, na mnipe MIMI lalamiko zenu. MIMI, YAHUVEH, sijakasirikia watoto WANGU wapendwa.
Nyakati zingine huwa mnaenda kando na kunitotii, na mbwa mwitu yupo tayari kuwala (kwa sababu mnakataa kutii)-kwa hivyo kama kondoo-Ninalazimika kuvunja miguu yenu ya nyuma, lakini kama MCHUNGAJI BORA, Ninawabeba kwa upendo Mikononi MWANGU. YAHUSHUA MASIHI NDIYE Anayewabeba Mikononi MWAKE mpaka mtakapopona na kuweza kutembea tena.
Je, Ni wapi ambapo mchungaji bora huwaacha kondoo wake bila kuwaangalia? Je, Ni wapi mchungaji bora huchapa kondoo na wanakondoo? HAMNA! Lakini Ninawaahidi kuwa Nitawafanya wale ambao wanataka kuwala nyinyi KUJUTA siku ambayo waliozaliwa.
Je, Si Nilimuonya Lutu na kumzuia yeye na malaika WANGU ili asiweze kuingia tena katika mji wa dhambi inayoitwa Sodoma & Gomora? Nilimlinda yeye na familia yake (isipokuwa bibi yake, aliyekataa kunitii MIMI) kutoka kwa moto na kiberiti, ambayo ilikuwa mfano ya dhiki kuu kwa Lutu na familia yake pia.
Je, Si MIMI, YAHUVEH, Nilimuonya Yosefu & Miriamu kutoweka na YAHUSHUA alipokuwa mtoto? Katika nyakati za kale, hiyo ilikuwa mfano wa dhiki kuu-kwa akina mama na watoto wao. Kwa kuwa watoto wote walikuwa wauliwe, kwa sababu wale waovu walikuwa wanatafuta MASIHI wa kweli kumuua YEYE! MIMI, YAHUVEH, Nikatuma malaika kumuonya Yosefu katika ndoto, na kumuambia yeye kutoweka na kumuambia ni lini atakaporudi.
Je, Wafikiria kuwa MIMI, YAHUVEH, sitafanya yaya haya tena?
Je, Si MIMI, YAHUVEH, Nilitoa safina kwa Nuhu na familia yake? Kabla ya dhiki kuu ya maji kufurika ulimwengu nzima?
Esta je? Mnafikiria kuwa hiyo haikuwa mfano wa dhiki kuu kuona Wayahudi wakiuwawa kote na lakini, si MIMI, YAHUVEH, Nilitoa njia ya kuepuka ya watu Wayahudi? Au hawangekuwa hata mmoja leo!
Je, Si MIMI, YAHUVEH Nilitumia silaha ile ile iliyokuwa ya kumuua Mordekai & Esta! (mahali pa kuanguka watu ambayo Hamani alijenga, akifikiria kuwa atamtega Mordekai & Esta-na watu wote Wayahudi wauawe! Na bado MIMI, YAHUVEH, Nilifanya Hamani kuuwawa mahali papo hapo pa kuangika watu-na wana wake kumi na bibi yake!)
Je, Wale ambao wanasema kuwa wanasikia Unabii hizi na wanaziamini, wanawezaje kukataa kuwa MIMI, YAHUVEH, daima Nimekuwa na njia ya kuwalinda watu WANGU? Jihadharini na wale wanaotabiri hizi vitu na kukuacha mkiwa hamna matumaini.
Haijalishi ni dhiki kuu ipi, MIMI, YAHUVEH, Nitatoa njia ya kuepuka kwa wale wanaoniamini na kunitegemea MIMI katika njia zote. Amini zaidi katika YAHUVEH na katika YAHUSHUA MASIHI wenu kushinda bibi, bwana, marafiki na ofisi tano-au serikali.
MIMI, YAHUVEH, sitawaahidi kuwa itakuwa njia rahisi kwa wote. Sitawaahidi kuwa hakutakuwa na wale watakaouwawa wakiweka maisha yao chini kwa YAHUVEH & YAHUSHUA; Nitawaahidi kuwa hawa waliouwawa wapo Mbinguni NAMI sasa na HAWATAWAHI tena kuteseka.
Sitawaahidi kuwa watoto WANGU wote watawekwa salama [katika kila njia ya kimwili], lakini MIMI, YAHUVEH, Nitawalinda kama Nilivyofanyia watoto wa Israeli katika nyakati za kale-wakati pigo, na giza, na kifo iliwajia-Niliwalinda wale waliokuwa na damu ya agano LANGU katika nyakati za kale. Je, Ni yapi zaidi Nitakayofanya sasa na DAMU MPYA YA AGANO YA YAHUSHUA MASIHI!
Enyi Mbwa Mwitu mjihadhari: Mtafichuliwa. Kondoo WANGU watajua majina yenu na mipango yenu. MIMI, YAHUVEH, naona na kujua kila mtu mwenye roho ya mbwa mwitu. MIMI, YAHUVEH, na YAHUSHUA MASIHI pekee ndio WACHUNGAJI BORA. MIMI, YAHUVEH, pekee Nitawaaibisha nyinyi mbwa mwitu-na viumbe vyenu na silaha za vita. MIMI, YAHUVEH & YAHUSHUA ndio GONGO LA GHADHABU itakayowachapa nyie mbali na kondoo na wanakondoo WANGU.
Msidanganyike! Nitawauwa hawa mbwa mwitu katika wakati WANGU na kuwatupa sio tu jehanamu, lakini katika Ziwa la Moto!
Kwa wote wanaotafuta uharibifu wa [wale wazuri] Marekani & Israeli na Wakristo & Wayahudi wote, gharama ya nafsi yenu ni nini? Na Ninazumgumza kwa dunia nzima sasa. Mnapoendelea kuyafanya haya, basi nafsi yenu itakataliwa milele! Mnapoachana na haya mtaokolewa milele!
Chaguo ni lenu.
Mwisho wa Unabii
Nikiwakosea Wengine; Nikiwafunua macho Wengine kwa upendo & Kutii & Utukufu wa YAHUVEH & YAHUSHUA MASIHI
Imepewa kwake Mtume, Nabii Elisheva Eliyahu
Ilipokewa kwanza Ijumaa Novemba 2, 2001 1:50 Usiku | Ikasomwa tena Machi 20,2020
Katika-mwaka ulikuwa 2001. Unabii 52 umesomwa tena chini ya Upako. Ninataka mjue, sitaki muogope maneno ambayo nimeweka kwenye Ukurasa wa mbele. Ni sasa, waweza kupata-kama mnataka kuenda kuangalia chini ya “Corona [virus] heroes & Information” [chini ya Amightywind.com media section]-mnaweza kuenda YAHStube, mahali sijazuiwa. Na tuna Ukurasa ambao una maelezo zaidi.
Na pia nataka kusema vile ninavyowapenda kila mmoja wenu anayeniandikia mimi na kuniambia kuwa Huduma hii imekuwa baraka kwao, na wamepea YAHUSHUA MASIHI maisha yao.
Siwezi hata kuanza kuwaambia vile Ninavyowathamini kupitia miaka hii ambayo sijakuwa na bwana na hakujakuwa na kiongozi msaidizi. Siwezi hata kuanza kuwapa asante. Kwa nyinyi Manabii Wayahudi, nyinyi wanaume, ninahitaji muendelee kujitokeza. Ninahitaji ndugu zangu katika YAHUSHUA MASIHI kunizunguka [na maombi yao] na kuwa kile kifuniko cha kiume kwangu.
Ninawapenda nyote katika Jina la YAHUSHUA MASIHI-kwa wale wanaonitambua mimi vilevile huduma hii pia kama baraka kwao.
Amina.
Mwisho wa Nakala
Omba upate kujua ni wapi katika dunia hii ambapo safina yako ipo na ni wakati upi wafaa kuingia ili kuepuka maovu yajayo. Omba katika Jina Takatifu la YAHUSHUA-Miryam (Miriamu) hakumpa mtoto wake wa Kiebrania jina la Kigiriki ‘Yesu’. Kuna nguvu za Upako katika Jina ambalo lamaanisha YAHUVEH Aokoa: YAHUSHUA.
Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!