Unabii 151

YAHUSHUA Asema, “MIMI NI MASIHI! Tubuni & Kuishi Katika Utakatifu! MSIOGOPE! NIAMINI MIMI! Uso kwa Uso na Elisheva Eliyahu!

Unabii 116 Upya, Mwanzoni Iliitwa: Lazima Muwe Watembea Maji wa Imani!

Imezungumzwa katika Upako wa RUACH HA KODESH Kupitia Elisheva Eliyahu, Septemba 30, Yom Kippur 2009 (Kama vile katika Kalenda ya Mwezi Mpya) Imezungumzwa Upya Machi 27, 2020 Wakati wa Janga.

Hapo awali ilipokewa miaka 10 iliyopita, YAHUSHUA MASIHI sasa amemuongoza Nabii Elisheva kutoa tena Unabii huu kwa dunia tena na katika Upako mpya. YAH Anataka kuwatia moyo waumini kuwa na imani ya kutembea juu ya maji, kwa mfano, katikati ya dhoruba zilizoko sasa na hivi karibuni kuja juu ya ulimwengu huu.

Mapema katika siku hii neno hili lilipewa kwanza, kwa dada mwingine katika YAHUSHUA aliyekuwa na maono akiomba: Aliona watoto wa YAH kama vifaranga wanaohitaji usaidizi na YAHUSHUA Akichukua Mikono YAKE, Akiwaongoza sote kama vifaranga wadogo.

Wakati Mtume Elisheva alipokea Unabii huu Septemba 30, tarehe hii iliwekwa na Huduma kama siku Takatifu ya mwaka, Yom Kippur. (Wakati huo, Amightywind ilikuwa inatumia mbala mwezi kujua tarehe za Bibilia. YAH Amesema kuwa hii ni kalenda ya Kiebrania ya kisasa inayotumika sasa, zote Amezikubali, lakini hii ya kisasa imetambulika na watu Wayahudi kote duniani, kwa hivyo kwa sasa, tunaitumia na hatufuatilii kuonekana kwa mwezi tena.)

* * * * * * *

Yafuatayo ni Unabii ulivyokuja

—na Nabii Elisheva, akizungumza katika "Ndimi Takatifu," kama ROHO wa MUNGU Alivyomjalia kutamka (Matendo ya Mitume 2:3-4) kwa lugha za wanadamu na malaika (1 Wakorintho 13:1). Elisheva anazungumza katika ndimi zinazoleta Unabii (1 Wakorintho 14:6).

Tunatumia MAJINA ya KIEBRANIA ya MUNGU:

YAH/YAHU יה ni JINA TAKATIFU la MUNGU, kama vile “Alleluia” au “Hallelu YAH” הללו–יה ambayo humaanisha “Msifu YAH”: YAHUVEH/YAHWEH י-ה-ו-ה MUNGU BABA; YAHUSHUA/YAHSHUA יהושוע MWANA WA PEKEE WA MUNGU—(HA MASHIACH המשיח inamaanisha “MASIHI”; ELOHIM אלוהים INAMAANISHA “MUNGU.”)

Ufunuo wa “SH’KHINYAH GLORY” שכניה תפארה —kama JINA la KIBINAFSI la RUACH HA KODESH רוח הקדש, (katika Kiiengereza “ROHO MTAKATIFU”) —upo kwenye tovuti hii. (HA SH’KHINAH {SHEKINAH} ni Kiebrania inamaanisha UWEPO WA MUNGU.)

Zaidi ya hayo, ABBA YAH אבא יה humaanisha “BABA YAH” na IMMA YAH אמא יה humaanisha “MAMA YAH.” Katika Kiebrania, ROHO WA MUNGU ni kike, Anatambulika kama “SHE” na kufananishwa hivi katika Unabii & Maandiko yaliyotajwa. Mahali Jina la MUNGU limetajwa lipo katika herufi kubwa.

Maandiko yaliyotajwa yametoka KJV/NKJV, CJB au ESV, isipokuwa pale palipotajwa vinginevyo.

* * * * * * *

Onyo ya YAHUVEH iliyoongezwa mbele ya Unabii zote:

Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako.

Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha.

Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo.

Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli.

‘‘MIMI NDIMI BWANA YAHUVEH:

hilo ndilo JINA LANGU! Sitampa mwingine UTUKUFU WANGU

wala sanamu SIFA ZANGU.” (Isaya 42:8).

(Unabii 105)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo kwa wale wanaokejeli:

“Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA YAHUVEH juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

—2 Mambo ya Nyakati 36:16

* * * * * * *

Msiogope!

Hii ilirekodiwa kwenye kinaza sauti. Hii ndiyo nakala.

Utangulizi wa Elisheva: Sitaogopa!

Shalom! Mimi ni Mtume, Nabii Elisheva Eliyahu, kiongozi wa Huduma hii ya Aleph & Tav Amightywind RUACH HA KODESH Fire Last Chance Ministry.

Huduma hii ni ya Kimataifa na Aprili 4, 2020 Huduma hii itakuwa imefikisha miaka 26 mtandaoni, ikitoa Unabii na pia kuongeza “Ushahidi wa Kuthibitisha Unabii,” mafunzo, ufunuo na kueneza injili ya YAHUSHUA MASIHI, Agano ya Kale ya Damu na pia Agano Mpya ya Damu.

Na Agano ya Kale ya Damu ni historia-kivuli cha yale yajayo- Agano Mpya ya Damu, YAHUSHUA MASIHI.

Na Nitasema haya tu mara moja kwa sababu wengi wenu mnajua tu Jina la “Yesu Kristo”: Katika Kiebrania, Jina LAKE ni YAHUSHUA na inamaanisha “YAH Aokoa”. Toleo la Bibilia la Mfalme James-waweza kuangalia mwenyewe-husema Jina YAH (kwa mfano Isaya 26:4). [Na MUNGU BABA katika herufi ya Kiebrania] YUD-HEY-VAV-HEY יהוה na ninapoitamka hutoka kama YAHUVEH.

Unabii huu ni spesheli sana wakati huu wa Machi 27, 2020 kwa sababu kuna COVID-19, virusi ya Wuhan, ambayo ni ya kutisha, inayopooza, ikituma vitisho na hofu; kama tu shetani anavyotaka kufanya kote duniani.

Imesababishwa na wale ambao wanataka kumiliki dunia nzima na kuthibitisha kuwa wanaweza kuifanya, wakikomesha uchumi, wakiwafanya watu kuogopa kuguzana. Hakujawahi kuwa na wakati kama huu sasa hivi.

Na Unabii huu ni-utasaidia sana wale wanaoipokea. Ilipewa kwangu mara ya kwanza Septemba 30 2009. Ilikuwa Yom Kippur na ilikuwa nyakati za mwisho na Yom Kippur ni Siku ya Upatanisho. (Na Huduma hii ni ya Kiebrania, Wayahudi wa Kimasihi na kwa hivyo tunasherehekea na kuheshimu Sherehe zote za Kiyahudi, ambayo kila mtu anapaswa [kuheshimu] (Mamabo ya Walawi 23)-hazifai hata kuitwa sherehe za “Kiyahudi”.)

Huu ni wakati ambao watu (katika Yom Kippur), wanaoabudu BABA YAHUVEH & YAHUSHUA MASIHI, hujiangalia na kuuliza msamaha kwa kila dhambi ambayo wamewahi kufanya-lakini hakufai kuwa na dhambi pale (1 Yohana 1:7) kwa sababu hiyo [kutubu] yafaa kufanywa kila siku.

Katika siku hii ya Machi 27, 2020 kuna tu uponyaji moja tu dhidi ya virusi hii, na ni Jina & Damu ya YAHUSHUA MASIHI. Ni ukweli utakaposema, “Sitaogopa. Kwa kuwa YAHUVEH hajanipa mimi roho ya kuogopa, lakini ya nguvu, upendo na akili timamu” (2 Timothy 1:7). Hofu ni mateso!

Ndio, hakikisha kuwa una vitu unavyohitaji-kwa kuwa wale wanaomiliki dunia hii watahakikisha kuwa rafu ni tupu, watahakikisha kuwa mnaogopa hamtakuwa na chakula ya kutosha na mahitaji mengine ya maisha-lakini msipokee hofu hiyo!

Tafuteni vitu mnavyohitaji na amini katika imani kuwa hakuna chochote kingine kina nguvu kushinda Jina na Damu ya YAHUSHUA MASIHI na kuwa watembea-maji na imani yako! YAHUSHUA Alitembea juu ya maji!

Siwaambii eti muende kule nje na kujaribu kutembea juu ya maji. [anacheka] Hapana. Mtazama! Na siwaambii kuwa mtaulenga mlima kwa kidole na utaruka na kuingia ndani ya bahari, lakini YEYE Alikuwa anajaribu kusema, na YAHUVEH & YAHUSHUA vitu vyote vyawezekana kama mtaamini (Marko 9:23)!

Kwa hivyo ninapofanya haya na kuzungumza katika Upako mpya, Upako wenye nguvu zaidi wa YAHUVEH & YAHUSHUA MASIHI, katika Upako wa RUACH HA KODESH, ROHO MTAKATIFU-kumbukeni, ushahidi wa kuthibitisha Unabii!

Msiamini kuwa yeyote ni Nabii. Wanaweza kuchukua habari na ghafla wao ni “nabii.” Tafuteni wapi ushahidi wa kuthibitisha Unabii!

Ninaweza kuthibitisha sasa hivi kwa mwaka huo…kama nilivyosema mwaka wa 2020, kwa sababu 2009 vitu hivi havikuwa vinafanyika, lakini haya ni ndiyo muwe watembea-maji wa imani na huu mwanzoni ulikuwa Unabii 116 na sasa…wakati tutakuwa [tumeiweka mtandaoni], itakuwa imepitisha Unabii 150 mtandaoni-lakini nimetabiri Maelfu juu ya Maelfu ya Unabii wakati huu.

2 Mambo ya Nyakati 36:16 “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA YAHUVEH juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

Hutaki kamwe kuwa adui wa BABA WA MBINGUNI YAHUVEH (Kumbukumbu la Torati 32:39-42). Hautaki kamwe kujipata kwa upande wake mbaya.

Kwa haraka, kwa haraka Tubuni. Na kuna tu njia moja ya kuingia Mbinguni na ni kupitia Jina & Damu ya YAHUSHUA MASIHI (Yohana 14:6; Mambo ya Walawi 4:12). Fanyeni haya kwa haraka na ombeni kwa imani ya aina hii iliyo katika Neno hili.

Kwa kuwa Neno hili ni tofauti kushinda zile zingine. Kwa kuwa YAH Anatingiza dunia hii sasa na hata wauaji waliotengeneza virusi hii.

YAH Aliruhusu iwafikie watu tena ili wawe na hekima! Kumuogopa MUUMBAJI (Mithali 9:10)! YEYE tu Ndiye tunafaa kuogopa (Luka 12:4-5).

Hata wafanye nini-wanaweza kuua mwili tu, lakini hawawezi kuua nafsi, na mwanzo wa hekima ni kuogopa YAH.

Unabii 151 Unaanza

Neno mpya lililokuja-lazima muitie maanani.

Na Neno hili ni tofauti kushinda zile zingine. Kwa kuwa tayari nimeithibitisha, kama Ninavyotingiza dunia hii katika ghadhabu YANGU katika siku hii ya hukumu!

Jitayarisheni kuona, MIMI, YAHUVEH Nikizigonga dominoes chini! Jitayarisheni kuona dominoes zikianguka!

Someni Zaburi 91-ingawa mwaona 10,000 wakianguka kando yenu na 10,000 kwenye ule upande mwingine-itakaa ni kama wote kando yako wanaanguka. Kwa kuwa ni MIMI, YAHUVEH, Ninayewaangusha chini.

Ninaitingiza dunia hii katika ghadhabu YANGU, lakini wale ambao ni WANGU, Watoto WANGU, hampaswi kuniogopa MIMI. Kwa kuwa mpo katika Kiganja cha Mkono WANGU na Mkono WANGU mwingine umewafunika kwa upendo.

Nyinyi ni kama vifaranga na Ninawaambia sasa ndio manyoya yenu yasivurugwe. Kwa sababu mtaona vitu ambavyo hamtaki kuona na mtasikia vitu ambavyo hamtaki kusikia lakini msiruhusu hofu kuwaangamiza.

Kumbukeni imani yenu ipo wapi.

Msiweke imani yenu katika uchumi, wala latika hela, wala katika kazi, ulipoajiriwa au katika biashara ambazo ni zako. Wekeni imani yenu PEKEE katika MIMI BABA YAHUVEH na MWANA WANGU WA KIPEKEE YAHUSHUA, MASIHI wenu na RUACH HA KODESH MPENDWA, ROHO MTAKATIFU.

Wekeni imani yenu na macho yenu kwenye ahadi Nilizowapa. Kueni watembea-maji wa imani!

Petro hangejua anaweza kutembea juu ya maji kama hangetoka kwenye mashua na kuchukua hiyo hatua ya kwanza, akitembea kuelekea YAHUSHUA MASIHI.

Ni hofu iliyomfanya akaanza kuzama, lakini wakati macho yake yalipomuona YAHUSHUA tena, akawa mtembea-maji na akamuangalia YAHUSHUA MASIHI-na muangalieni YEYE-na hakuzama-na hamtazama katika dhoruba zijazo!

Petro aliweza kutembea kwenye maji tena wakati YAHUSHUA Alipomuambia, “Njoo.” Haya ndiyo Ninayowauliza. Lazima muwe watembea-maji wa imani. Kwa sababu vitu ambavyo mtaona katika dunia hii, sanasana 2010, zitafanya nyoyo za wengi kufeli kwa hofu.

Msiweke imani yenu katika serikali yoyote ya dunia hii. Msiweke imani yenu katika mwanasiasa yeyote. Kwa kuwa nia zao ni zao wenyewe.

Haya ndiyo Maneno Ninayo ya kusema.

Kwa kuwa Nilianza mtingiko WANGU na hautakoma. Nimekataa kuomba msamaha kwa Sodoma & Gomora! Nyinyi, mataifa mnaoendelea kuhalalisha dhambi, TAZAMENI Nitakachowafanyia.

Wale mnaojiita “Wakristo” na [bado] mmebaki kimya, msinipigie kelele MIMI wakati hamna tena uhuru. Kwa kuwa mlibaki kimya. Mliacha wachache tu wapigane. Mliacha wengine wazungumze.

Je, Mmetazama kuwa maadui hawapo kimya? Je, Mmetazama kuwa wale wanaoeneza dhambi hawapo kimya? Wanapiga kelele kwa sauti za juu, hata walipokuwa wachache-watumishi wa shetani hawapo kimya.

Kwa nini watumishi wa YAHUSHHUA MASIHI wamenyamaza? Kwa nini watoto WANGU wapo kimya? Na Ninapozungumzia watumishi, sizungumzi nanyi ni kama nyinyi ni watumishi kama jina hili linavyotumika kwa kawaida. Ninazungumzia wale wanaomtumikia YAHUSHUA MASIHI, walio baraka KWAKE.

Ni wachache sana wanaozungumza! Ni wachache sana wanaotetea yale yaliyo Takatifu!

Kumbukeni, hukumu huanza katika Nyumba ya BWANA, 1 Petro 4:17.

Kwa nini makanisa yote haipigani? Ni makanisa ngapi yaliyopo? Katika kila nchi mbona makanisa hayapigani dhidi ya hizi amri mbovu zinazopitishwa?!

Wanavuta tu mabega zao. Wanajali tu shughuli zao!

Kwa hivyo msishangae, o nyinyi makanisa mliojipanga, wakati serikali zitawajia na kuchukua uhuru wenu wa kuhubiri na kuweka ishara milangoni kufunga makanisa yenu.

O msishangae wakati ardhi yenu inachukuliwa. O msishangae, nyinyi mliojidai na mamilioni yenu. Ninazungumzia matajiri sasa. Mnaweka imani yenu kwenye hela. O msishangae wakati haina maana na ni kama vumbi na jivu mikononi mwenu (Mathayo 19:24, Luka 16:19-31; Yakobo 5:1-6).

Nitawaonyesha. Nitaonyesha dunia hii!

Wengi wataanza kupata ujumbe 2010 ikianza, lakini Ninawaonya sasa, watoto, ili msiseme kuwa ABBA YAHUVEH, BABA YAH wenu, hakuwaonya. Ninawatayarisha sasa, ili hamtashangaa, na Ninawafariji sasa hivi.

Kwa kuwa BABA yenu hataki nyoyo zenu zisumbuke. Kwa kuwa Ninawapenda. Kama tu katika siku za kale, Nilifanya miujiza, na hakuna kilichobadilika.

Kwa hivyo shikilieni pindo la vazi la YAHUSHUA MASIHI. Endeleeni kuoshwa katika Damu YAKE iliyomwagwa! Simameni katika Mavazi YAKE ya utakatifu na Ninawaahidi haya, maombi yenu yote inasikika kule juu Mbinguni.

Tembeeni katika Utakatifu ndio shetani asiwashtaki. Tembeeni katika Utakatifu, ili msilete aibu yoyote kwa Jina la YAHUSHUA MASIHI, DAMU YA UPATANISHO YA PEKEE KWA DHAMBI (Warumi 3:25).

Masikio YANGU yamefunguliwa kwa njia spesheli sana.

Tena, Elisheva Eliyahu, umeyazungumza haya unapoomba. Ni kama uliweza kusikia sindano ikianguka Nilivyokuwa Ninazungumza Neno hili kwako.

Kwa kuwa siku hii imekuwa spesheli. Kwa wote wanaosherehekea Yom Kippur.

Nilipoona ukitubu juu ya chochote ambacho umekifanya kisichonifurahisha MIMI, kama kila lalamiko la maombi yako lilivyoletwa KWANGU, wakati uo huo, hasira ZANGU zilitingiza dunia hii-kama tu nyakati za kale na Moshe, watoto wa Israeli walilindwa na wale walioabudu muumbaji mwingine, hawakulindwa.

Hakuna chochote kilichobadilika. Nitawabariki wale walio baraka kwa MIMI, YAHUVEH, kwa MWANA WANGU WA KIPEKEE, MASIHI, YAHUSHUA MASIHI & RUACH HA KODESH, ROHO MTAKATIFU. Nitawalaani wale ambao ni laana kwa BABA YAHUVEH, YAHUSHUA MASIHI na RUACH HA KODESH.

Na hivi ndivyo Nilivyozungumza leo hii, BABA wenu wa MBINGUNI, BABA YAHUVEH.

Mwisho wa Unabii

Imezungumzwa, imeandikwa,

Septemba 29, 2009

Imezungumzwa chini ya Upako Mpya

Machi 27, 2020, Mtoto, Shujaa,

Bibi Arusi

Wa YAHUSHUA MASIHI

Mtume, Nabii Elisheva Eliyahu

Tembea juu ya maji!

Mathayo 14:28-31-hii ndiyo sababu lazima mjifunze kuwa watembea-maji wa imani.

Na Petro akamjibu, ‘‘BWANA, ikiwa ni WEWE unaniamuru nije KWAKO nikitembea juu ya maji… na YAHUSHUA Akamwambia, “Njoo.’’ Na akamwambia Petro, “Toka kwenye mashua” na njoo, tembea juu ya maji na YAHUSHUA.

Na akamwambia Petro, “Njoo,” kwa hivyo Petro akatoka kwenye mashua na kutembea kwenye maji, na Alipoanza kumuelekea YAHUSHUA MASIHI, lakini alipoona upepo mkali na mawimbi yanaanza kupanda na dhoruba ikaja, aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama. Alikuwa ameanza kuzama na akapiga kelele, “YAHUSHUA, niokoe!’’

Na YAHUSHUA Akanyosha mkono WAKE na kumshika, na akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini uliona shaka?’’

Waona, haya ndiyo yanayotufanyikia. Haya ndiyo yanayotendeka kote duniani kwa wale ambao hawana imani sasa hivi ya kuwa watembea maji.

Mnaangalia hii virusi ya COVID-19-na Ninawaambia kuwa hii haitakuwa ya mwisho. Haya ni mazoezi tu kwa sasa. Wanaomiliki ulimwengu huu, na wanajijua ni akina nani, wanawacheka.

Hii ni virusi iliyotengenezwa na binadamu. Hapo mwanzoni ilitengenezwa na A.I. Iliwapa wanasayansi ni nini cha kuweka pamoja kuona kama wanaweza kusimamisha dunia nzima-na kuwaweka katika hofu.

Serikali zenu-hamna hata moja ila moja tu; hakuna kiongozi yeyote ila mmoja tu ambao hawajui ni nini kinachoendelea.

Na kondoo wasio na hatia na wanakondoo wamewekwa katika hofu na sasa wameambiwa, “Kaeni nyumbani.” Wamefungiwa ndani ya nyumba zao. Sio kila mtu aliye na kadi na anaweza kununua mtandaoni, alafu ni wachache sana walio na vitu wanavyohitaji.

Nimekuwa nikitabiri kwa miaka nyingi sana, nikiwapa ujumbe ule ule kuwa BABA YAH & YAHUSHUA wameshinda wakiniambia niizungumze: Tayarisheni begi lenu la kuepuka. Hakikisha mna vitu mnavyohitaji tosha katika nyumba zenu. Kwa kuwa hautajua kama hauna kazi au kitu kikifanyika na wahitaji kuwa na vitu zaidi.

Lakini, ni wangapi walio na uwezo wa kuwa na kadi sasa? Ni wangapi kote duniani sasa wameamriwa kukaa nyumbani na hawaruhusiwi kuwa na kazi? Na wamefunga biashara zao na wana njaa?

Hamna njaa kama Mnaamini kile Daudi alichosema, “Sijawahi kuona watakatifu wakiachwa wala mbegu yao wakiomba mkate” (Zaburi 37:25). Hawakuwa na njaa, na watoto wa Israeli kule jangwani.

Lazima muamini. Lazima muwe na imani kuwa kama unamuabudu na umeuliza dhambi zako zisamehewe na YAHUSHUA MASIHI na unaishi katika utakatifu mbele YAKE-simama katika Zaburi 91!

Idai kupitia Jina & Damu ya YAHUSHUA MASIHI, na hautapata njaa. YEYE Anaweza kufanya chakula kijitokozee. YEYE ni MUNGU Anayesema, “Kila kitu chawezekana [kama waamini]” na “bila imani hauwezi kumfurahisha YEYE.’

Tii amri, kaeni ndani ya nyumba zenu, lakini jueni haya: Wekeni imani yenu katika YAHUSHUA. Mlilieni YEYE!

Kwa wale walio na uhuru wa kuwa na Bibilia, Someni, amini. Amini kuwa historia ya Agano ya Kale ya Damu-haya ndiyo iliyokuwa, ilikuwa kivuli-na YAHUSHUA Akasema, “Imemalizika”.

Haya [sasa] ndiyo Agano Mpya ya Damu. Kila kitu katika Torati tunayosoma katika Maandiko ya Torati, Vitabi Vitano vya Moshe-YAHUSHUA MASIHI Aliyakamilisha haya katika Agano Mpya ya Damu (Waebrania 8:13).

Ndio sababu Maneno Yake ya Mwisho, kama alivyosulubiwa-DHABIHU TAKATIFU YA PEKEE YA MWANAKONDOO WA YAH iliyokuwa kamili; YEYE Alitoka kwenye Kiti CHAKE cha Enzi kama mmoja wa WAUMBAJI. Kwa kuwa ni UTATU MTAKATIFU: BABA YAHUVEH, YAHUSHUA MASIHI na RUACH HA KODESH, ROHO MTAKATIFU. Hii ndiyo UTATU MTAKATIFU.

Na YEYE Alitoka kwenye Kiti CHAKE cha Enzi kwa sababu yenu na mimi, ili dhambi zetu zisamehewe. Na YEYE mwenyewe Akijitoa kama dhabihu. Kamili kabisa.

YEYE Alizaliwa kutoka kwa mwanamke bikira Myahudi. YEYE Aliwekwa na Mkono wa RUACH HA KODESH katika tumbo lake.

YEYE Alikuwa, kama tunavyosema, MUNGU KATIKA ROHO na YEYE Alikuwa MUNGU KATIKA MWILI (Yohana 1). Hivi ndivyo MUUMBAJI wetu ALIVYO. Na katika mwaka wa 33 baada ya Huduma YAKE ya miaka 3, Akaenda kwenye msalaba.

YEYE Aliruhusu miiba, misumari, kugongwa kwenye Mikono YAKE na Miguu YAKE. YEYE hakukubali tu kusulubiwa lakini kuteswa, ili Damu YAKE ingemwagwa.

Kwa kuwa “bila kumwagwa kwa damu, hamna msamaha wa dhambi” (Waebrania 9:22).

Na YEYE Aliyafanya yaya haya kwa sababu yenu na mimi katika muda wa masaa 3. Na Nilipewa ufunuo, kuwa wakati huo alipokuwa anateswa, eti aliona kila jina ambalo limeandikwa katika Kitabu cha Maisha cha MWANAKONDOO.

Kwa kuwa waona, yeyote anayemuabudu YAHUSHUA, anayelilia huruma na kuuliza msamaha na kuungama kila moja ya dhambi zao-Damu ile iliyomwagika kutoka KWAKE siku ile itafunika kila moja ya dhambi zako, ikiziosha [mbali kama] kulia ilivyo mbali na kushoto, kama tu mtamlilia YEYE, “YAHUSHUA MASIHI! Nihurumie mimi. Kwa kuwa mimi ni mtenda dhambi!”

Waona, hakuna yeyote aliye kamili! Tulizaliwa katika dhambi, kwa sababu wazazi wetu ni watenda dhambi-kwa sababu tunatoka kwa Adamu na Hawa-lakini mwaona, YEYE Ndiye MZABIBU na sisi ndio matawi yanayotokea KWAKE.

Na YEYE Ndiye MFALME WA ISRAELI, lakini YEYE pia ni MUUMBAJI. Aliona kila jina. Aliona kila uso. Anajua ni nini utakachofanya na Unabii huu.

Nimethibitisha “Ushahidi wa Kuthibitisha Unabii” kama nilivyozungumza haya katika Upako mkuu-na BABA YAH pia amebadilisha maneno mengine kuwa hata na nguvu zaidi.

Kwa hapo mwanzoni ilipopewa, nilikuwa nafupisha Jina la YAHUSHUA, lakini sasa YEYE Anasema, “Hakikisha kuwa unasema YAHUSHUA MASIHI. Hakikisha kuwa unakumbusha watu kuwa Jina hilo lamaanisha ‘YAH AOKOA’.”

Msiwahi kusema tena jina ‘Yeshua’. Mnatoa Uungu wa Jina la BABA katika Jina la MWANA. Je, Ni baba yupi ambaye hataki mwanaye kubeba jina lake?

Jina ni YAH na shetani anachukia Jina la YAHUSHUA na ndio, kama wataka waweza sema YAHSHUA. Inamaanisha ‘YAH AOKOA.’

Wayahudi wa Kimasihi watakufunza ‘Yeshua.’ Hakuna maana katika hilo jina. Wanaogopa tu Wayahudi wa orthodox sana. Hawataki kusema Jina ‘YAH’, lakini kama unaogopa kusema Jina la YAH, wakati Zaburi 91 inasema YEYE Ataokoa tu wale wanaolia katika JINA LAKE…

Jina LAKE ni YAH. YAHUVEH-na nimezungumza haya katika Upako mkuu siku hii.

Nimeweka ushahidi wa kuthibitisha Unabii ambao ulikuwa wa kitambo 2009 na sasa tupo katika machi 27, 2020.

Watu kitu cha pekee kitakachoshinda kile kinachotendeka sasa ni nyinyi kuamini-kama tunavyokaribia Pasaka Aprili 8 jioni, 2020. Fanya yale ambayo unaweza kusherehekea Pasaka. Tazama tunachofanya na sikiliza Unabii zijazo tena kuthibitisha, YEYE ni sawa jana, leo na milele (Waebrania 13:8).

Kama alivyokomboa Moshe na watoto wa Israeli-na walikuwa katika mamilioni, hakuna kilichobadilika-YAHUSHUA MASIHI Alimwaga Damu YAKE na hata tone moja ya Damu hiyo huosha dhambi, kama kwa kweli unatubu na kuungama na huzuni.

Na msitende dhambi kimaksudi. Msidharau neema na huruma na kusema, “O, nitatenda dhambi tena na nitarudi tu na kuuliza msamaha tena.”

O watu. Kueni makini sana na yale mnayoyafanya. YEYE hufungua Mikono YAKE wazi kwenu sasa. Kila mtu atawajibika kwa yale wanayojua. Kueni na imani.

Bila imani ni ngumu sana kumfurahisha YAH (Waebrania 11:6)-bila imani. Kuwa na ile imani ya kutembea juu ya maji, inamaanisha kuwa utayafanya yale ambayo wafikiria hayawezekani, utashikilia Pindo la vazi la YAHUSHUA.

Hautaiachilia hata kama watakuja na kukuambia, “Tutakuua kama hautachukua Alama ya Mnyama!” Kueni tayari kuweka maisha yenu chini kama yahitajika.

Kwa kuwa mnajua kuwa pumzi yenu ifuatayo itakuwa Mbinguni na mnajua YAHUSHUA Atachukua ROHO yenu kutoka mwili wenu na hata anayekuua hatapata nafasi ya kukusikia ukipiga mayowe yako ya mwisho ukifa.

Utakuwa Mbinguni.

YAHUSHUA Alikufa msalabani, lakini waona, hakuna binadamu yeyote aliyemuua YEYE. YEYE mwenyewe alitoa MAISHA YAKE, lakini hakubaki kifoni. Katika siku ya tatu alifufuka tena! HalleluYAH!

Mbele wa Mashahidi na katika siku 40, alitembea ulimwenguni humu. Mbele ya Mashahidi alifanya miujiza-kuzidi kile kitabu kinachoweza kurekodi (Yohana 21:25)-kote duniani. Na katika siku ya 40 mbele ya Mashahidi, alipaa angani hadi Mbinguni.

Na YEYE alisema kuwa alienda kutayarisha mahali petu nyinyi na mimi (Yohana 14:3), kwa yeyote anayeamini ndani YAKE.

Nimemuona uso kwa uso. Sababu ya kumuona YEYE kando yangu katika picha za Amightywind.com ni [kwa sababu] sina bwana pale. Nilikuwa na bwana aliyekuwa kando yangu, aliyekuwa kiongozi mwenza wa Huduma hii, mpaka alipodai kuwa awe mkuu wa Huduma.

Na waona, kuna tu MKUU mmoja tu (na ipo mbele [ya kila Unabii]-[kipande cha Unabii kutoka] Unabii 105, Niliambiwa kuiweka pale na sikuelewa kwa nini) na huyo ni UTATU MTAKATIFU: BABA YAHUVEH, YAHUSHUA MASIHI na RUACH HA KODESH, ROHO MTAKATIFU, AMBAYE pia ni IMMAYAH, SHEKHINYAH GLORY. YEYE ni MAMA HEKIMA. Hata toleo ya Bibilia ya Mfalme James humuita YEYE ‘SHE.’

Hakuna yeyote ambaye ni MKUU wa Huduma hii, ila tu WAUMBAJI WATAKATIFU. Mimi hupata tu maagizo kutoka Mbinguni na kuna tu kiongozi mmoja tu sasa-lakini ninangoja sana ile siku ambayo kutakuwa na usawa wa mwanamume tena.

Lakini nina YAHUSHUA MASIHI pale na Ninawaambia kuwa YEYE ana macho ya samawati.

Na nitatangaza mbele ya dunia nzima: nimemuona YEYE uso kwa uso kama alivyokuwa ameketi mwisho wa kitanda changu. Na nilihisi upendo mkubwa kama mawimbi ya tsunami! Nuru iliyong’aa kando YAKE ilikuwa kitu ambayo hata siwezi kuanza kuilinganisha na chochote kile. Na mawimbi hayo ya upendo kama tsunami-kila atomu, kila molekuli, kila sehemu yangu-upendo huo ulipenya ndani yangu.

Nuru YAKE iliniamsha. Ilikuwa zile siku ambazo nilikuwa na kitanda cha maji, na kulikuwa na reli ya ngozil na aliketi pale na kuniangalia mimi na kuniambia haya maneno-bila hata kufungua Mdomo WAKE-YEYE Alisema, “Pole sana kwa kuteseka hivi.”

Sikujua mateso ni nini. Nilidhania kuwa ninajua. Mengi yametendeka.

Kwa kuwa mwaona, Upako ukizidi, mateso yanazidi. Kumbukeni haya, kwa wale mnaotaka kudai kuwa nyinyi ni Manabii.

Kwa kuwa NABII MKUU aliyewahi kuwa, MMOJA tu, AMBAYE aliandika Kitabu cha Ufunuo, haikuwa Yohana. Hayo ni Maneno YAKE YAHUSHUA (Ufunuo wa Yohana 1:1-2). Na hakuna aliyeteseka kushinda YEYE. YEYE ni UNABII ndani yake MWENYEWE.

YEYE Ndiye NENO lililofanywa kuwa Mwili. Kwa hivyo mtu anaposema yeye ni Nabii, waulize wameonyesha nini ya kuyathibitisha.

Miaka iliyopita, kabla chochote kitendeke, tuna “Ushahidi wa Kuthibitisha Unabii” na BABA YAH Alisema, Je mtathibitisha vipi kuwa wewe ni nabii kama hautathibitisha kwa kutabiri vitu kabla ya wakati.

Na haya ndiyo niliyofanya. Na Ninawaambia haya, YEYE ana macho ya samawati. Ile picha ambayo msichana mdogo alichora ndiyo picha ninayoitumia. Kwa kuwa ipo karibu sana kufanana na YAHUSHUA.

Na yupo kando yangu, na ingawa sina bwana kando yangu, ninajua kuwa mimi ni mmoja wa Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI, na anashikilia mimi. Na ananijulisha kuwa YEYE yupo papo hapo kila wakati.

Bibilia inasema, ‘Wana baraka wale walioamini na hawajaona’ (Yohana 20:29).

Nimekuwa wa wageni malaika. Na vidole vyangu-nina ushuhuda kwenye tovuti [Amightywind.com] ambapo nimepitisha vidole vyangu kwenye mabawa ya Malaika Mkuu Mikaeli; na Malaika Mkuu Mikaeli hulinda Huduma hii, kama anavyolinda Israeli.

Na haya ni Kiebrania, yanaambatana Kibibilia-muhimu sana watu.

Ninajiita mimi Myahudi wa Kimasihi pia lakini pia mimi ni myahudi, lakini natamani sana ile usawa niliokuwa nayo hapo awali, na alikuwa mwanamume aliyezaliwa Israeli. Alikuwa usawa wa Yuda [kwa Efraimu] na ninajua YAH atamrudisha yule ambaye shetani alimdanganya, lakini sasa Ninazungumza katika Upako mkuu.

Huduma hii ipo katika Upako mkuu. Uzuri wake, hakuna nyingine inayoweza Kulingana nayo kwenye Intaneti hii na haina chochote cha kufanya na mimi ni nani. Ilibidi nimueke bwana yangu kwenye madhabahu ya dhabihu; yule ambaye nilimuita mwanamume aliye na upako mkuu kushinda wengine niliokutana nao.

Na lazima arudi na kutubu mbele ya watu-kwa dhambi alizozifanya mbele ya watu-lakini atakuwa na upako mkuu kushinda hapo awali, kama atachagua kuyafanya haya. Kama sio, YAH atamuinua mwanamume mwingine kutoka Yuda.

Ninataka tu muwe na imani. Hii [ilikuwa] Unabii 116, na sasa tupo katika Unabii 150 na sina uwezo wa kuwa na watengenezaji video zaidi wa…

Alipokuwa nami kutoka 2016 (Machi 7, 2016) hadi mahali 2018 [ambapo] vitu vilianza kuenda vibaya-lakini tulikuwa na Unabii 1000 pekee na ufunuo mpya ambazo zingekuwa baraka kwenu.

Ninataka muwe na imani na YAH anasema kuwa njia ya pekee ambayo utapata haya ni kuwa na imani ndani YAKE.

Kueni na imani kuwa virusi hii itakufa kabla haijaguza mtoto wa YAHUSHUA MASIHI.

Ninafunika Huduma hii na Damu ya YAHUSHUA MASIHI iliyomwagwa na kila mtu anayesema kuwa Huduma hii ya AMIGHTYWIND ni baraka kwao-wamelindwa na maombi yangu-Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI.

YAHUSHUA Alizungumza kwangu wazi na kuniambia kuwa mimi ni Ringmaiden na yule ambaye ni bwana yangu, atakuwa Ringbearer-na tunawafunika na Damu ya YAHUSHUA MASIHI na kuwalinda, lakini hamna Ringbearer kwa sasa, lakini Ringmaiden bado yupo.

Na o, kwa wale ambao mtakuwa Wageni, (wajua sio kila mtu anaweza kuwa Bibi Arusi), Wageni watakuwa katika Karamu ya Harusi ya MWANAKONDOO na Wageni watadensi na BWANA HARUSI. YAHUSHUA Alisema, “Baraka kwa WOTE walioalikwa katika Karamu ya Harusi ya MWANAKONDOO” (Ufunuo wa Yohana 19:19).

Someni Unabii. Oneni kama yale ambayo nimetabiri hayajakuja kutendeka.

Na yale ambayo bado hayajatendeka, Kumbukeni haya: Tupo katika mwanzo wa mateso makuu sasa, ambapo kutakuwa na ukame na tauni na YAHUSHUA mwenyewe alisema, ikianza, pale Mathayo 24:1.

Someni na mtajionea. Mathayo 24, na Maandiko yafuatayo ninazowapa kama maelezo ya chini kwa Unabii huu.

Mwaona, tupo katika mwanzo wa [itakavyokuwa] Dhiki Kuu. Na YAHUSHUA MASIHI Anatingiza dunia hii; Anafanya majaribio sasa: Ni nani ambaye anafaa kuitwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI?

Ombeni kuwa mtapatikana kama wale wanaostahili kuepuka. Endeni KWAKE.

Mtakapoyasikia haya na hamna imani, Ninawakumbusha haya, kuwa YAHUVEH hawezi kudanganya na YEYE Amesema kuwa Neno LAKE haliwezi kurudi KWAKE BURE (Isaya 55:11). Kumbuka NENO LAKE ni NANI: ni YAHUSHUA Aliye NENO ambalo lilifanywa kuwa mwili kutoka mwanzoni. Imesemwa pale kwenye kitabu cha Mwanzo [“Na MUNGU Alisema…” (Mwanzo 1:3, 6 nk.)].

Kila mtu amepewa kipimo cha imani-na kama wafikiria kuwa hauna imani, basi chukua pumzi yako ifuatayo. Sawa? Je, Ulifikiria hapo kuwa hakukua na oksijeni ya kupumua?

Hapana. Hii ndiyo inayoitwa imani.

Unapoingia kwenye lifti na unafinya kidude, wafikiria kuwa itaanguka au una imani kuwa ukifinya kile kidude itakupeleka unapotaka kuenda?

Hii ndiyo inayoitwa imani.

Unapokula chakula chako, je, una imani kuamini kuwa waweza kuimeza au wafikiria kuwa itakunyonga hadi ufe?

Hii ndiyo inayoitwa imani.

Kwa hivyo msifikirie kuwa hamna imani. Kueni na imani haijalishi ni nini unachopitia-kwa kuwa imeandikwa-‘Kila kitu hufanikiwa kwa uzuri [wa] wale wanaompenda YAH [na] wameitwa katika sababu ZAKE’ (Warumi 8:28).

Hii inamaanisha wale walioitwa katika sababu za YAHUSHUA pia. YEYE ana sababu ni kwa nini umezaliwa. Tafuta sababu hiyo ni nini. Sababu kuu ya yote-kumbukeni haya, YAHUSHUA hajawahi kuwa “mwana wa binadamu.”

Kila toleo la Bibilia linalomuita yeye kama “mwana wa binadamu”… YEYE PEKEE ni MWANA WA PEKEE WA YAHUVEH. YEYE hajawahi sema kuwa YEYE Alikuwa mwana wa Yosefu hata mara moja katika Maandiko.

YEYE Alisema-YEYE Aliona-kazi alizozifanya, Aliona BABA kule Mbinguni Akizifanya (Yohana 5:19). Alimpa YAHUVEH utukufu tena na tena na tena. Huyu Ndiye BABA YAKE.

Mna imani. Sasa kueni na imani ya kuamini YEYE Anaweza kuwasamehea dhambi zenu, hata kama chafu vipi-na isipokuwa moja tu kwa wale ambao wamemdharau ROHO MTAKATIFU, lakini kama umepokea Unabii huu kama ukweli, basi haujamdharau ROHO MTAKATIFU au hata hamngetaka kunisikiliza mimi au kuwa na chochote kufanya na Utakatifu.

Maadui wa Huduma hii, wale waliokataliwa-wanachukia Huduma hii, wanachukia kila kitu kilicho Takatifu na kabisa wananichukia mimi, lakini waona, lazima uwe tayari kuchukiwa (Mathayo 10:22). Lazima uwe tayari kuteswa (2 Timotheo 3:12).

Haya ndiyo maneno ya YAHUSHUA Aliyosema. Kama wote wangempenda YEYE, wangetupenda sisi (Yohana 15:19).

‘Wana baraka wale wanaoteswa na kuchukiwa kwa ajili ya Jina LANGU. Kwa makuu ndiyo baraka zenu Mbinguni’ (Mathayo 5:11-12).

Kwa hivyo nina matumaini na ninaomba siku hii-kama nilivyozungumza chini ya Upako mpya, Upako wenye nguvu zaidi-ninaomba kuwa utanitafuta mimi na kuniambia kuwa utatembea kwa imani na sio kwa kuona.

Msisikilize habari. Msisikilize televisheni. Kwanza, toeni televisheni kwenye nyumba zenu. Zinawatazama. Mnafikiria kuwa mnazitazama.

Na chochote mtakachofanya, msivae chochote vichwani mwenu: msivae airpods. Msivae headphones ambazo ni wireless.

Kutakuwa na Unabii mpya kuhusu haya, wanawafuatilia kutumia vitu hivi. Sasa, waweza kuchagua kuniamini sasa au mtajijulia haya baadaye, lakini wanaweka vitu hatari katika kitu chochote ambacho utakachovaa kichwani ambayo ni wireless.

Kueni na imani ya kuamini. Kueni na imani ya kuamini kuwa YAHUSHUA MASIHI Atafanya yote Aliyosema na nitawaona kule Mbinguni.

Kwa hivyo mnitafute mimi. Nitawatafuta. Na pia nitawatafuta mkiniandikia mimi mnapobonyesha kile kidude cha contact pale Amightywind.com-miaka 26-Aprili 4, 2020 ndio siku ya kuzaliwa ya Huduma hii ambayo sasa iko na trademark. [anacheka]

Ilibidi nitafute trademark na ikapitishwa Mnamo 2020 ile watu wasichafue jina tena-kuna faini ya $500,00 watakapoyafanya haya-kwa sababu shetani huja kuiba, kuua na kuharibu.

Kueni na imani. Someni Unabii hizo na mtaona imani yenu ikikua. Jifunzeni kutoka kwa mifano hata ya waliokataliwa na kukimbia mbali na wao.

YEYE hawaulizi kuwa kamili. YAHUSHUA Anajua kuwa hakuna yeyote ambaye anaweza kuwa kamili. YEYE NDIYE MTU PEKEE ALIYE KAMILI, AMBAYE ametembea duniani humu. YEYE Anataka tu ufanye vile uwezavyo na dhambi kuu ni unapoanguka, hautaki kuamka tena na kukimbia katika Mikono YAKE ya upendo!

Neno la Unabii

YAHUSHUA MASIHI Ndiye MCHUNGAJI BORA na Ata-mnaendelea kukimbia ndani ya shimo za mbwa mwitu na nyinyi ni WAKE au mwasema hivyo, lakini mnataka kuendelea kuishi katika dhambi mkitazama porn, au dhambi nyingine; nyinyi ni kama kondoo wadogo-na Atavunja miguu yenu ya nyuma, kama majina yenu yamo katika Kitabu cha Maisha cha MWANAKONDOO.

Na Ataruhusu mateso kali kuja ndani ya maisha yako ili ulazimike kumlilia YEYE. Kwa kuwa Atawashika kwa utaratibu Mikononi MWAKE na upendo karibu na kifua CHAKE kwa sababu hautaweza kutembea.

Mwisho wa Neno la Kinabii

Na hatufai kamwe, kufikiria kuwa tunatembea pekee yetu. Ndio kwa sababu mnamuona YAHUSHUA pale kando yangu katika picha zote mpaka nitakapokuwa na bwana kuchukua nafasi hiyo tena.

Kwa sababu kitu kimoja ambacho sikutaka ni picha yangu kuwa pekee yangu tena.

Inanikumbusha mimi, inanitia mimi moyo-unaweza kuweka uso wako pale [na YAHUSHUA]! Tayari nishawaambia vile YAHUSHUA Anavyofanana. Weka uso wako pale.

Huyo ni YAHUSHUA Anayekukumbatia. Huyo ni YAHUSHUA Anayesimama kando yako. Huyo ni YAHUSHUA Anayekupa penzi hilo la tsunami ambalo hakuna chochote kingine kinachoeweza kuifikia au yaweza kuelezwa.

Ninaomba ya kwamba haya yamekuwa baraka kwenu. Sikujua Nitasema haya yote. Ninawapenda-kama mnaabudu na kupenda YAHUSHUA MASIHI-niandikie mimi pale kwa [tovuti] ya Huduma pale kwa contacts.

Na ninawangoja ndugu zangu katika YAHUSHUA MASIHI, Manabii walio kule nje, sanasana wale ambao wamezaliwa na kulelewa kule Israeli, Wayahudi wa Kimasihi.

Kama unaamini kweli za Huduma hii, dada yenu anawahitaji. Hana ule ufuniko spesheli wa mwanamume Takatifu, wa bwana tena. (Lakini anao wana wengi katika YAHUSHUA MASIHI! Wanazunguka dunia na wananifunika mimi!) Lakini ndugu, inukeni!

Inukeni! Tafadhali Njooni. Nahitaji manabii, wanaume-ninahitaji tu mje na kumtia moyo huyu mtoto, shujaa, Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI.

Nimetengeneza trademark headband yangu. Huwa inanikumbusha juu ya Kabila zote za Israeli. Inanikumbusha mimi kuwa mimi ni Myahudi na inanikumbusha mimi kuwa lazima tuwe mashujaa. Hatuwezi kuwa waoga.

Na hiyo ndiyo utakayoona kwenye picha ambapo nipo na YAHUSHUA.

Kwa hivyo YAHUSHUA MASIHI-ninaomba BABA YAHUVEH katika Jina la YAHUSHUA MASIHI, Ulisema kuwa nina Upako, Upako mpya leo hii…

Ninaomba sasa hivi BABA wa MBINGUNI, kwa sababu ulisema kuwa mimi ni Eliyahu wa upya, nina Upako wa kuweza kuomba sasa dhidi ya COVID-19 (hii virusi ya Wuhan iliyotoka Uchina!) na ninaombea BABA YAHUVEH, kondoo wasio na hatia na wanakondoo…

Ninaombea karama ya kuzidisha chakula chao sasa, kwa wale ambao ni wa YAHUSHUA MASIHI; ninaomba sasa kama wanafikiria kuwa wana-mabaki ya mchele.

Kile walicho nacho, kuwa watakuwa na imani kuitoa KWAKO NA WEWE utatafuta njia ya kuizidisha kama ulivyowafanyia Watoto wa Israeli; WEWE utazidisha walicho nacho cha kukula.

Kwa kuwa WEWE ulisema kupitia Daudi, “Sijawahi kuona watakatifu wakiwa wameachwa wala mbegu yao kuomba mkate” (Psalms 37:25).

Ninaomba sasa-hiyo virusi ya kishetani-WAO wanaiita-kwangu jina linalofaa kwa kuwa linatoka kwa shetani, imetengenezwa na shetani na ni kuhusu ni nani anataka kumiliki ulimwengu huu, hata kisiasa-na wale wasio na hatia, wanaoteseka, kwa sababu wanataka kuingiza hizi chanjo ndani yao ambayo sio chanjo; ni kifo na baadaye kutakuja chip. Na wanataka kuondoa fedha zote. Ili kuwe na one world order, ambayo itakuwa dunia moja isiyo na mpango.

Ninaomba sasa, BABA YAHUVEH, kwa uponyaji wa watu.

Ninaomba sasa kwa urejeshaji wa watu.

Ninaomba sasa, BABA wa MBINGUNI, kuwa utafanya yale ambayo wanasema haiwezi kufanywa; na kuwa utakomesha virusi hii sasa hivi kwa kuumiza watu wengine; na vitisho vitakoma; na hofu itaenda-kila mtu anayesikia sauti yangu sasa-watajua kuwa hakuna chochote kitakachowafanyikia ambacho BABA YAH hajaruhusu. Hamna!

Na ninawashukuru NYINYI na ninawasifu kwa kuwa kila mtu ambaye ni mtoto wa MUNGU ALIYE JUU, wa BABA YAHUVEH, YAHUSHUA & RUACH HA KODESH sasa.

Katika kusikia sauti yangu, wote wameponywa na kurejeshwa kabisa-na imani yao imekua.

Ninaomba kuwa watambue: hamna hofu tena! Hofu ni mateso! Hii ndiyo sababu wanataka kumiliki ulimwengu. Hii ndiyo habari kila mwanahabari kote duniani wanapeperusha.

Badala ya hayo, sikilizeni Maneno ya YAHUSHUA Aliyoyazungumza, kama alivyozungumza kwa imani. Kama vile Zaburi 91! Ninaomba kuwa wataisoma tena na tena na wataidai.

Ninaomba janga hili-vitishi hivi-itakoma!

Ninaombea KIFO cha virusi hii na wote WALIOIUMBA AU WALIOHUSIKA NAYO KATIKA NJIA YOYOTE au yeyote anayetaka kuwamaliza binadamu ulimwenguni! NI WAO WATAKAOMALIZWA! NI WAO WATAKAOENDA KATIKA SHIMO ZA JEHANAMU WAKIWA HAI!

Funua ardhi, kama vile ulivyofanya wakati Moshe alisema kuwa wale walio upande wa YAH, njooni hapa, na wale walio katika upande wa Kora, Nendeni kule!

Na wale waliokuwa upande wa Kora-ardhi ilifunguka na kuwameza wote wakiwa hai na wakaenda hadi jehanamu.

HAYA NDIYO NINAYOOMBA! ACHA WALIOKATALIWA WAKUFE! LAKINI WAMEZWE WAKIWA HAI!

Acha wachomeke na ghadhabu ZAKO za kuchomeka ghafla! Sijali wao ni matajiri kivipi! Wana nguvu kiasi gani! Sijali siasa zao!

Tunajua serikali zipo juu ya Mabega ya NANI-na YAHUSHUA MASIHI Alisema kuwa serikali ipo juu ya Mabega YAKE (Isaya 9:6). YEYE Ndiye KIONGOZI WA [KWELI] wa DUNIA HII!-shetani anacheza michezo na hufanya watu kufikiria kuwa YEYE Ndiye anamiliki dunia hii.

Na YAHUVEH anacheka. Anacheza na maadui WAKE.

Kwa hivyo BABA YAHUVEH, ninaulizia Upako wa Eliyahu na Ninauliza kama tu vile haukuacha ule mkebe wa mafuta ukauke kwa yule mjane wa Zarepta, ninaomba yayo hayo sasa kwa kila mtu katika kusikia sauti yangu anayelia na kusema “YAHUSHUA MASIHI, ninakupenda. Nisamehe. Nihurumie.”

Na umetuahidi kuwa utajibu maombi wanapoungama na kutubu, kuwa utaiponya ardhi yao. Na hizi siasa-BABA, ni mbovu-za dunia hii na ajenda mbovu ni ya kuwaumiza kondoo na wanakondoo wengi wasio na hatia.

Kama majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Maisha cha MWANAKONDOO, hauwezi kuwapoteza hata mmoja, YAHUSHUA MASIHI. Ninajua utakuwa na mashahidi, lakini damu itamwagika ardhini na itainua wengine [ambao watakuwa na imani ya] mashahidi na itainua ushuhuda zaidi za ukuu wa MASIHI MPENDWA wetu, YAHUSHUA MASIHI.

Kwa hivyo hili ndilo ombi langu katika Jina la YAHUSHUA MASIHI-kwa uponyaji, ukombozi, urejeshaji, msamaha, NGUVU ya kukomboa ya YAHUSHUA MASIHI na sanasana ukombozi kutoka kwa HOFU!

Hamna hofu tena!

Haijalishi utasikia mwanahabari akisema nini. Haijalishi utasikia mwanasiasa akisema nini. HAMNA HOFU TENA! Kwa kuwa hofu ni kujifungua kwa virusi hiyo.

Badala ya hayo, sema, “Kupitia Jina na Damu ya YAHUSHUA MASIHI, siipokei!”

Bado osheni mikono yenu. Fanyeni yote waliyosema mfanye kuhusu hayo, lakini MSIWE NA HOFU! Msifanye mifumo yenu ya kinga kudhoofika na hofu.

YAHUSHUA MASIHI Awabariki!

Mimi ni mtoto tu, shujaa, mtumishi wa YAHUSHUA MASIHI. Mimi ni mjumbe tu, kwa hivyo msinirushie mawe. Nipo hapa kujenga imani yenu mahali imeraruliwa na ninaomba siku hii, haya ndiyo niliyoyafanya.

YAHUSHUA, bariki wote walio baraka KWAKO.

Amina.

Mwisho wa Nakala

Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred