UNABII 15

NI DAKIKA MOJA HADI USIKU WA MANANE!YAHUSHUA YUAJA KATIKA USIKU WA MANANE!

Imepewa Kwake Mtume Elisheva Eliyahu Februari 2, 1998

Haya yanatoka kwenye Unabii 105, YAHUVEH Alisema iwekwe mbele ya Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], Kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo kama onyo kwa wale wanaokejeli:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii Wake, hata ilipozidi Ghadhabu ya Bwana juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

Hili ni ono la kule Mbinguni ambapoYAHUSHUA Anawaombea kondoo waliopotea. Gabrieli anapuliza tarumbeta na Mikaeli ana upanga wake tayari, kuongoza jeshi la malaika katika vita. YAHUVEH, Baba, hakuna yeyote aliye hai ambaye ameona Uso Wake. Zile misalaba nyuma ya Kiti cha Enzi, ambayo haiwezi kuhesabiwa, ni kila mtu aliyekubali zawadi ya YAHUSHUA pale Kalivari, kwa sababu YEYE Alichukua nafasi yetu pale msalabani kwa kila mmoja wetu.

Ukurasa wa Wokovu

Ukurasa wa Jehanamu

Ono hili lilipewa kwake Mtume Elisheva Eliyahu wakati wa maombi na dada mwingine. Picha hii ina upako spesheli. Ionyeshe kwa mpendwa au rafiki kama wataka kujua kama jina lao limeandikwa kwenye Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo, roho yao itavutwa Mbinguni kama hawana chochote kibaya cha kusema juu yake.

Maelezo ya picha “Dakika Moja Hadi Usiku wa Manane”

Unabii ulipewa kwake Mtume Elisheva Eliyahu. Pia ina mafunzo.

* * * * * * *

Hivi Ndivyo Asemavyo YAHUVEH, mpaka taifa hili linyenyekee mbele YANGU na Mbinguni yote na ulimwengu, taifa hili, Marekani iliyotengwa kuniletea MIMI Sifa, Heshima na Utukufu, haitawahi kushinda vita nyingine tena. Imekuwa tu kwa neema YANGU hadi sasa, taifa hili limebaki huru. Lakini sasa viongozi wenu wamesaka miungu wengine, wamejiita eti ni WANGU, lakini wanakejeli yote ambayo ni takatifu. Hata hawadanganyi vile Farao alivyofanya.

Kiongozi wenu, Rais wenu, anaringa na yale ambayo ni takatifu, hata usafi wa ndoa katika uso WANGU na kuongoza nchi hii katika vita ambayo sijaamuru, lakini ataruhusu hekima YANGU, na mawaidha, na mwongozo kutoulizwa na viongozi hawa. Wananikejeli MIMI na Korti Kuu. Taifa hili lasema ‘Mungu Abariki Marekani’. Nitafanya hivyo, lakini kama Marekani watakuwa tena baraka KWANGU.

Nyinyi ni mwiba kwenye upande WANGU Marekani. Nimekasirika vikuu, Nilvyoona yale ambayo yanafunzwa mashuleni kama watoto wenu wanakaa kwenye shimo za mpinga kristo kama evolution inafunzwa na sio uumbaji. Moja baada ya uongo nyingine ikifuta mazuri ambayo wazazi waliolea watoto wao katika njia sawa inachukuliwa kutoka kwao. Watoto wenu wamelala pale wakiwa uchi na wamenajisiwa. Lakini, mnafanya kidogo sana kuwalinda. Ndio, Ninazungumza na Watu WANGU, sio wapagani ambao hawajui lolote. Watoto wenu wanalishwa misamiati ambayo Jina LANGU limetolewa na kutumika tu kama neno la kulaani. Wanafunzwa maovu na uasi dhidi ya yote iliyo takatifu.

Je, kwa nini Watu WANGU wamesimama tu na kubaki kimya? Muziki ambao uliumbwa kwa urembo na kwa kuponya nafsi na kunisifu na kuniabudu MIMI sasa inatumika na jehanamu na shetani kuwapotosha Watoto WANGU mbali na utakatifu na sasa kuweka pepo za uovu ndani yao. Je, Mnasikiliza muziki ya watoto wenu? Je, Mnafikiria kuwa haina athari yoyote? Wamejawa na mapepo kupitia muziki hii. Hamjawalinda watoto wenu; ukatili na uasi inajazwa ndani ya watoto wenu kila siku.

Je, Mnatazama michezo yao? Hizo ni uvumbuzi kutoka jehanamu. Je, Mnaangalia vile vipindi vya televisheni ambavyo wanavitazama? Sinema za kutisha wanazozitazama zinafanya nyoyo zao kuwa ngumu kwa mauaji na ukatili. Mpaka wakati ule shetani atafanya waone mauaji ya kweli kwenye habari na wanasema inanihusu nini? Haijalishi! Uasi dhidi ya wazazi na kule Marekani amri za nchi hii inasema kuwa sio sawa kuwachapa watoto wenu.

Shetani anayapanga sasa kwa kuchukua ule unyanyasaji wa watoto ambayo ulio kwa uchache na kusema, “Jihadharini, itasababisha wanyanyasaji wa watoto kujitokeza mnapowachapa watoto.” Someni Neno LANGU ambalo haliwezi kudanganya. Watoto wenu hawako katika uasi kwa sababu ya kuadhibiwa, lakini kwa sababu ya kutoadhibiwa. Niliumba makalio sio tu ya kukaa, lakini ya kuchapwa. Serikali inatafuta kuwalea watoto wenu. Wanayafanya haya tayari na hata hamuelewi ni nini kinachoendelea. Hata katika mashule wanawafunza kutii sheria zao, sio sheria za YAHUVEH. Heshimu serikali na amri za nchi zinasikika kote Marekani au utaadhibiwa. Lakini na sauti ile ile, inazungumzwa, “Fanya uasi dhidi ya utakatifu.” Wasichana wadogo wana haki ya kuavya mimba bila wazazi wao kujua. Majimbo haya yamechukua haki zenu.

Watoto hawa wanapewa kondomu na kuambiwa waendelee, wafanye vitendo vya ngono bila matokeo. Hatutaambia wazazi wenu. Amri zinapitishwa kuhamasisha uasi dhidi ya kile Nilichofunza. Hata rais wenu anakejeli Amri zangu Kumi. Je, Watu wanajali? Wanajali tu, inawaathiri kivipi. Wachungaji wana hofu ya kuzungumza kwa sababu hawawezi kupoteza hali yao ya kutolipa ushuru. Nitawaonyesha nani wa kuogopa, kwa kuwa mtapoteza hiyo hali yenu ya kutolipa ushuru.

Nyinyi mnaodharau wale wachungaji Niliowaita, kama huyu ambaye Ninampa Unabii huu. Mnamkejeli, kwa kuwa anatumia pesa zake pamoja na wengine wanaopeana sadaka za upendo au fungu la kumi lakini hajawahi kuchukua mshahara. Lakini atakua na mshahara, na watumishi WANGU wengine ambao wanahamasisha huduma kutoka mifukoni mwao. Kamwe hawachukui, wanapeana tu, watakuwa na baraka, kwa Neno LANGU linasema: Mali ya waovu imewekwa kwa wale watakatifu. Nitaichukua mali yenu na kuipa kwa wale ambao wataitumia kwa Utukufu WANGU. Sio ya kwao.

Nitawabariki wote ambao wanajaribu kusimama katika Jina LANGU na kuwakemea mbwa mwitu katika ngozi ya kondoo. Ingawa mwili wao unatetemeka, RUACH HA KODESH Anafurahia kwa sababu wananitii MIMI na sio mwanadamu. Nyinyi wachungaji mnaoendesha magari ya bei ghali na pesa za kongamano ambayo ilifaa iwe fungu ZANGU Takatifu. Nyinyi wachungaji mnaoishi katika nyumba za kifahari, kama ya mfalme ambayo ilitoka kwa pesa ZANGU za fungu. Nyinyi wachungaji ambao serikali inawapapasa migongoni, mliouza ukweli kwa uongo. Je, Hamuoni mmehongwa kubaki kimya au mtapoteza hali yenu ya kutolipa ushuru?

Mtapoteza hali yenu ya kutolipa ushuru na kwa kweli hizi baraka zenu za pesa zitakuja kuisha pia. Mmeonywa! Wale ambao wanawakejeli watawaona mkidhalalishwa mbele ya dunia kama hamtatubu leo. Nirudishieni MIMI fungu ZANGU na sadaka zilizoibiwa, zilizowekwa kwa siku ijayo. Mtakapoyasikia haya, mtajua thibitisho LANGU na mtajua neno hili ni la nani. Mnasimama mbele YANGU na mikono ya saa ipo pale kwenye dakika moja hadi usiku wa manane. Nimeudhika kama utakatifu unavyokejeliwa katika vipindi vya televisheni. Watoto wenu wanafunzwa kuwa ushoga ndiyo maisha nyingine mbadala. Clinton atafanya haya yawe halali kwa mashoga ndio wasidhalalishwe na mchungaji wala mwalimu.

Jitayarisheni! Vita vya amri zilizoko na mapepo vinakuja. Lakini wale ambao ni WANGU, mtajua ni nini ya kusema na mtayafanya yaya haya wakati huu. Rais na viongozi wa nchi hii wapo karibu kuhisi ghadhabu YANGU kwa kupotosha taifa hili. Msidanganyike, MIMI ni Mungu mwenye wivu! Kulipiza kisasi ni ya KWANGU Ndivyo Asemavyo YAHUVEH! TUBUNI, ni dakika moja hadi usiku wa manane. Kama tu siku za kale, Kutoka 11:4, itakuwa vivyo hivyo tena. Kwa sababu Nilimtuma Mwana WANGU kuwaokoa kama Nilivyomtuma Moshe kumuonya Farao, kwa hivyo Ninamtuma Nabii huyu kuwaonya, kuwatia moyo Bibi Arusi. Ni dakika moja hadi usiku wa manane. Je, Mtafanya nini? Nimezungumza haya kupitia huyu handmaiden, Nabii Elisheva Eliyahu, kuwaonya.

Ninazungumza onyo hii kwa wale wanaodai kuwa wao ni viongozi wa nchi hii. ACHENI WATU WANGU HURU kuishi katika utakatifu mbele YANGU. Waache waniabudu MIMI na yote Ninayosimamia. Acheni kuwatesa. Laana za Kumbukumbu la Torati 28 zimewekwa kwa wale wasiotii. Kutoka 11:4 itakuwa hukumu yenu tena. Rudini kwa Mungu wa Baba zenu tena. Rudini enyi viongozi wa taifa hili na muwe viongozi waliojazwa na RUACH HA KODESH (Roho Mtakatifu). Kemeeni dhambi na kuadhibu maovu au hatima ya Farao itakuwa yenu. ACHENI WATU WANGU HURU, Ndivyo Asemavyo YAHUVEH!

Nitathibitisha tena kuwa MIMI sio Mungu wa kukejeliwa wala kudharauliwa. Marekani kueni tayari! Dunia kueni tayari! Maadui wa Injili ya YAHUSHUA MASIHI kueni tayari! Wale ambao sio WANGU wataona tena utengo kati ya wale wanaoniabudu MIMI, wale wanaonichukia MIMI na kila kilicho takatifu. Mtaona vile Nitakavyowapunish wapagani na muone na macho yenu vile Nitakavyolinda watakatifu na kuwamaliza waovu na wote wanaosupport dhambi. Mali yenu yote haitaweza kukomesha kile Mungu Mwenyezi YAHUVEH Atakachofanya.

Kumbukeni pigo la panya lililoangukia Ikulu? Kwa sababu Niliwatuma Manabii WANGU na hamkusikiliza. Nilituma Unabii ZANGU na mkazichoma. MKIKEJELI! Itakuwa zaidi ya iliyokuwa hapo awali. Tubuni kabla wakati haujaisha. Ni dakika moja hadi usiku wa manane. Bado kuna wakati kabla sijawachukua Watoto wangu nyumbani NAMI na taifa hili litasaga meno yao kwa uchungu kwa kuwa walithubutu kumkejeli Mungu Mkuu YAHUVEH na YAHUSHUA! Usiku wa manane ghadhabu ZANGU zitaanguka. Hamjui ni usiku mgani Ninamtuma YAHUSHUA, Mwana WANGU Mpendwa. Jitayarisheni Bibi Arusi: baraka zenu bado zinakuja.

* * * * * * *

Imepewa kwake mtoto, shujaa, Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI.

Mtume Elisheva Eliyahu

2/2/98 6:20 Asubuhi

Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred