Unabii 148
DAMU ya YAHUSHUA MASIHI ni Yenu! Dakika Moja hadi Usiku wa Manane
Imezungumzwa katika Upako wa RUACH HA KODESH
Kupitia Mtume, Nabii Elisheva Eliyahu
Ilipokewa Oktoba 19 – Ikatolewa Novemba 27, 2019
* * * * * * *
Yafuatayo ni Unabii ulivyokuja
—na Nabii Elisheva, akizungumza katika “Ndimi Takatifu,” kama ROHO wa MUNGU Alivyomjalia kutamka (Matendo ya Mitume 2:3-4) kwa lugha za wanadamu na malaika (1 Wakorintho 13:1). Elisheva anazungumza katika ndimi Unabii ukitokea (1 Wakorintho 14:6).
Tunatumia MAJINA ya KIEBRANIA ya MUNGU:
YAH/YAHU יה ni JINA TAKATIFU la MUNGU, kama vile “Alleluia” au “Hallelu YAH” הללו–יה ambayo humaanisha “Msifu YAH”: YAHUVEH/YAHWEH י-ה-ו-ה MUNGU BABA; YAHUSHUA/YAHSHUA יהושוע MWANA WA PEKEE WA MUNGU—(HA MASHIACH המשיח inamaanisha “MASIHI”; ELOHIM אלוהים INAMAANISHA “MUNGU.”) Ufunuo wa “SH’KHINYAH GLORY” שכניה תפארה —kama JINA la KIBINAFSI la RUACH HA KODESH רוח הקדש, (katika Kiiengereza “ROHO MTAKATIFU”) —upo kwenye tovuti hii. (HA SH’KHINAH {SHEKINAH} ni Kiebrania inamaanisha UWEPO WA MUNGU.)
Zaidi ya hayo, ABBA YAH אבא יה humaanisha “BABA YAH” na IMMA YAH אמא יה humaanisha “MAMA YAH.” Katika Kiebrania, ROHO wa MUNGU ni kike, anajulikana kama “SHE,” na anaonyeshwa vivi hivi kwenye Unabii na Maandiko yanayofuata. Kila ambapo jina la MUNGU limetajwa lipo katika herufi kubwa.
Maandiko yaliyotajwa yametoka KJV au NKJV au CJB.
* * * * * * *
Maneno ya YAHUVEH yaliyoongezwa mbele ya Unabii zote:
Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo.
Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli.
‘‘Mimi Ndiye BWANA YAHUVEH: hilo ndilo JINA LANGU! Sitampa mwingine UTUKUFU WANGU, wala sanamu SIFA ZANGU.” Isaya 42:8
(Unabii 105)
Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kuwaonya wanaokejeli:
“Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”
—2 Mambo ya Nyakati 36:16
Unabii 148
Haya yalirekodiwa kwenye kinaza sauti. Haya ndio maneno yaliyomo.
Elisheva: Picha hii unayoiona ndio ya pekee, uchoraji wa mafuta wa kipekee ambayo nimeiona kwenye maono.
Unabii Unaanza:
Machozi ya DAMU ya YAHUSHUA, Analia-Anawalilia Israeli; Analilia wale wanaosema ni WAKE, na bado YEYE atawaambia, ‘Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu’ (Mathayo 7:23). Analia kwa yale ambayo lazima yafanywe katika Dhiki Kuu! Analia Machozi ya DAMU. Na mnaona Malaika watakatifu, Mkuu wa malaika Mikaeli-anakuja pale na upanga wake kupigana.
Elisheva: Je, waona hiyo picha nyuma ya hiyo? Kila kitu pale niliona kwenye maono, na hata ile saa pale. O! Ni sekunde tu kabla ya usiku wa manane. YAHUSHUA yuaja usiku wa manane. Na msiache YEYOTE awaambie kuwa itakuwa siku fulani.
Kwa kuwa YAHUVEH mwenyewe-BABA hajamuambia YEYE bado ni lini atakapoenda kuwachukua Bibi Arusi. Tunajua msimu tu (Marko 13:28-29; 1 Wathesalonike 5:2-4; Ufunuo wa Yohana 3:3) kwa sababu hayo [pia] yalikuwa kwenye Unabii [76].
Unabii Unaendelea:
Na hata Waebrania wanajua- na wanasherehekea Rosh HaShanah. Na Rosh HaShanah ndio siku ya Uumbaji. Pateni kujua juu ya Sherehe Takatifu. Lakini jihadharini! Kaeni mbali na chochote kando ya Maandiko ya Bibilia, kaeni mbali! Ila tu kama mnajua hizo “Vitabu Vilivyopotea” vimethibitishwa na Maandiko.
Elisheva: Na mnaweza kuamini zile zilizomo Amightywind.com. Kwa kuwa nimezisoma na mnaweza kuziamini Enoch 1 na Enoch 2, lakini [inayoitwa] “Enoch 3” imetoka kwa shetani.
Msiamini chochote kilicho kwenye kitabu kiitwaacho “Enoch 3”! Msiruhusu yeyote kukufunza hayo! Na USIWAHI kufikiria kuwa wewe ni mungu! Sisi-ambao tumeokolewa kwa JINA & DAMU YA YAHUSHUA- Bibilia inasema kuwa tumeokolewa kwa sehemu tu (1 Petro 4:18). Na ni nani aliye na nafasi, ambaye hana DAMU YA YAHUSHUA? Inayowaosha wawe wasafi! Na DHABIHU YAKE YA DAMU TAKATIFU na KAMILI ambayo BABA YAHUVEH [ameita] DHABIHU KAMILI YA MWANAKONDOO!
Unabii Unaendelea:
Kwa bila kumwagwa kwa damu, hakuna ondoleo la dhambi (Waebrania 9:22; Mambo ya Walawi 17:11).
O Israeli, dhabihu ya damu yenu iko wapi? Haya yaliyomo kwenye Unabii [63]. O Israeli! Yule atakayekuja, na kuketi kwenye Hekalu hiyo ya Tatu, atakuwa mwana wa shetani. Chukueni onyo. Chukueni onyo sasa watu!
Msikubali alama ya mnyama!
YAHUSHUA analia! Analilia waoga wote ambao watafanya vivyo hivyo [kukubali alama ya mnyama], lakini majina yenu hayakuwa yameandikwa kwenye Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo. Kwa kuwa YAHUSHUA anasema hawezi kupoteza hata mmoja. Atawaacha 99 watakatifu-wanaofuata amri ZAKE, na kumuabudu YEYE- kuenda na kutafuta yule mwanakondoo mweusi aliyepotea na aliyetoweka (Luka 15:3-7). Mnaendelea kuzurura tu kwenye malisho ya shetani. Mnashinda mkienda kwenye pango la mbwa mwitu.
Elisheva: Na sasa mnathubutu kujiita mungu? Hii ni kabala, sasa, ninayoizungumzia.
Jihadharini! Jihadhari na mafunzo ya giza! Jihadhari na yeyote anayekuambia kuwa kuna mungu mwingine kando ya utatu mtakatifu ambao nimewataja. Haya yamo kwenye Maandiko Matakatifu. Haya yamo kwenye Tanakh. Haya yamo kwenye Torati. Na pia, yamo kwenye Agano Jipya. Yamo kote kwenye Maandiko Matakatifu. O watu! Ninajua mamilioni wamekuja kwake YAHUSHUA, (kwa sababu Aliniambia, kuzalisha Huduma hii kwenye intaneti, miaka 25 iliyopita) […] Ani ohevet-!Ani ohevet-! Kwa wote waliopokea Huduma hii na mimi na wote wanaonisaidia mimi kwenye shamba hili la mavuno, kuleta nafsi kwa YAHUSHUA, ili-tukutane-kule Mbinguni!
Zaidi ya hayo. Ni kwa wokovu wa nafsi yako, lakini kumbuka, kwa wale watakaofika Mbinguni, tajeni jina langu, na nitakuja nikikimbia. Nitakupa kumbatio kubwa na tutasherehekea. Tutasherehekea kwa kazi ya ulimwengu ilimalizwa na tutasherehekea milele! Kwa GHARAMA YAHUSHUA MASIHI alitoa na MAISHA AYAKE MWENYEWE!
Aliteswa kwa niaba yetu. Alisulubiwa kwa niaba yetu. Na YAHUSHUA alinipa ufunuo. Ipo kwenye Unabii ujao. Na kwa yale masaa matatu aliteseka sana (na akakejeliwa na kutemewa mate, na akapewa siki kwenye mdomo WAKE alipokuwa na kiu), YEYE aliona kila jina kwa ghafla ambayo siwezi kuieleza-kwa kuwa ni MUNGU tu MWENYEWE anaweza kuyafanya hayo-lakini kila jina katika Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo.
Unabii Unaendelea:
DAMU hii ni yenu! DAMU hii ni yenu! DAMU hii ni yenu! Na kwa wote wanaoikataa, amewaona katika Kitabu cha Waliokataliwa na Kitabu cha Waliofutwa, akijua hata DHABIHU aliyotoa haitapokewa. Badala ya haya, JINA LAKE litakataliwa [kulaaniwa] au watajiita wao “mungu” au watamkataa YAHUSHUA na kumtumia tu-kama neno la matusi.
Picha hiyo pale, “Dakika Moja hadi Usiku wa Manane”-YAHUSHUA analia Machozi ya DAMU kama alivyofanya pale kwenye Bustani la Gethsemane (Luka 22:44). Je, Mnakumbuka haya? Hayo ndiyo picha hii inaonyesha.
Elisheva: Mnapoona mfano wake- [kwenye] ukuta wa aibu wa maadui wangu- na muione kwenye tovuti zao au kwenye chaneli yao ya Youtube: hawana ruhusa yangu ya kutumia picha ya IMMAYAH; hawana ruhusa ya kutumia uchoraji wa “Dakika moja hadi Usiku wa Manane”.
Haya yanaonyesha kuwa shetani huja kuiba, kuua na kuharibu (Yohana 10:10). Na mnapoona picha hiyo, kama wao sio sehemu ya Huduma ya Amightywind, na wao ni maadui wangu na maadui wa yote Takatifu-na ni Watakatifu tu ndio sehemu ya Huduma ya Amightywind-mtajua kuwa wao ni waongo; wao ni waongo.
Wanajaribu kujitokeza kama Watakatifu, na wao SIO. Mwaweza tayari kuenda kwenye ukuta wa aibu wa waliokataliwa. [Oneni pale Amightywind.com.] Na jueni haya. Wanafanya tu yale ambayo Nilisema watafanya, kuwachanganya kondoo na wanakondoo: “O niliona picha hiyo hapo awali-o, hawa watu, lazima ni Wakristo…” Hapo awali walikuwa “watoto katika wokovu,” lakini haikutosha. Walipeana maisha yao kwa shetani na wakapeana nafsi zao kwake shetani, na ithibati ipo kwenye “Ukuta wa Aibu ya Waliokataliwa.” Na tena…
Unabii Unaendelea:
YAHUSHUA MWENYEWE alisema watu wanataka tu kufunza juu ya upendo WAKE, huruma YAKE, msamaha WAKE, nguvu ZAKE za uponyaji, nguvu za ufufuo, nguvu za msamaha, lakini kila mtu anataka kusahau, YEYE aliwaonya zaidi juu ya jehanamu kushinda vile alivyozungumza juu ya Mbinguni, na ni wangapi wanataka kukumbuka, “Jihadharini na ghadhabu za MWANAKONDOO!” [Unabii 129]? YEYE hukanyagia zabibu, chini ya miguu YAKE (Ufunuo wa Yohana 19:15).
Elisheva: Na ni hivi tu juzi katika Unabii (ambao haujatolewa). Aliniambia mimi…
Unabii Unaendelea:
Hawa ndio matunda yaliyooza, zabibu zilizooza. Wale ambao walionja uzuri (Waebrania 6:5), na sasa wanajiita ‘mungu’-haya ni kama kumsulubisha YAHUSHUA tena (Waebrania 6:6).
Hauwezi kuleta aliyekataliwa katika toba (Waebrania 6:4-6). Na maneno yao, na mdomo wao, wanaweza kuzungumza yale ambayo ni Maandiko (Mathayo 15:8), lakini nyoyo zao sio za YAHUSHUA.
Elisheva: Ni lazima niyaseme haya yote, kwa sababu… Mnapoangalia picha hiyo, mnaona hao malaika wadogo pale? Kuna malaika wadogo pale pia-kuna malaika wa kila aina Mbinguni, lakini Mkuu wa malaika Mikaeli ndiye mkuu anayelinda Israeli, na mkuu ambaye nimemuona, hata nimegusa bawa lake (ambayo ni ushuda mwingine), pale 2005, ya Mkuu wa malaika Mikaeli.
Unabii Unaendelea:
Yeye hulinda huduma hii. Anapigana na maadui wa Huduma hii. Na YAHUSHUA NDIYE ANAYEMTUMA. Ndio sababu Israeli daima itakuwa pale. Na hata Yerusalemu mpya itakayotoka Mbinguni (Ufunuo wa Yohana 21:2) itakuwa pale Israeli.
O Israeli, kuna onyo. Dhiki kuu yaja. Ni nyinyi mtakaojenga hiyo Hekalu ya tatu na nyinyi mtakaoruhusu mwana wa shetani kuketi kwa kile kiti, mpaka atakapofanya machukizo ambayo hata-mtaficha nyuso zenu kwa aibu.
Elisheva: najua machukizo hayo ni yapi. Tena, ipo kwenye Unabii ambao bado haujatolewa kwa sababu nina Unabii nyingi-lakini sifa kwa YAHUSHUA, itatolewa kwa wakati WAKE.
Unabii Unaendelea:
Kwa hivyo tena, mnapoona picha hii [ya uchoraji], kama haujui kama wao ni sehemu ya Huduma ya Amightywind, basi jueni haya, wao ni wa shetani, wanataka kuwadanganya. Na pia kwa ile picha ya IMMAYAH. […]
Elisheva: Picha hii ni uchoraji wa mafuta. Huwa nami daima. Kwa miaka mingi sana! Ni ufunuo ambao nilikuwa nao [wakati] nilikuwa kwenye simu, nikiomba kwa simu. Ilikuwa ufunuo wazi. YAHUSHUA MASIHI awabariki wote wanaomuabudu YAHUSHUA MASIHI kwa ROHO na kwa ukweli; na wanaojaribu kumtii YEYE, na watakaotubu kwa dhambi zao-sio tu kwa maneno, lakini kwa matendo. Shalom.
Sukkot Njema! Na hongera kwa siku YAKO ya kuzaliwa MPENDWA YAHUSHUA!-ulipozaliwa hapa duniani wakati wa Sukkot na hii inaitwa pia Sherehe ya Vibanda. Na nitaka niwaelezee- walipoweka hema ya muda mfupi-pale kwenye Agano la Kale, Agano la Kale la Damu, kama nilivyosema, ilikuwa tu kivuli cha yale yatakayofanyika, YAHUSHUA aliposema, “Yote yamekwisha” (Yohana 19:30).
Miili hii yetu ndio hema ya muda mfupi kwa sasa (2 Wakorintho 5:1) na inangoja kuvaa ile miili ya kiroho ya utukufu (2 Wakorintho 5:2-5).
Unabii Unaendelea:
Je, Mnaelewa? Mnaposoma Agano la Kale la Damu, kumbuka YAHUSHUA alisema hakuja kufuta Sheria na Manabii, alikuja kuyatimiza (Mathayo 5:17). Alikuja kusema, Nimewapa-Ninawapa njia bora. Na akasema, “Yote yamekwisha” (Yohana 19:30). Na aliposema “Yote yamekwisha,” ilikwisha. Hakuna dhabihu zingine tena (Waebrania 10:1-10). Hakuna sadaka za kuteketezwa ambazo zitamfurahisha YAHUVEH (Waebrania 10:1-10). Kwa kuwa Moshe aliwaonya juu ya haya (Kumbukumbu la Torati 18:15-19)-Musa aliwaonya. Hilo ndilo jina la Moshe [Musa kwa Kiebrania]. Aliwaonya. YAHUVEH alisema hamna sadaka za kuteketezwa ambazo zitakuwa kifuniko cha dhambi (1 Samueli 15:22; Zaburi 40:6; Mithali 15:8 & 21:3; Isaya 1:10-12; Yeremia 6:20; Hosea 6:6). Na Moshe akawaonya, kulikuwa na AGANO JIPYA la DAMU linalokuja (Kumbukumbu la Torati 30:1-2, 6)! Kuosha dhambi! Na ni YAHUSHUA MKUU WA WAKUU-KUHANI-KATIKA MFANO WA MELKIZEDEKI (Waebrania 5:6; 10; 6:20: 7:11, 15-17) kwa sababu YEYE ni na YEYE alikuwa ‘Melkizedeki’ (Waebrania 7:3) [katika Kiebrania, MALKI ZEDEK, MFALME WANGU WA UTAKATIFU (Mwanzo 14:18)]. Na usiruhusu yeyote kukuambia tofauti. Tafadhali watu. Jifunzeni na kujionyesha kama wale walio kamili (2 Timotheo 2:15). Kueni wanyenyekevu na mtembee katika unyenyekevu, na kuomba msidanganywe.
Elisheva: Kwa wale ambao hapo awali tulidhania tunaweza kuwaamini, hatuwezi tena. Wamepotea njia. Wanaita… pepo, “mungu wa kike”-“Urea.”
Unabii Unaendelea:
Si ni ya ajabu haya? Je, Mnajua ni nini kitakachofanyika? Wakiendelea kuamini uongo huo?! Kukejeli RUACH HA KODESH/ROHO MTAKATIFU? NA jina “Urine”? Na wanasema kuwa huyu ni “binti” YAKE kule Mbinguni? “dadake” YAHUSHUA? Hawa ndio walio kwenye “Ukuta wa Aibu wa Waliokataliwa” na kila jina lipo pale, [lakini] wengine wataongezwa. Hawa ndio BABA YAHUVEH atawamaliza kwa kuwachoma ghafla, isipokuwa mmoja tu-na jina la mwanamume huyo ni Erez [Ezra Caleb], ingawa BABA YAH hamuiti na majina hayo tena-Erez tu. Yupo tu kidole kimoja karibu kuingia jehanamu. Kidole kimoja.
Elisheva: Na bado nimeuliza kila mtu aendelee kuomba atoke kwa haya, atoke kwa makubaliano haya na atambue, kuwa yule anayefikria ni mwanamke-amejificha kama mwanamke-anashirikiana na pepo- mungu wa kike aitwaye “Urea.” Nilichokuwa nakejeli, sikejeli tena. Kwa kuwa ni pepo-mungu wa kike. Na huyo mwanamume anasikiliza-sasa anajua-hawezi kubaki kimya. Nafsi yangu bado inampenda, kwa sababu YAHUSHUA anampenda. Sio upendo wangu [unao] unaendelea kumpigania. Ni BABA YAHUVEH, YAHUSHUA & RUACH HA KODESH!
Unabii Unaendelea:
Na YAHUSHUA analia Machozi ya DAMU kwa mwanamume huyu ambaye hapo awali alikuwa baraka kwa Huduma ya Amightywind, 2016, 2017 na sehemu kidogo ya 2018. Analia Machozi ya DAMU na kusema, “DAMU hii ni yako!” Rudi! Tambua kuwa umedanganywa! Upo karibu kuwa wazimu! Toka kwenye hiyo mafunzo ya giza! Toka kwa uchawi huo! Toka, nyinyi mlio ndani ya giza-mkiamini kuwa jicho lako la tatu lazima lifunguliwe-uliza YAHUSHUA aifunge na DAMU YAKE ILIYOMWAGWA! Tubu. YAHUSHUA analia Machozi ya DAMU kwenu. Kama wewe sio nyoka mkataliwa, bado kuna matumaini kwako. […]
Elisheva: Kumbuka unaposoma Agano la Kale, ni historia-ni kivuli cha kila kitu YAHUSHUA alitufanyia kama ONDOLEO KAMILI YA DAMU kwa dhambi. Kwa kuwa hakuna yeyote [ambaye] alitembea dunia hii katika umbo kamili ya mwanadamu isipokuwa MMOJA tu na ilikuwa YAHUSHUA MASIHI. Kila mtu anahitaji kutubu. Kwa kuwa hakuna yeyote ambaye ni kamili.
Unabii Unaendelea:
Kwa wale ambao ni wa YAHUSHUA MASIHI, hatafanya dhambi kimaksudi. Wanaogopa RUACH HA KODESH, AMBAYE wengine wanamuita ROHO MTAKATIFU, kwa sababu hautaki kumtukana ROHO MTAKATIFU (Mathayo 12:31), (RUACH HA KODESH SHEKHINYAH GLORY). Akitoka nafsini mwako, umekataliwa!!! Je, mnanisikia? Mtakuwa [wale] waliokataliwa! Na tayari tuna UKUTA WA AIBU kwa waliokataliwa ambapo hapo awali walikuwa na watoto katika wokovu. Lakini hii ni sherehe, na yale ninayo ya kusema ni ole kwa wale ambao wataanguka chini ya YULE ANAYEKETI KWENYE KITI CHA ENZI na ghadhabu ya MWANAKONDOO, ambayo ni onyo kwa Ufunuo wa Yohana 6.
Elisheva: Tafadhali watu! Tubuni! Mimi ni Myahudi, lakini sikuzaliwa Israeli, kwa hivyo mimi ni “wa kabila ya Efraimu.” Na ninamgonja “Yuda wangu” kuja kuungana na Efraimu tena. Sijui yuko wapi lakini najua haya-YAHUSHUA hakuanza kazi nzuri na kukosa kuimaliza. Tumetumwa kwa Israeli.
Unabii Unaendelea:
Vitabu vya RUACH HA KODESH, Siri za RUACH HA KODESH, vilichukua miaka 7 kuiweka pamoja Ushahidi wote wa Hawa aliumbwa katika mfano wa nani na Wayahudi tayari wana ujuzi huo. Tayari wanajua kuwa RUACH HA KODESH-hata JINA-ni ya jinsia [ya] kike. Tayari wanajua.
Elisheva: Lakini ilichukua mtu kama mimi, kwa Unabii 89 & 90 kufanya iwezekanavyo, ambaye hakujua Hawa aliumbwa katika mfano wa nani mpaka Unabii huo. O kongamano langu la Amightywind nianaowapenda na wageni waliokuja na kutazama na kusherehekea vile tunavyomheshimu MASIHI, MMOJA NA WA KIPEKEE.
Unabii Unaendelea:
Na ole kwa Israeli msipokubali YULE ambaye DAMU YAKE bado imeloweka kwenye mchanga wenu ambayo sasa imeenda kote duniani na kwa kila mtu anayetambua na kusema: Tafadhali nisamehe YAHUSHUA kwa dhambi zangu! Nioshe niwe msafi na DAMU YAKO! Ninatubu kwa maovu niliyoyafanya, na Ninaungama dhambi zangu KWAKO. ASANTE kwa kunisamehe! ASANTE-kwa kuchukua dhambi hizo na kuziweka mbali nami kama mashariki ilivyo mbali na magharibi (Zaburi 103:12). ASANTE kwa kumueka RUACH HA KODESH WAKO ndani ya nafsi yangu! ASANTE! Kama ombi ambalo Daudi alisema, RUACH HA KODESH ‘tafadhali usiwahi kuacha nafsi yangu’ (Zaburi 51:11). Hili ndilo ombi lake. Hili lafaa kuwa ombi la kila mtu. Kuwa Upako wa RUACH HA KODESH, ROHO MTAKATIFU aendelee kuzidi ndani yenu na kila siku.
Mwisho wa Unabii
Elisheva: Watu! tafadhali tambueni-Israeli amkeni! DAMU YA MASIHI bado ipo mchangani mwenu. YEYE Alizaliwa Myahudi kutoka kwa Mwanamke Myahudi bikira. Miujiza [ambayo] aliyafanya na yaliyorekodiwa yalitendeka Israeli.
O Israeli, tunawapenda! O Israeli, rudini! Rudini! YAHUVEH amewaahidi kuwaoa tena! Rudini katika JINA LA YAHUSHUA MASIHI! Shema bado [ni juu ya] MUNGU MMOJA WA KIPEKEE lakini ni WATATU [NDANI YA MOJA]: YAHUVEH, YAHUSHUA MASIHI (MWANA WA KIPEKEE WA YAHUVEH) & RUACH HA KODESH, ROHO MTAKATIFU MPENDWA. Mnapoona sherehe, haijalishi kama mmejua haya hapo awali au la. Ninazungumza na Waebrania wote kote duniani. Bado hamjachelewa. Njooni kwenye Mikono ya YAHUSHUA.
Na tarajieni video zingine zinazokuja kwa sababu hivi karibuni tutakuwa na Hanukkah!-ambayo tunaiita Sherehe ya Nuru kwa sababu YAHUSHUA Ndiye NURU WA MILELE. Wakati huo ndipo YAHUSHUA alipowekwa tumboni mwa mamake! Tunasherehekea Hanukkah-ndio najua Agano la Kale la Damu, inasema ilikuwa-kwa kuweka wakfu kwa Hekalu. Hekalu ilikuwa imechafuliwa. Miili isiyo na uhai ilikuwa pale kote (Maccabbees 1&2). Na hakukuwa na mafuta ya kutosha kuwasha mishumaa-menorah. Muujiza uliofanyika, na tena, ilifanyika kule Israeli, lakini ilikuwa historia. Ilikuwa kivuli cha kukuja kwa YAHUSHUA MASIHI! NURU WA MILELE ambayo haitawahi kuzimwa!
Na unapokuwa na RUACH HA KODESH ndani yako, una upako ndani yako (1 Yohana 2:20), NURU WA MILELE ambayo haitawahi kuzimwa-ilhali tu uthibitishe kuwa umemkubali YAHUSHUA MASIHI kama MASIHI, MWOKOZI, au na jina [au cheo] nyingine unavyotaka kumuita. YEYE alitupenda sana. Alisema kuwa hata kama kungekuwa tu na mmoja [YEYE angetoa MAISHA YAKE]-kila mtu ambaye jina lake limeandikwa katika KITABU CHA UZIMA cha MWANAKONDOO, wangekuja tu katika JINA LA YAHUSHUA MASIHI pia anavyojulikana kama YESU KRISTO. Anafaa kuwa KIPENZI CHA NAFSI YAKO. Kwa kuwa YEYE ni KIPENZI CHA NAFSI YAKO.
Mnafaa kusherehekea [sherehe za Bibilia] na ole kwenu, enyi Makanisa maarufu ya Kikristo. Kwa kuwa kwanza niliokolewa katika Kanisa la Pentekoste. Hata hamfunzi Sherehe za Kiyahudi. Hata hamuambii watu ukweli wa siku ya kuzaliwa [ya YAHUSHUA]. Na sio Disemba 25… Kataeni uongo wa shetani, nyinyi makanisa maarufua. Jipangeni na Maandiko Matakatifu. YEYE ni “MFALME WA ISRAELI.” Na hawakuweza kukubali haya-hayo Maneno yalikuwa pale juu msalabani ambapo YEYE aliposulubiwa. Lakini hallelu YAH! Katika siku ya tatu ([kutoka kwa kifo chake] baada ya YEYE kusema, “Yote yamekwisha”), YEYE alifufuka tena. Alifufuliwa, na kutoka kwa kaburi hiyo. Na tunayajua haya-kwa wale ambao wamefariki na wale ambao ni wa YAHUSHUA, “kukosekana kwa mwili” ni “kuwa pamoja na BWANA,” YAHUSHUA MASIHI (2 Wakorintho 5:8).
Simameni katika Maandiko ya Agano JIPYA LA DAMU, inayoitwa AGANO JIPYA. Someni Agano la Kale la Damu, Agano la Kale, lakini mtamuona kuwa YAHUSHUA yupo pale-KILA MAHALI-kutoka mwanzo hadi Ufunuo wa Yohana. Na msiyaamini mafunzo mengine. Kwa sababu Yanaweza kuwa mafunzo ya shetani-na kuna mengi kule nje sasa hivi. Msiamini kuwa kuna zaidi ya wale WATAKATIFU WATATU, WAUMBAJI: BABA WA MBINGUNI, MWANAWE YAHUSHUA MASIHI [&] ROHO MTAKATIFU / RUACH HA KODESH. Tafadhali, mnataka kuenda Mbinguni. Je, mnapenda YAHUSHUA?
Maandiko yanasema kuwa YAHUSHUA alisema, ‘Je, Mbona mnaniita mimi BWANA na hamnitii MIMI:’ (Luka 6:46). Toleo lingine lasema, ‘Je, Mnawezaje kusema kuwa mnanipenda MIMI na hamnitii MIMI?’ (Yohana 14:15; 1 Yohana 2:5).
Kama YEYE kwa kweli ni MUNGU WA MAISHA YAKO, mta-na akili, mwili, roho na nafsi yenu yote-mnataka kuwa na ushuda kama wa Enoki na kupatikana kumfurahisha YAHUVEH (Waebrania 11:5). Kwa kuwa hakukufa. Mwili wake ulibadilishwa kuwa mwili wa utukufu (Mwanzo 5:24; Filemoni 3:21).
Kwa kuwa mwili na damu haiwezi kuingia katika Ufalme wa Mbinguni (1 Wakorintho 15:50). Haikuumbwa kwa mwili na damu. Iliumbwa kwa miili yetu ya kiroho ambayo ni ya kupendeza. Watu, hakuna njia yoyote ingine Mbinguni, isipokuwa kupitia JINA & DAMU YA YAHUSHUA. Ndiposa twasema, “Sukkot Njema! Hongear kwa Siku yako ya kuzaliwa!” MPENDWA wetu, ani ohevet-TUNAKUABUDU! TUNAKUABUDU! Tunakuabudu WEWE YAHUSHUA MASIHI! Sisi sote twasherehekea! Sisi sote twasherehekea, na kwa kongamano la Amightywind na wale wageni, rudini na mjionee wenyewe na muonje na kuona matunda ya Huduma hii ni mazuri (Mathayo 7:16). Kwa kuwa hamtawahi kusikia mambo ambayo haiambatani na Maandiko Matakatifu! Shalom.
Mwisho wa Mahubiri Matakatifu
Imezungumzwa, Imeandikwa
Siku hii katika JINA LA YAHUSHUA MASIHI
Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!