UNABII 14
TUBUNI MAREKANI, DAMU IPO MIKONONI MWENU!
Unabii umepewa kwake Elisheva Eliyahu Aprili 10, 1993
Haya yanatoka kwenye Unabii 105, YAHUVEH Alisema iwekwe mbele ya Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], Kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)
Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo kama onyo kwa wale wanaokejeli:
2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii Wake, hata ilipozidi Ghadhabu ya Bwana juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”
* * * * * * *
Walipa ushuru jihadharini, damu ya watoto walio tumboni mwa mama zao zitakuwa mikononi mwa kila Mkristo na wale ambao sio Wakristo, kama Clinton atafaulu kupitisha kuavya mimba za kulipwa. Wale walio na masikio ya kusikiliza-sikizeni, wengine bakini Viziwi. Nyinyi ambao hamuezi kabisa kuwaua watoto wenu mtakuwa mnatenda haya mauaji ya kuavya mimba, kwa kuruhusu serikali kutumia dola zenu za ushuru kulipia uhalifu huu wa kutisha dhidi ya YAHUVEH na Binadamu. Hamtakuwa mnalipia tu kuavya mimba moja, kuua moja, lakini mamilioni ya watoto watauawa, na kupitia pesa Nilizowapa nyinyi kufanikiwa.
Damu hii isiyo na hatia itakuwa mikononi mwenu nyote. Ghadhabu yangu itaangukia taifa hili na dunia hii isiyo na kifani na nyinyi watu WANGU mtakuwa mmenikasirisha MIMI kwa kukaa kimya. Jihadharini kwa kuwa MIMI sio tu Mungu wa upendo, lakini MIMI ni Mungu wa Ghadhabu kuu Ninapokasirishwa. Anzeni kuandamana sasa. Acheni sauti zenu zisikike. Simamieni yale ambayo mnajua ni sawa, sasa hivi kabla wakati hamna. Clinton anahamasisha ushoga kwenye jeshi. Anawataka nyinyi kuhamasisha maisha haya mbadala ya dhambi.
Nyinyi Watoto WANGU, nyinyi walipa ushuru mtakuwa mnahamasisha haya kwa kulipia mishahara yao, na kwa kuyafanya haya sitabariki Marekani tena. Marekani haitawahi tena kushinda vita vya dunia, imekuwa tu kwa neema YANGU, hamjapoteza nchi hii bado. Wale wote walio na masikio ya kusikia, sikilizeni, wengine bakini viziwi.
Nyinyi mnaoitwa kwa Jina LANGU (Wakristo) mmefanya kidogo sana, kukomesha mauaji haya ya wale ambao hawajazaliwa. Mnaomba Mungu wenu kukomesha haya, lakini hamfanyi kingine. Ni wachache wanaoweka chini sifa zao, uhuru, pesa na maisha yao chini. Hawa ndio Watoto WANGU Ninaowafurahia, na makuu Yatakuwa baraka zao kule mbinguni. Je, Si Neno LANGU husema, hakuna upendo mkuu kwa binadamu yeyote ila tu yule anayeweka maisha yake chini kwa mwingine? Hawa ndio hawatakuwa na damu ya kuavya mimba mikononi mwao kwa kuwa walifanya zaidi ya kuongea tu. Waliweka matendo nyuma ya maandamano.
“Imani bila matendo imekufa!” wakati Watoto WANGU wanaporudi nyumbani Mbinguni, mnataka wale watoto hawakuzaliwa kuja kwako kukuuliza mbona pesa zako zililipia mauji yao? Mbona hamkujaribu zaidi kukomesha zile kuavya mimba, kuambia serikali, hapana? Watu wa YAHUVEH (Yesu) wana nguvu zaidi kushinda wapagani na miungu yao bandia! Ithibitisheni, kwa kuinuka katika Jina LANGU. Ambieni serikali tosha ni tosha. Watoto wangu, oneni ono hili la mikono misafi, sasa oneni mikono iliyolowa damu, sasa oneni mikono hiyo ikijaribu kutoa hiyo damu.
Kama mikono yenu imelowa upako wa RUACH HA KODESH (Roho Mtakatifu) na uweke matendo yako, pesa zako nyuma ya maombi haya na kuwaonya watu, kuandamana kwa serikali hizi na kukataa pesa zenu kuenda kwa mauaji ya watoto wasio na hatia. Basi nyinyi pia hamtakuwa na damu ya watoto wasio na hatia mikononi mwenu. Mnapozidi kuandamana na kuomba, damu itazidi kupungua mikononi mwenu. Wale walio na masikio ya kusikia sikilizeni, wengine wote bakini viziwi.
Acheni Ikulu ijue, Watu WANGU hatukubali damu ya watoto wasio na hatia mikononi mwao, wala kukubali uvundo wa dhambi za ushoga, na mmekataa kulipia jeshi ambazo zinahamasisha ushoga na maisha mbadala yao. Msiruhusu shule kufunza uongo huu ambao utawaharibu vijana wa taifa hili, zikiwatuma wengi jehanamu.
Ushoga upo katika uchache sasa lakini haitaendelea kuwa vivi hivi, kama vitu hivi vinafunzwa kama maisha mbadala iliyokubalika kule mashuleni, jihadharini tena. Walipa ushuru, mnalipia shule hizi na dhambi hii tena itakuwa mikononi mwenu kama hamtainuka sasa hivi na kuweka matendo nyuma ya maombi yenu. Marekani ilipewa kwa Watu WANGU; chukueni kile ambacho wapagani wamewaibia kabla wakati hamna. (Mwanzo 19:1-28) “Mkuu ni yule aliye ndani yenu kushinda yule aliye duniani.”
Inukeni, zungumzeni na kuyathibitisha haya sasa hivi! Neno LANGU linasema, “Mpe Kaisari ambacho ni cha Kaisari” lakini kwa kweli Ninasema Kaisari hakufanya mambo haya ya kusikitisha kama Clinton anavyojaribu kufanya. Kwa kweli Ninawaambia Sodoma na Gomora watakuwa ni heri kushinda Marekani. Taifa hili, Marekani, lilitengwa kwa mkono WANGU, ili muwe huru kuabudu na kuheshimu Mungu wenu YAHUVEH. Mnawezaje kuniambia MIMI kubariki Marekani? Wakati Marekani hainibariki MIMI?
Nyinyi Watoto WANGU, kwa kubaki kimya mmehamasisha matendo ya wapagani, wakati serikali, kwa sababu ya watu kadhaa iliamua kuwa hakuna Mungu kwa shule, bibilia, hakuna maombi; mliiruhusu na sasa mnashangaa kwa nini shule zenu na vijana wenu wanakaa kulaaniwa. Mnawezaje kuniuliza MIMI kubariki, yale ambayo watu wamesema sio YANGU. Chukueni shule hizo katika Jina LANGU na toeni watoto wenu katika hizi shimo za dhambi. Kwa kuwa bila mwangaza WANGU, uwepo WANGU, ukweli WANGU, shimo hizi zitazidi kuwa na giza zaidi na watoto pia. Hizi shule kwa haraka zinakuwa shimo za mpinga kristo na kimya yenu na dola zenu za ushuru zinawahamasisha.
Wale walio na masikio ya kusikia, sikizeni, wale waliokataa bakini viziwi. Wakristo hapo awali walikuwa wanatupwa kwa simba, wanauwawa, wanateswa, lakini bado walisimamia YAHUVEH! Makuu ndiyo baraka zao kule mbinguni. Sasa Watoto WANGU, wale wanaoitwa kwa Jina LANGU (Wakristo) wanakataa kuinuka, kusimama na kuambia shetani na wapagani wanyamaze katika Jina LANGU! Wanaogopa kupoteza kazi zao, au sifa, wakisahau ni Mungu wao Aliwapa hizo kazi na ukuzaji, na Ninaweza kuzichukua kwa urahisi. Wakristo wanaogopa kukwaza wapagani au miungi yao bandia lakini wanaona ni heri kukutana na uso wa Baba YAHUVEH Aliyekasirika! Ole kwa watoto WANGU waasi Ninapowaambia inukeni, zungumzeni, na kuambia shetani anyamaze na watoto wake wapagani, na Watoto WANGU wanasema lakini Bwana tunaogopa kwa kweli Nitawachapa wale Ninaowapenda kwa kuwasahihisha, Nikiwapa mtu wa kuniogopa MIMI.
Nyinyi Watoto WANGU, mmekuwa wengi walio kimya kwa muda mrefu sasa. Mna nguvu za Baba wa Mbinguni ndani yenu; itumieni kushinda adui. Lazima muanze mahali, kwa hivyo wekeni saini kwenye petitions; zichukue kila mahali muendapo, kanisa, malls, makazini, endeni mlango kwa mlango; kuna nguvu katika Nambari, ANDAMANA, ANDAMANA, ANDAMANA! Hadi maadui wenu waogope kuja kwenu, kwa kuwa sio kwa uwezo wenu, wala nguvu zenu, lakini kwa Roho YANGU, mtapata ushindi-mkichukua yote ambayo adui ameiba-tumieni uwezo WANGU, nguvu ZANGU, hekima YANGU na mtakuwa washindi, acheni Clinton na wapagani wasikie mgurumo wa Simba wa Yuda na kusikia mgurumo wa watoto wa Simba wa Yuda.
Gurumeni kwa sauti kuu hadi Clinton na wapagani pale kwenye Ikulu watambue, nyinyi watu WANGU mna zaidi ya umbo la utakatifu, mna utakatifu ndani yenu. “Shetani jihadhari, kama watu WANGU walioitwa kwa jina LANGU (Wakristo) watanyeyekea, kuanguka usoni mwao, mbele ya Baba YAHUVEH, Nitaiponya nchi yao.” Milima ya kinyesi hainuki wakati ipo kwa jirani yako. Unaiangalia, unatingiza kichwa chako, na kusema hiyo ni shida ya jirani yangu, inasikitisha, lakini sio wajibu wangu!
Lakini sasa Ninawaambia, milima hii ya kinyesi ipo kwenu sasa, kwa kila mtu kuona na sasa ni wajibu wenu kuisafisha. Kwa sababu nyinyi ndio walipa ushuru, nyinyi Watoto WANGU lazima muandamane. Watoto wasio na hatia ambao hawajazaliwa hawana sauti wala mayowe ya kuandamana ila yenu, hakuna yeyote huwasikia wakilia ila MIMI. Acheni Clinton na wapagani wasikie vilio vyenu vya hasira. Mnafikiria kama YAHUSHUA Angekuwa Anatembea duniani humu hangeandamana. Wapi Watoto WANGU ambao wamepewa Roho za Yeremia, au Yohana Mbatizaji?
Njooni Watoto WANGU ambao mna Roho ya Mungu Anayeishi ndani yenu, wale wote ambao wanajua, na wako na nguvu ya RUACH HA KODESH, Njooni wote ambao ni mashujaa katika Jina la YAHUSHUA. Njooni, nyinyi mnaojua ni nini sasa na ni nini kibaya. Njooni nyinyi mnaoelewa. Serikali inataka kuwapa wanyonge huduma bure za kuavya mimba na wengi wao ni Wahispania au waafrika watakaokuwa wanajaribu kutenda mauaji kwa wale ambao hawawezi kujiokoa.
Niliumba yote kilicho hai. Maisha yote ina thamani machoni MWANGU, inukeni, zungumzeni na kuonyesha wapagani hawa kuwa maisha yote ina thamani machoni mwenu. Wale wanyonge hata watambui kuwa serikali inafanya mauaji haya. Ni rahisi kumrarua mtoto akiwa tumboni mwa mamake, wakijifanya kuwa ni kwa uzuri wa mama na mtoto, kumbe sababu ya kweli ni kwamba serikali haitaki kulipa gharama ya mama huyo mnyonge na mwanawe. Wanyonge lazima waamke na kugundua kuwa wanadanganywa. Je, Ni hadi lini kabla wanyonge waanze kulazimishwa kuavya mimba?
AMKENI! Je, Ni lini hadi serikali hii ianze kuwalazimisha Wakristo kuavya mimba? Haiwezi fanyika? Tayari waliofanya yaya haya kwa Wayahudi. Hitler karibu awamalize kizazi kizima cha watu. Ni nani atakayefuata? Watu gani? Mwaka gani? Sasa wanasema wataua wazee, eti hawana maana tena. Walio tumboni mwa mamao hawakuishi kwa hivyo ina maana gani? Ina maana KWANGU, Mungu Mkuu wa Viumbe vyote Anawashtaki nyinyi, msibaki kimya tena.
Amkeni Watu WANGU. Mmelala kwa muda mrefu sasa. Ndoto mbaya zimeanza tu. Milima ya kinyesi sasa ipo kwenu, pamoja tunaweza kuisafisha. Sauti moja pekee yake ni ngumu kusikia, lakini sauti ya mamilioni ikiungana pamoja, katika roho moja, katika Jina moja, Jina la YAHUSHUA MASIHI, dunia nzima haitasikia tu bali pia jehanamu itasikia. Njooni Watoto WANGU, inukeni, zungumzeni, ambieni wapagani na mapepo wanyamaze katika Jina la YAHUSHUA na mko na nguvu, itumieni kwa hekima kwa Utukufu WANGU na kwa binafsi ya binadamu wote.
Kuna wale ambao wanajiita kwa Jina LANGU ambao sio WANGU na hawajawahi kuwa, wao sio wa RUACH HA KODESH WANGU, ingawa hawa nabii bandia hukaa makanisani wakijifananisha na kondoo, mtawatambua kuwa wao ni nani, watoto wa shetani, watahamasisha uongo wa shetani kuwa kuavya mimba sio uuaji, ushoga sio mbaya. Waone kwa rangi zao kamili, kwa kuwa wanasema vitu hivi katika Jina la YAHUSHUA, kumbe hakuna RUACH HA KODESH ndani yao. Jihadharini nao! Wale ambao wana masikio ya kusikia, sikilizeni, wale wengine bakini viziwi!
Hivi Ndivyo Asemavyo YAHUVEH siku hii ya 4-10-93, iliyopewa kwa chombo hiki kilichovunjika cha udongo na shujaa mkuu katika YAHUSHUA MASIHI, Elisheva Eliyahu. Wale walio na masikio ya kusikia, “Sikilizeni” wale wengine bakini viziwi!
* * * * * * *
Ujumbe mpya kuhusu Unabii huu ulioandikwa Disemba 22, 2015: Unabii huu ulipewa kwangu mwaka wa 1993, ni Unabii wa kale zaidi niliyoweka kati ya Unabii zingine hapa kwenye tovuti. YAHUSHUA Alinipa Unabii huu hata kabla sina kompyuta! Haikuwa mpaka miaka baadaye ndiyo YAHUSHUA Aliniambia kuwa niweke Unabii huu kwenye tovuti. YAHUSHUA Aliniambia kuiita Unabii 14. Kwa wakati huo sikuelewa, lakini sasa nimebarikiwa kuona kuwa YAHUSHUA Alinisababisha mimi kuipa Unabii huu Nambari 14. Ni kumbusho la Bibi Arusi wa Ufunuo wa Yohana 14. Sikujua kwa wakati huo, lakini sasa ninajua.
Nilikuwa Mwinjilisti/Nabii wa kupita tu kwa wakati huo, niliumba jina hilo kueleza, nilichokuwa ninafanya. Ningeenda pale YAHUSHUA Amenituma, hili ndilo jina la pekee nililiojua kitambo, na ningeenda na kuhubiri katika makanisa kadhaa. Kama Mchungaji angeweza kukubali ukweli ningeambiwa nirudi. Kama sivyo, niliita kupita tu. LOL. Ndio, hivi ndivyo nilivyoitazama kwa sababu nilitumwa kuwagonga na ukweli, na waliikimbia!
Unabii huu haukuwa baraka kwa Wachungaji kadhaa, niliwapa Wachungaji hawa na kongamano na sikualikwa kurudi tena na wengi wa Wachungaji hawa. Ninashangaa kwa nini! LOL. Sikujua vile vya kutoa Neno hili la YAH kwa watu wengi kwa hivyo nikaiweka kwenye gazeti kubwa la Indiana. Niligharamika kwa $500.00 kwa ad ya Ukurasa moja tu, katika Maandiko makubwa nyekundu na ilikuwa Unabii huu! 1993! Hata kabla niwe na kompyuta! Nina huzuni kuwa sina gazeti hilo tena, lakini sikuwahi ota kuwa ningekuwa Nabii na kama nilivyosema, sikujua lolote kuhusu intaneti. Ilikuwa mwaka wa 1995 nilipopata tovuti ya kwanza inayoitwa Amightywind HOLY GHOST Fire Church na nilijua tu Jina la YESU KRISTO wakati huo, na nilikuwa ninaongoza nafsi kwa YESU katika Jina hilo. Nilitoa Unabii huu wakati huo.
Wakati huu YAHUSHUA Aliponipa Unabii huu nilijua tu Sabato kama Jumapili. Haikuwa wakati kwa mimi kujua haya lakini kwa haraka nilijifunza juu ya Sabato na Jina Takatifu la YAHUSHUA. Hapo awali nilifunzwa Yeshua, mpaka niliposoma Bibilia ya Aramaic na nikaona hivyo sivyo njia ya kutaja Jina hilo. Sikujua kuwa Jina la Yeshua lilikuwa linakana Jina la YAH. Nilimuita YAH kwa Jina Jehovah. Unabii hizi ni Maneno ya Ramah, Maneno ya Maisha, kama tu Bibilia! Kila wakati unaposoma Maandiko utapata ufunuo mpya, na vilevile tu na Unabii hizi, laini itajitokeza tu ambapo haukuiona mbeleni.
Nilijua tu kile ambacho Makanisa ya Pentekoste iliyonifunza. YAH Alijua mwaka wa 1993 hakuna yeyote atakayepokea Majina Takatifu ya Kiebrania, na tayari tuna vita mwaka wa 2015 kusaidia watu kuelewa umuhimu wa kujua Majina haya Matakatifu ya Kiebrania, na kufuata Sabato ya kweli, jinsia ya ROHO MTAKATIFU. Ilichukua miaka 7 kuandika kitabu ambapo kuna ushahidi nyingi kuyathibitisha haya sasa. Kitabu cha Waamuzi ndicho kilichojaa ushahidi. Kila wakati mnapoona KJV mnaona Hekima huitwa She. Lakini mwaka wa 1993 hakukuwa na ushahidu huu wala ufunuo hizi nilizopewa, nimekuwa wa kwanza kufunza Jinsia ya ROHO MTAKATIFU kwenye intaneti nafikiri lakini sina uhakika.
YAH Aliniruhusu kuita YAHUSHUA, YESU, na ROHO MTAKATIFU, HE, kwa sababu kuna wakati wa kila msimu. Ninashukuru sana BABA YAH haweki juu ya Manabii WAKE, ukweli zaidi ya yale wanayoweza kwa sababu hakungekuwa na imani ya kuyathibitisha Maneno haya, kama Alivyofanya 1993. Nilijifunza Alipokuwa Anazungumza kila Ufunuo wa Kinabii.
Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!