Unabii 139
Shairi ya “Mfupa wa Mifupa Wangu, Nyama ya Nyama Yangu”
Imezungumwa katika Upako wa RUACH HA KODESH
Kupitia Mtume Elisheva Eliyahu
Imepokewa Oktoba 23, 1999, Sabato Jumamosi
Ilitolewa tena Januari 11, 2019
Mwanzo 2:18, 23 BWANA Mungu akasema, ‘‘Si vema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa. […]Huyo mwanaume akasema, “Huyu sasa ni Mfupa wa Mifupa yangu na Nyama ya Nyama yangu, ataitwa ‘Mwanamke,’ kwa kuwa alitolewa katika Mwanaume.’’
Shairi hii ni Unabii na ni ahadi kwa dada zangu katika YAHUSHUA (‘YESU KRISTO’)-ambaye ingawa walipeana akili, mwili, roho na nafsi zao kwa YAHUSHUA, bado wametekwa nyara kwa ndoa za mateso au wametekwa nyara na fikra za ndoa za mateso ambazo zilitoka jehanamu. Ni YAHUSHUA pekee ambaye Anaweza kukuweka huru kwa wale ambao walikuumiza au walikutia vidonda akilini, mwilini, rohoni na nafsini. Hii ni ahadi yako na yangu, ambapo umejua mabaya kabisa utajua bora zaidi.
Niliamka BWANA YAHUVEH Akizungumza haya Maneno kwangu, “Nilikutumia Mchungaji Harry Regan. Kwa misimu minne utajua kama thibitisho. Alifunga ili uweze kusikia…”
BWANA Aliniambia “Amka na yaandike.” BABA YAHUVEH Alitupa shairi hii kuiandika, kama MUNGU Alivyozungumza kwenye ndoto, Akiniamsha na Mananeo haya ya shairi ifuatayo. Nilidhani kuwa Maneno haya ni ahadi kwangu pekee. Sasa ninajua kuwa ni ya dada zangu WOTE, katika ‘YESU KRISTO’ (YAHUSHUA MASIHI wetu), waliotembea katika viatu ambavyo nimevitembelea.
Hii ni ahadi kutoka kwa MUNGU Aliyonipea, na sasa nitaitoa kwa wale wanaongoja mazuri katika bwana aliyekadiriwa na MUNGU, ambapo wamejua tu mabaya kabisa kutoka jehanamu. Someni haya na yadai kama ahadi yenu.
Wanaume ambao wamekadiriwa kwa wanawake hawa wanajua haya: una mwanamke ambaye ameepuka tanuu ya moto na kutoka msafi kushinda dhahabu. Atakujali kwa njia ambazo mwanamke ambaye hajateseka kwa njia ambazo tumeteseka hatawahi kumthamini bwana mtakatifu. Kama kuna yeyote anayetaka kusambaza haya kwa tovuti zao niandikie na kunijulisha. Sifa, Heshima na Utukufu kwa YAHUVEH!
Yafuatayo ni Unabii ulivyokuja
—na Nabii Elisheva, akizungumza katika "Ndimi Takatifu," kama ROHO wa MUNGU Alivyomjalia kutamka (Matendo ya Mitume 2:3-4) kwa lugha za wanadamu na malaika (1 Wakorintho 13:1). Elisheva anazungumza katika ndimi zinazoleta Unabii (1 Wakorintho 14:6).
Inayo MAJINA ya KIEBRANIA ya MUNGU:
YAH/YAHU יה ni JINA TAKATIFU la MUNGU, kama vile “Alleluia” au “Hallelu YAH” הללו–יה ambayo humaanisha “Msifu YAH”: YAHUVEH/YAHWEH י-ה-ו-ה MUNGU BABA; YAHUSHUA/YAHSHUA יהושוע MWANA WA PEKEE WA MUNGU—(HA MASHIACH המשיח inamaanisha “MASIHI”; ELOHIM אלוהים INAMAANISHA “MUNGU.”) Ufunuo wa “SH’KHINYAH GLORY” שכניה תפארה —kama JINA la KIBINAFSI la RUACH HA KODESH רוח הקדש, (katika Kiiengereza “ROHO MTAKATIFU”) —upo kwenye tovuti hii. (HA SH’KHINAH {SHEKINAH} ni Kiebrania inamaanisha UWEPO WA MUNGU.)
Zaidi ya hayo, ABBA YAH אבא יה humaanisha “BABA YAH” na IMMA YAH אמא יה humaanisha “MAMA YAH.” Katika Kiebrania, ROHO WA MUNGU ni kike, anajulikana kama “SHE” na anaonyeshwa hivi katika Unabii & matamshi ya Maandiko yafuatayo. Matamshi yote ya MUNGU yapo kwenye herufi kubwa.
Maandiko yaliyotajwa yametoka KJV/NKJV au CJB, isipokuwa pale palipotajwa vinginevyo.
Onyo ya YAHUVEH iliyoongezwa mbele ya Unabii zote:
Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako.
Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha.
Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo.
Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli.
‘‘MIMI NDIMI BWANA YAHUVEH:
hilo ndilo JINA LANGU! Sitampa mwingine UTUKUFU WANGU
wala sanamu SIFA ZANGU.” (Isaya 42:8).
(Unabii 105)
Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo kwa wale wanaokejeli:
“Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA YAHUVEH juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”
—2 Mambo ya Nyakati 36:16
Alafu, Julai 2016:
Ole kwa yeyote atakayethubutu kujaribu kuwadhuru— hawa wawili walio na upako. Mtajuta kuzaliwa kwenu. Msiwaguse masihi WANGU, msiwadhuru Manabii WANGU (Zaburi 105:15; 1 Mambo ya Nyakati 16:22). Ingekuwa ni heri kwenu kama MIMI, BABA YAHUVEH, Ningerarua ndimi zenu! (Unabii 128)
Na kutoka kwa Nabii Ezra:
Ole kwa wote-wanaokuja dhidi ya Huduma hii NA UNABII HIZI na Elisheva na MIMI, na Wahudumu wote wa Huduma ya Amightywind-Ninawaonya sasa, ‘Msiwaguse masihi WANGU, msiwadhuru Manabii WANGU (Zaburi 105:15; 1 Mambo ya Nyakati 16:22) kabla ghadhabu ya Fimbo ya YAH haijawaangukia. Lakini kwa wale ambao ni baraka kwa Huduma hii, na waaminifu, na wanaopokea Unabii, baraka tele zitawajia-kwa ajili ya kulinda yote ambayo ni ya YAH katika JINA LA YAHUSHUA.
Unabii 139 Unaanza
WOTE watajua kuwa ni “MIMI”- niliowaleta pamoja na HAKUNA mwanamume au mwanamke-au pepo kutoka jehanamu inayoweza kusimamisha yale ambayo MUNGU amepanga.
Ingawa wakati mwingine mtakuwa na wasiwasi, jueni tu kuwa “MIMI” nilipanga wakati, na mahali, na vile mtakavyopatana.
Ninakuletea mwanamume ambaye anajua Amani YANGU, kumuunganisha pamoja na mwanamke ambaye hajawahi kujua Amani hii….
Na hata hivyo, mwanamume huyu amejawa na Huruma YANGU & Upendo WANGU, ana Utulivu WANGU, Upako WANGU, kumuonyesha na kumfunza kutafuta mazuri ya Mbinguni, na kumuombea zaidi, na yeye kumuombea zaidi, na sio chini ya hayo.
Ninamleta mwanamume ambaye anajua tu Furaha YANGU & Kicheko CHANGU… kuungana na mwanamke, atapaswa kumfunza na kumuelezea Furaha YANGU na vile vya kucheka naye.
Ninamleta mwanamume ambaye hajui kuogopa, kuungana na mwanamke ambaye, kama oksijeni, amepumua hofu kwa miaka yake yote.
Ninakuletea mwanamke ambaye amejua tu kila aina ya hofu, kutumiwa na kutusiwa, kuungana na mwanamume ambaye ana Upako WANGU kulinda na kupanguza uchungu na machozi kutoka machoni mwake kutoka kwa wale wanaomshtaki na wote wanaomtukana, akifunua ukweli na kukanusha uongo za maadui!
Ninakuletea mwanamke ambaye anajua tu ukosefu wa usalama, kuungana na mwanamume ambaye anajua tu Usalama WANGU.
Ninakuletea mwanamke ambaye hajajua faraja ya ulimwengu, kuungana na mwanamume ambaye anajua Faraja YANGU ya Kiulimwengu na pia ya Kiroho.
Ninakuletea mwanamke ambaye hajui kupendwa ni nini, kuungana na mwanamume ambaye ana Upendo WANGU iliyochanganywa na upendo wake utakaomfunza na wengine maana ya Upendo wa Kweli.
Ninakuletea mwanamke ambaye hajakuwa na hamu ya kuishi, kuungana na mwanaume ambaye anaishi kila siku kwa ukamili na anaulizia miaka zaidi kutoka KWANGU niwape.
Ninakuletea mwanamke ambaye hajifikirii kama mrembo, kuungana na mwanamume ambaye atamthamini na sio umbo lake tu lakini urembo wake wa ndani wa kiroho. Atamuonyesha kile ambacho adui hakumruhusu kuona na haya yatamfanya asonge karibu naye na MIMI!
Ninamletea mwanamume huyu mwanamke ambaye amejua tu machozi ya kuvunjwa roho, kupitia miaka yake yote, kuungana na mwanamume ambayr ana UPAKO wa ROHO MTAKATIFU WANGU kuyaondoa yote, pamoja na hofu zake na fikra za hatia, aibu na upweke, uchungu na lawama.
Ninakuletea mwanamke ambaye haamini mwanamume yeyote.-alijifunza kupigana nao, alijifunza kwa mwili wake kujitetea- kuungana na mwanamume atakeyejionyesha kuwa wa thamani wa kuitwa WANGU.
Ninampa ishara hii ya kumfariji:
Katika Upako WANGU atamtetea mara kwa mara, kama inavyohitajika, atakuwa tayari kutoa maisha yake kwa yule ambaye anaitwa bibi yake.
Ninakuletea mwanamke ambaye hajawahi kuwa na faraja ya kumbatio la upendo, kuungana na mwanamume anayemsaidia, kumtia moyo na kumueka mbali na madhara yote, kuungana na mwanamume ambaye ana Kumbatio LANGU la Upako kumshika, kumlinda na kumfunika kama manyoya.
Ndiposa, atajua kwa kweli kile ambacho MUNGU anataka ajue, vile ilivyo wakati wawili wapo kama akili, mwili, roho, na nafsi moja. Katika maelewano kamili, pamoja, watatembea ndani YANGU.
Ninakuletea mwanamke, ambaye ingawa amepewa busu, hajui shauku ya upendo ambayo hajapata kuungana na mwanamume ambaye pia ana Upendo WANGU wa Upako katika mipapaso na busu zake.
Ninakuletea mwanamke ambaye anajua tu ubaya, uchafu, na mateso ya ngono, kuungana pamoja na bwana aliye na upako anayejua uzuri wa pumziko takatifu ambapo akili, miili, roho na nafsi mbili zimekadiriwa na MUNGU na bila mwingine hawatawahi kuwa sawa tena.
Mwanamume huyu na mwanamke huyu wataona wanapokuja pamoja katika umoja KWANGU, Upendo WANGU & Tumaini la Amani na baraka & Maelewano. Bwana huyu na bibi kwa kweli watakuwa kitu kimoja ndani YANGU-Akifuta uchungu, mchafuko kutoka kwa fikra zake za mateso.
Ninakuletea mwanamke anayekataa kufunzwa na mwanamume, ingawa haya ndio ametaka na kutafuta, kuungana na mwanamume Niliyempa upako wa kumfunza, kwa ukamilifu wa upendo mpya wa upako ambayo hajafikia bado.
Ninakuletea mwanamke aliye laini, nyeti, tete na mwenye mhemuko kama kipepeo aliye na mabawa yaliyovunjwa, kukatwa na kuraruliwa, kujiunga na mwanamume aliye na UPAKO WANGU WA ROHO MTAKATIFU kuzungumza Uponyaji, Upendo, Huruma, Amani & Kicheko, na katika Upako WANGU, atatengeneza hayo mabawa yaliyoraruliwa-ili aweze kupepea, juu, angani-na nyimbo za upako ambazo Nitampa yeye kuimba.
Ninakuletea mwanamke ambaye huhesabu dakika na masaa ni kama ni miaka, anayekataa kuhesabu umri wa miaka yake kwa kuwa anahisi kuwa hajaishi. Sasa Ninampa, kuungana na mwanamume ambaye hajui dhana ya miaka au wakati na hujua tu kila umri wa miaka yake, yote yamekuwa YANGU.
Ninakuletea mwanamke ambaye, nyakati nyingine, hukosa imani, kuungana na mwanamume ambaye anajua tu Imani YANGU.
Ninakuletea mwanamume ambaye hutembea kwenye ukamilifu wa Upako WANGU kujiunga na mwanamke ambaye anafunzwa ukamilifu wa Upako WANGU.
Ninakuletea mwanamke ambaye amejifunza na mdomo wake kupigana vita, kuungana na mwanamume ambaye hutumia maombi yake kupigana vita, kuyavunja milango ya maadui.
Ninakuletea mwanamke ambaye hajui kiburi, kuungana na mwanamume ambaye atahitaji unyenyekevu kusimama kando yake.
Ninakuletea mwanamume ambaye ni mwerevu katika macho ya wanadamu, kuungana na mwanamke ambaye huwashutua wale wanaojifikiria werevu!
Ninakuletea mwanamke ambaye atakuweka zaidi Miguuni MWANGU, unapojaribu kumuelewa kila siku, ukizipata tu majibu chini ya Upako WANGU wakati mwana WANGU anaabudu, kuimba, kusifu na kuomba!
Ninakuletea mwanamke ambaye amejua tu kushindwa, maadui walipomgonga tena na tena akaanguka, kuungana na mwanamume ambaye anajua tu Ushindi katika JINA la YAHUSHUA. Nilichounganisha pamoja hakitawahi kuwa sawa tena!
Ninakuletea mwanamke ambaye maishani ana vidonda vilivyo na makovu, kuungana na Upako wa Mikono ya Mpasuaji WANGU Niliyoiweka ndani ya mwanamume huyu.
Ninakuletea mwanamke ambaye hajawahi kuwa huru, ametekwa nyara nyuma ya bars zisizoonekana-ana uzito- mizigo na utumwa ndicho alichokiona, kuungana na mwanamume atakayemfunza vile vya kuwa huru ndani YANGU!
Ninakuletea mwanamke aliye na upako wa ROHO MTAKATIFU usio wa kawaida, kuungana na mwanamume kumfunza vile ya kuitumia kwa Sifa, Heshima & Utukufu!
Ninakuletea mwanamke ambaye hajui maana ya pumziko, kuungana na mwanamume ambaye hukaa ndani ya UWEPO WANGU wenye UPAKO, ambapo kuna pumziko kweli! Atamfunza vile ya kukaa ndani ya amani na kubaki katika baraka!
Ninakuletea mwanamke ambaye hajajua afya njema, kuungana na mwanamume ambaye anatembea tu katika Afya YANGU Kamili; anajua kuwa hii ndio mali kweli! Atasaidia kulinda, kulinda akili, roho, nafsi na mwili, akiomba katika JINA la YAHUSHUA na kutembea katika Mamlaka YANGU ya Kiroho, ni wazi…
Zawadi ambayo Nimewapa nyote, kuwaokoa kutokana na aina za udhaifu, ugonjwa, sickness, na umaskini!
Ninakuletea mwanamke ambaye Nimempa Gongo LANGU, kuungana pamoja na mwanamume Nimempa Fimbo YANGU.
Ninakuletea mwanamke ambaye anakasirika kwa haraka, kuungana na mwanamume ambaye ana kiberiti mkononi.
Ninakuletea mwanamke ambaye atagusa dunia hii kwa ajili YANGU, kuungana na mwanamume ambaye upako wake ni ile nusu nyingine na pamoja wataona ushindi na sio kishindo!
Bila mwingine hamtaweza kufanikiwa katika yale Niliyoyakadiri kwenu kufanya kwa Utukufu WANGU-mkileta Mana kutoka Mbinguni!
Ninawatuma nyinyi wawili kuwalisha Kondoo na Wanakondoo WANGU, kuwapa maji na kuwalisha chini ya Upako WANGU. Maziwa, Mvinyo Mpya & Nyama watasherehekea na kula.
Ninawashauri nyote sasa. Msisikize yeyote. Ingawa watakuwa na nia nzuri, hawaelewi. Nilipoumba nafsi zenu, Niliziumba kwa mwingine. Hakuna vipande vingine vya fumbo vitaweza kutosha, hata mkihangaika, kupigana na kugombana.
Kwa kuwa hamtaki vitu vibadilike bado, lakini wapendwa WANGU, siku ishakadiriwa. Haya ndiyo Mapenzi YANGU Yaliyokadiriwa. Hamtafeli.
Ninawaleta nyinyi wawili pamoja. UPAKO utawaweka pamoja kwa UPENDO WANGU na GUNDI la UPAKO wa ROHO MTAKATIFU! Ili kuwathibitisha “MIMI NIKO” ni MUNGU anayeshangaza wale werevu. Kumbukeni, na MUNGU vitu vyote yawezekana. Haya, hamtawahi kuyakataa.
Kila siku mnapokumbatiana mtahisi kipimo kipya cha upendo kwangu MIMI. Pamoja mtayaona haya.
Nimekadiri kuwa wakati macho yenu yatakutana mara ya kwanza. Mtajua na kuona, ahadi hii Niliyoizungumzia. Nimekadiri wakati ambapo nyoyo na mikono yenu itakutana.
Kwa kuwa hapo ndipo Upako hizo mbili zitaungana pamoja kama moja na itaanza kutiririka bila kipimo. Ninawaahidi haya.
Itanibidi kutoa maana mpya ya “haraka”-kwa kuwa inagawa nyote mnapinga sasa-mtakuwa kama kiberiti inayowasha utambi wa taa ya mafuta ya mwingine.
Ninawaleta pamoja kufikia dunia hii kwa ajili ya waliopotea na nafsi wanaoumia-siku moja mtaelewa, kwa kuwa vitu vingine bado hamjui.
Hakuna chochote ambacho kitakuwa ngumu kama pamoja mtasimama; wakati mmoja ni mnyonge yule mwingine lazima awe na nguvu, haijalishi kama ni mwanamke au mwanamume! Peaneni nafasi kama Nilivyokadiri na msiwahi kuruhusu upendo wenu kuchukua nafasi ya upendo WANGU.
Ninawaleta pamoja na kuwaonya sasa. Chungeni hasira zenu! Haikuwa ili mpigane! Roho, nafsi, upako, maombi zenu-nyoyo, macho, mikono, masikio, miili iliumbwa kwa mwingine. Lakini sio hasira zenu na ubishi! Zimetumwa kutoka jehanamu.
Roho zenu za shujaa walio na upako ziliwekwa ndani yenu. Hizi roho za shujaa sio za kutumika dhidi ya mwingine, lakini imewekewa shetani, adui wenu! MSIWAHI kuruhusu ndimi zenu kuumizana. Ubishi zote lazima zipelekwe KWANGU kwa maombi ya upako mkiwa kwa magoti.
Pamoja mnaleta hizi shida! MSIWAHI kuzungumza maneno ya chuki! Kwa kuwa “MIMI NIKO” Ndiye REFA WA PEKEE. Na Hukumu YANGU ndio mwisho na Nimeyakadiri haya. KUSIWE na ubishi kwa niaba ya sisi SOTE!
Sitaruhusu mhuzunishe ROHO MTAKATIFU! Kwa kuwa Ndoa hii & Huduma hii itakuwa vile Nilivyokadiri, na SIO kufanywa vile mnavyofikiria au mnavyotaka iwe! Mmoja akiwa na hasira, jua lisishuke kabla katika Upendo & Amani YANGU, wote mmepeana busu na kukutana.
Ninakuletea mwanamke ambaye yupo na upako. Ninakuletea mwanamume ambaye anatembea kwa Upako WANGU. MSIWAHI jaribu kugusa, kuleta uharibifu kwa UPAKO! Kwa kuwa hii itatuma alamu ya onyo kwa ROHO MTAKATIFU! Kama hamtaki Niwapige kwa njia kuu, heri mtubu na kuuliza msamaha siku io hiyo! Msichelewe!
“MIMI NIKO” Ndiye PEKEE Anayeamua ni yupi yuko sahihi na ni yupi amefeli! “MIMI NIKO” Ndiye wa PEKEE aliye na ujuzi wa kilicho mbele na nyuma!
Ninajua mwanzo kutoka mwisho na “MIMI NIKO” Ninawaamuru wote. Kwa Mapenzi ya “MIMI NIKO”-ingawa nyinyi wote ni wasumbufu, mtanitii MIMI na kwa Mapenzi YANGU, mtainama!
YEYOTE asifikirie kuwa wako kwa kiwango kikubwa au kiwango kidogo cha kiroho! Kwa kuwa ni “MIMI NIKO” Ninayewapa upako na “MIMI NIKO” Nitakayewagonga kutoka kwenye kiimo cha kujiona wa haki kushinda wengine, maringo, kiburi!
Nimempa huyu handmaiden shairi hii kwa nyinyi wawili kuisoma, kwa kuwa kitambo mlinipa MIMI maisha yenu, mlipokubali ZAWADI YANGU pale Kalivari.
Ninataka kila siku myasome haya na kuomba, kuwa mtakuwa yale YOTE ambayo Nilikadiri mtakuwa, mkifanya haya bila kuchelewa.
Mtakuwa hapa Ulimwenguni marafiki wa dhati na wapenzi. Kumbukeni kuwa huu haukuwa mpango wenu kwa hivyo hata msijaribu kuelewa. Ilikuwa kwa ajili yenu “MIMI NIKO” Nilipanga hatma yenu. Pamoja mtanibariki MIMI na dunia itayaona haya! “MIMI NIKO” huwa sifanyi makosa!
Msiweke siri ZOZOTE kwa mwingine. Mtakuwa na ukweli na waaminifu, kama mlivyo KWANGU, au “MIMI NIKO” Nitazungumza na kumuambia yule mwingine kile unachojaribu kuficha.
SASA, kimbieni kwa zawadi ya mbio za mwito mkuu! Chini ya UPAKO WANGU wa ROHO MTAKATIFU, haraka, fanyeni haraka! HAKUNA tena kukataa kile mnachojua ni ukweli kwa mara kwa mara, Nimewaambia:
Ninakuletea mwanamke ambaye kwa wanaume amejua mabaya kabisa kama laana. Ninamletea mwanamume ambaye “MIMI NIKO” Najua kuwa yeye ndiye anayemfaa na amechaguliwa kwake kati ya wengine wote.
Ninakuletea mwanamke ambaye “MIMI NIKO” Amekadiri-upendo wako ulikuwa wa kwake na upendo wake ulikuwa wa kwako-SIO sasa tu, lakini milele YOTE!
Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!