Unabii 135

Kutahiriwa na Agano la Abrahamu.

Imeandikwa katika Upako wa RUACH HA KODESH
Kupitia Mtume Elisheva Eliyahu
Ilipokewa Novemba 27, 2016-
Ilitolewa Mei 10,2017

Kueni katika amani Watoto WANGU. Kwa kuwa nyinyi mpo kwenye kiganja cha Mkono WANGU. Mpo chini ya ufuniko wa mabawa YANGU. Hawa vijana wametahiriwa katika moyo na sasa wanataka kufuata na kutengeneza agano mpya na MIMI kama vile Abrahamu alivyofanya (Mwanzo 17:3-14). Kwa nini, kwa nini, kwa nini, Nitaruhusu kitu kibaya kufanyika? Kwa kuwa mikono yako Ezra ina upako.

O Mwana WANGU Ezra! Nitabariki kila kitu ambacho mkono wako hugusa-kila chombo unachotumia, omba baraka juu yake. Kumbusha kila mwana kuwa YAH Amefurahishwa nao. Kwa kuwa wanathibitisha upendo wao kwa njia nyingine wanapokuja chini ya agano lingine, agano mpya kwa kuwa tayari wana AGANO LA DAMU YA YAHUSHUA. Ezra utatengeneza video na itakuwa ulivyosema, ulikuwa pale kama baba, baba wa kiroho, mkuu wa Huduma, kuwa na wao kabla hawajaingia kwenye chumba cha upasuaji. Na vilevile tu walivyofuata na kuvaa kofia, angalia sasa wanavyofuata na kutahiriwa.

Wewe zungumza tu katika maneno ambayo wanaweza kuelewa Ezra. Ifanye iwe rahisi kabisa mpaka mtoto aweza kuelewa. Kwa hizi ndizo kanuni ambazo MIMI Nimempa [daima] Elisheva.

Na Ezra unapotengeneza video hii, uwajulishe wote wanaosikiliza, ambao hawakuweza kuwa hapo kwa wewe kuwawekelea mikono na kuwapa baraka hii ya baba wa kiroho-wajue haya: Wanaponitii MIMI na kuingia katika Agano hili la Abrahamu ni kama walikuwa wanasimama pale [na wewe].

Watie moyo waandikie Huduma hii. Kwa wale wote waliotahiriwa moyoni na sasa wametahiriwa kimwili, wapo chini ya AGANO MPYA YA DAMU YA YAHUSHUA na Agano la Abrahamu ya MIMI, YAHUVEH, hii ni baraka maradufu-kwa wanaume wote watakaopokea haya, haya yana Upako maradufu pia!

Ezra, hausemi kuwa kutahiriwa kunaokoa mtu yeyote. Kwa wale maadui ambao watakushambulia na kusema kuwa unasema haya. Haya sio kweli. Daima mtafunza kuwa ni pekee katika JINA & DAMU YA YAHUSHUA ndio kuna ondoleo, msamaha wa dhambi. Lakini Agano la Abrahamu, inachukua haya mbali zaidi, Ikisema “Nataka kufanya yote ambayo umeniamuru WEWE kufanya BABA YAHUVEH,” kama vijana na pia wazee wanapozungumza, walio WANGU.

Ni haya tu: MIMI Nitawatuma watoto WANGU-wengine ambao hata bado hawajui kuwa ni watoto WANGU-kutoka pande zote nne za ulimwengu kusikia juu ya Huduma hii; hata ikiwa kwa neno la mdomo au intaneti au kwa kompyuta, Ninawaambia haya, watakuja! Na sasa wamekuja tayari katika lugha 34 tofauti.

Unanifurahisha MIMI Ezra na utakaporudi utafunza juu ya kutahiriwa, Mwanzo 17:1-27, na moja kwa moja watoto ambao sio watoto lakini vijana [pia]-kwa kuwa itakuwa ni wale vijana wengine ambao watafuata mfano wao na ushuhuda wao-baada ya kupona na wataelezea ni kwa nini walitaka kuwa china ya agano la Abrahamu. Na wewe Ezra utafanya mafunzo juu yake, kama Nilivyosema. Na video ya Adam pia itakuwa pale. Kwa kuwa watu hawaelewi kwa nini ni muhimu kama wapo tayari chini ya DAMU YA YAHUSHUA.

Alafu [baada ya wokovu] huja kutahiriwa kimwili katika kutii kwa Sheria ZANGU ili muingie chini ya Agano la Abrahamu (Mwanzo 17:1-27). Mlitoa mwili wenu-mlikuwa tayari kupitia uchungu ambayo ni ya muda tu. Na hata mnapoona ile damu: Kumbukeni kuwa hii sio tu Agano la Abrahamu, lakini hii ni kumbusho la DAMU iliyomwagwa kwa sababu yenu pale Kalivari na YAHUSHUA MASIHI.

Mwana WANGU mpendwa Ezra, Ninasema kazi nzuri! Nimefurahishwa nawe sana kwa kufunza juu ya Agano la Abrahamu.

Nimefurahi sana nawe. Kwa kuwa sasa wote watatembea katika Upako mpya. Walikuwa tayari kupitia uchungu wa kimwili kutii ROHO na MIMI Nimefurahishwa nao. Haya ni kwa kila mtu aliyefuata mfano huu ya kila mmoja-mlipoongoza njia na funzo hili.

Sasa lazima ufunze kila mtu pale kwenye huduma ya Amightywind.

Tena kila mmoja ya watoto hawa watatembea katika Upako mkuu kushinda [hapo awali]-wale ambao uliwatahiri juzi na pia haya ni kwa wote, wote, wote ambao watatahiriwa kwa mara ya kwanza.

[katika hospitali, ilikuwa sera kuwa kila mtoto atahiriwe]-ilidhaniwa tu, kuwa haikuwa na chochote kufanya na Utakatifu. Alafu, kanuni zikabadlika. Kwa kuwa shetani hakutaka watembee katika hilo agano lipya kama vile tu hataki watembee katika AGANO LIPYA LA DAMU YA YAHUSHUA, lakini mtatia mkazo kwa umuhimu wake na hata kutoa ushuda ya vile mapepo yalipotoweka na itakuwa rahisi sasa kunitii MIMI, YAHUVEH na MWANA WANGU YAHUSHUA na IMMAYAH RUACH HA KODESH MPENDWA, ROHO MTAKATIFU.

Nimefurahishwa nawe mwanangu kwa jukumu hili ulilolichukua na kulifanya kwa wote waliotahiriwa. Na mwana WANGU mpendwa ninataka uzungumze kwa kongamano la Poland, kuchukua wakati kuwaambia umuhimu wa na vile MIMI YAHUVEH Nimefurahishwa na wale walio katika Agano la Abrahamu. Kwa wakati WANGU mwanangu, mtaweka hiyo video pamoja na kuyafunza haya, na umuhimu wake. Kwa kuwa haikuwa wewe Elisheva uliyefaa kuyafunza haya, katika miaka hii yote. Haikuwa wewe Elisheva uliyefaa kufunza Torati. Umeyafanya yale uliyoambiwa ufanye. Ulipaswa tu kumngoja Ezra kuja kutimiza na kusaidia kumaliza kile Ninachotaka kifanywe!

Elisheva: BABA YAHUVEH, kuna chochote kikingine WEWE Unataka kusema?

Hivi ndivyo wanielekeza kuomba sasa BABA YAHUVEH. Na unaniambia niombe amani, amani, amani juu ya hawa vijana na amani-Ninataka tu ujue kuwa ninasikia haya tena na tena vile YAH amefurahishwa nawe. Anazidi tu kuniambia vile alivyofurahishwa na nyinyi wote, na vile anavyowapenda! Vile unavyowaongoza hawa vijana kwa mkono, YAH Ataongoza mkono wako, Ezra. Kwa kuwa wewe ndiye Baba yao wa kiroho. Wewe pia ni mchungaji wao.

Na anakutumia wewe, kama tu ulivyosema, lazima uwaambie YAH amesema yale ambayo ulinifunza. Wakumbushe kuwa mama hafai kuwa pale [lakini] ni baba ndiye hushika mtoto (akiwa siku na 8, kama vile tu YAHUSHUA Alivyotahiriwa akiwa tu siku na 8). Haya yatawafariji hawa vijana.

Na omba juu ya kila mmoja wao. Ombea kila mmoja amani. Nimeona maono na YAHUSHUA Atasimama kando ya kila mmoja wao, kila mmoja wenu. Na YAHUSHUA Atakuwa anasimama pale kando yenu, kama mmelala pale kwenye meza. Na YAHUSHUA Ananiambia kuwatia moyo kuwa atakuwa pale kuwatuliza.

Elisheva, Ninawapenda wote, hata zaidi ya uwapendavyo. Na sitaruhusu madhara yoyote kuwajia sanasana bwana yako mpendwa Ezra. MIMI BABA YAHUVEH & MIMI YAHUSHUA & MIMI IMMAYAH tunawakumbusha kuwa tunawapenda: nyinyi wote, Wana WETU wote na Binti WETU wote.

Kumbukeni kuwaweka katika maombi. Kwa kuwa nimewatuma malaika watakatifu kuwalinda wote.

Kwa hivyo endelea kuwaita wafasiri Ezra, wafasiri Waebrania ili wakusaidie! Ili uwalishe. Ili uwatunze. Bibi Arusi wa YAHUSHUA wa kimataifa wametawanyika katika kila pande 4 za ulimwengu na pia wageni watakaokuwa katika Karamu ya Ndoa ya Mwanakondoo.

Mwisho wa neno.

Elisheva: BABA YAHUVEH, haya ndiyo nimeyasikia ya kusema. Asante na sifa KWAKO! Watoto wetu wa kiroho wanavyoenda kwenye safari hii ndefu na Ezra kwa upasuaji.

Imezungumzwa

Imeandikwa

Imepewa kwangu Elisheva Eliyahu

Mwisho wa Neno

Elisheva: Asante. Hayo ndiyo ninayoyasikia! Sifa kwa YAHUSHUA, ABBA YAHUVEH! HalleluYAH MPENDWA RUACH HA KODESH! Asante. Asante. Asante.

Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred