Unabii 129

Jihadharini na Ghadhabu ya MWANAKONDOO! YAHUSHUA Aleta Upanga WAKE Wa Kugawa!

Imeandikwa/Imezungumzwa katika Upako wa ROHO MTAKATIFU (RUACH HA KODESH)

Kupitia Mtume & Nabii Elisheva Eliyahu-Julai 5, 2016

Wakaiita milima na miamba wakisema, “Tuangukieni, mkatufiche na uso Wake Yeye aketiye kwenye kiti cha enzi na mkatuepushe na ghadhabu ya Mwana-Kondoo.

-Ufunuo wa Yohana 6:16

Unabii huu una MAJINA ya KIEBRANIA ya MUNGU:

YAH/YAHU יה ni JINA TAKATIFU la MUNGU, kama vile “Alleluia” au “Hallelu YAH” הללו–יה ambayo humaanisha “Msifu YAH”: YAHUVEH/YAHWEH י-ה-ו-ה MUNGU BABA; YAHUSHUA/YAHSHUA יהושוע MWANA WA PEKEE WA MUNGU—(HA MASHIACH המשיח inamaanisha “MASIHI”; ELOHIM אלוהים INAMAANISHA “MUNGU.”)

Ufunuo wa “SH’KHINYAH GLORY” שכניה תפארה —kama JINA la KIBINAFSI la RUACH HA KODESH רוח הקדש, (katika Kiiengereza “ROHO MTAKATIFU”) —upo kwenye tovuti hii. (HA SH’KHINAH {SHEKINAH} ni Kiebrania inamaanisha UWEPO WA MUNGU.)

Zaidi ya hayo, ABBA YAH אבא יה humaanisha “BABA YAH” na IMMA YAH אמא יה humaanisha “MAMA YAH.”

Maandiko yaliyotajwa yametoka KJV au NKJV, isipokuwa pale palipotajwa vinginevyo.

Maneno ya YAHUVEH kwake Elisheva iliyoongezwa mbele ya Unabii zote:

Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako.

Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako.

Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha.

Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha.

Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo.

Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli.

‘‘MIMI NDIMI BWANA YAHUVEH:

hilo ndilo JINA LANGU! Sitampa mwingine UTUKUFU WANGU

wala sanamu SIFA ZANGU.”

-Isaya 42:8

(Unabii 105)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo kwa wale wanaokejeli:

“Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA YAHUVEH juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

—2 Mambo ya Nyakati 36:16

Elisheva: Sawa Ezra. Ningependa Ezra uombe katika ndimi tena.

[Ezra azungumza katika Ndimi Takatifu.]

Elisheva: Je, Wataka [YAH] tuseme nini? Tafadhali nipe upako.

Ninakemea na kumfunga shetani mbali nami katika JINA la YAHUSHUA MASIHI. Hallelu YAH, hallelu YAH! [Ezra & Elisheva wanaomba katika Ndimi Takatifu.] O BABA YAHUVEH guza mdomo wangu! Guza mdomo wangu YAHUSHUA! Guza ulimi wangu IMMAYAH!

[“Rungu” ya ndimi Takatifu laanza kutoka…]

Unabii 129 Unaanza:

Julai 5, 2016

Nendeni mbali NAMI enyi manabii bandia! Enyi Mitume bandia! Enyi bibi arusi bandia! Nimeinua Huduma hii! Nimeinua Hudama hii ya Amightywind kufunua mahali ambapo magugu na mbwa mwitu wapo!

Ninakupa upako mkuu zaidi Ezra na wewe Elisheva kufanya yale ambayo yule aliyekataliwa Paul Hellem alikataa kufanya! Ninawapa upako mkuu kuwafukuza wale walio na roho za yezebeli-wanaokuja wakitafuta kuharibu Huduma hii ambayo ni ya MIMI, YAHUVEH, ambayo ni ya MIMI, YAHUSHUA na ni ya IMMAYAH! Kwa kuwa jina la Elisheva halipo pale!

Ninawapa upako kuwafukuza mbwa mwitu – Ninawapa upako nyinyi kuzirarua nyuso za wale wanaokuja kama kondoo au mwanakondoo na kumbe wao ni mbwa mwitu hatari-Ezra, leo hii ambapo hakutaka kuzungumza Neno lolote juu ya hawa wachungaji bandia, hawa manabii bandia, wale ambao walinitumikia MIMI hapo mbeleni (kama Elisheva anavyosema kuwa hapo mbeleni walikuwa wanatembea katika Utakatifu mbele YANGU).

Ndio! Ndio! Rick Joyner, Joyce Meyer, Marylin Hickey, orodha Niliyowapa katika Unabii kabla ya Unabii [91, 92, 93]!- katika Unabii. Lakini ilikuwa maamuzi yao kuuza Nilichowapa bure. Hauwezi kunitumikia MIMI, YAHUVEH na kutumikia pesa pia! Hauwezi kuwa na mabwana wawili (Mathayo 6:24). Kwa kuwa utamchukia mmoja na kumpenda mwingine!

Mathayo 6:24

Hakuna mtu ye yote awezaye kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa ama atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine, au atashikamana sana na huyu na kumdharau huyu mwingine. Ninyi hamwezi kumtumikia Mungu na mali.

Ni wangapi wameniacha? Kwa sababu tu ya umaarufu na bahati?

Na Ninakupa upako Ezra. Elisheva amekuwa akiyafanya haya kwa miaka mingi-kwa miaka 21 pekee yake kwenye Intaneti. Na haya hata hatujahesabu kutoka alipokuwa katika ujana wakati Nilimtuma kwenye makanisa kuziondoa barakoa nyusoni mwa hawa wachungaji. Na wakaogopa kuwa Nabii wa kweli alikuwa pale. Lakini sasa Ezra, hawezi kuwa pekee yake.

Ninakupa upako leo hii mwana WANGU Ninapokuambia na kukuonyesha kuwa yule ambaye hapo awali alifuata ukweli ZANGU-na hakuenda kando ya njia kushoto wala kulia lakini alibaki kwenye njia panda, ambapo mtazamo ulikuwa YAHUSHUA (hata kama wanamuita na jina ‘Yesu Kristo’), lakini macho yao yakatoka kwenye lengo-macho yao yakatoka kwenye KIPENZI CHAO CHA KWANZA, MIMI, YAHUSHUA na wakaweka macho yao kwa umaarufu na bahati.

Ninakuambia mwana WANGU.

Yeye hawezi kusimama pekee yake kwa haya. Hauwezi kufunga mdomo wako na kusema, “Sitasema haya.” Haiwezi kuwa tu kutoka kwa mdomo wake pekee. Ninawahitaji wote wawili. Kuwafunua mbwa mwitu! Kuwafukuza na Rungu ya Ghadhabu YANGU! Au watawala wanakondoo WANGU wadogo na kondoo ambao Ninawatuma kwa Huduma hii… Ninakuhitaji mwana WANGU kufanya haya ambayo hautaki kufanya.

Lakini ni kwa nini Ninakuonyesha kama sio kwa kuwaonya wengine? Kumbuka Ezra kuwa kulikuwa na wakati ulipokuja KWANGU na watu walikuumiza [vibaya] na kukuweka vidonda [vibaya]. Na wakafikiria kuwa ilikuwa haki yao. Walisema kuwa wanazungumza kwa niaba YANGU.

O lakini Ezra! Kulikuwa na wakati ulichukua tu vidonda hivyo na kukaa tu kimya na kuenda zako na machozi machoni mwako. Na ukasema, “Wapi upendo? Wapi upendo? Wapi upendo kwenye mwili huu unaofaa kuwa YAHUSHUA, ‘YESU KRISTO’?”

Lakini Ezra! Nisikilize MIMI. Lazima Nihakikishe wewe na Elisheva mmejifunza funzo hili vizuri. Watu hawa hawakunizungumzia MIMI. Haya hayakuwa Maneno YANGU mliyoyasikia. Walikuwa na umbo la utakatifu, lakini hamna utakatifu ndani yao (2 Timotheo 3:5). Siwezi kuwaumiza hivyo! Siwezi kuwararua hivyo na maneno. MIMI siyafanyi haya.

Lakini sasa Ezra, haya hayatafanyika tena. Na Elisheva haya hayatafanyika tena. Kwa kuwa Nimeiweka kipaji cha uso wenu kama jiwe (Ezekieli 3:9; Isaya 50:7)!

Ezekieli 3:9,

Kama vile almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume ndivyo nilivyokifanya kipaji cha uso wako. Usiwaogope wala usiwahofu, wajapokuwa ni nyumba ya kuasi.

Isaya 50:7

Kwa sababu BWANA Mwenyezi

ananisaidia, sitatahayarika. Kwa hiyo nimekaza uso wangu kama jiwe la

gumegume, nami ninajua sitaaibika.

MIMI Ninatumia chuma kunoa chuma (Mithali 27:17).

Mithali 27:17

Kama vile chuma kinoavyo chuma,

ndivyo mtu amnoavyo mwenzake.

Unapojua maneno haya sio ya KWANGU-na kuwa yana nia ya kukumaliza na wale ambao wameletwa kwa Huduma hii, sanasana uongozi-utatumia Meneno YANGU ya kukemea! Hakutakuwepo na machozi tena kwa sababu ya hawa waliokataliwa!

Ezra hautaenda vivyo hivyo tu kimya. Na Elisheva hakuna yeyote kati ya nyinyi wawili atasema kuwa-au hata kufikiria haya maneno yametoka KWANGU, MIMI, YAHUSHUA. Hakutakuwa tena na machozi kwa macho yenu! Mtatambua kuwa MIMI, YAHUSHUA, huchukua Rungu YANGU. Na MIMI, YAHUSHUA, Nalinda kondoo na wanakondoo. Na huo ndio upako ambao NYINYI WAWILI mtasimama [nayo]! Sio mmoja tu.

Ninapokupa onyo, Sijali huyu mtu alikuaje hapo awali! Je, hamjajifunza funzo kutoka kwa Paul Hellem! Hamjajifunza funzo kutoka kwa Yudasi!-ambao hapo awali alikuwa mmoja wa wanafunzi WANGU?

Je, Mnafikria ni kwa nini Niliruhusu haya kufanyika? Kuonyesha kuwa ni MIMI, YAHUSHUA Niliyeleta upanga wa kugawa!

Ni MIMI, YAHUSHUA Niliyewaonya [na maswali], “Ni nani mama yangu? Ni nani baba yangu? Ni nani dada yangu? Ni nani ndugu yangu?” (ona Mathayo 12:48-50; Luka 8:21).

Ni MIMI, YAHUSHUA!

Hauwezi kuleta mtu [Mtakatifu] katika umoja na shetani! Hauwezi kuheshimu kile ambalo siheshimu! Mnanisikia? Hauwezi kuheshimu kile ambacho hakina heshima! Hawasikizi Neno LANGU! Hauwezi kuambia watoto waungane na kile Nilichogawa.

Huu ndio Ujumbe Ninayowapa.

MIMI Ninagawa ngano kutoka kwa magugu! Je, Si panasema “Maadui zako wabaya zaidi watapatikana ndani ya nyumba zenu” (ona Mathayo 10:36)?

Mathayo 10:36

Nao adui za mtu watakuwa ni wale watu wa nyumbani kwake.

Sikiliza! Sikiliza! Sikiliza! Nasema tena, sikiliza!

Ninawatenga mabwana na mabibi, Ninawatenga watoto kutoka kwa mama zao na baba zao-kwa usalama wa nafsi zao, ninawatenga-kama Nilivyosema Nitafanya (Mathayo 10:34-38; Luka 12:49-53). Sio tofauti na “Waoto wa Israeli” [B’nei Israel] walivyoambiwa kujitenga (Walawi 20:23-26). Ilibidi watengwe! Sikutaka wachafuke.

Mathayo 10:34

“Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga.

Luka 12:51

Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani? La, nawaamba sivyo, nimekuja kuleta mafarakano. Kuanzia sasa, kutakuwa na watu watano katika nyumba moja, watatu dhidi ya wawili na wawili dhidi ya watatu. Watafarakana baba dhidi ya mwanawe na mwana dhidi ya babaye, mama dhidi ya bintiye na binti dhidi ya mamaye, mama mkwe dhidi ya mkwewe. Naye mkwe dhidi ya mama mkwe wake.”

Kunakuja wakati huu kwa haraka! Familia, kama sitazigawa, watasiliti wenzao-mmoja akiwa wa KWANGU na mwingine akiwa dhidi YANGU, mmoja anapotaka kutembea katika Utakatifu na mwingine anapotaka kutembea katika njia ya dunia. Na Ninazungumzia ‘familia’!

Kunakuja wakati huu kwa haraka! Mama na baba watauza watoto wao kama Yudasi alivyonifanyia MIMI-kwa sababu ya hela: Watawashtaki watoto wao! Watoto watawashtaki wazazi wao! Bwana atashtaki bibi! Na Ninazungumza kuwa watawashtaki [Watu Watakatifu] watashtakiwa-kwa maserikali!

Ninagawa kwa binafsi yao. MSIUNGANE na yale Ninayogawa! Kueni makini ni ndoa gani mnazoziombea kurejeshwa! Kueni makini watoto WANGU!

Nimeisema mara moja na Ninaisema tena!

Ni nani mama na ni nani baba? Ni wale wanaofanya mapenzi ya BABA YAHUVEH-ni wale wanaopiga magoti KWANGU na wale wanaotii na kuniita MIMI “BWANA MUNGU MWENYEZI”: Huyu ndiye mama. Huyu ndiye baba. Huyu ndiye dada. Huyu ndiye ndugu.

Ni nani Bibi Arusi wa kweli wa, MIMI YAHUSHUA? Ni wale wanaofanya mapenzi ya BABA ALIYE MBINGUNI & MIMI, YAHUSHUA. La sivyo, wao ni bibi arusi bandia. Na bibi arusi bandia ni akina nani? Ni bibi arusi wa shetani!

Kwa hivyo kueni makini watoto WANGU. Kueni makini. Msiwatetee mbwa mwitu-hata kama hapo awali walifanana kama kondoo au mwanakondoo.

Kuwa makini Ezra. Kuwa makini Elisheva. Na Ninapowaambia kuinua Rungu ya Ghadhabu ya YAH, msiangalie kule ilikotumwa. Msiwahi kuangalia [kule] na huruma. Kwa kuwa kuna wale watakaotambua [kwa njia ngumu]-kwa sababu wachungaji wao hawatawaambia sasa.

Usitabiri tu kwa masikio yanayowasha ukitaka kusema tu yale ambayo watu wanataka kusikia, unawapapasa vichwani na kuwakumbatia na kuwarudisha kwao na maneno ‘mazuri’ ambayo hayatawafikisha Mbinguni. Kile ambacho kimefanyika ni umepumzisha mwili tu!

HAPANA! Manabii WANGU wa kweli wanaotumiwa katika Nyakati hizi za mwisho na sasa Nitawahukumu wale WANAOJIDAI KUWA WANGU-NA KUMBE WAO NI ‘MANABII WANAOPENDA PESA’!

Je, Mnanisikia MIMI? Je, Mnanisikia MIMI?

Kim Clement! Unalipia na afya yako! Wewe ni mmoja wao! Hapo awali ulianza na MIMI Nilikuwa MTAZAMO wako na KIPENZI chako. Alafu macho yako yakaangukia umaarufu na bahati! Sasa unalipa gharama! Ulitabiri uongo!

Na sio yeye pekee. Ole kwa hawa ‘manabii wanaopenda pesa’!

O ndio! Watasimama kwenye laini ndio wapate ‘unabii’ kutoka kwako. O ndio! Umekaribishwa-na dunia-kuyazungumza ‘maneno mazuri’ wanayotaka kuyasikia. Lakini ‘ole-kwa nabii-katika macho ya dunia hii, atakaowakemea kama Manabii wa Kale, kama Ninavyomtumia Elisheva & Ezra.

Mmeamrishwa! Msiogope kuumiza mwili! Kwa kuwa haya hayatawalinda na haya hayatawaonya kondoo WANGU na wanakondoo WANGU.

Nimewapa upako! Na Nimeweka Maneno YANGU midomoni mwenu! Ninawalinda kondoo na wanakondoo wangu! Na ni huduma ngapi ambazo ziko tayari? Kuteswa na kuumizwa? Kufanya yale ambayo MIMI [YAH] Nafanya?

O hapana! Ni rahisi sana kuwa na huduma mahali maneno ya upendo inazungumzwa, ambapo maziwa tu yanapewa. O! Nina Huduma chache sana! )! Je, Ni Manabii wagani & Mitume wagani Ninao-walio tayari kulipa gharama?

Si Nilisema, “Mtumishi sio mkubwa zaidi kushinda Bwana” (Yohana 13:16; 15:20)? Wanachokufanyia, tayari wamenifanyia MIMI. Unawaonya. Hawasikilizi.

Elisheva, kutoka umri mchanga ulinipa maisha yako. Na ukahubiri kutoka huo wakati uliponiuliza Niingie moyoni MWAKO. Nimekuwa KIPENZI chako. MIMI ni KIPENZI chako JUU YA YOTE. Na Nilikutuma katika makanisa haya. Na waliogopa walichokiona. Wachungaji hawa waliona Uso WANGU juu yako na wakajua kuwa walikuwa karibu na nabii wa kweli. Na kwa hivyo uliteswa. Lakini bado Nilikutumia-kwa kuwa hakuna hata wakati mmoja ambapo mtu hakuwekwa huru.

Sasa Ninawatumia katika Huduma ya Kimataifa! Ndio Nitawabariki! Ndio Nimewabariki!-kifedha, lakini msinisaliti.

Sio lazima mfikirie au kushangaa-Ninapotaja majina haya-ni kwa binafsi yao. Kuwakumbusha kurudi kwa KIPENZI chao cha KWANZA! Je, Ni wangapi wamepoteza KIPENZI chao cha KWANZA? Na ni wangapi wanasema kuwa MIMI bado ni KIPENZI chao cha KWANZA na kumbe wako mbali, mbali, mbali NAMI?

Kwa hivyo ndio, wasamehe. Lakini fanya haya. Waache Mikononi MWANGU. Kwa Kumbukeni katika Kitabu cha Ufunuo wa Yohana Ghadhabu itakapokuja, ni kutoka kwa BABA YAH Anayekaa kwenye Kiti cha Enzi lakini pia-wanahitaji kuwa na hofu ya GHADHABU ya MWANAKONDOO (Mithali 9:10; Ufunuo wa Yohana 6:16; Zaburi 2:12)!

Mithali 9:10

“Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima

na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.

Ufunuo wa Yohana 6:16

Wakaiita milima na miamba wakisema, “Tuangukieni, mkatufiche na uso Wake Yeye aketiye kwenye kiti cha enzi na mkatuepushe na ghadhabu ya Mwana-Kondoo, kwa maana siku ile kuu ya ghadhabu yao imewadia. Je, ni nani awezaye kusimama?’’

Zaburi 2:12

Mbusu Mwana, asije akakasirika nawe

ukaangamizwa katika njia yako,

kwa maana hasira yake inaweza kuwaka

ghafula.

Heri wote wanaomkimbilia.

Hakuna yeyote-wachache sana wanaotaka kufunza kuwa MIMI, YAHUSHUA Nitakuja tena lakini haitakuwa tu kwa upendo! Haitakuwa tu kwa huruma! Lakini itakuwa NA GHADHABU YA MWANAKONDOO!

Na watalia na kusema, “Milima tuangukie! Tufiche kwa YULE AKAAYE kwenye Kiti cha Enzi na kutoka kwa Ghadhabu ya MWANAKONDOO!” (ona Luka 23:30; Ufunuo wa Yohana 6:16). Ni nani atakayefunza haya-kama sio nyinyi wawili? O ndio Ninao wengine lakini ni wachache sana. Ni nani atakayefunza haya? Ni nani atayafunza haya-Nisipotumia Huduma hii-ni nani atakayeonya?

O maadui wa YAH! Mtapeperushwa-whoosh! [YAHUSHUA Anafanya sauti ya upepo ukivumia maadui]-kama uchafu upeponi!

Zaburi 1:4

Sivyo walivyo waovu!

Wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

Nina sababu nyingine Ninaita Huduma hii, “Amightywind!” kwa kuwa sio kwa sababu tu ya Chumba cha Juu (Mitume 2). Ni kwa sababu Nimeipa upako kuwapeperusha maaudui waliokataliwa-whoosh! [YAHUSHUA Anafanya sauti kama ya upepo]-uchafu upeponi!

Ni kwa sababu kuna Upako juu ya Huduma hii imekuwa ikikua kupita miaka 21-na ilizalishwa hata kabla ya intaneti kuwepo-lakini sasa [ni] ya Upako ya nyinyi wawili pamoja!

Utakapoanza kutembea katika Upako mkuu na kila mtu kuona upendo ambao mlio nao kwa mwingine ambayo inaongezea Upako-na Ninawaambia haya-kila mtu atakayepokea Huduma hii na Unabii hizi kwa baraka, kila mtu atakayeinua uongozi huu na maombi ya baraka na kuibariki Huduma hii, kuifunika Huduma hii na maombi ya usalama-Upako wao ni kama hivi, whoosh [YAHUSHUA Anafanya sauti ya upepo], na itawajia kote duniani!

Hii ni Amightywind!

Kwa hivyo mnaona watoto WANGU hii sio Huduma ambayo huenda kwa lugha ya Kiiengereza tu. Itakuwa katika kila lugha na ndimi. Na tayari ishaanza “katika ‘zaidi’ ya lugha 28.” Na Mimi husema kila wakati kuwa hata hamuelewi (kwa sababu hawawaandikii): Unabii hizi zimewekwa katika lugha zaidi [kushinda] yale ambayo waweza kuelewa sasa. Kwa kuwa hamna yeyote, wasema, anayetafsiri katika lugha hizi bado.

Hata sasa baada ya Neno hili kuzungumzwa wengi watakuja kwako na kusema, “Ninataka kusaidia kutafsiri Unabii hizi. Ninataka kuwafikia watu wangu. Ninataka kufikia nchi yangu. Ninataka kufikia nyumbani kwangu. Ninataka kufikia kisiwa changu. Ninataka kuwafikia na sioni lugha inayonizungumzia mimi. Hakuna lugha inayozungumzia watu wangu.”

Kwa hivyo watoto WANGU haya ndio Maneno Ninayo ya kusema. Kumbukeni MIMI, YAHUSHUA Nilileta upanga wa kugawa, na sio tofauti hata sasa kama ilivyokuwa na Watoto wa Israeli. Ninatenga wale ambao ni watakatifu na wale wasio Watakatifu. Ninatenga ngano kutoka kwa magugu. Ninatenga wale waliooshwa katika DAMU YANGU ILIYOMWAGWA na waliokataliwa.

Jihadharini nyinyi mlio baridi! Nyinyi mnaonikejeli! Nyinyi wafuasi wa kishetani, mliozaliwa na kijiko cha fedha mdomoni! Sikilizeni Nabii huyu akizungumza. Mmesoma Unabii. Na mnakejeli! Kwa kuwa mnasema, “Mimi sio moto na wala sio vuguvugu. Sisi ni walio baridi. Nyoyo zetu ni za mawe.”

Wafuasi wa kishetani husoma Maandiko. Wafuasi wa kishetani huja kwa umbo nyingi. Wafuasi wa kishetani watachukua Unabii na, kwa njia yao, fanya vitu vitendeke kwa binafsi yao wenyewe. Na hakuna lolote linalowaelekeza kwa wokovu.

Ni kwa uharibifu-wanataka kuleta vurugu. Ni kwa uharibifu-hata watoto WANGU waliooshwa katika DAMU YANGU, wanaobeba USHUHUDA WANGU (Zaburi 94:21; Ufunuo wa Yohana 12:11). Na wanataka uharibifu wao!-kama Nilivyoonya tena katika Unabii hizi-jihadharini na kila serikali iliyomo duniani humu. Kwa kuwa Ninawaambia haya, hawaniwakilishi MIMI.

Zaburi 94:21

Huungana kuwashambulia wenye haki, kuwahukumu kufa wasio na hatia.

Ufunuo wa Yohana 12:11

Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo na kwa neno la ushuhuda wao. Wala wao hawakuyapenda maisha yao hata kufa.

Jihadharini, jihadharini kwa sababu ni mtego wa panya-na wanaoweka ile jibini pale, wakimchanganya yule panya kuja kwenye mtego huo-kukata kichwa chake.

Lakini msiogope watoto WANGU! Msiogope!

Msiogope Watoto, Bibi Arusi, Wachaguliwa & Wateule WANGU mnapoona hivi vitu vikitendeka, hizi njia zote za kuwanyanganya uhuru wenu. Msiogope! Msiogope watoto WANGU! Nitawaonyesha. Nitawaonyesha njia za usalama ambazo siwezi kuzungumza sasa. Na Nitawacheka hawa maadui! Kwa kuwa wanafikiria kuwa wanaweza kunishinda MIMI MUUMBAJI!

Kwa hivyo haya ndiyo Maneno Ninayo ya kusema. Nimeipa Huduma hii upako katika njia mpya. Na haya ni kuwafunua mbwa mwitu waliojivalia nguo za kondoo. Na haya ni kuwafunua hawa mbwa mwitu hatari-ambao hata hawajaribu hata kuvaa barakoa ya kondoo. Watakaposikia Neno hili, watasaga meno yao kwa hasira kwa sababu watajua kuwa wamefunuliwa! Na Ninakutumia tena mara nyingine kuwakumbusha yale ambayo makanisa hayataki kuwafunza. Na MIMI, YAHUSHUA Nilileta upanga wa kugawa. Na Nimewaambia ni nani mnaweza kuwaamini na ni wale tu wanaonitii MIMI!

Hakuna Bibi Arusi WANGU yeyote ambaye atatoka ulimwenguni huku katika Kunyakuliwa kama hawatachagua kuniweka MIMI kwanza katika maisha yao na upendo wao. Na inamaanisha haya: kujitenga kabisa na wale Ninaowaita waliokataliwa. Lazima wanililie MIMI na kuniuliza MIMI kuwaokoa msifungwe nira na wasioamini (2 Wakorintho 6:14-18) hata ikiwa biashara, hata ikiwa familia-lazima wanililie MIMI na kusema, “YAHUSHUA nitenge mimi, hata kama ni kutoka kwa wale wanaosema wananipenda.”

2 Wakorintho 6:14-18

14Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? 15Kuna mapatano gani kati ya Kristo na Belialia? Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini? 16Kuna mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema : ‘‘Nitakaa pamoja nao na kutembea katikati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.’’ 17‘‘Kwa hiyo tokeni miongoni mwao, mkatengwe nao, asema Bwana. Msiguse kitu cho chote kilicho najisi, Nami nitawakaribisha.’’ 18‘‘Mimi nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa wanangu na binti zangu, asema Bwana Mwenyezi.’’

Lazima waelewe jinsi hali hii ilivyo hatari kwa bwana na bibi. Tena Ninasema, Nililieni MIMI kabla wakati haujapita.

Na kama Nilivyomuokoa Elisheva [kutoka kwa mmoja]-ambaye alisema ombi la wokovu na sasa nimembandika kama aliyekataliwa, (kwa kuwa hakuweza kutembea tena kama mtoto na hakukuwa na tunda linakua kwenye mzabibu kwa miaka mingi)-na Neno LANGU linasema nini?-Nitawatoa kwenye mzabibu (Yohana 15:2; Mathayo 3:10; 7:19). Wasipokua, tunda huharibika.

Kwa hivyo chungeni tunda lenu! Kueni waangaliaji wa tunda! Sio wewe unaohukumu lakini Ninakupa uwezo wa kubainisha roho-kuangalia matunda ya wengine ili ujue kama kweli ni ya KWANGU, wanaonizungumzia MIMI.

Kwa hivyo jihadharini ni akina nani mnakutana nao na kuomba. Msiruhusu tu yeyote kuandamana pamoja katika maombi [nanyi]-kama huelewi ile roho iliyomo ndani ya yule mwingine ni ya KWANGU kweli-msiguse mikono yao. Kwa kuwa kutakuwa na usambazaji wa mapepo.

Kueni makini watoto WANGU! Sio yote ambayo ipo inavyokaa. Wengi hujiita “Wakristo” na Nimesema Nendeni mbali NAMI enyi wafanyikazi wa maovu! Jihadharini watoto WANGU!

Na ndio sababu siku hii, Ezra & Elisheva, Nimewapa karama zaidi ya utambuzi, ya ujasiri, kushinda yale ambayo mmekuwa nayo hapo awali. Na lazima muweke nyuso zenu na kipaji kama jiwe. Na mlisema, “Sitakoma. Kwa kuwa ninaogopa kumkasirisha BABA YAHUVEH & YAHUSHUA kushinda ninavyoogopa kuwakasirisha mwanamke au mwanamume yeyote.”

Na kwa niaba za nafsi zao, mtazungumza yale ambayo Nimewaambia mseme. Mtafanya Nilichowaambia mfanye, kwa niaba ya Ufalme wa Mbinguni. Kwa kuwa Ninapenda sana hata nikawakasirisha. Kamwe Kumbukeni haya-o mwanamke Mtakatifu na o mwanamume Mtakatifu, wanaowachukia wanajua tu kuchukia. Waliokataliwa watachukia yale ambayo ni Takatifu na watakaribia-kama roho ya yezebeli, kama tu Hamani-watakaribia na kushambulia. Lakini Nimewapa silaha kutoka Ufalme wa Mbinguni kupigana katika JINA LANGU.

Haya ndio Maneno Ninayo ya kusema kama mnavyokusanyika NAMI leo hii.

Ishara, maajabu na miujiza kila siku-tayari imewafuata kwa sababu mnafuata MIMI, YAHUSHUA na BABA yenu YAHUVEH. SHKHINYAH GLORY Amewaonyesha katika njia-hata sasa-haya hayafai kuwashangaza. Kwa kuwa kila siku Ninawapa kipimo kipya cha imani mnapoona ishara, maajabu na miujiza zaidi.

Zingine mtatoa. Zingine hamtatoa. Zingine ni za kibinafsi: inafaa kuwa tu ya nyinyi wawili. Zingine ni karama Ninawapa kupeana kwa mwingine.

Mtaona, hata kama hamuelewi sasa.

Lakini kumbukeni maelezo ya muziki-haya ni funzo kwenu: jinsi upendo wenu ulivyo muhimu, kwa yule mwingine, kwa sababu sio tu upendo wa binadamu. Imechanganywa, mchanganyo wa MIMI, YAHUSHUA, wa BABA YAHUVEH na wa IMMAYAH, SHKHINYAH GLORY.

Na Ninawaambia haya. Watu wataona na watatiwa moyo na maneno na upendo Nitakayoonyesha kati ya nyinyi wawili. Mnavyocheka pamoja! Mnavyofunzana! Upako! Upako! Upako!-unakuja juu ya watu katika njia mpya!

Na wakati neno hili litatolewa, mtasikia na watawajibu. Na wale walio na karama ya Kutabiri waliojificha wataandika na kukutabiria wakijua Watabarikiwa wanapokupa baraka hii.

Haya ndio Ninayo ya kusema. Sasa Nendeni kwa amani.

Kwa tena, Elisheva & Ezra, mnapokusanyika pamoja na kuinua JINA LANGU na Kathrynyah kando yako-na wote ambao hata sasa, katika kona nne za ulimwengu, Ninao mabaki (na wanajua Amightywind: wanaweza kuwa hawajui jina la Huduma, lakini wanajua kuwa kuna Huduma inayohitaji usalama spesheli) na hata katika ndimi zao takatifu wanaita jina lako, ingawa hata hawajui-Nimewafunika mwana na binti.

Nimewafunika sio nyinyi tu [na] wale wanaokuja kwenye Huduma hii kupitia intaneti, kupitia Vitabu, kupitia Unabii, lakini Nimewafunika mwana na binti YANGU katika maombi na kwa uhakika nyinyi huwa chini ya usalama wa mabawa ya BABA YAHUVEH. Kwa kuwa Zaburi 91, mnaiishi kila siku. Nimewafunika na jeshi la malaika WANGU mashujaa.

Nimewafunika na kwa hivyo hamna haja ya kuogopa.

Mmefunikwa-sanasana na DAMU YANGU ILIYOMWAGWA pale Kalivari. Mmefunikwa- mnapochukua maombi haya katika JINA LANGU, YAHUSHUA.

Wote wanaonisikiliza na wote watakaosoma Unabii huu mpya na Ninamaanisha wale watakaposikia Sauti YANGU kama Nilivyozungumza kupitia Elisheva, Upepo Mpya wa Uamsho-[YAHUSHUA Anavuma Pumzi LAKE la Uamsho]-unavuma juu yako kama Upako wa RUACH HA HODESH sasa umeongezeka juu yako.

Na utatembea katika baraka mpya. Utatembea na imani mpya unapotambua kuwa MIMI sio mbaguaji kwa watu (Matendo ya Mitume 10:34). Ninataka kuwasiliana nanyi kama Ninavyofanya na Ezra & Elisheva.

Amini tu! Kuwa na imani tu! Na utatembea katika ishara, maajabu na miujiza-kama, kama utanitii MIMI, YAHUSHUA, kama unamueka BABA YAHUVEH kwanza katika maisha yako na upendo wako na kutii na kutubu na kutambua kuwa shetani ana bandia. Msifukuze ishara, maajabu na miujiza! Badala ya haya, MIMI, YAHUSHUA Nitazileta kwenu.

Mwisho wa Neno.

Elisheva: Whew! Asante! Asante! Asante! Hallelu YAH! BABA YAHUVEH asante! Haiya mpendwa.

Ezra: Hallelu YAH! Asante BABA YAHUVEH, asante YAHUSHUA, asante IMMAYAH kwa neno hili ambayo imekuja kwetu BABA YAHUVEH. Tunakushukuru! Tunakupa utukufu! Tunakupa utukufu YAHUSHUA! Tunakupa utukufu IMMAYAH SHKHINYAH GLORY! Tunainua JINA LAKO juu ya vitu vyote. Na tunakutii WEWE pekee-katika JINA la YAHUSHUA-Tunakubariki! Tunakubariki! Tunakubariki!

Elisheva: Oh ndio.

Ezra: Asante! Asante! Asante!

Elisheva: Asante kwa baraka hii. Asante kwa mpendwa wangu Ezra! Asante! Kwa kuwa ninamuona mwanamume huyu Mtakatifu na tangu aje maishani mwangu ambayo ni miezi 4 tangu Julai 7, [2016]-

BABA YAHUVEH [sasa] hata kabla ya kumbusho la 4 ya mwezi-haya ni ya ajabu! Na upako! Kila siku! Watu lazima muelewe! Angalieni nambari za Unabii ambazo zimewekwa mbele ya dunia na ingawa kulikuwa na elfu ya Maelfu-na Kathrynyah na wengine ni Mashahidi-hazikuwa zimewekwa mbele ya dunia kwa hivyo tieni maanani tu yale ambayo yalikuwa yamewekwa tayari.

Lakini tangu huyu mwanamume Mtakatifu wa YAH ninayemthamini [yupo hapa]-anayeshikilia moyo wangu na nafsi na ninampenda zaidi ya mtu yeyote atakayewahi kujua (kwa kuwa ni BABA YAHUVEH, YAHUSHUA & IMMAYAH pekee walio kwanza katika maisha yangu na upendo lakini akaja mwanamume huyu) kwa sababu unapokuwa na Upako sawa na una mpenzi wa kweli: Utakua-na ninataka kusema kuwa-katika hii miezi 4 hivi karibuni, o! Kila siku, nafikiria kuna Unabii mpya!

Na sio tu kwa sisi pekee! Inapaswa kuwa baraka kwa nyinyi wote mliongoja sana-mliongoja sana. Na sasa oneni, BABA ameweka mbele yako meza. Hatuwezi kutengeneza video hizi kwa haraka zaidi. Hatuwezi kutafsiri hizi Unabii kwa haraka zaidi. Tunayashughulikia haya, lakini BABA YAHUVEH Anasema itabidi tukimbie ili tuweze kusonga kwa mwendo ambao YEYE Anafanya vitu kwa Huduma hii na yote haya yalianza Machi 7, 2016.

Na kwa hivyo ninawauliza mumueke Ezra katika maombi spesheli na ninawauliza mniweke kwa maombi yenu spesheli kwa sababu vita ni vikali, vita dhidi ya mazuri na maovu. Kwa hivyo YAHUSHUA Awabariki wote! Tunawapenda! Ezra una ya kusema kwa watu? Una kitu kingine cha kuongezea?

Ezra: Ndio.

Elisheva: Una yapi ya kusema?

Ezra: Ndio, ninataka kukushukuru kwa kutufunika kwa maombi na kungoja BWANA kusonga ndani yao na kutofukuza ishara, maajabu na miujiza lakini kwa kumfukuza YULE AMBAYE anazipeana!

Elisheva: Amina!

Ezra: Basi watafuata vitu vyote ambavyo YEYE Amewaahidi. Kueni waaminifu, watiifu na kila wakati kuomba na kumtafuta YEYE na kila kitu ulicho nacho. Haya ndiyo ninayo ya kusema.

Elisheva: Na amina kubwa kwa hayo!

Mwisho wa Rekodi.

Imezungumzwa, imeandikwa katika JINA LA YAHUSHUA,

Julai 5, 2016

Mtume, Nabii Elisheva Eliyahu,

Imezungumzwa wakati wa maombi na mpendwa Nabii Ezra kutoka Israeli

Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred