Unabii 128
Unabii wa Shavu’ot 2016
Mbinguni Wanasherehekea Uongozi Mpya wa Amightywind
Imeandikwa/Imezungumzwa katika Upako wa ROHO MTAKATIFU (RUACH HA KODESH)
Kupitia Mtume & Nabii Elisheva Eliyahu
Shavu’ot/Pentekoste 2016 – 12 Juni 2016
Unabii huu una MAJINA ya KIEBRANIA ya MUNGU:
YAH/YAHU יה ni JINA TAKATIFU la MUNGU, kama vile “Alleluia” au “Hallelu YAH” הללו–יה ambayo humaanisha “Msifu YAH”: YAHUVEH/YAHWEH י-ה-ו-ה MUNGU BABA; YAHUSHUA/YAHSHUA יהושוע MWANA WA PEKEE WA MUNGU—(HA MASHIACH המשיח inamaanisha “MASIHI”; ELOHIM אלוהים INAMAANISHA “MUNGU.”)
Ufunuo wa “SH’KHINYAH GLORY” שכניה תפארה —kama JINA la KIBINAFSI la RUACH HA KODESH רוח הקדש, (katika Kiiengereza “ROHO MTAKATIFU”) —upo kwenye tovuti hii.
(HA SH’KHINAH {SHEKINAH} ni Kiebrania inamaanisha UWEPO WA MUNGU.)
Zaidi ya hayo, ABBA YAH אבא יה humaanisha “BABA YAH” na IMMA YAH אמא יה humaanisha “MAMA YAH.”
Maandiko yaliyotajwa yametoka KJV au NKJV, isipokuwa pale palipotajwa vinginevyo. Bonyeza kwa upande wa kulia zile nambari za maelezo ya chini (footnote) kufungua ukurasa mwingine.
* * * * * * *
Maneno ya YAHUVEH kwa Elisheva Aliyosema yaongezwe mbele ya Unabii zote:
Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako.
Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako.
Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha.
Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo.
Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli.
‘‘Mimi ndimi BWANA YAHUVEH: hilo ndilo JINA LANGU! Sitampa mwingine UTUKUFU WANGU, wala sanamu SIFA ZANGU.” Isaya 42:8
(Unabii 105)
Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kutoka Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati:
“Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”
—2 Mambo ya Nyakati 36:16
* * * * * * *
Unabii Unaanza:
Shavu’ot/Pentekoste 2016 – 12 Juni 2016
Ole kwa yeyote atakayethubutu kujaribu kuwadhuru— hawa wawili walio na upako. Mtajuta kuzaliwa kwenu. Msiwaguse masihi WANGU, msiwadhuru Manabii WANGU (Zaburi 105:15; 1 Mambo ya Nyakati 16:22). Ingekuwa ni heri kwenu kama MIMI, BABA YAHUVEH, Ningerarua ndimi zenu!
Vita vimekuwa vikizidi! Hii sio huduma ya kawaida! Je, kwani mwafikiria kuwa shetani hajui haya?-amepoteza baadhi ya majenerali wake wakuu!-amepoteza baadhi ya makamanda wake wakuu!
Hili sio tu tangazo la kiongozi wa kiume- yeye (shetani) ilimbidi kupigana kwa viwango viwili: ilimbidi apigane na Elisheva katika njia ambazo hajui; na ilimbidi apigane na wale ambao waliofanya miujiza hii iwe- YDS ambao wanaweka upendo na kazi na upako. Na hii ndiyo sababu Nilibariki kila kitu walichogusa.
Lakini yeye ni ‘mku-‘ (“mkuu wa ulimwengu huu,” Yohana 12:31; 14:30; 16:11)-shetani ni mtawala na nguvu na mfalme wa anga (Waefeso 2:2) kwa hivyo Ilibidi YDS wapigane naye kule. Alafu kuna ‘Mfupa wa Mfupa’: alafu kuna wewe Ezra na wewe Elisheva ambaye Nilitabiri kitambo-ingawa hamkujua.
Na leo ni siku ya Ushindi! Siku hii ya Shavu’ot (Pentecost) ni siku ya Ushindi! Kwa kuwa “Goliathi” ataanguka! Na ninazungumzia Goliathi zaidi ya mmoja!
Leo ni siku ya Ushindi! Na itatambulika vivyo hivyo. Na sio tu sherehe ya siku moja. Kwa muda ambao Huduma ya Amightywind itakuwa kwenye intaneti itakumbuka siku hii-kwa wiki moja-mtasherehekea!
Mtanipa MIMI Heshima & Utukufu! Na wote mnaochukulia Huduma hii kama baraka na kwa wote ambao wanabariki ndoa hii Niliyoiweka pamoja leo-mbele ya umati, mbele ya dunia-Nitawabariki sana!
Upako juu ya nyinyi wawili itamwagika kwa kila Mhudumu, kila msaidizi, kila mtu anayesema, “Huduma hii ni baraka na nitaitetea, hata kuitetea katika maombi”-Sikio LANGU litasikia!
Ninawaambia haya!
Mbinguni inasherehekea! Malaika wanasherehekea! Kwa sababu mmefanya haya-siku hii-mmeharakisha wakati [ambao] YAHUSHUA MASIHI Atawajia Bibi Arusi WAKE. Na joka anasaga meno yake kwa hasira (Ufunuo wa Yohana 12:7-9, 12) kwa sababu hakuweza kuzuia kilichotendeka leo!
Sio tu uongozi, ni upendo unaotoka tu juu Mbinguni: umekadiriwa, umeteuliwa, umechaguliwa, “ukamilifu wa Upako” uliotabiriwa ambao haukuwahi fanyika-mpaka Nilipomleta Ezra kando yako. Kwa hivyo, Sherehekeeni kwa Ushindi huu!
Si Niliwaonya wewe Ezra & Elisheva kuwa kuna vita Mbinguni?-vita-kama vile vikundi vya malaika mashujaa kutoka Mbinguni walishuka chini na kupigana.
Lakini Ninawaambia haya, MIMI YAHUSHUA nilishinda vita pale Msalabani! Hii vita ilikuwa YANGU. Kwa kuwa Huduma hii sio ya mwanamume au mwanamke. Huduma hii ni ya YAHUVEH, MIMI YAHUSHUA & IMMAYAH! Huu ni Ushindi WETU. Na sasa SISI tunasherehekea nanyi. Na mamilioni na mamilioni watafikiwa!
Mtaona na watu wataitambua Upako huu mpya katika Unabii! Mahali ambapo “Ringmaiden” alisimama pekee yake bila kiongozi wa kiume kando yake-hatatabiri tena katika utumwa tena, hatatabiri akiteswa tena.
Sasa!-atatabiri-katika uhuru! Na kiongozi anayependa na kulinda tu, atakayemtia moyo kuendelea kusonga mbele! Kwa kuwa wote wawili wanasonga mbele! Kwa Upako mkuu na sio mdogo zaidi.
Kwa hivyo kwa wale wanaokuja kwa Huduma hii katika Shavu’ot, Ninawaambia haya.
Msihuzunike kwa sababu ya yule ambaye hapo awali aliitwa ‘Nikomia’! Kueni na hasira kwa yule aliyeitwa hapo awali ‘Nikomia’! Je, Mlihuzunika [juu] ya Yudasi? Kwa hivyo msihuzunike [juu] ya ‘Yudasi’ huyu.
Badala ya hayo, Sherehekeeni! Kwa kuwa nimewapea zaidi! Sio tu Mtume mmoja, Mitume wawili! Sio Nabii mmoja tu, manabii wawili! Sio mmoja tu! Sio Mchungaji mmoja tu, lakini Wachungaji wawili wakuu! Sio Mwalimu mmoja tu, lakini Walimu wawili. Sio Mhubiri mmoja tu, lakini Wahubiri wawili!
MIMI YAHUVEH Nasema mahali kulikuwa na kiongozi mmoja, daima [ilikuwa] kiongozi mmoja-ilikuwa udanganyifu [kuwa] kulikuwa ni kiongozi wa kiume!-sasa Nimewapa kiongozi wa kiume aliye na upako, aliyechaguliwa, aliyeteuliwa. Na katika umoja Ezra & Elisheva watasimama pamoja, mkono kwa mkono-wapendanao-na upendo ambao dunia hii haitawahi kuelewa. Kwa kuwa hata wao hutingiza vichwa vyao kwa mshangao.
Na mkiona ile video ya kwanza wakizungumza Mechi 7, 2016 mtaona mbele ya macho yenu ni nini tayari nilichokuwa nafanya. Mtaona Elisheva akisema kuwa yeye haamini wanaume virahisi ila tu watoto wake pale YDS na Adam pia. Lakini utamuona akiisema kuwa Ezra anaweza kuaminiwa.
Mtaona furaha. Mtasikia furaha. Mtaona upendo. Mtaona Upako. Mtasikia mafunzo-ambapo Elisheva anafurahia na hachoki kamwe kumsikia akifunza-mahali ambapo hakuna mwanamume yeyote, mwanamume yeyote, mwanamume yeyote hajawahi kufika. Kwa kuwa sikuiruhusu.
Ilikuwa kwa huu muda uliopangwa na kukadiriwa.
Elisheva aliweza kumuamini huyu mwanamume, kufunzwa na mwanamume huyu. Na kwa sababu anaamini, kongamano laweza kuamini.
Unajua sauti YANGU-wale ambao wamesikiliza Unabii na kuamini-kwa hivyo mnajua kuwa ni MIMI, YAHUVEH sasa ninayezungumza. Sherehekeeni!
Sherehekeeni kwa kuwa haya ni kwa sababu moja. Kuletea YAHUSHUA Sifa, Heshima & Utukufu anapowaleta nafsi na kuwaonyesha vile anavyowapenda! YEYE Alikuwa tayari kulipa GHARAMA pale Kalivari kwa sababu anapenda kwa njia ambayo hakuna yeyote anayeweza kuelewa na YEYE husamehe kama vile mashariki ilivyo mbali na magharibi (Zaburi 103:12)! Tubuni. Huduma hii inainua JINA LA YAHUSHUA na inawaleta wanaume na wanawake karibu (Yohana 12:32).
Lakini nawaambia haya!
Yale majina yaliyoandikwa katika Kitabu cha Uzima cha mwanakondoo-hakuna yeyote atakayekataa kuwa Huduma hii inatoa utukufu kwa MIMI YAHUVEH, YAHUSHUA & IMMAYAH.
Na ole kwa wale ambao wamevutwa kwa Huduma hii kwa sababu ya shetani kuwatumia kujaribu kuharibu huyu mwanamke na mwanamume.
Huduma hii imekuja chini ya mashambulizi makali. Lakini sasa ndio wakati! Wale mashujaa 500,000 waliokusanyika kote duniani-wanaposikia Kweli hizi-watapigana! Kwa kuwa kuna nguvu katika nambari!
Kwa hivyo Bibi Arusi wa YAHUSHUA siku ii hii MIMI, YAHUVEH, nawapa baraka-na mnapobariki huyu mwanamume na mwanamke, viongozi niliowateua, mnapobariki Wahudumu wote, mnapobariki “Wakanyaga mapepo wa YAHUSHUA,” mnapobariki wasaidizi-Ninawaambia haya. Baraka zitawajia nyinyi.
Kwa wale ambao wanataka kukuchukia, wale walio na [roho/akili] ya wakataliwa, mmeletwa hapa kwa hukumu yenu na adhabu yenu, kwa Ghadhabu na hasira ya MIMI YAHUVEH. Mmeonywa. Ni heri mfunge midomo yenu na kutoka kwenye intaneti. Kwa kuwa mmeonywa.
Na Ninawabariki kila mmoja ya YDS waliomwaga upendo wao na kazi yao katika kila video. Na ninawabariki sana mameneja wa tovuti.
Na Ninawaambia haya. Mnaweza kutafuta kwenye intaneti nzima na hamtapata Huduma iliyo na upako zaidi ya hii! Hamtapata video nzuri-video nzuri kushinda hii. “Hamna nzuri kuishinda” kwa kuwa nilimuambia kitambo kuwa lazima wafurahishe pia wanavyopasha hiki Kizazi cha nyakati za mwisho.
Miaka ishirini na moja iliyopita haya hayakuwezekana! Sasa tazameni tovuti nzuri kabisa niliyotumia mikono iliyo na upako kuitengeneza!
Hii ni vita isiyofanana na nyingine, kwenye intaneti! Lakini MIMI, BABA YAHUVEH, BABA YAHUVEH wenu ninawaahidi haya. Mmeshinda! Kama vile Daudi alivyommaliza Goliathi, kama vile Danieli alivyookolewa kutoka kwa shimo la simba, kama vile Yona alivyotoka kwenye mdomo wa tumbo la samaki mkubwa-ni vilevile tu nilivyoleta Ukombozi siku hii.
Na malaika mashujaa na Mkuu wa malaika Mikaeli & Gabrieli na wengine pia-ninawaambia haya-wataendelea kupigana vita kwa niaba yenu!
Leo hii ninavuta meno kutoka mdomoni mwa simba anayenguruma aliyejaribu kuwamaliza.
Na kitu cha mwisho nitakachosema: kuna yeyote ambaye hapendi kubadilika kwa uongozi mpya wa kiume?-ingawa haukuwahi kumjua [yule aliyeitwa ‘Niko’]-KUJA KWANGU MIMI! Uyapeleka yote katika maombi KWANGU!
Jaribuni kulalamika! Kwa kuwa mmeona Ukweli hapa. Muilete KWANGU MIMI. Mpingane NAMI! Mlete malalamishi yenu mbele ya YAHUSHUA MASIHI-MIMI YAHUVEH nasema, jaribuni.
Jaribuni.
Kwa hivyo maadui wa Huduma hii, ni heri mtoke mkikimbia!
Kwa kuwa kuna mwanamume hapa ambaye hatatishika, hatasaliti, na sio mvivu, ambaye ana upako mkuu-kama upako hizo mbili zinapokuja pamoja-ni bora mtoke mkikimbia! Maadui, katika njia saba! Kwa sababu Gogo la Ghadhabu YANGU litawaangukia siku hii!
Ni heri mfikirie mara mbili! Kwa sababu Kumbukumbu la Torati 28, laana, zitawekwa juu yenu ambayo MIMI YAHUVEH niliandika-mkitamka tu neno moja, kuandika neno moja, kashifa, uongo, au jaribu kuchafua-hamna ghadhabu ya mwanamke au mwanamume, mtakuwa na, na kuhisi PUMZI YA MIMI YAHUVEH itakayowapeperusha kama uchafu hewani!
Sitavumilia yale ambayo yamefanywa miaka iliyopita.
Kwa kila adui aliyefanya haya, mtatoa majibu kwa haya. Kwa kuwa mmejichimbia hadi jehanamu na maneno ya mdomo wenu.
Na kwa kila mtu ambaye ameamini uongo na bado hudai eti ni WANGU-wanaodai wameoshwa na DAMU YA YAHUSHUA na bado wamerudia na “wameamini uongo,” (2 Wathesalonike 2:11) ni heri mtubu haraka au jueni haya: Nitawalazimisha kuwajibika kwa kila neno mliyozungumza, kila neno mliyoandika na kila uongo mliyoamini-mtakapokuja mbele ya kiti cha Hukumu.
Na kwa watetezi, wasaidizi, watiaji moyo-MIMI YAHUVEH nasema haya kwenu. Asante. Mtatuzwa. Kwa kuwa mlisikia Sauti ya MIMI YAHUVEH na Sauti ya YAHUSHUA MASIHI & IMMAYAH. Mliweza kuhisi Upako huo. Na mlioga kwenye Upako huo. Mlisherehekea kwenye Upako huo. Na mkatubu kwa sababu ya Upako huo. Na makuu Yatakuwa tuzo zenu mnapoendelea kufanya vivyo hivyo.
Kwa hakuna yeyote katika Bibi Arusi wa YAHUSHUA hawatawahi kutupia huyu Nabii [Elisheva] mawe na sasa huyu Nabii mpya [Ezra].
Na ilikuwa maombi ya mwenye haki yanayo nguvu tena yanayofaa sana. (Yakobo 5:16) kote duniani, maombi ya “Wakanyaga mapepo wa YAHUSHUA” yamefaa sana-ni kwa vita ya malaika mashujaa-walioshinda Ushindi huu. Na ni kwa sababu ya DAMU YA YAHUSHUA ILIYOMWAGWA pale Kalivari kwa sababu yenu!
Mwisho wa Neno
Elisheva: O, wow! Sifa kwa YAHUSHUA!
[Kathrynyah pia anasikika kwa umbali: Amina, sifa kwa WEWE BABA YAHUVEH, YAHUSHUA, IMMAYAH…!]
Ezra: O, sifa kwa BABA YAHUVEH! Sifa kwa WEWE YAHUSHUA! Sifa kwa WEWE RUACH HA KODESH! Asante! Asante BABA kwa Ushindi huu-kwa haya-kushinda vita na yote uliyofanya WEWE kwa niaba yetu.
Kathrynyah: Amina.
Ezra: Tunakushukuru BABA YAHUVEH! Tunakubariki! Tunakupa utukufu na tutasherehekea kwa siku hizo zote 7 kama ulivyotuamuru sisi kufanya. Kufurahia na kusherehekea!
[Elisheva anacheka kwa furaha.]
Ezra: Kwa sababu Ushindi ni wetu! Ushindi ni WETU! WEWE Ulipigana kwa niaba yetu-tulipokuwa tunaimba nyimbo za sifa kwa JINA LAKO BABA. Wewe ni wa ajabu! JINA LAKO ni kuu. Majina YENU ni makuu (Zekaria 14:9)!
Elisheva: Amina! Amina! Amina!
Ezra: Amina na Amina!
Mwisho wa Rekodi
Ilizungumzwa, iliandikwa katika JINA la YAHUSHUA, 12 Juni 2016
Mtume, Nabii Elisheva Eliyahu
Unahitaji maombi au Wokovu? Je, una maoni au maswali? Tafadhali tuma barua pepe kwake Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!